Uchaguzi 2020 Geita: Nyumba ya Mgombea Ubunge Chato wa CHADEMA Massai, yadaiwa kuchomwa moto na kubomolewa

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,483
54,839
Salaam Wakuu,

Inadaiwa kuna mambo hayaendi Vizuri huko Chato Mkoani Geita. Tunaomba Jeshi la Polisi lihakikishe amani kwa Wakazi wa Chato wa vyama vyote.

Hapa chini ni Taarifa kutoka Viongozi wa CHADEMA nliyotumiwa Usiku wa leo.

"Tumevamiwa na kuchomwa Moto kwa Mgombea Ubunge Maalum Massai Chato. Nyumba yachomwa Moto , Bajaji zachomwa Moto Katika Wilaya ya Chato.

Walio tuvamia Wana sema eti tumemleta Tundu Lissu Chato. CCM wameandaa magaiti Wana piga watu Usiku huu.

Usiku huu wa Saa 12:25 Ndo tumevamiwa ni hatari, watoto wetu wamenusulika kwa mgombea Ubunge Wilaya ya Chato leo hii Ucku Huu

Mimi Kamanda Husna Amri Said"

Ninalaani watu wote wanaopanga kuharibu amani ya Nchi kisa Siasa.

Mia

=========================

Jeshi la Polisi mkoani Geita, linawasaka watu zaidi ya 10 waliofanya uharibifu wa mali kwenye nyumba 3 tofauti za wagombea Udiwani na Ubunge jimbo la Chato kupitia CHADEMA.

Tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia Oktoba 13, 2020, ambapo walikuwa wanatarajia kumpokea mgombea Urais wa chama hicho, Tundu Lissu.

Kamanda wa polisi mkoa wa Geita, Henry Mwaibambe, amesema mali zilizoharibiwa kuwa ni pamoja na bajaji mbili kuchomwa moto, kuvunjwa kwa vioo vya madirisha baada ya kupondwa mawe, pamoja na kubomoa madirisha mawili ya nyumba.

Katika hatua nyingine Kamanda huyo amewasisitiza wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi, kuzingatia muda wa kufanya kampeni ili kuepusha vurugu zinazotokea baada ya muda uliowekwa na Tume kuisha.
IMG-20201013-WA0000.jpg
IMG-20201013-WA0001.jpg
 
Ni kwa nini kila tukio mchukulie ni serikali? Wanaofanyiwa ni malaika hawanaga maadui?vyama hivyo hivyo walipo hawana uadui? Serikali ihangaike na mtu mdogo wa kazi gani? Watu wengi mmejaa UPUMBAVU mwingi sana juu ya haya mambo ya siasa
Tunasema serikali ni ya kishamba kwasababu matukio haya yameshamiri awamu hii na hakuna hatua zinazochukuliwa kama walioathirika ni wapinzani!Shwain
 
Ni kwa nini kila tukio mchukulie ni serikali? Wanaofanyiwa ni malaika hawanaga maadui?vyama hivyo hivyo walipo hawana uadui? Serikali ihangaike na mtu mdogo wa kazi gani? Watu wengi mmejaa UPUMBAVU mwingi sana juu ya haya mambo ya siasa
wanajiponda wenyewe ili wasingizie serikali, kule Hai walienda na marungu na mipini walikodi wahuni kutoka rombo
 
Hili haliwezi kwenda sawa, maana kwa kweli hapo ni pagumu, ila najua akili ya Tundu Lissu na hisia zake, keshafika mahali ajali tena kabisa, yupo tayari kwa lolote!
Chato ni Tanzania na ni ngome ya CHADEMA na wanachato wanahaki ya kusikiliza sera za mgombea wao wa urais.

Aende wakamsikilize mbona wanaikungi hawakumfanyia vurugu Magufuli kwenye mikutano yake.

Tumeongoza serikali za mitaa asilimia 94 chato toka 2014 mpaka 2019.

Hivyo chato lazima mgombea wetu wa urais afike kukutana na wanachama wetu na watanzania wa chato ambao pamoja na kuzungukwa na ziwa hawana maji badala yake wakapelekewa taa za barabarani na uwanja wa ndege, hawana malisho na wakapelekewa reserve na simba yale mifugo yao.

Sent from my SM-A105F using JamiiForums mobile app
 
11 Reactions
Reply
Back
Top Bottom