Generali Ojukwu Ni Kwanini?

Anachungulia tu huyu dirishani. Hawamfungulii mlango.

Ndio hapo sasa....yale yale ya kila siku ndani ya nchi yetu hii. Alliance zetu nyingi zimekaa kula kula tu maana kwa maneno kama kutesa kwa zamu, sijapata kuelewa bado maudhui yake yanalenga nini zaidi ya kutengeneza strategy za kujiweka kwenye group lenye nguvu kwa wakati huo. Naam, ndio maana namuheshimu sana Nyerere. Pamoja na mapungufu yake yote, hakuwa "opportunist" na wala "unethical". Na haya mambo mawili yanaendelea kuwadondosha wengi walio kwenye medani za kisiasa ndani ya nchi yetu. Hawajulikani wana simamia nini zaidi ya chakula chao cha kila siku. kama siku ya leo watu wanakula hivi basi na wao wamo...kesho wakiwa wanakula vile, no matter what the consequenses are, na wao wamo tu. Baadae wanaanzisha mikakati ya kutuonyesha eti walikuwa tofauti! Kivipi, na wakati wote huo wamekuwa ni sehemu ya mambo karibu yote yaliyokuwa yanaendelea.
Binafsi nashukuru sana utandawazi maana ingekuwa rahisi sana kwa watu ambao hawana kabisa mshiko na sifa za kuongoza umma, kutudanganya kama na wao ni viongozi wenye nia ya kututumikia sisi wananchi.Taratibu tumeanza kuona dalili za wazi....wengi sio viongozi ingawa wanapenda tuwatambue hivyo.....
 
Wewe ulikuwepo enzi hizo? Huwezi kusema kuwa sio Watanzania waliokuwa wanamuunga mkono Ojukwu. Nilikuwepo na nilikuwa mwanafunzi enzi hizo na tuliandamana kuunga mkono uamuzi wa Biafra kujitenga. Katika suala la vita vya Nigeria mimi naweza kujiita authority hapa JF. Leta hoja nyingine.

Mkuu uungaji mkono unaouzungumzia ni ule wa kulazimishwa na dola. Ritz yuko sahihi kabisa kuhusu vita vya Biafra. Wewe kuwepo enzi hizo si issue kwani facts nyingi zipo kwenye vitabu na watu wanasoma. Nyerere alishauriwa na akina Kambona asiiunge mkono Biafra dhidi ya kujitenga na serikali ya shirikisho lkn aliakataa. Matokeo yake mwisho wa siku akaaibika kwa Biafra kuchakazwa vibaya.
 
Hapana. Sisi hatukulazimishwa na dola. Mimi sikuwa yusi ligi au kada wa TANU. Tulipanga wenyewe kuandamana shuleni kwetu tukalizungumzia hilo jambo na waalimu wetu ingawa wanafunzi wa Kihindi walipinga wakikumbuka madhara yaliyotokea katika kutengana kwa India na Pakistani mwaka 1947. Hatukulazimishwa na dola hata kidogo na Ritz anazungumzia hisia tu kwa sababu hakuwepo wakati huo. Na si kweli kwamba Nyerere alishauriwa na Kambona asiunge mkono Biafra kwa sababu tuliitambua Biafra April 1968 wakati Kambona alikimbilia Uingereza Juni 1967. Sasa angemshauri vipi? Kwa simu?
 
Inakuaje mnaondoa posti mkishindwa hoja??? Mods rudisha posti "Hivi Obote ilikuwa ni lazima? Mnaleta hoja mkizidiwa na hoja mnakimbilia kuziondoa hatupo kwenye ligi hapa tunelemishana na kupanuana mawazo

Chama
Gongo la Mboto DSM
 
Mkuu Jasusi
Sasa wewe ulikuwepo halafu unaongea hisia tu...30 Mei 1967 Kanali Ojukwu alitangaza taifa la Biafra na Tanzania wakautambua utawala wa Biafra.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu uungaji mkono unaouzungumzia ni ule wa kulazimishwa na dola. Ritz yuko sahihi kabisa kuhusu vita vya Biafra. Wewe kuwepo enzi hizo si issue kwani facts nyingi zipo kwenye vitabu na watu wanasoma. Nyerere alishauriwa na akina Kambona asiiunge mkono Biafra dhidi ya kujitenga na serikali ya shirikisho lkn aliakataa. Matokeo yake mwisho wa siku akaaibika kwa Biafra kuchakazwa vibaya.

Mzee Kijana.
Vita vya Biafra vilianza 6 Julai 1967...Biafra walichezea kichapo ilivyofika 13 Janauri 1970 mabaki ya Jeshi la Biafra yalijisalimisha mjini Amich.

General Ojukwu alikimbia kwenda kujificha Code d Ivoire, wakati ule, kakaa uhamishoni muda wa miaka 10 mwaka 1980 karudi Nigeria baada ya kuomba msamaha.
 
Last edited by a moderator:
Mimi naliwahi mshauri kaka yangu William awe anafikiria sana kabla hajasema na kuweka mawazo yake katika maandishi.
Nalimshauri pia awe anasoma sana. Nikajitolea kupendekeza vitabu vya kusoma kama atakuwa na utayari huo....
Ninachokiona hapa,kaka yetu ana ubishi wa ligi..ana majibu yake tayari so ukimshawishi kwa hoja,anarudia swali lake lile lile alilokariri mithili ya CD iliyokwama.

Amenikumbusha mtoto wa Idi Amini. Alirudishwa kutoka Urusi. Alikopelekwa na baba yake kusoma. Walisema neno moja tu kuwa mwanao is UNTEACHABLE
 
Mkuu Jasusi
Sasa wewe ulikuwepo halafu unaongea hisia tu...30 Mei 1967 Kanali Ojukwu alitangaza taifa la Biafra na Tanzania wakautambua utawala wa Biafra.
Ritz,
Soma tena lile tamshi la Ikulu alilotubandikia humu jokaKuu. Tanzania iliitambua Biafra April 13, 1968, karibia miaka miwili baada ya civil war kuanza.
 
Inakuaje mnaondoa posti mkishindwa hoja??? Mods rudisha posti "Hivi Obote ilikuwa ni lazima? Mnaleta hoja mkizidiwa na hoja mnakimbilia kuziondoa hatupo kwenye ligi hapa tunelemishana na kupanuana mawazo

Chama
Gongo la Mboto DSM
Chama,
Nadhani hii imehamishiwa kwenye forumu ya Great Thinkers.
 
Back
Top Bottom