Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 2,808
- 11,973
Geita yaridhia kuanzishwa Mkoa wa Chato. RCC yatoa mapendekezo. Baadhi ya maeneo kutoka mikoa jirani. RC Geita Mhe Rosemary Sitaki awashukuru Wananchi kukubaliana kwa hekima bila ushabiki.
Kikao cha Kamati ya Ushauri ya mkoa - REGIONAL CONSULTATIVE COMMITTEE (RCC), Kilichokaa kama kikao Maalum leo kwaajili ya Mapendekezo ya kuunda Mkoa Mpya wa Chato, Kimependekeza yafuatayo:
1. Mkoa Mama wa Geita ubakiwe na Wilaya tatu ambazo ni Wilaya ya Geita, Mbogwe na Wilaya ya Nyang'hwale.
2. Imependeleza iombwe Wilaya ya Sengerema ambayo ipo Mkoa wa Mwanza, ili iweze kukamilisha Wilaya nne za Geita pamoja na Wilaya Pendekezwa ya Busanda.
3. Mkoa wa Chato imependekezwa kwa iundwe na Wilaya za Geita ambazo ni Chato yenyewe, na Wilaya ya Bukombe.
4. Pia imependekezwa kutoka Kigoma, iombwe eneo kutoka Wilaya ya Kakonko, pia kutoka Kagera imependekezwa ziombwe Wilaya mbili ambazo ni Biharamulo na Wilaya ya Ngara.
Mapendekezo haya yamekamilika na yamekubaliwa na wajumbe wote wa RCC.
Sasa yatapelekwa kwenye Wizara husika ili yaweze kufanyiwa kazi.
Zaidi, soma; Geita: Baraza la Madiwani laukataa Mkoa mpya wa Chato