Gazeti Mwananchi: CHADEMA sasa Vipande viwili!

Gazeti Mwananchi: CHADEMA sasa Vipande viwili!

Aaah,bora nichukue zangu time...jamaa hawa so pointless trying to make them see reality.
 
Gazeti la Mwananchi limetoa habari ambayo ni tofauti kabisa na Maudhui yake.

Habari hiyo inasema CHADEMA SASA VIPANDE VIWILI kuhusu Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe kumtangaza Dr Slaa kugombea Urais 2015. Lakini ukisoma habari yenyewe hakuna mahali popote panapoonyesha CHADEMA sasa ni vipande vipande.

Ni habari iliyowekwa Heading hiyo kwa malengo yasiyofahamika. Endelea....

=================

SIKU moja baada ya Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe kumtangaza Dk Willibrod Slaa kuwa ndiye mgombea wa urais mwaka 2015 kwa tiketi ya chama hicho, makada wa chama hicho wamegawanyika baadhi wakimponda na wengine kumuunga mkono.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti jana, baadhi ya makada wa chama hicho walisema mwenyekiti wao amekosea kumtangaza mgombea kabla ya wakati, huku wanaomuunga mkono wakisema hajakosea kwa sababu hatua hiyo itasaidia kuondoa makundi ndani ya chama hicho.

Juzi, Mbowe akihutubia mkutano wa hadhara katika Uwanja wa Karatu mkoani Arusha, alisema Katibu Mkuu wa Chadema Dk Willibrod Slaa atapewa fursa ya kuwania tena urais kwenye Uchaguzi Mkuu wa 2015, huku mwenyewe akijiweka kando kuwania nafasi hiyo.

Hata hivyo, Dk Slaa alipoulizwa iwapo ana nia ya kuwania nafasi hiyo alihoji: "Kwani mwaka 2010 nilijitangaza mwenyewe,? Iwapo wanachama wa Chadema watanipendekeza nitafikiria kufanya hivyo." Mwasisi wa chama hicho Edwin Mtei, Wajumbe wa Kamati Kuu; Profesa Mwesiga Baregu na Dk Kitila Mkumbo, Naibu Katibu Mkuu Zitto Kabwe, Mwenyekiti wa Bavicha John Heche na Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema walitoa maoni yanayopingana kuhusu kauli hiyo ya Mbowe.

Wanaounga mkono

Mtei alisema anaunga mkono kauli ya Mbowe akisema kiongozi huyo hajakosea kumtangaza Dk Slaa kuwania urais mwaka 2015.

"Ninaunga mkono Dk Slaa kuwania tena nafasi ya urais mwaka 2015. Mwenyekiti amemtangaza baada ya kupata baraka ya vikao vya chama," alisema Mtei.

Ingawa Mtei hakuwa tayari kusema ni kikao gani kilichopitisha jina la Dk Slaa kuwania nafasi hiyo, alisisitiza: "Kuna vikao vya Kamati Kuu vimefanyika hivi karibuni, vinaweza kuwa vimefanya uamuzi huo. Mwenyekiti hawezi kuzungumza jambo bila baraka za vikao vya chama."

Hata hivyo, kauli hiyo ya Mtei inapingana na ile aliyoitoa Oktoba 6, mwaka huu baada ya Zitto ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini kutangaza kutogombea tena ubunge badala yake kusema anataka kugombea urais katika uchaguzi wa mwaka 2015.

Mtei alisema hatua ya Zitto kutangaza kuwania urais mapema kungesababisha mzozo na mpasuko ndani ya chama hicho.

Mtei alisema amekuwa akimshauri Zitto mara kwa mara kuhusu hatua yake hiyo akimtaka kuwaunganisha wana Chadema na siyo kuwagawa au kuwavuruga.

"Hakuna shida kuonyesha hisia, lakini unatengeneza mzozo mkubwa sana ukitangaza sasa. Mimi nimeshamshauri sana Zitto, ahakikishe anakiunganisha chama na siyo kukigawa wala kukivuruga."

Alisema mbunge huyo kutangaza kutogombea tena ubunge na badala yake kujipanga kuwania urais mwaka 2015 kumekuja mapema mno na kuonya kuwa itaibua mzozo ndani ya Chadema.

Mtei ambaye aliwahi kuwa Waziri wa Fedha na Gavana wa Benki Kuu enzi za utawala wa Mwalimu Julius Nyerere, alisema kwamba wakati mwafaka ukiwadia, Chadema kitaamua ni nani mwenye sifa za kugombea urais huku akisema kina utaratibu wake wa kuwapata wagombea mbalimbali wa uongozi.

Hata hivyo, Zitto jana alikataa kuzungumzia suala hilo akisema: "Nimesikia hata mimi kwenye vyombo vya habari ila sina cha kuzungumza kuhusu hilo."

Mwenyekiti wa Taifa wa Baraza la Vijana wa Chadema (Bavicha), John Heche alisema kauli hiyo Mbowe siyo yake binafsi, bali ni ya wananchi.

"Ni kauli na maoni ya Watanzania wanaomwamini Dk Slaa kuwa anaweza kumudu kuliongoza taifa hili kama walivyoonyesha kwa kumpigia kura nyingi kuliko mgombea yeyote wa upinzani katika nafasi ya urais (mwaka 2010)," alisema Heche.

Heche alisema ingawa ndani ya Chadema kuna viongozi wengi wenye uwezo wa kuliongoza taifa, nyota ya Dk Slaa bado inang'ara.

Msimamo wa Heche uliungwa mkono na Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema ambaye alisema ni sahihi Dk Slaa kugombea urais mwaka 2015.

Lema alisema katika historia ya chaguzi za vyama vingi nchini, hakuna mgombea wa upinzani aliyewahi kupata kura nyingi kama Dk Slaa mwaka 2010 akadai kwamba ndiyo maana hivi sasa CCM kinafanya kila njama kumdhoofisha.

Lema alisema hatua ya kumtangaza Dk Slaa kuwa mgombea wa urais mwaka 2015, itaondoa harakati za chinichini zilizokuwa zikifanywa na watu ndani na nje ya Chadema kuwagombanisha viongozi wakuu wa chama hicho, hasa Mbowe na Dk Slaa.

Wanaopinga

Wakati Mtei akieleza kuwa Mbowe amepata Baraka za chama, Profesa Baregu alisema kutangazwa kwa jina la Dk Slaa kuwania urais ni maoni binafsi ya mwenyekiti huyo.

"
Hayo ni maoni yake, lakini vikao vya chama ndivyo vyenye uamuzi wa mwisho kuteua jina la mgombea urais na havijakaa," alisema Profesa Baregu.

Alipoulizwa maoni yake kuhusu sababu za Mbowe kumtangaza mgombea urais sasa kabla ya wakati, Profesa Baregu alisema: "Mbowe atakuwa amefanya hivyo kwa sababu watu wengi walikuwa wanadhani kwamba yeye pia anawania nafasi hiyo ya urais."

"Hivyo ili kuweka mambo sawa ameamua kutangaza mapema kuwa hatawania urais na kwamba Dk Slaa ndiye anayefaa kuwania nafasi hiyo," alisema.

Profesa Baregu alisema haoni tatizo kwa wanachama wa Chadema kutangaza nia mapema kwa sababu hiyo ni haki yao kwa mujibu wa katiba... "Hata kama watu wengi watatangaza nia ya kuwania urais, siyo jambo baya katika ujenzi wa demokrasia, lakini uamuzi wa mwisho ni wa vikao vya chama."

Kauli ya Profesa Baregu kuhusu vikao iliungwa mkono na Dk Mkumbo ambaye alisema kwamba anachojua vikao vya chama ndivyo vyenye uamuzi wa mwisho kuhusu uteuzi wa wagombea wa ngazi ya urais.

Dk Mkumbo alionyesha shaka kama kweli Mbowe alimtaja Dk Slaa kuwa ndiye atakayewania nafasi hiyo akisisitiza: "Ninachofahamu ni kwamba yeye ametangaza kuwa hatagombea nafasi hiyo."
:drum::behindsofa:
 
maoni ya mtei aachiwe yeye
anatoa maon kam raia yeyote yule.
ila maoni ya mtei sio ya chadema ingawwaje ni muasisi
Chadema inaendeshwa kwa sheria na taratbu na sio maoni ya mtu mmoja.
 
Utumbo mtupu, address issue siyo kuzunguka tu kama unacheza mdundiko hapa ni kwa ma-intellectuals anaochambua mambo kama yalivyo

Huwezi kujua kama issue iko addressed kwa sababu hili siyo eneo lako. Jaribu kule chit chat ndiyo atakapozijua kwa urahisi kama issue ziko addressed.
 
its interesting kuona Gazeti ambalo sio la udaku linaandika kichwa cha habari kwa style hii. Who knows.,may be.,wanatafuta hisia za watu zitasemaje au ndo mauzo yameshuka:yo:
 
Huyo ndio Tido Mhando (ex TBC) akiwa kazini!!
 
Chadema wanazidi kuwavueni nguo.

Ninawaambia tena nyie Magamba/Masalia/CUF and alike kwamba Yule mtu ambaye CCM hawamtaki kabisa ndiye anafaa kuwa Rais.

Sikuzote ukiona asichokitaka adui yako kishikilie hicho hicho wala usiachie ili uzidi kumuumiza Adui.

kama ilivyo kwa nape na mwigulu jinsi walivyo mwiba kwa chadema
 
Ningeshangaa kama usinge changia kwa kauli kama hii! Hebu nenda mbele zaidi na useme kwa kusadifu mizania. Zk nae alikuwa kwa maagizo ya nani?! Kabla kamati kuu haijapitisha mgombea weka kwenye mizani majina mawili uone la nani linamzidi mwenzake uzito halafu peleka ripoti Lumumba uone ukiwa una wakabidhi ripoti nyuso zao zitakuwaje.

Asubuhi njema! Naona wewe ndio umeingia kazini rasmi kama kawaida 24/7 baadae kidogo kaka.

Mtoi nakubaliana na wewe 101%. Hata CCM wanajua kuwa Dr. Slaa ni tishio na ndo maana hawashughuliki na ZZK. Zito anatakiwa amlinde Dr Slaa kama mboni la jicho lake kama kweli hatumiki. Tunamtaka rais atakeafanya usafi ataikibidi kuwanyonga watu wengine kwa maslahi ya Watanzania. Naamini ZZK mda wake bado, atafuata baada ya Dr. Slaa. Hakuna mpasuko hapo hata kdgo. Najua masalia na magamba watajipanga na kuja kivingine
 
Tumaini Makene ni kweli gazeti la Mwananchi limekuza sana habari ya vipande viwili ndani ya CHADEMA na yawezekana imetokana na kubanwa kwa Zitto Kabwe ambaye gazeti hili limekuwa likimpigia debe kila mara.

Lakini hebu twende mbele turudi nyuma Freeman Mbowe angeishia kwenye RED colour hapo juu kungekuwa na tatizo gani? Kwa nini aliamua kuvunja constitutional procedures za chama chenu katika kumpata mgombea hadi kufikia hatua ya kutaja jina la mgombea? Kweli mgombea anapatikana kwa Mwenyekiti mwenyewe kuamua na kukurupukia jukwaani kumtangaza? This can not be the right way any where unless kama chama ni individual driven.

Ni kweli Dkt. Slaa kwa sasa ndani ya CHADEMA nyota yake iko juu na hata uwezekano wa kupata kura za kutosha na kumuwezesha kuwa Rais ajaye upo sana lakini Freeman Mbowe kwa nafasi yake inabidi achunge sana ulimi vinginevyo atakuwa ni agent wa mitafaruku isiyo ya lazima ndani ya chama. Ukishakuwa Mwenyekiti au kiongozi ni vema kuepuka kauli zinazoleta mitafaruku isiyo ya lazima.

Nimependa sana Comment ya Professor Baregu kwenye habari hii anasema "Hayo ni mawazo binafsi ya Mwenyekiti Mbowe na si ya chama" lakini bado nashindwa kuelewa ni wakati gani kauli ya kiongozi itahesabika ni ya chama na wakati gani si ya chama? Hili nalo lina ukakasi mwingi tu.

Umakini wa viongozi ndiyo kuaminika kwa chama machoni pa watu makini na weledi vinginevyo bado nadhani media zilimnukuu visivyo Mbowe na Kurugenzi ya Habari na Uenezi ina nafasi ya kunyoosha hili maana halina afya kwa demokrasia ya chama chenu.

Natamani kweli kweli kukusaidia mkuu ili uweze kuelewa. Waliokuwepo Karatu wanajua alichokisema Mwenyekiti. Alifanya mambo mawili kwa uwazi, la tatu ambalo sijaona mwandishi wa habari yeyote aliyeliona mpaka sasa kwa sababu lilikuwa kubwa pia, ngoja tuendelee kuliweka home work kwa wenzetu wa habari.

Kwanza Mwenyekiti alitangaza wazi kuwa hana mpango wa kugombea urais. Kauli hii magamba hawakuitegemea. Maadui wa CHADEMA hawajaipenda. Maana kwa muda mrefu walikuwa wanapika migogoro isiyokuwepo kuwa kuna makundi na mgogoro mkubwa ndani ya CHADEMA hasa kati ya Mwenyekiti na Katibu Mkuu. Hilo limegonga mwamba.

Unajua kwa nini walitaka iwe hivyo...kati ya vitu vinavyowaumiza maadui wa CHADEMA ni mshikamano walionao viongozi wakuu, in principles katika uendeshaji wa chama na kutoa utumishi bora kwa umma.

Pili, akasema watu wamekuwa wakizusha kuwa kuna mgogoro ndani ya CHADEMA kjwa sababu ya urais na kuwa yeye na Katibu Mkuu hawaelewani kwa sababu ya urais, akasema hilo hakuna. Kunaweza kuwa na misigano ya mitizamo hapa na pale, lakini si mpasuko. Wao wanaheshimiana. Akasema anamheshimu sana Katibu Mkuu wake kutokana na uwezo wake alionao, ndiyo maana alimpisha kugombea urais mwaka 2010 na kila mtu anajua alitosha.

Tatu, ambalo ndilo kubwa na muhimu kabisa, alisema yeye atasimamia vikao vya chama kuhakikisha CHADEMA inapata mgombea urais atakayeipeleka CHADEMA ikulu. Akasema umakini huo pia utatumika sana katika kuwapata wagombea wa udiwani na ubunge kwa uchaguzi wa mwaka 2015.

Wapi Mwenyekiti amevunja katiba ya chama, achilia mbali demokrasia na haki. Hakuna.

Ni biashara tu, siku hizi ukitaka kuuza gazeti basi andika SLAA au CHADEMA!
 
Mkuu Tumaini Makene kama hiki ndicho kilichotokea Karatu na nyinyi kama Kurugenzi ya Habari na Uenezi mnaamini habari inayoendelea sasa kwamba Mbowe kampitisha Dkt. Salaa kugombea urais bila kufuata taratibu za chama chenu si ya kweli bali inapotoshwa makusudi kwa nini mko kimya? Yaani kunapokuwa na habari inayopotoshwa kiasi hicho hamuoni inaleta madhara kwa chama chenu.

Hiki ulichokiandika kingetosha kabisa kuclear upepo mchafu uliovuma (Kama ni kweli aliishia katika hayo uliyoyaandika). Ndiyo maana huwa kuna makanusho au ufafanuzi kunapokuwa na upotoshaji. Ushauri tu.
 
Last edited by a moderator:

Natamani kweli kweli kukusaidia mkuu ili uweze kuelewa. Waliokuwepo Karatu wanajua alichokisema Mwenyekiti. Alifanya mambo mawili kwa uwazi, la tatu ambalo sijaona mwandishi wa habari yeyote aliyeliona mpaka sasa kwa sababu lilikuwa kubwa pia, ngoja tuendelee kuliweka home work kwa wenzetu wa habari.

Kwanza Mwenyekiti alitangaza wazi kuwa hana mpango wa kugombea urais. Kauli hii magamba hawakuitegemea. Maadui wa CHADEMA hawajaipenda. Maana kwa muda mrefu walikuwa wanapika migogoro isiyokuwepo kuwa kuna makundi na mgogoro mkubwa ndani ya CHADEMA hasa kati ya Mwenyekiti na Katibu Mkuu. Hilo limegonga mwamba.

Unajua kwa nini walitaka iwe hivyo...kati ya vitu vinavyowaumiza maadui wa CHADEMA ni mshikamano walionao viongozi wakuu, in principles katika uendeshaji wa chama na kutoa utumishi bora kwa umma.

Pili, akasema watu wamekuwa wakizusha kuwa kuna mgogoro ndani ya CHADEMA kjwa sababu ya urais na kuwa yeye na Katibu Mkuu hawaelewani kwa sababu ya urais, akasema hilo hakuna. Kunaweza kuwa na misigano ya mitizamo hapa na pale, lakini si mpasuko. Wao wanaheshimiana. Akasema anamheshimu sana Katibu Mkuu wake kutokana na uwezo wake alionao, ndiyo maana alimpisha kugombea urais mwaka 2010 na kila mtu anajua alitosha.

Tatu, ambalo ndilo kubwa na muhimu kabisa, alisema yeye atasimamia vikao vya chama kuhakikisha CHADEMA inapata mgombea urais atakayeipeleka CHADEMA ikulu. Akasema umakini huo pia utatumika sana katika kuwapata wagombea wa udiwani na ubunge kwa uchaguzi wa mwaka 2015.

Wapi Mwenyekiti amevunja katiba ya chama, achilia mbali demokrasia na haki. Hakuna.

asante makene kwa kujibu hoja hii
 
Back
Top Bottom