Gazeti Mwananchi: CHADEMA sasa Vipande viwili!

Gazeti Mwananchi: CHADEMA sasa Vipande viwili!

Molemo

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2010
Posts
14,620
Reaction score
13,361
Gazeti la Mwananchi limetoa habari ambayo ni tofauti kabisa na Maudhui yake.

Habari hiyo inasema CHADEMA SASA VIPANDE VIWILI kuhusu Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe kumtangaza Dr Slaa kugombea Urais 2015. Lakini ukisoma habari yenyewe hakuna mahali popote panapoonyesha CHADEMA sasa ni vipande vipande.

Ni habari iliyowekwa Heading hiyo kwa malengo yasiyofahamika. Endelea....

=================

SIKU moja baada ya Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe kumtangaza Dk Willibrod Slaa kuwa ndiye mgombea wa urais mwaka 2015 kwa tiketi ya chama hicho, makada wa chama hicho wamegawanyika baadhi wakimponda na wengine kumuunga mkono.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti jana, baadhi ya makada wa chama hicho walisema mwenyekiti wao amekosea kumtangaza mgombea kabla ya wakati, huku wanaomuunga mkono wakisema hajakosea kwa sababu hatua hiyo itasaidia kuondoa makundi ndani ya chama hicho.

Juzi, Mbowe akihutubia mkutano wa hadhara katika Uwanja wa Karatu mkoani Arusha, alisema Katibu Mkuu wa Chadema Dk Willibrod Slaa atapewa fursa ya kuwania tena urais kwenye Uchaguzi Mkuu wa 2015, huku mwenyewe akijiweka kando kuwania nafasi hiyo.

Hata hivyo, Dk Slaa alipoulizwa iwapo ana nia ya kuwania nafasi hiyo alihoji: "Kwani mwaka 2010 nilijitangaza mwenyewe,? Iwapo wanachama wa Chadema watanipendekeza nitafikiria kufanya hivyo." Mwasisi wa chama hicho Edwin Mtei, Wajumbe wa Kamati Kuu; Profesa Mwesiga Baregu na Dk Kitila Mkumbo, Naibu Katibu Mkuu Zitto Kabwe, Mwenyekiti wa Bavicha John Heche na Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema walitoa maoni yanayopingana kuhusu kauli hiyo ya Mbowe.

Wanaounga mkono

Mtei alisema anaunga mkono kauli ya Mbowe akisema kiongozi huyo hajakosea kumtangaza Dk Slaa kuwania urais mwaka 2015.

"Ninaunga mkono Dk Slaa kuwania tena nafasi ya urais mwaka 2015. Mwenyekiti amemtangaza baada ya kupata baraka ya vikao vya chama," alisema Mtei.

Ingawa Mtei hakuwa tayari kusema ni kikao gani kilichopitisha jina la Dk Slaa kuwania nafasi hiyo, alisisitiza: "Kuna vikao vya Kamati Kuu vimefanyika hivi karibuni, vinaweza kuwa vimefanya uamuzi huo. Mwenyekiti hawezi kuzungumza jambo bila baraka za vikao vya chama."

Hata hivyo, kauli hiyo ya Mtei inapingana na ile aliyoitoa Oktoba 6, mwaka huu baada ya Zitto ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini kutangaza kutogombea tena ubunge badala yake kusema anataka kugombea urais katika uchaguzi wa mwaka 2015.

Mtei alisema hatua ya Zitto kutangaza kuwania urais mapema kungesababisha mzozo na mpasuko ndani ya chama hicho.

Mtei alisema amekuwa akimshauri Zitto mara kwa mara kuhusu hatua yake hiyo akimtaka kuwaunganisha wana Chadema na siyo kuwagawa au kuwavuruga.

"Hakuna shida kuonyesha hisia, lakini unatengeneza mzozo mkubwa sana ukitangaza sasa. Mimi nimeshamshauri sana Zitto, ahakikishe anakiunganisha chama na siyo kukigawa wala kukivuruga."

Alisema mbunge huyo kutangaza kutogombea tena ubunge na badala yake kujipanga kuwania urais mwaka 2015 kumekuja mapema mno na kuonya kuwa itaibua mzozo ndani ya Chadema.

Mtei ambaye aliwahi kuwa Waziri wa Fedha na Gavana wa Benki Kuu enzi za utawala wa Mwalimu Julius Nyerere, alisema kwamba wakati mwafaka ukiwadia, Chadema kitaamua ni nani mwenye sifa za kugombea urais huku akisema kina utaratibu wake wa kuwapata wagombea mbalimbali wa uongozi.

Hata hivyo, Zitto jana alikataa kuzungumzia suala hilo akisema: "Nimesikia hata mimi kwenye vyombo vya habari ila sina cha kuzungumza kuhusu hilo."

Mwenyekiti wa Taifa wa Baraza la Vijana wa Chadema (Bavicha), John Heche alisema kauli hiyo Mbowe siyo yake binafsi, bali ni ya wananchi.

"Ni kauli na maoni ya Watanzania wanaomwamini Dk Slaa kuwa anaweza kumudu kuliongoza taifa hili kama walivyoonyesha kwa kumpigia kura nyingi kuliko mgombea yeyote wa upinzani katika nafasi ya urais (mwaka 2010)," alisema Heche.

Heche alisema ingawa ndani ya Chadema kuna viongozi wengi wenye uwezo wa kuliongoza taifa, nyota ya Dk Slaa bado inang'ara.

Msimamo wa Heche uliungwa mkono na Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema ambaye alisema ni sahihi Dk Slaa kugombea urais mwaka 2015.

Lema alisema katika historia ya chaguzi za vyama vingi nchini, hakuna mgombea wa upinzani aliyewahi kupata kura nyingi kama Dk Slaa mwaka 2010 akadai kwamba ndiyo maana hivi sasa CCM kinafanya kila njama kumdhoofisha.

Lema alisema hatua ya kumtangaza Dk Slaa kuwa mgombea wa urais mwaka 2015, itaondoa harakati za chinichini zilizokuwa zikifanywa na watu ndani na nje ya Chadema kuwagombanisha viongozi wakuu wa chama hicho, hasa Mbowe na Dk Slaa.

Wanaopinga

Wakati Mtei akieleza kuwa Mbowe amepata Baraka za chama, Profesa Baregu alisema kutangazwa kwa jina la Dk Slaa kuwania urais ni maoni binafsi ya mwenyekiti huyo.

"Hayo ni maoni yake, lakini vikao vya chama ndivyo vyenye uamuzi wa mwisho kuteua jina la mgombea urais na havijakaa," alisema Profesa Baregu.

Alipoulizwa maoni yake kuhusu sababu za Mbowe kumtangaza mgombea urais sasa kabla ya wakati, Profesa Baregu alisema: "Mbowe atakuwa amefanya hivyo kwa sababu watu wengi walikuwa wanadhani kwamba yeye pia anawania nafasi hiyo ya urais."

"Hivyo ili kuweka mambo sawa ameamua kutangaza mapema kuwa hatawania urais na kwamba Dk Slaa ndiye anayefaa kuwania nafasi hiyo," alisema.

Profesa Baregu alisema haoni tatizo kwa wanachama wa Chadema kutangaza nia mapema kwa sababu hiyo ni haki yao kwa mujibu wa katiba... "Hata kama watu wengi watatangaza nia ya kuwania urais, siyo jambo baya katika ujenzi wa demokrasia, lakini uamuzi wa mwisho ni wa vikao vya chama."

Kauli ya Profesa Baregu kuhusu vikao iliungwa mkono na Dk Mkumbo ambaye alisema kwamba anachojua vikao vya chama ndivyo vyenye uamuzi wa mwisho kuhusu uteuzi wa wagombea wa ngazi ya urais.

Dk Mkumbo alionyesha shaka kama kweli Mbowe alimtaja Dk Slaa kuwa ndiye atakayewania nafasi hiyo akisisitiza: "Ninachofahamu ni kwamba yeye ametangaza kuwa hatagombea nafasi hiyo."
 
Nimerudia kusoma marambili mbili bado sijaona mgawanyiko wa mawazo.yote yanalenga kumoja! sioni tatizo.
 
Itakuwa imenunuliwa sijui!yaan kichwa cha habari haiakisi habari yenyewe!wapi vipande viwili hapo?
 
Ukisoma vyema kabisa utaona umakini wa wajumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA hao ambao kimantiki wanakubaliana na kauli ya Mwenyekiti ambaye alisema wazi kuwa kwa nafasi yake ataongoza vikao ili kusimamia chama kipate wagombea sahihi, huku akitilia mkazo kwenye nafasi ya urais kuwa ni nafasi nyeti ambayo chama kupitia vikao hakiwezi kuifanyia mzaha.
 
Nafikiri kwa mtazamo wa muandishi vipande viwili anavyo visema yeye ni kuonekana kuna wagombea 2. Yaani pande moja ni upande wa Zitto na pande lingine ni upande wa Slaa, jumla mapande mawili.

Sasa pa kujiuliza katika hayo mapande mawili yamegawa vipi chama na wanachadema hadi kuonekana chadema iko vipande?! Muandishi alitakiwa aonyesha bila chembe ya shaka kwenye hili.

Kwa kuwa ameonyesha obwe na matobo kwenye habari yake, kwangu naona mwandishi ameandika akiwa anafikiria sana mapande kuliko walaji watakavyo yapokea mapnde hayo na kuya-digest.
 
Sioni tatizo hapo, Mbona Zitto alipotangaza mara kibao kuwa anagombea urais kupitia Chama chake huku akijua wazi kabisa ndani na nje ya CHADEMA mgombea anayeungwa mkono na wengi ni Dr. Slaa, Gazeti maarufu linalompigia debe halikuandika kwamba CHADEMA sas ni vipande viwili? Kwa kuwa anaona ameguswa maslahi yake ndiyo ameelekeza Gazeti lake liandike maneno hayo?

Jamani kama ni wakati wa mtu kukubalika huwa hakuna kutumia nguvu wala ujanja ujanja!
 
Molemo Haya sasa Ngoma Inogile, Alilianzisha Zitto: Kama Zitto angeweza kutulia mpaka muda muafaka pengine haya yasingejitokeza. Dr. Slaa ni mjanja sana "Hajawahi na wala hakuna siku hata moja kaibuka na kusema anautaka urais au hautaki" including 2010 general elections when appointed by the party, he came out with the so called "A Great Probable Request kwa watanzania" wamuindorse kwanza ndipo afanye uamuzi. Hicho ndo kilichotokea.

The mistake which Zitto made lina implication zifuatazo kwa Zitto na CHADEMA:

1. Laweza kumcost kisiasa (atajikuta hana support kutoka kwa mtu yeyote wa maana in the party except wanaosikika kwa jina la masalia)

2. In case ikitokea (Kila anayehisi anataka kuwa rais akatamka hadharani kama yeye), siliamini sana hili, utakuwa mwanzo wa mkanganyiko kwa Watanzania juu ya CHADEMA.

3. Kila atakayetangaza anautaka urais at this time e.g Mnyika akitangaza, Lisu akitangaza, Mdee akitangaza, Sugu akitangaza, ndo utakuwa mwanza wa makundi hasimu ndani ya CHAMA, kwa sababu wanaomuona Zitto anfaa kuwa rais wataanza kuambatana na Zitto e.g Masalia, wanaoona Lisu nafaa n.k watamufuata. Hii itapunguza kasi ya kujenga chama kwa sabubu kila kundi litafanya kazi kivyake.

4. Kwa wale wanaofanya "the politics of anything goes", ndo wataanza kuibuka na sababu kwamba: Ni udini, Ukanda, tribalism, rangi, umimi, uyeye n.k. kama sababu kwa nini kapata au kakosa. Ni hatari sana kuwa na wanasiasa wanaokurupuka kuongea chochote wakati wowote kwa sababu tu za kulewa sifa au kulazimisha kutimiza jambo ambalo hata bila kulazimisha ni lazima litatimia kwa namna yake.

Note: Hata CCM wanaoonekana kuna makundi ya kuutaka Urais hakuna hata mmoja kati yao aliyetoka na kusema anautaka Urais BOLDLY, what they are playing is the so called "a Probable Request", Kusikia upepo unavumaje while waiting for the right time to make a formal announcement and follow party procedures.

Naomba kuwasilisha.
 
Last edited by a moderator:
Uandishi njaa at work, anataka kuuaminisha umma huku hana vigezo mwisho wa siku ni blah blah blah!!!!
 
Molemo Sijaona mahusiano ya mojakwamoja ya kichwa cha habari hii na ?maelezo yaliyotolewa Dr mwenyewe kasema wanachama wakiamua na si mwenyekiti akiamua haya kwa mtazamo wangu ni mawazo ya mwenyekiti. Ingekuwa upande wa piloi mawazo ya mwenyekiti ni amri lakini hukui CHADEMA hakuna kitu hicho.
 
Last edited by a moderator:
Kumbe ni maagizo ya Mtei.

Ningeshangaa kama usinge changia kwa kauli kama hii! Hebu nenda mbele zaidi na useme kwa kusadifu mizania. Zk nae alikuwa kwa maagizo ya nani?! Kabla kamati kuu haijapitisha mgombea weka kwenye mizani majina mawili uone la nani linamzidi mwenzake uzito halafu peleka ripoti Lumumba uone ukiwa una wakabidhi ripoti nyuso zao zitakuwaje.

Asubuhi njema! Naona wewe ndio umeingia kazini rasmi kama kawaida 24/7 baadae kidogo kaka.
 
Tatizo liko wapi hapo.

w umeuona huo mgawanyiko wa vipande viwili???
coz zzk hajasema lolote, mtei na heche wamekubaliana na kauli ya mwenyekt wao, huo mgawanyiko upo wapi??
mi nimelisoma nkabaki hata sielewi
 
Back
Top Bottom