Gavana wa BOT amemaliza muda wake au amestaafu?

Resilience

JF-Expert Member
Jan 4, 2023
792
3,812
Rais amemteua Gavana mpya Kwa taarifa kwamba aliyekuwepo amemaliza muda wake.

Lakini kiutumishi au kiutendaji kumaliza muda wako kwaweza maanisha kwamba bado ana umri wakuhudumu lakini mkataba wake BOT umeisha hivyo anarejea KAZI yake ya awali.

Au alishastaafu akaongezewa muda na kipindi alichoongezewa kimeisha? Au amestaafu rasmi?

Gavana wa sasa amestaafu au mkataba umeisha? Sheria inasemaje kuhusu ajira na kustaafu au kuondolewa ofisini kwa Gavana? Siyo kama CAG?
 
Mhe. Rais amemteua Gavana mpya Kwa taarifa kwamba aliyekuwepo amemaliza muda wake.

Lakini kiutumishi au kiutendaji kumaliza muda wako kwaweza maanisha kwamba bado ana umri wakuhudumu lakini mkataba wake BOT umeisha hivyo anarejea KAZI yake ya awali.

Au alishastaafu akaongezewa muda na kipindi alichoongezewa kimeisha

Au amestaafu rasmi.

Gavana wa sasa amestaafu au mkataba umeisha? Sheria inasemaje kuhusu ajira na kustaafu au kuondolewa ofisini kwa Gavana? Siyo kama CAG?
Muulize mhusika
 
Gavana umri wake kisheria usizidi miaka 65, pia anakaa madarakani kwa muda wa miaka 5 anaweza ongezewa muda wa miaka 5 mingine na haruhusiwi kuzidi hapo.
Na tar rasmi ya wao kuondoka kazini ni TAR 07/01

BALALI alikaa miaka 10 (08/0/1998 - 07/01/2008)

BENO NDULU alikaa miaka 10
(08/01/2008 - 07/01/2018)

PROF LUOGA amekaa miaka 5
(08/01/2018 - 07/01/2023)

Hii ni kutokana wakati anateuliwa UMRI WAKE ULIKUWA MIAKA 60 na hivyo haruhusiwi kuzidi miaka 65 KISHERIA
Labda awe umri wake wakati anateuliwa ulikuwa umesogea kiasi kwamba ataweza kumalizia muda akiwa amezidi miaka kadhaa. Na hii hutokea kama ni kwa awamu ya pili ya Uongozi wake.
NB. GAVANA HARUHUSIWI KUZIDI VIPINDI VIWILI VYA MIHULA YA MIAKA 5 KILA MMOJA.

GAVANA UMRI WAKE WA KUSTAAFU NI MIAKA 65 LABDA KWA DHARULA SANA KAMA ILIVYOTOKEA KWA BENO NDULU.
 
Umeshaambiwa amemaliza muda wake
Sheria ya benki kuu imesema Gavana wa benki kuu atashika Kwa kipindi Cha miaka mitano and "shall be eligible for reappointment " sheria hiyo ya benki kuu imeweka ulazima kwamba Gavana wa benki kuu atakuwa na haki ya kuongezewa muda wa awamu ya pili Ili kukamilisha vipindi viwili vya miaka mitano mitano
 
Gavana umri wake kisheria usizidi miaka 65, pia anakaa madarakani kwa muda wa miaka 5 anaweza ongezewa muda wa miaka 5 mingine na haruhusiwi kuzidi hapo.
Na tar rasmi ya wao kuondoka kazini ni TAR 07/01

BALALI alikaa miaka 10 (08/0/1998 - 07/01/2008)

BENO NDULU alikaa miaka 10
(08/01/2008 - 07/01/2018)

PROF LUOGA amekaa miaka 5
(08/01/2018 - 07/01/2023)

Hii ni kutokana wakati anateuliwa UMRI WAKE ULIKUWA MIAKA 60 na hivyo haruhusiwi kuzidi miaka 65 KIKATIBA.
Ibara Gani kwenye katiba?
 
8 Reactions
Reply
Back
Top Bottom