Gazeti Mwananchi: CHADEMA sasa Vipande viwili!

Gazeti Mwananchi: CHADEMA sasa Vipande viwili!

Molemo hapo hujaelewa nini wakati unaambiwa kuna wanaomponda na wanaomunga mkono wewe huoni ni pande mbili hizo
 
Last edited by a moderator:
upo sahihi mkuu, ndio maana pasipo na mgawanyiko wengine mmeona mgawanyiko, kweli masalia wamedhamiria kuchafua

Masalia ni Looser...Hata wakitumia vyombo vya habari tutawajua tu.
 
Vipande viwili mbona vinaonekana wazi kwenye hiyo habari. Nilitegemea ukanushe kuwa Mtei hakutoa kauli kuwa kauli ya Mbowe ina baraka ya chama. Ila cha kushangaza kundi moja la Pr Baregu na Kitila Mkumbo hawana taarifa na maamuzi hayo ya chama. Wakati huo huo Godbless Lema anakubaliana na hiyo kauli ya Mbowe. Mwandish ametaja vipande viwili nilivyobold hapo.

Msijitie upofu wa mawazo, ni kitu kibaya sana kwa chama kama CHADEMA kinachojiita chama cha DEMOKRASIA![Lema ukamwabie eti mbowe kasema hivi apinge? ujue kesho yake ni mwisho wa dunia kwa maana kila analosema mbowe kwake ni sawa utfikiri yeye ni malaika
 
Hapo ni ngoma droo! Zitto alianza kwa kusema kwa kauli yake ya mara ya kwanza bila editing kuwa atagombea Urais kupitia CHADEMA 2015, hata kabla ya hapo alianza mwaka 2010 aliposema jimboni kwake kuwa atagombea urais 2015 na sio ubunge.

Hapo hakuna mapande 2 maana Dk.slaa bado hajatangaza nia ila tatizo hili gazeti la mwananchi ambalo ndio huwa linampigia debe Zitto leo limeamua kupotosha umma kwani limeguswa penyewe kwa kusikia kuwa Dk.Slaa ndiye tosha CHADEMA.

UKISIKIA PAAA UJUE LIMEKUPATA, NA UKISKIA MTU AMELIA MAMAAAAAA....! UJUE LIMEMPATA PENYEWE"

Dkt.Slaa tosha 2015.
 
Nilikutana siku moja na afisa masoko wa mwananchi,aliniambia siku wakiandika habari za CDM gazeti huwa linanunuliwa sana. Ndiyo maana leo unakuta limeandika hivyo ili wale wanaopenda migogoro ndani ya chama wanunue, na wale wasio penda migogoro wanunue wakitaka kujua ni mgogoro gani huo ili hali mwenye kiti amesema hakuna makundi? Kwa ujumla gazeti la mwananchi linafanya biashara, wanafanya hivyo ili watu tujue kuna mgogoro ili gazeti linunuliwe kwa wingi.

Point Noted...
 
Mtei bana... ZZK alipotanganiza nia, Mtei alikuja juu na kumwambia huu si wakati muafaka na atakivuruga chama. Mbowe kamtangaza Slaa..Mtei anaona ni wakati muafaka na si kuvuruga chama. Siasa za Bongo ni full usanii na Umimi.

Mbowe ni mkaza mwana na Zitto ni Kyasaka.
 
Now, I have read between the line....

Hakuna kitu kinachochukiza na kuudhi nchini kama kuwa na humbug, hypocrite, and sanctimonious politician.

Kwa wale mnaotaka demokrasia ya kweli, close your eye kwa vile wenye chama wanawapeni ujumbe kwa kusema, if you can't fight them, join them and remember, your fighting a losing battle.

Democracy at work. It's hard to swallow but that's the truth.

Mzee Mtei word reinforce notion ambao wenye macho mawili walifahamu baada ya yeye kutoa ushauri kuhusu tamko la Mh. Zitto Kabwe early this year.

Watu design ya Profesa Baregu hata hawafai kuwa washauri katika siasa kwa jinsi alivyotoa maelezo yake kwa sababu kauli zake zinakuwa ni kama za wachumia tumbo.

Majibu ya Dr. Kitila Mkumbo yamebeba hekima na ujumbe mpana kwa wenye macho mawili na fikra pana.

Kupata kauli zinazokinzana na wenye chama kutoka kwa John Heche na Mh. Gobless Lema labda mpaka hapo majira yatakapokuwa in anticlockwise.

Hapo ni ngoma droo! Zitto alianza kwa kusema kwa kauli yake ya mara ya kwanza bila editing kuwa atagombea Urais kupitia CHADEMA 2015, hata kabla ya hapo alianza mwaka 2010 aliposema jimboni kwake kuwa atagombea urais 2015 na sio ubunge.

Hapo hakuna mapande 2 maana Dk.slaa bado hajatangaza nia ila tatizo hili gazeti la mwananchi ambalo ndio huwa linampigia debe Zitto leo limeamua kupotosha umma kwani limeguswa penyewe kwa kusikia kuwa Dk.Slaa ndiye tosha CHADEMA.

UKISIKIA PAAA UJUE LIMEKUPATA, NA UKISKIA MTU AMELIA MAMAAAAAA....! UJUE LIMEMPATA PENYEWE"

Dkt.Slaa tosha 2015.

Mkuu Shardcole huwa ninachukizwa sana na uandishi wa habari wa kipuuzi na kishabiki.Kuna watu wanahaha usiku na mchana ili Chadema iwe vipande vipande.

Ukisoma walichosema wajumbe wa Kamati Kuu kama Dr Kitila Mkumbo na Professor Baregu hakuna mahali popote wamepinga zaidi ya kutoa maoni yao.

Uandishi wa aina hii ni ukanjanja..!
 
Last edited by a moderator:
ukisoma tz daima la jana utaona wamem quote mbowe akisema " hatagombea kazi yake itakuwa ni kuakikisha cdm inampata mgombea urais makini".
 
Mtei bana... ZZK alipotanganiza nia, Mtei alikuja juu na kumwambia huu si wakati muafaka na atakivuruga chama. Mbowe kamtangaza Slaa..Mtei anaona ni wakati muafaka na si kuvuruga chama. Siasa za Bongo ni full usanii na Umimi.

Ukisikia mmaaaaaaaa! Ujue mtu kaguswa penyewe.

Dkt.Slaa tosha 2015.
 
Mtei bana... ZZK alipotanganiza nia, Mtei alikuja juu na kumwambia huu si wakati muafaka na atakivuruga chama. Mbowe kamtangaza Slaa..Mtei anaona ni wakati muafaka na si kuvuruga chama. Siasa za Bongo ni full usanii na Umimi.

Chadema wanazidi kuwavueni nguo.

Ninawaambia tena nyie Magamba/Masalia/CUF and alike kwamba Yule mtu ambaye CCM hawamtaki kabisa ndiye anafaa kuwa Rais.

Sikuzote ukiona asichokitaka adui yako kishikilie hicho hicho wala usiachie ili uzidi kumuumiza Adui.
 
Ningeshangaa kama usinge changia kwa kauli kama hii! Hebu nenda mbele zaidi na useme kwa kusadifu mizania. Zk nae alikuwa kwa maagizo ya nani?! Kabla kamati kuu haijapitisha mgombea weka kwenye mizani majina mawili uone la nani linamzidi mwenzake uzito halafu peleka ripoti Lumumba uone ukiwa una wakabidhi ripoti nyuso zao zitakuwaje.

Asubuhi njema! Naona wewe ndio umeingia kazini rasmi kama kawaida 24/7 baadae kidogo kaka.

utenzi wa ngojela
 
Nido uandishi wa wachumi matumbo wakina Msaki, sasa kama mwenyekiti akiongea kwa nini wao wana question? lakini cha msingi tujiulize tangu Tido Mhando aende pale gazeti badala ya kupanda juu limeishia kuwa la Udaku, ndio maana mpaka leo kwa wanaosema alitolewa TBC kwa kuwa na msimamo nawakatalia, hakuwa na msimamo wowote, kama maswala ya ile midahalo yalikua contractual alisaini makubaliana na mabwana zake wa CCM walivyomlazimisha afute, wale client wakakataa unless walipwe kwa uvunjaji wa mkataba, Tido akawa hana la kufanya bali kusubiri hatima yake. Sasa gazeti kama hilo utamuachiaje Msaki? Theophil Makunga wamempeleke kuwa Business Manager (Editor) unless corrected here kwa faida ya nani? At least huyu bwana pamoja na kuwatumikia makafiri alikua na maturity fulani ya kuweza kufunika funika na kuweka mguu chini inapobidi kulinda heshima yake, hii ni kabla ya tukio la ripoti ya Mwangosya. Sasa huko alikopelekwa kilichonishangaza ni kukubali kwake, nilifikiri wangempeleka kwenye U DC kulinda heshima yake, mark my word hiyo ndio safari ya kuelekea wanakotokeaga, correspondent maana sioni atatoka vipi pale, ndio faida ya kukaa ki siasa zaidi kuliko kisayansi, Nation wana nafasi kibao tena za heshima, kama angeheshimika ki technical wasingemgalagaza hivyo mbona yule mwandishi mwahanasheria aliyekua burea wa lake zone kapaa, hakuwa muendekeza njaa nakumbuka alisema pale habari kama Muhingo atakua ME mi sipo, na kweli muhingo aliporipoti yeye hakutokea tena chumba cha habari,
 
Siku za karibuni nimeona mwananchi wanaandika 'very big heading' lakini content hewa! Mfano nimeisoma hiyo habari huoni hizo pande mbili. Wapo ambao wametajwa kuwa wametoa maoni. Hayaonekani popote!
 
“Ninaunga mkono Dk Slaa kuwania tena nafasi ya urais mwaka 2015. Mwenyekiti amemtangaza baada ya kupata baraka ya vikao vya chama,” alisema Mtei.( mwananchi dec 21,2012)
....kikao kimefanyika lini??mbona hamjibu??
 
Ningeshangaa kama usinge changia kwa kauli kama hii! Hebu nenda mbele zaidi na useme kwa kusadifu mizania. Zk nae alikuwa kwa maagizo ya nani?! Kabla kamati kuu haijapitisha mgombea weka kwenye mizani majina mawili uone la nani linamzidi mwenzake uzito halafu peleka ripoti Lumumba uone ukiwa una wakabidhi ripoti nyuso zao zitakuwaje.

Asubuhi njema! Naona wewe ndio umeingia kazini rasmi kama kawaida 24/7 baadae kidogo kaka.

Mkuu mohamed Mtoi heshima kubwa kwa mchango wako huu.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom