Uchaguzi 2020 Geita: Nyumba ya Mgombea Ubunge Chato wa CHADEMA Massai, yadaiwa kuchomwa moto na kubomolewa

Jamani acheni uchochezi hii nyumba ndio unasema imebomolewa? si imeanguka yenyewe, usiku wa leo mvua kubwa imenyesha maeneo ya geita nzera na katoro, huu unafiki hata mungu unamkera, mhandisi wa mji hebu chunguza hii nyumba kama ilijengwa chini ya kiwango mmiliki afikishwe mahakamani haraka, na hako katoto kaliko chuchumaa mbona kana macho ka ya bundi? katakuwa kachawi.
 
Ila nacho amini ni kwamba ipo siku haya yote yataisha na kubaki history! Naamini Mwenyezi Mungu yupo na atatenda haki dhidi ya dhuluma hizi za chama tawala na viongozi wake.
Inauma sana lakini furaha itakuja sio muda!
Tukisubiri Mungu atende miujiza haitatokea tutaendelea kuonewa.

Watawala wanaotumia mabavu hawakuondolewa na Mungu bali waliondolewa na nguvu ya umma.

Nigeria wangesubiri Mungu aondoe SARS wangeendelea kuuliwa lakini they took it to the road na kila kitu kikabadilika within hours.

Tunakila sababu ya kuondoa utawala huu kwa heri ama kwa shari

Sent from my SM-A105F using JamiiForums mobile app
 
Ni kwa nini kila tukio mchukulie ni serikali? Wanaofanyiwa ni malaika hawanaga maadui?vyama hivyo hivyo walipo hawana uadui? Serikali ihangaike na mtu mdogo wa kazi gani? Watu wengi mmejaa UPUMBAVU mwingi sana juu ya haya mambo ya siasa
Acha ubaguzi we kila mtu ana haki ya kulindwa mdogo au mkubwa.

Sent from my SM-A105F using JamiiForums mobile app
 
Huu siyo muda wa kulialia, anayekupiga ngumi ya sikio na wewe mpige ngumi ya macho, akikuuliza unajisikiaje na wewe muulize unaonaje.

Sioendi siasa za kindezindezi za kulalamika kila siku.

Nilimkubali Maalim Seif kwa sera ya jino kwa jino mpaka CCM ikasalimu amri na kuleta muhafaka wa kutawala pamoja.

Na mwaka huu Maalim ameshawaambia mapema sasa basi imetosha
 
Ni kwa nini kila tukio mchukulie ni serikali? Wanaofanyiwa ni malaika hawanaga maadui?vyama hivyo hivyo walipo hawana uadui? Serikali ihangaike na mtu mdogo wa kazi gani? Watu wengi mmejaa UPUMBAVU mwingi sana juu ya haya mambo ya siasa
Mbona unaumia sana! Hiyo serikali ni baba yako kiasi cha kuumia kupitiliza inaposemwa? Ina haki gani sasa ya kuwatawala wananchi iwapo inafanya vitendo vya kibaguzi na kushindwa kuwalinda baadhi ya raia na mali zao?

Unafiki tu umekujaa.
 
Kachomwa.nani..Husna...Masaai au vipi..tulia utueleweshe vuzuri au na wewe unaungua.mkuu.Poleni.sana
 
Polisi wa Tanzania utasikia wakisema kachoma mwenyewe au Chadema walichoma hiyo nyumba ili kutafuta kiki ngoja tusubiri tuone.
 
Katika hali ya kusikitisha, kadri tunavyozidi kukaribia uchaguzi mkuu, kumekuwepo na vitendo vya kihuni vya kutumia nguvu kupiga, kuumiza na kunyanyasa wananchi.

Katika mazingira yanayoonyesha kuwa matendo hayo si bahati mbaya, kumekuwepo na mfululizo wa kuvamia na kuharibu mali za wagombea wa Chadema katuka kile kinachoonekana ni vitendo vilivyoratibiwa.

Inavyoonekana, Wanufaika wa vitendo hivyo wameshaona kuwa hawakubaliki, wananchi wamewakataa, kwa hiyo waneamua kuleta fujo na vurugu ili kuwatisha wananchi wahofu kutumia haki yao ya kidemokrasia kujitokeza kwa wingi kupiga kura ya kuwakataa.

Pia vinalenga kuwaogopesha wagmbea wa upinzani, kuwatoa kwenye reli ili wasiconcentrate na kampeni bali wabaki na hofu ya maisha yao.

Siku za karibuni tumeona polisi wakijiingiza katika matendo ya kuonea na kusumbua wapinzani bila kosa lolote, hayo tumeyaoba huko Arusha, Tarime kwa Heche walipovamia ofisi na kuharibu vitu vya ofisi, Shinyanga walipojaribu kumbambikizia mbunge kosa la kuchana bango la Magufuli.

Huko Chato leo watu wasiojulikana wamevamia nyumba ya mgombea mbunge na kuichoma moto. Humo ndani kulikuwa na watoto, almanusra waungue wakiwa ndani.

Ninachotaka kuwaambia wahuni hawa ni kuwa, Hakuna fujo itakayorudisha nyuma maamuzi ya wananchi. Wananchi wameshawakataa, hawana tena kibali wala ridhaa ya kutawala, wanachoweza sasa ni kuchakachua tu lakini si kwa ridhaa ya wananchi.

Hii nchi imewahi kufanya chaguzi za vyama vingi lakini hatukuwahi kushuhudia kiwango cha utesi na ukatili tunaoushuhudia kwenye awamu hii ya tano. Ipo hsja kwa wananchi kuzuia ukatili wa kiwango hiki kabla hajujakomaa na hatimaye kutuletea shida huko mbeleni.

Hapa chini ni video ya nyumba ya mgombea ubunge wa Chadema huko Chato imepigwa kibiriti
 

Attachments

  • Chato_Mbunge_Chadema.mp4
    14.7 MB
Back
Top Bottom