figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,492
- 54,895
Salaam Wakuu,
Inadaiwa kuna mambo hayaendi Vizuri huko Chato Mkoani Geita. Tunaomba Jeshi la Polisi lihakikishe amani kwa Wakazi wa Chato wa vyama vyote.
Hapa chini ni Taarifa kutoka Viongozi wa CHADEMA nliyotumiwa Usiku wa leo.
"Tumevamiwa na kuchomwa Moto kwa Mgombea Ubunge Maalum Massai Chato. Nyumba yachomwa Moto , Bajaji zachomwa Moto Katika Wilaya ya Chato.
Walio tuvamia Wana sema eti tumemleta Tundu Lissu Chato. CCM wameandaa magaiti Wana piga watu Usiku huu.
Usiku huu wa Saa 12:25 Ndo tumevamiwa ni hatari, watoto wetu wamenusulika kwa mgombea Ubunge Wilaya ya Chato leo hii Ucku Huu
Mimi Kamanda Husna Amri Said"
Ninalaani watu wote wanaopanga kuharibu amani ya Nchi kisa Siasa.
Mia
=========================
Jeshi la Polisi mkoani Geita, linawasaka watu zaidi ya 10 waliofanya uharibifu wa mali kwenye nyumba 3 tofauti za wagombea Udiwani na Ubunge jimbo la Chato kupitia CHADEMA.
Tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia Oktoba 13, 2020, ambapo walikuwa wanatarajia kumpokea mgombea Urais wa chama hicho, Tundu Lissu.
Kamanda wa polisi mkoa wa Geita, Henry Mwaibambe, amesema mali zilizoharibiwa kuwa ni pamoja na bajaji mbili kuchomwa moto, kuvunjwa kwa vioo vya madirisha baada ya kupondwa mawe, pamoja na kubomoa madirisha mawili ya nyumba.
Katika hatua nyingine Kamanda huyo amewasisitiza wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi, kuzingatia muda wa kufanya kampeni ili kuepusha vurugu zinazotokea baada ya muda uliowekwa na Tume kuisha.