ritz nashukuru sana leo kwa kuamuwa kunipa darasa, nami kwa sababu nia yangu ni kujifunza natumaini nitajifunza mengi kutoka kwako.
Umesema Isarel siyo Taifa la kikristo na Wakristo ni wachache mno sasa hapa najawa na maswali zaidi je ni kwa nini Chuki za wachukia Israel huwa zinafungamanishwa na Wakristo?
Ningependa kujuwa kumbe Palestina ina Wakristo na wanamgambo kama Hizbollah yana Wakristu wengi tu je ni kwa nini Waislamu wao ndio mashabiki wa makundi haya ya Wanamgambo?
Kwa ufahamu wangu mdogo Syria ina Waislamu wengi sana na wanauwawa kwa dozens na Majeshi ya Rais ambaye ni mwislamu, ila natatizo mpaka leo sijaona makundi kama Bakwata, shura ya Maimamu, Uamsho kufanya maandamano makubwa kupinga mauwaji ya waislamu hawa ma Syria?
Ni nini kimejificha nyuma ya Uislamu? Je unaweza kunitajia hasa
Crusaders ni kina nani hasa?