Gavana wa BOT amemaliza muda wake au amestaafu?

Naunga mkono hoja. Tuna wachumi na wataalamu wengi sana kustahili kuwa Gavana.

Hata Luoga sheria ilikuwa inamlinda kuendelea sijui nani kamshauri Rais amtoe.

Ukiangalia mustakabali wa usalama na maendeleo yetu kiuchumi na hata kimaendeleo huko mbeleni hizi teuzi za mama yetu zinatupa ukakasi sana
Ili jambo linatakiwa likemewe Magufuli alitaka kulipeleka mpaka jeshi la polisi. Yeye akifurahishwa na kazi ya mtu anaagiza apewe chao papo hapo, Ernest Mangu akamwambia huku tuna mafunzo na taratibu zetu atupandishi tuu watu vyeo.

Huyu mama anaendeleza hizi tabia. I can see kutaka mtu makini wa kumsaidia Mwigulu kazi wizara ya fedha, ila alikuwa hajui huyo katibu mkuu ampeleke wapi akaona BoT ndio mahala pake.
 
Benki Kuu, ndiyo taasisi inayoitegemewa kuandaa monetary and fiscal policies za nchi yoyote ,
-kwenye mtikisiko wa uchumi duniani uliosababishwa na ugonjwa wa Covid-19 na vita vya Urusi-Ukraine
- Gavana Ni vema akawa mbobezi kwenye masuala ya uchumi na fedha ili aweze kuongea lugha moja na mataifa na taasisi zingine za fedha na uchumi duniani kwenye masuala ya micro na macro economic policies .
-Mamlaka ya uteuzi inawezekana imezingia sifa hizo
-Siku za hivi karibuni Mamlaka za uteuzi zimekuwa zikiteua Gavana wa Benki Kuu kisiasa au kwa mtizamo kuwa ile Ni nafasi ya uongozi, siyo lazima awe mbobezi kwenye masuala ya uchumi na fedha,atasaidiwa na watalaam wa chini yake.
-Kama Gavana ni slow learner huwa kunakuwa na ombwe la kiutendaji kati ya Wasaidizi wake na Gavana.
-Kila la Heri Gavana mpya na kila Heri Gavana mstaafu,kuna maisha baada ya kustaafu

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
Only monetary policy.
Fiscal policy sio jukumu la central bank
 
Hujui sheria na ukieleweshwa na wanasheria unakuwa mbishi

Sheria ya Benki Kuu imesema ni lazima gavana apewe kipindi cha pili! Unadhani waliotunga hawakujua kuna suala la umri? Na pia Sheria ya utumishi wa Umma hakuna ilipoelezea umri wa kustaafu wa Gavana
Sheria ya utumishi wa umma haitaji umri wa kustaafu kwa vyeo,inataja kwa ujumla umri wa kustaafu wa watumishi wa umma ambao ni 60 years (last time i checked kuhusu umri)
Gavana naye ni mtumishi wa umma.
 
Gavana akiongea na wafanyakazi wizara mambo ya nje



Umahiri wa gavana Prof. Benno Ndulu akizungumzia mada mbalimbali kwa lugha nyepesi kwa wasio na uelewa mpana wa masuala ya uchumi n.k

Financial dollarization nchini Tanzania toka mwaka 1992 nchi ilipofunguka

Sababu ya watu kutoipenda sarafu / currency yao na threshold ya 30% ya matumizi ya fedha ya kigeni ina maana gani katika uchumi wa nchi

Transaction dollarization .... kuporomoka kwa thamani ya shilingi ndiyo kunafanya watu kukimbilia kwenye matumizi ya dola na siyo kinyume chake anasisitiza Prof. Benno Ndulu ...

Madhara ya kuweka fixed exchange rates kule Malawi n.k yalisababisha sarafu ya dola ya Kimarekani kupotea ... Rais Mzee Ali H. Mwinyi alipewa fungate ya kukuta kikapu kikiwa na dola chache benki kuu pia Zambia walijaribu kudhibiti kiwango cha thamani ya kubadilishana kwacha kwa dola, cha moto walikiona ... hivyo sera hii Prof. Benno Ndulu anasema ...

Utafiti wa bei za bidhaa na huduma kujua wafanyabiashara Tanzania wanapaga bei kwa kuzingatia sarafu ya dola ya marekani au shilingi? Utafiti wa BoT prof. Ndulu ulifanyika Dsm, Moro, Mwz, Arusha, Zanziba, Mjini Magharibi, Pemba Kaskazini na kusini na kubaini kuwa ... nchini Tanzania kote Bara na Zanzibar ... lakini maeneo ya Masaki, Mikocheni, Upanga

masuala ya hati fungani, sarafu ya dola ya marekani , mafuta gesi kilimo ...


Uchumi wa Marekani unaongoza uchumi wa dunia.....

Teknolojia ya Marekani kupata Gesi na mafuta kutoka katika mawe badala ya baharini au jangwani ...

Bidhaa za viwanda vya ndani lakini malighafi wanaagiza kwa dola ya marekani ...
 
Na yeye asubiri "Mama" atoke madarakani ndiyo aanze kulialia kama Prof Assad.
 
Back
Top Bottom