Generali Ojukwu Ni Kwanini?

Generali Ojukwu Ni Kwanini?

Wakuu Nyerere alimuunga mkono Ujukwu kwa sababu ya imani za kidini. Hakuna sababu nyingine. Hutaki unaacha

Kimbunga,

..kwa kumbukumbu zangu Nyerere pia aliwahi kupeleka majeshi kusaidia serikali ya Comoro.

..sasa sote tunaelewa kule Comoro wanachi wake ni wa imani gani.

..pia alisaidia Frelimo dhidi ya Wareno ambao wanajinasaba zaidi na Ukatoliki.

..hapa Tanzania alitaifisha shule za Kanisa nyingi zikiwa za kanisa Katoliki.

..I think Nyerere is such a complex figure huwezi kumfungia kwenye "boksi" moja.

NB:

..mtizamo wa Mwalimu kuhusu Ukristo na Kanisa unapatikana ktk hotuba yake ya "The Church and Society" aliyoitoa kwa watawa wa Maryknoll.
 
- Kila ninapoangalia tulikotokea hili Taifa, ninapatwa wasi wasi sana kwamba hatukufika hapa tulipo kwa makosa, tumefanya makosa mengi sana nyuma in terms of policies mpaka leo hii kurekebisha inakuwa ni almost impossible, ingawa watawala wa sasa wanajitahidi sana.

- Eti ni kwa nini Tanzania tuliunga mkono Waasi wa Nigeria waliokuwa wanaongozwa na General Ojukwu, kwenye kiu yao ya kujitenga na Nigeria Federation? Ninakumbuka tukiwa wadogo Shuleni, tulivyokuwa tunaimbishwa nyimbo za kumsifu Ojukwu, why? I mean ni policies ngapi huko nyuma we were wrong maana inaonekana ni nyingi sana that ni vigumu sana sasa kurekebisha njia!

- JE have we ever
apologize to the Nigerians kwa makosa yetu ya kuuunga mkono uasi wa Ojukwu, dhidi ya serikali halali ya nchi hiyo?

- MUNGU AIBARIKI TANZANIA!

William J. Malecela.

Mh. Mbunge mtarajiwa, kuna ka-herufi hapo kamesahulika ingawa objective ya huu uzi ikiwa imefikiwa.
 
Ninachokiona bila kificho ni kuwa Nyerere was never " a smiling boy" na maamuzi yake yameacha majeruhi wengi sana. Lakini siku zote matendo yanaongea zaidi kuliko maneno. Kama leo tunataka kumgaragaza Nyerere chali yeye pamoja na utawala wake, basi pasipo na shaka, lazima performance yetu leo iwe zaidi ya utawala wa Nyerere tena kwa vitendo. Mfano mdogo tu...enzi za awamu ya pili, zile Pajero mbofu mbofu alizileta nani???
na hata leo hii, utawala wetu unajengwaje? kwa mtindo wa aliyejuu afatwe huko huko juu aliko hata kama hana uwezo wa kuongoza? Uongo si kitu cha kukikumbatia maana mwisho wa uongo ni aibu, na Taifa lolote linalojaribu kusimama kwa msingi ya uongo litaanguka.
Mungu Ibariki Tanzania
 
Kimbunga,

..kwa kumbukumbu zangu Nyerere pia aliwahi kupeleka majeshi kusaidia serikali ya Comoro.

..sasa sote tunaelewa kule Comoro wanachi wake ni wa imani gani.

..pia alisaidia Frelimo dhidi ya Wareno ambao wanajinasaba zaidi na Ukatoliki.

..hapa Tanzania alitaifisha shule za Kanisa nyingi zikiwa za kanisa Katoliki.

..I think Nyerere is such a complex figure huwezi kumfungia kwenye "boksi" moja.

NB:

..mtizamo wa Mwalimu kuhusu Ukristo na Kanisa unapatikana ktk hotuba yake ya "The Church and Society" aliyoitoa kwa watawa wa Maryknoll.
Jokakuu,
So far todate, Nyerere is the only political master of this country...wengine wanachechemea. Badala ya kutengeneza image na character zao, wanajaribu kuipiga ngumi sanamu yake. What a tidious job!
 
Biafra alikuwa anatetea dagaa?

Robo tatu ya Dunia inawaunga mkono PLO kwa sababu wanaporwa ardhi yao wanauwawa na Israel wanafanyiwa dhulma nyingi ndio maana unaona Wapelstine wanapewa hifadhi karibia dunia nzima, wapo Chile, Canada, Marekani, Ujerumani, Uingereza, Urusi, Saudia Arabia, Dubai, Argentina, Jordan, Lebanon, na sehemu zingine za dunia nchi zote hizo zimeamua kutoa hifadhi kwa Palestine sababu wanajua wanadhulumiwa haki yao..

Biafra ilikuwa ni uasi ndio maana nchi nyingi za ulaya Urusi, Uingereza, Czechoslovakia, ziliwasaidia majesi ya shirikisho kuzima huo uasi...Urusi na Chzechoslovakia walitoa ndege mpya za jeshi kuwashambuilia waasi.

Usifananishe mgogoro wa Mashariki ya kati na mgogoro wa Biafra Nigeria, kama utakuwa upande wa Israel basi wewe unatakuwa Jewish.
 
Zomba,
No 3) umenoa. $1 ya Kimarekani ilikuwa ni shillingi saba. Pauni moja ilikuwa ni shillingi 20.
No4) pia ni misinformation. Azimio la Arusha limetangazwa Februari 1967. Tumetangaza kuitambua Biafra April 13, 1968.
Wapi na wapi?

Uko mbali sana ndugu yangu hata mwaka 1974, ndio mara yangu ya kwanza kusafiri nje ya Tanzania Pauni moja ilikuwa haijafika bei hiyo.
 
Jibu muhamasishaji (UAMUSHO) acha kung'ata ulimi. Umweulizwa Tanzania ilikuwa inawunga mkono wapalestina kwa sababu ni wakrito?

Tatizo lako uvivu wa kusoma rudi nyuma utakutana na majibu yangu.
 
Zomba,
No 3) umenoa. $1 ya Kimarekani ilikuwa ni shillingi saba. Pauni moja ilikuwa ni shillingi 20.
No4) pia ni misinformation. Azimio la Arusha limetangazwa Februari 1967. Tumetangaza kuitambua Biafra April 13, 1968.
Wapi na wapi?

Vita ya biafra imeanza 1967 na kama tuliitambua 1968 hapo ilikuwa baada ya wao ku declare nchi mpya isiyokuwepo na Nyerere akawatambua (sio sisi). Nyerere alikuwa anaisaidia Biafra kabla ya kutangaza kuitambua. Kwa hiyo mwaka niliyouweka "1967" kwa kuisadia Biafra kwa kuichangia kwa vikopo na ndio mwaka uliotangazwa Azimio la Arusha, na ndio mwaka Tanzania ilianza kuingia kwenye lindi la umaskini usio na mfano ni sahihi kabisa. Huwa sikisii! Nilikuwepo.
 
Robo tatu ya Dunia inawaunga mkono PLO kwa sababu wanaporwa ardhi yao wanauwawa na Israel wanafanyiwa dhulma nyingi ndio maana unaona Waperstine wanapewa hifadhi karibia dunia nzima, wapo Chile, Canada, Marekani, Ujerumani, Uingereza, Urusi, Saudia Arabia, Dubai, Argentina, Jordan, Lebanon, na sehemu zingine za dunia nchi zote hizo zimeamua kutoa hifadhi kwa Palestine sababu wanajua wanadhulumiwa haki yao..

Biafra ilikuwa ni uasi ndio maana nchi nyingi za ulaya Urusi, Uingereza, Czechoslovakia, ziliwasaidia majesi ya shirikisho kuzima huo uasi...Urusi na Chzechoslovakia walitoa ndege mpya za jeshi kuwashambuilia waasi.

Usifananishe mgogoro wa Mashariki ya kati na mgogoro wa Biafra Nigeria, kama utakuwa upande wa Israel basi wewe unatakuwa Jewish.

Kama robo tatu ya Dunia inawaunga mkono PLO maana yake robo moja ya Dunia haiwaungi mkono. Sasa, kwa nini Tanzania ikachagua kuungana na robo tatu na sio hii robo iliyobakia? Kuna sheria pengine iliyolazimisha Tanzania kusimama upande wa robo tatu ya Dunia?
 
wakuu Nawasoma kwa umakini endeleeni kudadavua.!
 
Kama robo tatu ya Dunia inawaunga mkono PLO maana yake robo moja ya Dunia haiwaungi mkono. Sasa, kwa nini Tanzania ikachagua kuungana na robo tatu na sio hii robo iliyobakia? Kuna sheria pengine iliyolazimisha Tanzania kusimama upande wa robo tatu ya Dunia?

Hiyo robo hawafungamani na upande wowote ndio maana unaona ni nchi moja tu duniani Marekani peke yao ndio wanawaunga mkono Israel sababu nimekuambia ni Jewish wenzao...Nyerere aliwaunga mkono waasi wa Biafra sababu ya dini ukitaka chukuwa ukitaka acha.
 
- Kila ninapoangalia tulikotokea hili Taifa, ninapatwa wasi wasi sana kwamba hatukufika hapa tulipo kwa makosa, tumefanya makosa mengi sana nyuma in terms of policies mpaka leo hii kurekebisha inakuwa ni almost impossible, ingawa watawala wa sasa wanajitahidi sana.

- Eti ni kwa nini Tanzania tuliunga mkono Waasi wa Nigeria waliokuwa wanaongozwa na General Ojukwu, kwenye kiu yao ya kujitenga na Nigeria Federation? Ninakumbuka tukiwa wadogo Shuleni, tulivyokuwa tunaimbishwa nyimbo za kumsifu Ojukwu, why? I mean ni policies ngapi huko nyuma we were wrong maana inaonekana ni nyingi sana that ni vigumu sana sasa kurekebisha njia!

- JE have we ever apologize to the Nigerians kwa makosa yetu ya kuuunga mkono uasi wa Ojukwu, dhidi ya serikali halali ya nchi hiyo?

- MUNGU AIBARIKI TANZANIA!

William J. Malecela.

I think you are simply on a mission to discredit Mwalimu Nyerere. It seems that you have some grudges against him. One can get such conclusions from your recent threads including that of Arusha declaration.

How old are you?
Were you there, in a party organized by your mdingi when he was tipped for PM post (before Sokoine) only to be dissapointed later when Sokoine was announced as PM? If you were there, then I can understand your grudges.

You obviously were an adult capable of understanding National Politics in 1995 when again, your mdingi was removed at some stages, from the list of CCM presidential nominees. You never and will never forgive Mwalimu for that, will you?
 
Hiyo robo hawafungamani na upande wowote ndio maana unaona ni nchi moja tu duniani Marekani peke yao ndio wanawaunga mkono Israel sababu nimekuambia ni Jewish wenzao...Nyerere aliwaunga mkono waasi wa Biafra sababu ya dini ukitaka chukuwa ukitaka acha.

Kwa hiyo Nyerere alikuwa na sababu tofauti kwa Biafra na Palestina, sio? Je, how about Western Sahara? sababu nayo ni ipi?
 
zomba

Tatizo la Mkandara ana mahaba sana na Mwl Nyerere hawezi kabisa kuyataja mapungufu yake kama ili la Biafra ukweli unajulikana na nafsi yake inajua kuwa Mwl Nyerere aliwaunga mkono waasi wa Biafra sababu kubwa ni dini, lakini hawezi kuandika hayo kwa mahaba makubwa na Mwl Nyerere.
Ritz, nakushauri sana kabla yakuandika jambo ufanye utafiti wako japo kidogo.

Nenda kasome historia ya Waingereza wakiwa Nigeria tangu 1922 wakati Nyerere anazaliwa. Halafu angalia Nigeria ilianza na majombo 4 kwanini yameongezeka mara tatu!
Soma harakati za Nigeria katika uhuru mwaka 1960, wakati ambapo Nigeria ilifunika tofauti za kisiasa, kiuchumi na kijamii.

Kwa taarifa yako Nigeria ni taifa lililogawanyika sana katika maeneo ya kiuchumi, kisiasa na kiutamaduni. Hili la Waislam na Wakristo siyo tatizo pekee la Nigeria. Hata waislam katika majimbo yao au wakristo wanatofauti sana.
Haya sisomi wala kusimuliwa nimeyaona mwenyewe na namshukuru mungu.

Then, soma historia ya Nnandi Azikiwe, Balewa, Obafemi Awololo, Yakoub Gown! kabla hujafika 'biafran'.
Ukipata uelewa wa Biafran, enenda zaidi kusoma habari za akina Murtala Mohamed, Obasanjo, Othman Shehu Shagari, Muhamd Buhari, Abdisalaam, Sani Abacha ili uelewe tatizo kubwa la Nigeria ni nini.

Hoja yako kuwa Nyerere aliunga mkono kwasababu ya dini inaweza kuwa sawa kwasababu ukishaaminishwa kuwa Nyerere alikuwa mwanaume kwasababu ya dini hakuna anayeweza kukuzuia kuamini! watu wanaweza kukusaidia kujitambua tu

Jibu la swali lako ni kuwa, Nyerere aliunga mkono Waisrael kwanza. Baada ya wao kuanza kuwafukuza Wapaelstina kwasababu zile zile zilizomfanya aunge mkono, Nyerere akavunja uhusiano na Israel na wala si kulaani tu.
Sijui kama unajua ubalozi wa PLO pale Upanga! Na marehemu Yaser Arafat hakusita kukutana na Nyerere fursa ilipotokea,
Sasa hapo udini uko wapi?

Nyerere alivunja uhusiano na Uingereza mwaka 1965 kwasababu UK ilimtambua Ian Smith ambaye ni mkristo.
Serikali ya Nyerere iliunga mkono wapiganaji wa POLISARIO.
Alikuwa rafiki na mshirika mzuri wa Marehem Huari Boumodiane wa Algeria kwenye waislam.

Aliunga mkono kwa silaha, makazi na askari juhudi za kumuondoa mreno ambaye ni Mkatoliki kweli kweli kule Angola na Msumbiji.

Na mwisho nikumbumbushe maneno ya Nyerere kuhusu Biafra katika bandiko langu lililotangulia. Kwa ufupi amesema sababu zilizomfanya aunge mkono Biafra ni zile zilizomfanya aunge mkono Isreal kuhusu haki ya wanadamu kuishi.
Na ndizo sababu hizo hizo zilimfanya aunge mkono Palestina.

Ritz, kama kuna mtu amekufundisha kumchukia Nyerere bila sababu hiyo ni hiari yako,lakini basi hiari hiyo usiisukimize kooni kwa wengine. Kuna vijana wanataka kuelewa wape nafasi waweze kuchambua na kuwa na fikra zao.
 
Compromise wa MWalimu hata siku moja hamuwezi kukubali alipokosea, lazima mje na hadithi nyingi za ujanja ujanja, badala ya kukubali tu kwamba kwenye hiyo policy tulikosea na sio hiyo zipo nyingi sana tulikosea ndio maana mpaka leo Taifa linayumba yumba tu!

William.

Mzee W. J. Malecela, kuna tofauti kati ya sera (policy), tamko (statement) na msimamo (stand). Sasa suala la serikali ya JMT kuunga mkono na kutambua eneo la Biafra si sera bali ni msimamo wa serikali hiyo ulitolewa kwa njia ya tamko katika kushinikiza madai ya waibo. Suala hilo halikuwa policy issue kwa serikali ya Tanzania,kwani sera haina budi kutungwa ikiwa na madhumuni ya kufanikisha malengo fulani yenye kuheshimu imani za wale ambao malengo hayo yatakuwa yana faida kwao.

Suala la Biafra lilikuwa ni msimamo ulioamuliwa na serikali ya Tanzania tu.
 
Last edited by a moderator:
Kwa hiyo Nyerere alikuwa na sababu tofauti kwa Biafra na Palestina, sio? Je, how about Western Sahara? sababu nayo ni ipi?

FJM

Hiyo ni Subject ingine itabidi tuanzishie thread yake kwa sasa tujikite zaidi na Biafra na Mwl Nyerere.
 
Nimekuelewa. Mtu mzima akibanwa hapigi kelele, anakuna kichwa!.
 
Mzee W. J. Malecela, kuna tofauti kati ya sera (policy), tamko (statement) na msimamo (stand). Sasa suala la serikali ya JMT kuunga mkono na kutambua eneo la Biafra si sera bali ni msimamo wa serikali hiyo ulitolewa kwa njia ya tamko katika kushinikiza madai ya waibo. Suala hilo halikuwa policy issue kwa serikali ya Tanzania,kwani sera haina budi kutungwa ikiwa na madhumuni ya kufanikisha malengo fulani yenye kuheshimu imani za wale ambao malengo hayo yatakuwa yana faida kwao.

Suala la Biafra lilikuwa ni msimamo ulioamuliwa na serikali ya Tanzania tu.
Nzi, walishabilisha sera hawa wasanii wala wasizuge. Inaitwa Economic Diplomacy. Sasa hivi Tanzania stands for nothing.
 
Back
Top Bottom