UZUSHI Gazeti la "The Star": Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Kenya alihongwa ili kuipa zabuni kampuni ya Ugiriki

Baada ya tathmini, tumebaini kuwa taarifa hii ni ya uzushi
Gazeti la The Star limechapisha taarifa kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Kenya, Wafula Chebukati na wenzake walihongwa Dola Milioni 3 ( Takriban Tsh bilioni 7) ili kuwaba zabuni kampuni ya kigiriki kutengeneza karatasi za kupigia kura.

Ukweli wake upoje?

VDhQUcglBTz5e6DHAGFzWPRG49isOOtNW1ukR6VI.jpg
 
Tunachokijua
Agosti 17, 2022, taarifa ya Shirika la Polisi wa Kimataifa Interpol kutoa taarifa inayomuanika Mwenyekiti wa Tume Huru na Mipaka ya Uchaguzi Kenya (IEBC) Bwana Wafula Chebukati na makamishna wawili wa tume hiyo kuwa walipokea rushwa ya Dola Milioni Tatu za Kimarrekani ili kuidhinisha kampuni iyakayochapisha karatasi za kupigia kura kwenye Uchaguzi mkuu wa Kenya.

img-20220817-wa0002-jpg.2325908

Sehemu ya mbele ya gazeti la The Star inayodaiwa kutoa tuhuma hizo
Taarifa zilizovuma zilitumia picha iliyofanana na gazeti la Kenya la The Star, kuifanya taarifa hiyo kuonekana imechapishwa na gazeti hilo la Julai 7, 2022.

Gazeti hilo limetoa kauli kukanusha taarifa hiyo na kuthibitisha kuwa taarifa iliyowekwa kwenye tarehe husika haikuwa na Habari ya kuhusu Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Kenya.

1660803818610-png.2327128

Picha halisi ya gazeti hilo kabla haijahaririwa
Hivyo, JamiiForums imebaini kuwa taaarifa hiyo haina ukweli, imehaririwa na haijatolewa na Gazeti la The Star kama inavyodaiwa.

Interpol Shirika la Polisi wa Uhalifu wa Kimataifa ikiwa na wanachama 195, na husaidia polisi katika nchi hizo zote kufanya kazi pamoja ili kufanya ulimwengu kuwa mahali salama zaidi.

Ili kufanya hivyo, huziwezesha nchi wanachama kushiriki na kufikia data kuhusu uhalifu na wahalifu, na tunatoa usaidizi mbalimbali wa kiufundi na uendeshaji.
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom