Uchaguzi 2020 Geita: Nyumba ya Mgombea Ubunge Chato wa CHADEMA Massai, yadaiwa kuchomwa moto na kubomolewa

Kumbe nyumba ilikuwa bado inajengwa kwa kutumia matofali ya kuchoma na uchomaji huo ulikuwa unafanyika hapohapo saiti.
 
Dhuluma, hujuma na kila tone linaongeza nguvu na ari kusaka uhuru na haki toka mkoloni mweusi.Poleni sana wahanga. Nashauri CDM wawe na utaratibu kuratibu wahanga na kutangaza Watanzania wema tuwasitiri.
Watakao kamatwa ni wanachama wa Chadema badala ya kufanya uchunguzi makini
 
Kuna mahali Matola amezungumza maneno yenye uzito. Wapinzani hebu msomeni vizuri
Heshima ni two way traffic na wala Wapinzani wasidhani CCM na serikali na vyombo vyao hawajui haya

Msajili wa vyama anaona hatari ya kuunga mgombea wa chama kingine, haoni ya kuchomeana nyumba.
Laiti ingelikuwa Upinzani leo angeshinda katika vikao, barua na TV akifoka na kulaani.
Hili amekaa kimya, maana wanaotenda ni CCM ambao mwenyekiti wao ndiye mteuzi wake

Tume ya uchaguzi nayo kama Msajili ni kama vile hawaoni, nao pia M/kiti wa CCM ndiye amteuzi wao

Chadema wana matatizo. Haya mambo bila kuyaweka hadharani nchi na dunia ikayaona ipo siku mtakapojibu CCM na vyombo vyao wakapiga zumari mkaonekana ninyi ndio wabaya hata kama mnajitetea

Mbowe na Mnyika akina Husna ndio wenye jukumu? Ingalikuwa ACT Wazalendo reaction ingekuwa tofauti

Msajili wa vyama na NEC, Kenya ilianza hivi hivi !! Jiulizeni, uvumilivu ukiisha kwa wananchi mnaweza kuzuia gharika? Matasema nini? Kenya walikuwa na Jeshi na Polisi lakini nchi ilisambaratika. Hamjiulizi ilikuwaje?

Ninyi, NEC na Msajili,ninyi ndio wenye sheria hamuwezi kukwepa maswali,hoja wala kujitetea ikitokea dhoruba.Mtajificha nyuma ya CCM, ukweli ukitimia CCM watawakana mtasimama wenyewe!

Kivuitu wa Kenya alikuwa mtiifu, ilipotimia alisimama mwenyewe na kufariki katika dhalili kubwa sana
kwa msongo. Waliomtumia hawakumjua, hata familia yake haitaki kujihusisha na jina la Kivuitu.

Viongozi wa DINI, nanyi endeleeni kukaa kimya wala hakuna haja ya sala za kuliombea Taifa.
Endelezeni unafiki wenu bila kuwahusisha wananchi, waacheni wananchi na nchi yao

JokaKuu Pascal Mayalla (kada FYI) Mag3 tindo
 
Back
Top Bottom