George Mwakalinga: Wazee na Wazazi wasaidie kuwahamasisha Watoto wao kushiriki shughuli za maendeleo kwa Jamii

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,813
11,991
Mkurugenzi wa Redio ya Jamii ya Kyela FM iliyopo Mkoani Mbeya, George Mwakalinga ameuomba Umoja wa Wazawa wa Kyela waishio ndani na nje ya Kyela kuwatafuta wazawa wengine ambao bado hawajajiunga ili kuweka umoja wenye nguvu na mshikamano kwa ajili ya kuijenga wilaya yao.

Mwakalinga ametoa rai hiyo akizungumza na Wanakyela kwa njia ya simu ambapo amesema ni jambo jema la kuwakutanisha na kuwaunganisha wazawa katika kusaidia jamii katika nyanja mbalimbali na kwamba ni wakati sasa kufanya shughuli za maendeleo.
53eee7d9-7e98-41c4-b037-331cde3cb0d4.jpeg

6128ad3c-dc4f-430b-bccb-f2275451e38b.jpeg
Amesema katika kufanikisha jambo hilo wazee na wazazi wasaidie kuwahamasisha watoto wao kushiriki shughuli za maendeleo kwa Jamii ya Kyela na kuweka utaratibu wa kurudi nyumbani.

“Napenda kile wanachokifanya Kyela Ibasa kuhamasishana kurudi nyumbani kila unapofika mwisho wa mwaka wanachangishana fedha kusaidia jamii, nimekuwa miongoni mwa Wanaibasa na nimeona faida, najua tutafanya mambo mengi kwa ustawi wa wilaya yetu,” amesema Mwakalinga.

Mmoja wa WanaIbasa, Faraja Mwakapala amesema wameyapokea maoni ya Mkurugenzi wa Kyela FM, George Mwakalinga la kuwatafuta Wanakyela popote walipo kujiunga na Ibasa.

Naye, Dismas Mwakatundu, amesema amelipokea wazo la Mwakalinga kuhusu Ibasa kupanda miti maeneo mbalimbali ya eneo hilo kama sehemu ya utunzaji na uhifadhi wa mazingira.

Amedai watafanya mazungumzo na taasisi mbalimbali za misitu ili kupata miche ambayo itapandwa kwenye maeneo yenye uhitaji.
 
Back
Top Bottom