Generali Ojukwu Ni Kwanini?

Generali Ojukwu Ni Kwanini?

Ikiwa Nyerere aliwaunga mkono Biafra kwa sababu ya dini, ina maana waliokuwa wakiteswa walikuwa wakristu hivyo kkuwafanya wale walopigana dhidi yao kuwa Waislaam sio?.. Mkuu wangu nyie mnatazama vitu gani?... ndio maana Jasusi na wengine wamewaambia kuwa mnafanya makosa sana kuifikiria udini kwa sababu aliyekuwa rais wakati huo alikuwa Gowon sio Mkandara ama Ustadhi akitetea dini yake, huu udini mkuu wangu unatoka wapi?.

Pia wamekuwepo marais wengine ktk Federation hiyo ya Nigeria ambao ni Waislaam na wakristu lakini wote hadi leo wanapingana na kujitenga kwa Biafra kama tunavyopinga kujitenga kwa Zanzibar, na hivyo usitake kabisa kusema anayewaunga mkono Zanzibar lazima awe Muislaam na anafanya hivyo kwa mapenzi ya Usilaam - huu ni ufinyu wa kufikiri na hufanywa sana na watu wasiokuwa na Ilimu dunia, walopoteza imani na matumaini isipokuwa kumtafuta mchawi. Sitopenda kabisa kuamini kwamba ndivyo Ulivyo, mkuu wangu.

Tatu, labda niongezee kusema tena Biafra haikuwa wala sii sehemu ya wakristu ila ni jimbo la kabila la Waibo ilihali Nigeria kuna makabila mengine mengi tu wakristu ambao hawaishi ktk jimbo hilo la mashariki. Na usije fananisha kabisa Biafra na Sudan ya Kusini maana Wapo Wakristu wengi Nigeria ilobakia ndani ya Federation kuliko walokuwa Biafra, hivyo sielewi hii habari unaipata wapi kuwa Biafra ni ya Wakristu wakati yule Ojukwu hata kanisani alikuwa hapajui isipokuwa msituni kama kina Che. Pengine ukisema Ojukwu alikuwa Mjamaa kwa kutazama magwanda alokuwa akivaa, akitumia mbinu za Che na support kutoka nchi za Kijamaa hapo naweza kubaliana nawe hata kama hakuna ukweli huo maana vitu vingi vinashabihiana na ushabiki wa Ukomunist...

Mengine mkuu wangu nakuachieni kwa sababu sifikirii ndani ya box la udini kila siku. Natumia sana kipimo cha Uhuru, Haki na usawa na pale kimojawapo kinapokosekana huwaunga mkono wale waotoa madai yao na sii watu wanaotaka Uhuru wa nchi kwa jina lake japokuwa wao wenyewe wako huru, na wana haki sawa na wengine.

Mkandara kwa nini Biafra walikuwa wakipinga utawala wa wanajeshi Waislam?

Na yale mauaji ya watu milioni 2 yalisababishwa na nini?
 
Last edited by a moderator:
Unstoppable,
William hayuko sahihi. Na historia inamsuta. Mwalimu ameondoka mamlakani mwaka 1985. Poland na nchi za Ulaya mashariki zilitupilia mbali utawala wa kikomunist baada ya 1989. Wenzetu wamepiga hatua kubwa na huwasikii wakilalamika kama anavyofanya William and his ilk eti Mwalimu alifanya hiki au kile ambacho kiliturudisha nyuma. Angalia Ujerumani mashariki, wameacha kulalamika na ni mwendo mdundo mbele tu. Hawa waliokuja baada ya Mwalimu akiwemo na William na baba yake hawana vision kabisa. Wameshindwa kuendesha gurudumu la maendeleo sasa imebaki kumlaumu Mwalimu tu. Lakini historia inawasuta! Kama Mwalimu alishindwa wangetuonyesha ni wapi aliposhindwa na wao wamefanya nini kutuletea mafanikio. .

Well said Jasusi, na mimi hapo penye red ndio ninajiuliza zaidi. Je toka Mwalimu aondoke walikua hawajashtuka ndio wameshtuka sasa au Mwalimu anafanywa a scapegoat?
 
Mkandara kwa nini Biafra walikuwa wakipinga utawala wa wanajeshi Waislam?

Na yale mauaji ya watu milioni 2 yalisababishwa na nini?

ritz,

..zilitumika mbinu za kikatili sana kuzima maasi hayo ikiwemo kuwa-starve wananchi wa Biafra.

..kwa kweli ingekuwa ni zama hizi nadhani Gowon angenyakuliwa na Mzee Ocampo na kupelekwa kwenye mahakama ya ICC.
 
Mkandara kwa nini Biafra walikuwa wakipinga utawala wa wanajeshi Waislam?

Na yale mauaji ya watu milioni 2 yalisababishwa na nini?
Ritz1
Unakosea unapoingiza Uislamu kwenye kisa hiki cha Nigeria na Biafra. Ni kweli wote Gowon na Ojukwu walishiriki katika kupindua serikali halali ya Tafawa Balewa. Lakini wote Ojukwu na Gowon hawakuwa waislamu. Mapinduzi hayo ya kijeshi yalianzia eneo la Waislamu la Kaduna, January 15, 1966. Wakati huo kiongozi wa jeshi alikuwa ni Muibo Meja Jenerali Aguiyi Ironsi, ambaye yeye alikuwa anaunga mkono serikali ya shirikisho. Lakini baada ya waziri mkuu kuuawa, pamoja na waziri wa fedha na maafisa kadhaa wa kijeshi, alikubali kuongoza nchi. Lakini kukatokea mapinduzi mengine July 28-29 1966 ambapo Ironsi na maafisa wengine wa Kiibo waliuawa. Hapo ndipo uhasama ulipoanza baina ya Waibo na Gowon ambaye alichukua uongozi baada ya mapinduzi ya pili. Kwa hiyo unafanya kosa kubwa kuhusisha kadhia hiyo ya Nigeria na udini. Ungesema ukabila, ningekubali. Lakini endelea kubukua mabuku.
 
:A S cry: It's a pity kuwa we cannot talk about our situation here -- kweli Mwl. Nyerere amefanya makosa sana lakini pia amekua na busara sana in the sense that he got rid of Ukabila ambae inatesa sana wenzetu wa Kenya na wa Ganda. Lakini kwa maendeleo kweli amkill kabisa laiti akiacha wale wazungu kutuendeleza at least we would have been very far and the best country all over Africa. Moreover, Mwl. thought tukiweza wenyewe lakini ulafi, uchi ya madaraka n.k. ndio imetufikisha nchi yetu hapo tulipo. I think we should concentrate on our country problems kuliko kuzugumza mambo ya Nigeria. Au baba anatupa adisi ya Alfa Ulela ulela ???? Ongea zako.
 
Mkandara kwa nini Biafra walikuwa wakipinga utawala wa wanajeshi Waislam?

Na yale mauaji ya watu milioni 2 yalisababishwa na nini?
Kwasababu ni masultan, na hawakutaka utawala wa kisultan, same as waliofanya mapinduzi ya Zanzibar, tatizo si uislam, ni usultan.

Sasa nyie misukule ndo hamjui utofauti,mnaenda kichwa kichwa tu mkiimbishwa kama kasuku, poor you!Pole sana.
 
Hayo ni maneno ya kujifariji angekuwa anapendwa angekimbilia Ivory Coast?
Wakumshukuru ni Rais wa Nigeria kipindi hicho Shehu Usman Shagari, kumsamehe.
ritz, asingemsamehe, nchi ingeingia matatani, alikuwa na influence, especialy politicaly.Na ushahidi ni kabla na hata baada ya kufa.
 
- Mkuu a very smart prepared story, swali ni kwa nini Tanzania tuliunga mkono waasi kujitenga, umeleta habari nyingi ambazo hazihusiki kabisa, unasema justification ni Mwalimu alitaka Rais wa Federation akae chini na waasi kujadiliana na a compromise ya katiba ya Federation under the gun, unasema kuna Rais Duniani anaweza kukubali hiyo? Yaani hoja zako ni so weak ingawa zimepangiliwa sana lakini ni very weak!

- Kusaidiwa na kina Kaunda ndio kunahalallisha kuunga mkono waasi wa Taifa lao? Then kwa nini Uingereza haikshiriki? I mean you are so manipulative unasema sababu ya mafuta ndio Uingereza wasadia kuprotect Federation, lakini sisi sababu ilikuwa ni amani tu, my God na tunaosoma tunatakiwa kuwa nini mkuu? Tumelala au what?

- Compromise wa MWalimu hata siku moja hamuwezi kukubali alipokosea, lazima mje na hadithi nyingi za ujanja ujanja, badala ya kukubali tu kwamba kwenye hiyo policy tulikosea na sio hiyo zipo nyingi sana tulikosea ndio maana mpaka leo Taifa linayumba yumba tu!

William.
Kumbe Wlly wewe una majibu yako unayoyajua umekuja humu kutuchanganya tu mbona kila unachoambiwa hutaki? Umeambiwa reja vitabu umekataa umepewa taarifa ya aliyekuwepo siku Mwalimu alivyotoa uamuzi wa kuiunga mkono Biafra huku akijilaumu bado unapinga tu sasa unataka kwenda polisi au unataka jibu gani litakalofurahisha mtima wako?
 
Ni kwasababu ya visirani tu........visirani vinawafanya watu washindwe kufikiri.......na hata kuzuia ability ya kufikiri.......it is pathetic..........

- ha! ha! ha! yaani hoja zingine bwana, sasa visirani na pathetic hapa ni nani hasa? ha! ha! ha!

William.
 
Well said Jasusi, na mimi hapo penye red ndio ninajiuliza zaidi. Je toka Mwalimu aondoke walikua hawajashtuka ndio wameshtuka sasa au Mwalimu anafanywa a scapegoat?

- Angeanza na kuongela hilo lijumba la Balali kwanza ndio aseme mengine ya binafsi za watu, kutesa ni kwa zamu zamu yao iliiisha sasa ni ya wengine ndio maisha!!!

William.
 
- ha! ha! ha! yaani hoja zingine bwana, sasa visirani na pathetic hapa ni nani hasa? ha! ha! ha!

William.

Ulishindwa kujenga hoja na kutia huruma kwenye kinyang'anyiro cha ubunge wa EAC.........sasa unaleta visirani na vioja.........haitakusaidia........hata kidogo.......
 
Mkuu ritz naona umezama sana kuhusu historia ya Nigeria! Unawajua mageneral wote waliokuwa wakitamba wakati huo
 
Last edited by a moderator:
Kwasababu ni masultan, na hawakutaka utawala wa kisultan, same as waliofanya mapinduzi ya Zanzibar, tatizo si uislam, ni usultan.

Sasa nyie misukule ndo hamjui utofauti,mnaenda kichwa kichwa tu mkiimbishwa kama kasuku, poor you!Pole sana.

jmushi1.

Kabla ya ukoloni Nigeria ilikuwa na falme mbalimbali Kaskazini ilikuwa chini sultani za kiislam Kano na Sokoto...Kusini ilikuwa na falme za Benin, Ife na Oyo.

Naimani wewe unapenda kujua na kufahamu jaribu kuangalia historia ya Nigeria kwenye mjimbo yao Kebbi, Niger, Kaduna, Yobe, Borno, Zamfara, Kastina, Bauchi, Kano, kwa nini wanatumia Sharia.

Labda nikuulize mwaka 1966 sehemu ya jeshi la Nigeria walifanya uasi na wakamuua Waziri Mkuu Abubakar Tafawa Balewa, aliyekuwa na asili ya Kaskazini, kwa nini walifanya hivyo?
 
jmushi1.

Kabla ya ukoloni Nigeria ilikuwa na falme mbalimbali Kaskazini ilikuwa chini sultani za kiislam Kano na Sokoto...Kusini ilikuwa na falme za Benin, Ife na Oyo.

Naimani wewe unapenda kujua na kufahamu jaribu kuangalia historia ya Nigeria kwenye mjimbo yao Kebbi, Niger, Kaduna, Yobe, Borno, Zamfara, Kastina, Bauchi, Kano, kwa nini wanatumia Sharia.

Labda nikuulize mwaka 1966 sehemu ya jeshi la Nigeria walifanya uasi na wakamuua Waziri Mkuu Abubakar Tafawa Balewa, aliyekuwa na asili ya Kaskazini, kwa nini walifanya hivyo?
Mkuu ritz narudia tena, tatizo halikuwa uislam, bali usultan, waislam wengine mnaunganishia tu, lakini usultan si uislam, naomba kusahihishwa.

Sasa kama hayo majimbo yanatumia sharia ndo waibo wakusini wauwawe?Ama ndo Naijeria nzima watumie sharia? Hiyo ya 1966 lazima walikuwa waki "defend themselves" kutokana na mauwaji hayo ya serikali ya kinyama ya masultan.
 
Ulishindwa kujenga hoja na kutia huruma kwenye kinyang'anyiro cha ubunge wa EAC.........sasa unaleta visirani na vioja.........haitakusaidia........hata kidogo.......

- Fungua thread ya EAC hapa ni ya Biafra! ha! ha! ha! ha! kinyonga wewe! ha! ha! ha!, ndio unasema unakuaj bongo uje nikutembeze kwenye viwanja! ha! ha! ha! ha!

William.
 
Mkandara kwa nini Biafra walikuwa wakipinga utawala wa wanajeshi Waislam?

Na yale mauaji ya watu milioni 2 yalisababishwa na nini?
@ritz, kwanza nieseme kweli sikuelewi kabisa hapa. Lakini nadhani unachozungumzia ni mfululizo wa vita baina ya vyama na ushabiki ulotokana na mgogoro wa uongozi ndani ya chama cha Chief Awolowo - AG baada ya Shangari kuunda muafaka na chama hicho kwa kumteua Akintola kwa Premier wa jimbo lao.

Ikumbukwe tu kwamba anayoyafanya JK ndio historia ya Nigeria hivyo, nimesema sana hapa JF kuhusu wapi tunakwenda lakini inaonyesha watu mmeweka pamba masikioni. Matatizo hayakuanza na wakristu vs waislaam hata kidogo isipokuwa matatizo yalianza kwa wayoruba. SDijui kama unaelewa kwamba uongozi wa kwanza wa nchi hiyo ulikuwa wa mseto baina ya chama cha wa Hausa who happened to be dominant Muslim na kile cha wa Ibo ambao pia dominant ni wakristu kwa sababu NDC hawakupata majority vote ktk uchaguzi mkuu..

Sasa sikuelewi unaposema Biafra walikuwa wakipinga uongozi wa wanajeshi Waislaam wakati aliyekuwa rais wa nchi hiyo toka uhuru alikuwa Azikiwe Myoruba na mkristu maana Balewa alikuwa Prime minister tu. Vijana wa kijeshi waliompindua Azikiwe inasemekana walikuwa Waibo sawa lakini inahusiana nini na Uislaam na Ukiristu ikiwa rais alopinduliwa alikuwa Mkristu?..Na hawa vijana nao wakaja pinduliwa na Generali Johson (mkristu) aliyetaka kuvunja Federation na kuunda Republic... Wewe unazungumzia wakati gani haswa?

Kuhusu Biafra mkuu wangu nimeshasema sana kwamba sababu kubwa ya Biafra kupingana na the rest of Nigeria ni pale walipoona rasilimali zao zote zinakwenda North kujenga kwa Wahausa na Wayoruba ambao walikuwa na mseto wao. Kweli Waibo walikiunga mkono zaidi chama cha NCNC kwa sababu strong hold yake ni jimbo la East na kwao, na kuna ukweli kwamba Waibo wengi ni wakristu lakini haina maana kabisa kwamba kilikuwa chama cha Wakristu, wala sikubaliani na wale wanaodai kwamba NDC kilikuwa chama cha waislaam wakati chama hicho kilikuwa cha Wahausa who happened to be dominant Muslim. Lakini Biafra imetokana na nchi kutokuwa na UMOJA, kutokuwa na rais aliyechaguliwa na wananchi baada ya wanajeshi kupigania madaraka wao kwa wao hadi Gowon kuingia kati..

Sikubaliani na dhana inayotaka mimi niamini kwamba CUF ni chama cha Waislaam na Chadema ni chama cha Wakristu japokuwa kuna ukweli kwamba waumini wengi wa dini hizo wamejiunga na vyama hivyo lakini the main reason ni strong hold za vyama hivi zimekuwa sehemu ambazo wananchi wake wengi ni wa dhehebu mojawapo. Haiwezekani kabisa strong hold ya CUF iwe Zanzibar halafu wanachama wake wawe dominant wakristu au Chadema kuwa Moshi na Arusha tukitegemea Waislaam ndio watakuwa wengi ndani ya chama hicho. Mbona hatujiulizi kwa nini CUF kimejaa Wangazija, Wanyamwezi, Waoman na shihiri ambao ni makabila ya Zanzibar ya leo kama wanavyosema Chadema ni ya wachagga? Lini mchagga akawa Muislaam kama sii kutiliwa ubani na shahada?.

Kwa hiyo Biafra walipigania haki yao, na haya maswala ya kuchimba Gas Mtwara na kuisafirisha Dar inaujenga mji wa Dar na Arusha wakati Mtwara mnaiacha haina kitu itakuja watokea puani mkisema waislaam hivi na vile. Shinyanga mnaiacha na mashimo na toxic ktk mito yao - Yarabi Maghfir mtasema Wakristu wamechachamaa Shinganya. Ipo siku watu tutamalizana vibaya. Kuna Uzuri wa serikali ya Majimbo na kuna ubaya wake lakini binafsi yangu naanza kuamini ni bora madhara yanayoweza kutokana na majimbo kuliko madhara tunayoyajenga ktk mfumo huu wa Chukua Chako Mapema. Je, unajua ya kwamba ile Biafra ilisambaratishwa iligawanywa into 12 states ktk mpango wa divide and rule, hivi sasa chuki imeingia hadi kwa Waibo wenyewe kwa wenyewe kugombania sinia la biriani kwa umaskini walokuwa nao?. That's what I expect kwa Zanzibar baada ya kuvunja Muungano.
 
- Angeanza na kuongela hilo lijumba la Balali kwanza ndio aseme mengine ya binafsi za watu, kutesa ni kwa zamu zamu yao iliiisha sasa ni ya wengine ndio maisha!!!

William.
Na wewe mkuu uko kwenye zamu ya wanaotesa sasa hivi?
 
- Angeanza na kuongela hilo lijumba la Balali kwanza ndio aseme mengine ya binafsi za watu, kutesa ni kwa zamu zamu yao iliiisha sasa ni ya wengine ndio maisha!!!

William.
Na wewe utaendelea kuishi tu outside looking in. Muongo mkubwa wewe!
 
Back
Top Bottom