Geita yakubali kuundwa Mkoa wa Chato; Kakonko, Biharamulo na Ngara kumegwa. Sengerema kwenda Geita..

Utakuwa ni mkoa unaofikika kiurahisi toka pande zote za Tanzania maana unafikika kwa barabara, maji na ndege.

Makao makuu ya mkoa yatakuwa Chato na hapa kuna kila aina ya fursa, utalii,kilimo na uvuvi.

Hivyo ni kipindi cha watanzania waende kuwekeza Chato kwenye kila sekta kama kilimo, uvuvi na viwanda.

My take: Chato kuwa mkoa ni sehemu ya kuenzi kazi kubwa aliyoifanya JPM kwa taifa letu
Hivi mnasubiri nini kuhamia Chato nyie viwavi wake?
Hakuna mfanya biashara ataenda huko,aliwatesa sana na kuwapora Mali zao,
Jikusanyeni muhamie huko nyie wenye mapenzi na marehemu
 
Wazo zuri kweli
Ungeanza wewe kwenda kuwekeza huko
Onesha mfano

Ova
 
Geita yaridhia kuanzishwa Mkoa wa Chato. RCC yatoa mapendekezo. Baadhi ya maeneo kutoka mikoa jirani. RC Geita Mhe Rosemary Sitaki awashukuru Wananchi kukubaliana kwa hekima bila ushabiki.

Kikao cha Kamati ya Ushauri ya mkoa - REGIONAL CONSULTATIVE COMMITTEE (RCC), Kilichokaa kama kikao Maalum leo kwaajili ya Mapendekezo ya kuunda Mkoa Mpya wa Chato, Kimependekeza yafuatayo:

1. Mkoa Mama wa Geita ubakiwe na Wilaya tatu ambazo ni Wilaya ya Geita, Mbogwe na Wilaya ya Nyang'hwale.

2. Imependeleza iombwe Wilaya ya Sengerema ambayo ipo Mkoa wa Mwanza, ili iweze kukamilisha Wilaya nne za Geita pamoja na Wilaya Pendekezwa ya Busanda.

3. Mkoa wa Chato imependekezwa kwa iundwe na Wilaya za Geita ambazo ni Chato yenyewe, na Wilaya ya Bukombe.

4. Pia imependekezwa kutoka Kigoma, iombwe eneo kutoka Wilaya ya Kakonko, pia kutoka Kagera imependekezwa ziombwe Wilaya mbili ambazo ni Biharamulo na Wilaya ya Ngara.

Mapendekezo haya yamekamilika na yamekubaliwa na wajumbe wote wa RCC.

Sasa yatapelekwa kwenye Wizara husika ili yaweze kufanyiwa kazi.

Zaidi, soma; News Alert: - Geita: Baraza la Madiwani laukataa Mkoa mpya wa Chato
Hamna lolote hapo wanatafuta jimbo la kumpa mtu 2025.
 
Utakuwa ni mkoa unaofikika kiurahisi toka pande zote za Tanzania maana unafikika kwa barabara, maji na ndege.

Makao makuu ya mkoa yatakuwa Chato na hapa kuna kila aina ya fursa, utalii,kilimo na uvuvi.

Hivyo ni kipindi cha watanzania waende kuwekeza Chato kwenye kila sekta kama kilimo, uvuvi na viwanda.

My take: Chato kuwa mkoa ni sehemu ya kuenzi kazi kubwa aliyoifanya JPM kwa taifa letu
hakuna haja. watu wanawekeza penye hela. penye fursa.
mtu hawez toka dar kawekeza.. atokea arusha kawekeza..atoke mbeya mwanza kawekeza. tena biashara kubwa ..kampuni.
eti aende chato? kufanya nn?

Inafuatwa pesa sio mtu ambae alishapita zake
 
hakuna haja. watu wanawekeza penye hela. penye fursa.
mtu hawez toka dar kawekeza.. atokea arusha kawekeza..atoke mbeya mwanza kawekeza. tena biashara kubwa ..kampuni.
eti aende chato? kufanya nn?

Inafuatwa pesa sio mtu ambae alishapita zake
Umeishia darasa la ngapi?
 
Jambo la kufurahisha ni kwamba Sengerema imerudi kwao. Maana ilikuwa ndani ya wilaya ya Geita kabla ya mwaka 1975
 
Kumekuwa na mjadala mkali kuhusu uhalali wa wilaya ya chato kupewa hadhi ya makao makuu ya mkoa mpya , na pia kumegwa wilaya za mikoa mingine ya karbu ili kuunda mkoa huo mpya , jonzi hii ilikuwa ni ya aliyekuwa Raisi wa jamhur wa muungano wa Tanzania hayati J.P.J.Maghufuli.

Kimsingi inakuwa ni ngumu kuizima jonzi hyo hata kama mkoa huo mpya wa chato hasa wilaya ya chato kutokuwa na hadhi hyo ,

Hayati alikuwa ameanza kuwekeza miradi mizito wilayani chato , kiukweli miradi hyo ili iweze kufanya kazi Kwa ufanisi ni lazima chato iwe makao makuu ya mkoa mpya zaidi ya hapo miradi hyo itakuwa dead project ...
Ujenzi wa uwanja wa ndege , hospital kubwa ya kisasa, kufunguliwa Kwa matawi ya huduma za kibank , ujenzi wa barabara ,na hifadhi ya burigi na Bandari pia naskia ipo kule ..N.K .miradi hii yote ingekufa kibudu na ingekuwa bonge la hasara Kama wilaya ya chato haitakuwa mkoa ....

Kupewa hadhi ya mkoa kutavutia shughuli za kiserikali na hii itafanya miardi hyo iwe na tija. ....

Kimsingi jamaa kafariki akiwa ameisogeza chato kwenye point of no return thus why hata viongozi waliopo wameshindwa kupiga U-Turn.
 
Midhali ni kaugonjwa iko siku atakuja mwendawazimu mwingine itagawika... usishangae hii meguamegua iko mikoa au wilaya zitamegwa ili kuongezea maeneo sehemu zingine!!! Siasa zikitawala weledi 'upumbavu hutamalaki!' Ati mzee fulani alitoa ombi... haya shime na butiama iwe mkoa tumuenzi Mwalimu ila tusisahau Liwale, Masasi na... na... na....
Buriani Geita. Ni ushamba kuna ulazima gani? Mbona Morogoro haigawiki?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom