William Mkuu, hoja yako (pengine) ni nzuri lakini imekuja wakati ambapo tuna mengi muhimu "ya sasa" ya kujadili. Kwa hivyo sitaki kujiingiza katika kuhakiki kama TZ ilipatia au ilikosea kuunga mkono unaowaita "waasi ndani ya serikali halali", hasa kwa suala lililotokea mwaka 1967, (what a coincidence) mwaka ambao tulianzisha sera za Azimio la Arusha, baadaye likaja Azimio la Zanzibar, bila ya kusahau donda ndugu la Muungano wa 1964, marekebisho ya katiba ya 1977. kuingiza mfumo wa vyama vingi 1992... ubinafsishaji, sera ya madini, ukubwa wa serikali, madaraka mikoani, sera ya elimu.... na madudu mengine mengi yanayoendelea hadi leo, yanayohitaji kujadiliwa na kurekebishwa SASA.
Kwa maslahi ya ustawi wa Taznania kisiasa, kiuchumi na kijamii, ninaunga mkono hoja yako kuwa TZ ilifanya madudu, lakini kwa nini tujadili madudu ya 67 ya Nigeria wakati tuna "lori la shehena ya madudu" nchini? Tujadili haya, tuwafumbue macho viongozi wetu wakubali kutibu pale palipooza. Maisha ya sasa yanakwenda mbio sana, ukipoteza hatua moja tu wenzako wanakuacha nyuma miaka mia moja. Tanzania tumeachwa nyuma ya 1961 tulipopata "uhuru" - Tujadili haya.