Gazeti Mwananchi: CHADEMA sasa Vipande viwili!

Gazeti Mwananchi: CHADEMA sasa Vipande viwili!

Nafikiri kwa mtazamo wa muandishi vipande viwili anavyo visema yeye ni kuonekana kuna wagombea 2. Yaani pande moja ni upande wa Zitto na pande lingine ni upande wa Slaa, jumla mapande mawili.

Sasa pa kujiuliza katika hayo mapande mawili yamegawa vipi chama na wanachadema hadi kuonekana chadema iko vipande?! Muandishi alitakiwa aonyesha bila chembe ya shaka kwenye hili.

Kwa kuwa ameonyesha obwe na matobo kwenye habari yake, kwangu naona mwandishi ameandika akiwa anafikiria sana mapande kuliko walaji watakavyo yapokea mapnde hayo na kuya-digest.
hapo mi naona hao viongoz wanajaribu kufu nika mambo tu CDM hakuna demokrasia
 
UPUUZI wa Wananchi tuliowengi.

Nchi jirani ya KENYA mtu akitangaza nia ya kugombea URAIS wala hakuna longo longo, husubiriwa kwenye kura za MAONI.

Nchi za Ulaya ndiyo usiseme yaani mtu anajitangazia nia ya kupeperusha bendera ya Chama chake hata kama uchaguzi utafanyika miaka 6 ijayo.
Je, Mbona tunahusudu SIASA zao?

Sisi tunashindwa nini kukubali uamuzi wa mtu ili tumsubiri kwenye kura za MAONI?
#ZITTO , SHIBUDA, SLAA, MBOWE na Wengineyo msiogope kusema ya MOYONI.... Mimi binafsi natangaza rasmi nitawania nafasi ya UENYEKITI TAIFA CHADEMA hata ikiwa MIAKA 50 IJAYO ......
 
Habari haiendani na kichwa cha habari............ni mbinu ya kuuza gazeti kwa wingi...ukizingatia haya masikukuu yalioandamana toka xmass mpaka kesho mauzo yao hushuka sana siku hizo....nawaza tuuu
 
UPUUZI wa Wananchi tuliowengi.

Nchi jirani ya KENYA mtu akitangaza nia ya kugombea URAIS wala hakuna longo longo, husubiriwa kwenye kura za MAONI.

Nchi za Ulaya ndiyo usiseme yaani mtu anajitangazia nia ya kupeperusha bendera ya Chama chake hata kama uchaguzi utafanyika miaka 6 ijayo.
Je, Mbona tunahusudu SIASA zao?

Sisi tunashindwa nini kukubali uamuzi wa mtu ili tumsubiri kwenye kura za MAONI?
#ZITTO , SHIBUDA, SLAA, MBOWE na Wengineyo msiogope kusema ya MOYONI.... Mimi binafsi natangaza rasmi nitawania nafasi ya UENYEKITI TAIFA CHADEMA hata ikiwa MIAKA 50 IJAYO ......
 
so sad kuona magazeti yalokuwa yanaaminika nayo yameanza udaku!professionalism iko wapi?
Nilisoma tena 'makala' moja kwenye gazeti nililokuwa naliamini sana 'Raia Mwema' yenye haeding 'chadema wasitafute miguu ya nyoka,haipo'-nlivutiwa sana na hiyo haeding ila soma sasa content!full udaku/umbea etc ni kama vile iliandikwa na Nape! SO SAD
 
atapitishwaje huyo mwingine wakati Tayari mwenyekiti wa cdm ameshamtolea chapuo dr.slaa ,mzee mtei mwenye chama tayari ameshatoa tamko..

Kamati kuu sio lidude tu,inajumuisha watu wenye maoni tofauti.Hao waliotoa maoni yao watayatoa kwenye kamati pamoja na wanakamati wengine ambao kura zao kama ni tofauti zinaweza kuzididi kura za akina Mbowe na hatimaye mgombea wako/wenu kuibuka kidedea.Mumshauri tu azidi kuwavutia wanakamati wengi.Huenda hata kura zingine akazibadilisha zikawa zake akicheza vizuri na muda!Have a nice day
 
Gazeti la Mwananchi limetoa habari ambayo ni tofauti kabisa na Maudhui yake.

Habari hiyo inasema CHADEMA SASA VIPANDE VIWILI kuhusu Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe kumtangaza Dr Slaa kugombea Urais 2015. Lakini ukisoma habari yenyewe hakuna mahali popote panapoonyesha CHADEMA sasa ni vipande vipande.

Ni habari iliyowekwa Heading hiyo kwa malengo yasiyofahamika. Endelea....

=================

SIKU moja baada ya Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe kumtangaza Dk Willibrod Slaa kuwa ndiye mgombea wa urais mwaka 2015 kwa tiketi ya chama hicho, makada wa chama hicho wamegawanyika baadhi wakimponda na wengine kumuunga mkono.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti jana, baadhi ya makada wa chama hicho walisema mwenyekiti wao amekosea kumtangaza mgombea kabla ya wakati, huku wanaomuunga mkono wakisema hajakosea kwa sababu hatua hiyo itasaidia kuondoa makundi ndani ya chama hicho.

Juzi, Mbowe akihutubia mkutano wa hadhara katika Uwanja wa Karatu mkoani Arusha, alisema Katibu Mkuu wa Chadema Dk Willibrod Slaa atapewa fursa ya kuwania tena urais kwenye Uchaguzi Mkuu wa 2015, huku mwenyewe akijiweka kando kuwania nafasi hiyo.

Hata hivyo, Dk Slaa alipoulizwa iwapo ana nia ya kuwania nafasi hiyo alihoji: “Kwani mwaka 2010 nilijitangaza mwenyewe,? Iwapo wanachama wa Chadema watanipendekeza nitafikiria kufanya hivyo.” Mwasisi wa chama hicho Edwin Mtei, Wajumbe wa Kamati Kuu; Profesa Mwesiga Baregu na Dk Kitila Mkumbo, Naibu Katibu Mkuu Zitto Kabwe, Mwenyekiti wa Bavicha John Heche na Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema walitoa maoni yanayopingana kuhusu kauli hiyo ya Mbowe.

Wanaounga mkono

Mtei alisema anaunga mkono kauli ya Mbowe akisema kiongozi huyo hajakosea kumtangaza Dk Slaa kuwania urais mwaka 2015.

“Ninaunga mkono Dk Slaa kuwania tena nafasi ya urais mwaka 2015. Mwenyekiti amemtangaza baada ya kupata baraka ya vikao vya chama,” alisema Mtei.

Ingawa Mtei hakuwa tayari kusema ni kikao gani kilichopitisha jina la Dk Slaa kuwania nafasi hiyo, alisisitiza: “Kuna vikao vya Kamati Kuu vimefanyika hivi karibuni, vinaweza kuwa vimefanya uamuzi huo. Mwenyekiti hawezi kuzungumza jambo bila baraka za vikao vya chama.”

Hata hivyo, kauli hiyo ya Mtei inapingana na ile aliyoitoa Oktoba 6, mwaka huu baada ya Zitto ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini kutangaza kutogombea tena ubunge badala yake kusema anataka kugombea urais katika uchaguzi wa mwaka 2015.

Mtei alisema hatua ya Zitto kutangaza kuwania urais mapema kungesababisha mzozo na mpasuko ndani ya chama hicho.

Mtei alisema amekuwa akimshauri Zitto mara kwa mara kuhusu hatua yake hiyo akimtaka kuwaunganisha wana Chadema na siyo kuwagawa au kuwavuruga.

“Hakuna shida kuonyesha hisia, lakini unatengeneza mzozo mkubwa sana ukitangaza sasa. Mimi nimeshamshauri sana Zitto, ahakikishe anakiunganisha chama na siyo kukigawa wala kukivuruga.”

Alisema mbunge huyo kutangaza kutogombea tena ubunge na badala yake kujipanga kuwania urais mwaka 2015 kumekuja mapema mno na kuonya kuwa itaibua mzozo ndani ya Chadema.

Mtei ambaye aliwahi kuwa Waziri wa Fedha na Gavana wa Benki Kuu enzi za utawala wa Mwalimu Julius Nyerere, alisema kwamba wakati mwafaka ukiwadia, Chadema kitaamua ni nani mwenye sifa za kugombea urais huku akisema kina utaratibu wake wa kuwapata wagombea mbalimbali wa uongozi.

Hata hivyo, Zitto jana alikataa kuzungumzia suala hilo akisema: “Nimesikia hata mimi kwenye vyombo vya habari ila sina cha kuzungumza kuhusu hilo.”

Mwenyekiti wa Taifa wa Baraza la Vijana wa Chadema (Bavicha), John Heche alisema kauli hiyo Mbowe siyo yake binafsi, bali ni ya wananchi.

“Ni kauli na maoni ya Watanzania wanaomwamini Dk Slaa kuwa anaweza kumudu kuliongoza taifa hili kama walivyoonyesha kwa kumpigia kura nyingi kuliko mgombea yeyote wa upinzani katika nafasi ya urais (mwaka 2010),” alisema Heche.

Heche alisema ingawa ndani ya Chadema kuna viongozi wengi wenye uwezo wa kuliongoza taifa, nyota ya Dk Slaa bado inang’ara.

Msimamo wa Heche uliungwa mkono na Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema ambaye alisema ni sahihi Dk Slaa kugombea urais mwaka 2015.

Lema alisema katika historia ya chaguzi za vyama vingi nchini, hakuna mgombea wa upinzani aliyewahi kupata kura nyingi kama Dk Slaa mwaka 2010 akadai kwamba ndiyo maana hivi sasa CCM kinafanya kila njama kumdhoofisha.

Lema alisema hatua ya kumtangaza Dk Slaa kuwa mgombea wa urais mwaka 2015, itaondoa harakati za chinichini zilizokuwa zikifanywa na watu ndani na nje ya Chadema kuwagombanisha viongozi wakuu wa chama hicho, hasa Mbowe na Dk Slaa.

Wanaopinga

Wakati Mtei akieleza kuwa Mbowe amepata Baraka za chama, Profesa Baregu alisema kutangazwa kwa jina la Dk Slaa kuwania urais ni maoni binafsi ya mwenyekiti huyo.

“Hayo ni maoni yake, lakini vikao vya chama ndivyo vyenye uamuzi wa mwisho kuteua jina la mgombea urais na havijakaa,” alisema Profesa Baregu.

Alipoulizwa maoni yake kuhusu sababu za Mbowe kumtangaza mgombea urais sasa kabla ya wakati, Profesa Baregu alisema: “Mbowe atakuwa amefanya hivyo kwa sababu watu wengi walikuwa wanadhani kwamba yeye pia anawania nafasi hiyo ya urais.”

“Hivyo ili kuweka mambo sawa ameamua kutangaza mapema kuwa hatawania urais na kwamba Dk Slaa ndiye anayefaa kuwania nafasi hiyo,” alisema.

Profesa Baregu alisema haoni tatizo kwa wanachama wa Chadema kutangaza nia mapema kwa sababu hiyo ni haki yao kwa mujibu wa katiba... “Hata kama watu wengi watatangaza nia ya kuwania urais, siyo jambo baya katika ujenzi wa demokrasia, lakini uamuzi wa mwisho ni wa vikao vya chama.”

Kauli ya Profesa Baregu kuhusu vikao iliungwa mkono na Dk Mkumbo ambaye alisema kwamba anachojua vikao vya chama ndivyo vyenye uamuzi wa mwisho kuhusu uteuzi wa wagombea wa ngazi ya urais.

Dk Mkumbo alionyesha shaka kama kweli Mbowe alimtaja Dk Slaa kuwa ndiye atakayewania nafasi hiyo akisisitiza: “Ninachofahamu ni kwamba yeye ametangaza kuwa hatagombea nafasi hiyo.”
Kama makundi ya mitazamo ndiyo vipande basi CCM ina zaidi ya Vipande Vinne!!!
Ila Historia inaonyesha kuwa Gzt Mwananchi lilianzishwa na Rostam Kwa lengo la kutetea CCM na baadaye likauzwa kwa Wakenya lakini Mbegu za wafanyakazi wa Rostam zilibaki mpaka sasa wapo upande wa Lowasa!!
Utashanga gazeti hilo lenye sifa ya uhuru hliwezi kuandika uchafu wa Lowasa na Rostam!!!
Zitto ni pando la Rostam hata zile simu zao zimeonyesha hilo!!!
 
MTEI NI MNAFIKI
iweje kwa zitto aseme kutangaza kwake nia ya kugombea urais kutakigawa chama lkn kwa slaa hajasema hivyo!? domokrasia iko wapi?
 
upuuzi wa wananchi tuliowengi.

Nchi jirani ya kenya mtu akitangaza nia ya kugombea urais wala hakuna longo longo, husubiriwa kwenye kura za maoni.

Nchi za ulaya ndiyo usiseme yaani mtu anajitangazia nia ya kupeperusha bendera ya chama chake hata kama uchaguzi utafanyika miaka 6 ijayo.
Je, mbona tunahusudu siasa zao?

Sisi tunashindwa nini kukubali uamuzi wa mtu ili tumsubiri kwenye kura za maoni?
#zitto , shibuda, slaa, mbowe na wengineyo msiogope kusema ya moyoni.... Mimi binafsi natangaza rasmi nitawania nafasi ya uenyekiti taifa chadema hata ikiwa miaka 50 ijayo ......

yani uko sahihi kabisa ....kikubwa watu wanahoji mbona zitto alipotangaza nia ya urais 2015 mbowe ,mtei,dr.slaa walitokwa na povu lenye kutu lakini iweje leo wao ndo watangaze nia ndo waonekane wako sahihi..lakini zito akaonekana anakigawa chama
 
kamati kuu sio lidude tu,inajumuisha watu wenye maoni tofauti.hao waliotoa maoni yao watayatoa kwenye kamati pamoja na wanakamati wengine ambao kura zao kama ni tofauti zinaweza kuzididi kura za akina mbowe na hatimaye mgombea wako/wenu kuibuka kidedea.mumshauri tu azidi kuwavutia wanakamati wengi.huenda hata kura zingine akazibadilisha zikawa zake akicheza vizuri na muda!have a nice day

na kwa sasa hakuna mgombe mwingine ambaye atagombea urais 2015 zaidi ya dr.slaa mwenyekiti na mwenye chama wameshasema dr.slaa ni mgombe 2015 ...hata povu likutoke vipi hakuna mwingine hivyo vikao ni danganya toto tu.......
 
na kwa sasa hakuna mgombe mwingine ambaye atagombea urais 2015 zaidi ya dr.slaa mwenyekiti na mwenye chama wameshasema dr.slaa ni mgombe 2015 ...hata povu likutoke vipi hakuna mwingine hivyo vikao ni danganya toto tu.......
Kama huamini vikaohilo ni tatizo lako sasa!
 
Kama ni kweli CHADEMA kina vipande viwili,sipati picha chama cha zamani kitakuwa na vipande vingapi?
 
Kuweweseka ni kubaya sana, Jiandae tu kuwa katibu mwenezi wa CHAUUMA.

Mkuu wangu Shardcole naona huwapi hata chance ya kupumua.Masalia wanakuona Nuksi.

Ukifuatilia hii thread utagundua Masalia aliyeko zamu anabadilisha ID kama 5 hivi ndizo anazitumia kukashifu kwa kila aina ya matusi viongozi wakuu wa Chadema.

Bahati njema sana wanajulikana na ndiyo maana Chadema haiwasumbui.

Hawa Masalia ndiyo walianzisha kundi haramu la PM7 yaani Pindua Mbowe Group 7

Tunaelezwa na Kamanda asiyeyumba Ben Saanane kwamba aliagizwa na Dr Kitila Mkumbo ahakikishe anatumia kila njia kusambaratisha hilo kundi haramu kwani lina nia ya kuua chama.

Sasa kundi hili haramu baada ya Ben Saanane kulisambaratisha limeona likimbilie kwenye mitandao kushambulia na kuwatukana mashujaa wa Chadema Dr Wilbroad Slaa na Freeman Mbowe.

Nawahakikishia hawataweza...!
 
Last edited by a moderator:
“Ninaunga mkono Dk Slaa kuwania tena nafasi ya urais mwaka 2015. Mwenyekiti amemtangaza baada ya kupata baraka ya vikao vya chama,” alisema Mtei.( mwananchi dec 21,2012)
....kikao kimefanyika lini??mbona hamjibu??
Nina wasiwasi sana na taarifa za Mwananchi, maana magazeti mengine ya jana
hayakuripoti kama Mbowe kamtangaza Dr Slaa kuwa mgombea.
Zaidi ya yote, Mwananchi limekuwa likimpigia sana Zitto parapanda
 
MTEI NI MNAFIKI
iweje kwa zitto aseme kutangaza kwake nia ya kugombea urais kutakigawa chama lkn kwa slaa hajasema hivyo!? domokrasia iko wapi?

CHADEMA ni mali binafsi ya Mtei. Aliianzisha kwa jasho lake na anaiendesha anavyotaka.
 
Gazeti la mwananchi lina maslahi na mtia nia mmoja wa Chadema katika kuusaka uraisi. Sina shaka hiyo heading pamoja na habari nzima itakuwa imeandikwa na kuhaririwa na mtia nia ndipo sasa ikaingizwa mtamboni kuchapwa.
Wacha waendelee na sarakasi zao tu lakini watambue kwamba sisi wenyewe tunajua nani atakayepeperusha bendera ya Chama chetu.
Na jambo la bahati nzuri ni kwamba hakuna vipande wala mapande ndani ya Chadema.
 
Back
Top Bottom