Chato: Kituo cha Polisi Muganza chachomwa moto na wananchi kupinga mauaji ya mtuhumiwa anayedaiwa kusababibishiwa kifo na Polisi

exalioth

JF-Expert Member
Jun 22, 2016
2,190
3,685
Bodaboda Amepigwa Na Polisi Na Kumsababishia Kifo Ndipo Wananchi Wameandamana Na Kuvunja Kituo Cha Polisi inadaiwa Watu Wawili Wamesha Poteza Maisha Kutokana Na Ufyatuaji Wa Risasi Na Mabomu Ya Machozi.

Chanzo cha tukio hili ni mwendesha boda boda aliuziwa betri ya gari kumbe ilikua ya wizi badae akakamatwa na polisi, ndipo polisi walimpiga hali yake ikawa mbaya akapelekwa hosptal chato.

Hali ilibadilika ghafla mwendesha bodaboda akafariki, mama mwenye mtoto akaichukua mwili kwaajiri ya kwenda kuzika nyumbani kwao kijiji cha kasenda ndipo ushirikiano wa bodaboda wakagoma kuzika na kuamua kuandamana na jeneza wakajue polisi kwanini wamesababisha kifo.

Na kuna duka limesambalatishwa na mali kuchukuliwa na wananchi sababu ni.

Mfanyabiashara mwenye duka ndiye boss wa mwendesha bodaboda. Wananchi walihoji nikwanini uliemuajiri anakamatwa na polisi hata kwenda kituoni kumuona hakuna

Hicho ndicho chazo cha duka kuvujwa kwamba na yeye ni wale wale

Mambo hayajaisha hapa Kata ya Mganza Wilayani Chato maaana mabomu yameanza upya f.f.u wamefika

Nitazidi kuwapa kinachoendelea naripoti kutoka kwenye tukio Hapa mganza.

===========




---
Jeshi la Polisi wilayani Chato mkoani Geita limelazimika kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya waombolezaji na wananchi wa Kata ya Mganza, kufuatia vurugu zilizotokea wakati wa maziko ya kijana Enos Misalaba (32) anayedaiwa kukamatwa na polisi kisha kupigwa na kusababisha kifo chake.

Mkuu wa Wilaya ya Chato, Deusdedith Katwale amethibitisha kutokea tukio hilo na kusema yupo njiani kuelekea eneo la tukio na taarifa zaidi atazitoa baada ya kufika Mganza.

Kaka wa marehemu, Samweli Misalaba akizungumza na Mwananchi kwa njia ya simu, amesema wakiwa kwenye eneo la maziko kwa taratibu za mazishi, wananchi walikataa kuendelea na maziko baada ya msomaji risala ya marehemu kusema amekufa kwa ugonjwa wa kifua na siYo kupigwa kama jamii inavyoamini.

“Tulikubali kuzika, tumeshachimba kaburi wakati wa historia ya marehemu msomaji alisoma kuwa amekufa kwa kuugua kifua ndio wananchi wakakataa na kubeba jeneza na kuurudisha mwili kituoni wakitaka waelezwe kifo cha marehemu kimetokana na nini.

Wakarudisha mwili kituoni polisi, wakaanza kupiga mabomu ya machozi na wananchi wakaendelea kuandamana,” amesema ndugu wa marehemu.

Enos Misalaba anadaiwa kukamatwa siku ya Jumatatu Machi 27 akituhumiwa kuiba betri ya gari na alikamatwa na polisi wa Kituo cha Mganza.

Inadaiwa alipigwa na kuzidiwa kisha kupelekwa kwenye Kituo cha Afya Mganza na Jumanne asubuhi alipoteza maisha akipatiwa matibabu.
 
Screenshot_20230325-120232_Gallery.jpg
 
Bodaboda Amepigwa Na Polisi Na Kumsababishia Kifo Ndipo Wananchi Wameandamana Na Kuvunja Kituo Cha Polisi Watu Wawili Wamesha Poteza Maisha Kutokana Na Ufyatuaji Wa Risasi Na Mabomu Ya Machozi

Npo Kwenye Tukio Nitaendelea Kuwapa Taarifa

Tulia andika vizuri mkuu.. Sindikiza na picha.. Hii habari yako, inasubiriwa na online tv, na wengineo.. Tafadhari toa taarifa sahihi
 
Back
Top Bottom