Gavana Prof. Ndulu: Benki wapo sahihi

Gavana Prof. Ndulu: Benki wapo sahihi

Prof. Ndulu yuko sahihi!
Nashukuru Sana prof amewaeleza watanzania waelewe, hapa sasa ndiyo mtawajua wabunge wetu kama wanapitisha vitu hivi vitakuwa na athari gani kwa wananchi, wabunge wetu hawafahamu haya mambo, pamoja kule bungeni Kuna wasomi lakini hawakusituka kuhusu hili.
Sharia ya VAT ndiyo inavyosema, wewe mtoza VAT unakuwa wakala wa kukusanya kodi kwa watu unaowahudumia, ndiyo ilivyo, sasa kama mabenki wameambiwa watoze VAT ni lazima waseme kwa bei ya huduma hii pamoja na VAT ni kiasi hiki, watanzania tusilalamike tuwalaumu wabunge wetu.
Mfano unakwenda kwa patel anakwambia TV hii bila VAT ni 600000/= pamoja na VAT ni 708000/= hivyo kwa huduma za miamala ya pesa ni lazima liwepo ongezeko la 18%.
Hapa sasa ndiyo tutaelewa kweli hawa wabunge wanawakilisha wananchi au wanakwenda bungeni kusema imepita makofi twatwatwatwa.......
 
Huyu gavana hana msaada wowote nchini..ndio maana BOT ina mauzauza kibao..atoke tu hizi nyakati zimemzidi uwezo.
Acha roho ya kichawi wewe mswahili akitimuliwa we utapata faida gani?
Kwa taarifa yako Gavanna wetu ni kichwa pia ni mzalendo na ndo mana Jpm kamuacha aendelee usikurupuke wewe
 
Nyie wa vyuoni mnakariri tu.mkija kazini ni kupiga dili na kutuharibia uchumi wetu.huyo wa Tra na yeye si ndo nyie?
wewe wa wapi sasa, ndio wale wavijiweni anayejua kupayuka ndio mshindi
 
Usiwasemee wabunge wa upinzani kwa kuwa walisusia kuwawakilisha wananchi kwa sababu "Ubinafsi" uliwatawala zaidi kuliko uaminifu wetu sisi tuliowapa tikiti ta kuingia mjengoni.

Swala la utata wa BOT na TRA kuhusu VAT, kwenye miamala ya simu na benki, tunalichangia kwa ushabiki wa mitazamo ya kisiasa, kichama, kuliko "jinsi inavyogusa" shughuli za kibenki na wateja wake.

Naamini Gavana wa BOT na Mkurugenzi Mkuu wa TRA, kama Watanzania, watatumia taaluma zao kisahihi kutafsiri hiyo VAT kwa usahihi.
Hapa ndio ninapo washangaa wasomi wetu,msomi anang'ang'ania vat inalipwa na mlaji sawa,sasa ufafanuzi umetoka hatakiwi kulipa mlaji ni hao watoa huduma hivi hapo kisicho eleweka ni nini,kosa ni kutumia hilo neno vat so change it wamekalia majungu tu kisicho eleweka hapo ni nini
 
ata jambo dogo kama hili at a mtoto wa form one anayesoma bookkeeping na commerce analielewa vizuri tu.
Tukubari tu hii wizara imeshakuwa ngumu.
ok, hapa naiona kama kuna double taxation kwa wafanyakazi
 
Maprofesa kama huyu wamejaa mtaani kwetu,wanaagua tu
 
TRA - How does VAT works?

Each registered person in the chain between the first supplier and the final purchaser or user is charged tax on taxable supplies made to him (input tax) and charges tax on taxable supplies made by him (output tax). He pays to the TRA the excess of output tax over input tax, or recovers the excess of input tax over output tax from the Authority. The broad effect of the scheme is that businesses are not affected by VAT except in so far as they are required to administer it, and the burden of the tax falls to the final consumer.

How does VAT works? Lugha, lugha, lugha....ni vigumu kuamini kwamba hiyo ni tovuti rasmi ya TRA! Ni heri ingetumika tu lugha yetu ya madafu...
 
Ndulu hajasoma/hajaielewa taarifa ya TRA.Amekurupuka. Kwanza huyu mtu ni jipu. Nashangaa mpaka leo hajatumbuliwa.
Wewe ndio watakiwa kujielimisha, au katafute wa kukuelimisha VAT ni kodi gani?
 
Tusiwe wavivu wa kupata taarifa sahihi mabenki yapo sahihi na prof yuko sahihi tatizo tuna wabunge wengi wa ccm uelewa wao wa mambo ni mdogo saaana hawasomi.Naomba watu waaome income tax practise notice number 05/2013 iliyotiwa sahihi tarehe 1/11/2013 inayozungumzia business income ndio utajua sasa wakuu wameamua kwa makusudi kupindisha sheria za nchi.

Na lazima tujue VAT as per international taxation laws mlipaji ni final consumer and not otherwise.kama tumeamua kuwa na ' VAT' ya definition ya kibongo kibongo well and good lakini is not health kwa elimu yetu watu wako vyuoni wanasoma hivi halafu in practices wanakuta vike its ridiculous and shame kwa watu walioshiriki kupitisha mambo ya hovyo kama haya
Sijui tunakuwa hatufikirii sawa sawa au ni makusudi tu. Hv opposition kutohudhuria Bunge la budget ni sahihi kweli? Tusipowaambia ukweli opposition kususia bunge la budget kuwa ni hasara kwa nchi hatutendi haki. hizi ni kelele za chura tu sasa! Wasishangae yanayoendelea
 
Sijui tunakuwa hatufikirii sawa sawa au ni makusudi tu. Hv opposition kutohudhuria Bunge la budget ni sahihi kweli? Tusipowaambia ukweli opposition kususia bunge la budget kuwa ni hasara kwa nchi hatutendi haki. hizi ni kelele za chura tu sasa! Wasishangae yanayoendelea

Kwani kiini cha wao kutohudhuria ni nini? Hivi kumbe ni busara kuangalia tulipoangukia na sio tulipojikwaa?

Tujiulize hivi nchi hii tuna wazee wenye hakima na busara? Mi binafsi nachelea kuamini kuwa uchama unameza hekima na busara za wazee wetu
 
Gazeti la Mwananchi: Wakati TRA ikiitaka BOT izichukulie hatua bank zilizotangaza kuongeza gharama za huduma za kibenk, BOT imesema mabenki yapo sawa!

Prof.Ndulu anasema mabenk watakuwa mawakala wa TRA tu katika kukusanya VAT lakini si walipaji,kwa hiyo hawezi kuwachukulia hatua.

Beno Ndulu ametolea mfano unapokua unauza duka unakuwa wakala tu wa TRA na sio mlipaji.....KUMEKUCHA

View attachment 362128

TRA jana na waandishi wa habari walipinga ongezeko hilo la gharama za kifedha kwa wananchi iliyofanywa na mabenki wakisema ni upotoshaji na kutaka BOT iwashughulikie

naona huu mtanange sasa umefika pazuri.....yule MBWA (BoT) anayeamrishwa na MTOTO WA BOSI (TRA) kuwakamata WEZI (mabenki na makampuni ya simu), yeye anaona wezi wako sahihi kuiba na kuondoka na mali ya BOSI (wananchi) wake. mwaka 2020 kitakuwa ni kipimo halisi kwa akili za BOSI kama bado ataendelea kumlea MFUGA MBWA (CCM) asiyekamata wezi au la. yetu macho!
 
Sijui tunakuwa hatufikirii sawa sawa au ni makusudi tu. Hv opposition kutohudhuria Bunge la budget ni sahihi kweli? Tusipowaambia ukweli opposition kususia bunge la budget kuwa ni hasara kwa nchi hatutendi haki. hizi ni kelele za chura tu sasa! Wasishangae yanayoendelea
ina maana OPPOSITION ndio WATETEZI pekee wa WANANCHI, lakini CCM wanatetea matumbo yao tu? kama ndivyo, kwanini wananchi mliwarudisha CCM bungeni kwa wingi kuliko opposition? hapa ndipo kuna tatizo...usitazame ulipoangukia bali tazama ulipojikwalia.
 
Wabunge wetu wapendwa waliipitisha bajeti kwa kishindo
 
ina maana OPPOSITION ndio WATETEZI pekee wa WANANCHI, lakini CCM wanatetea matumbo yao tu? kama ndivyo, kwanini wananchi mliwarudisha CCM bungeni kwa wingi kuliko opposition? hapa ndipo kuna tatizo...usitazame ulipoangukia bali tazama ulipojikwalia.
Ccm nao ni wtz wala tusiwadharau maana ndio walichaguliwa kwa wingi na ndio reflection ya wtz
 
Jamani hili linanipa taabu kidogo kulielewa. Ninaomba wajuzi wa masuala ya kodi waliomo humu wanijuze. VAT ni kodi ya ongezeko la thamani ambayo hulipwa na mlaji au mpokea huduma wa mwisho yaani last consumer. Mtoa huduma au muuzaji yeye ni wakala tu wa mamlaka ya mapato kukusanya na kuwasilisha TRA. Ili kuthibitisha kuwa amekusanya, wakala huyo hutoa risiti ya EFD kwa mlaji kama uthibitisho kuwa kodi hiyo imepokelewa kihalali na huyo mtoa Huduma Kwa niaba ya TRA. Hii taarifa ya Kamishna Mkuu wa TRA kuwa taasisi za fedha na kampuni za simu kuwa walikuwa wanakusanya kodi hiyo lakini walikuwa hawapeliki TRA inaacha maswali yasiyo na majibu. Kwanza, watoa huduma walitakiwa wawe wamesajiliwa na TRA kama mawakala wa kukusanya kodi hiyo na walitakiwa watoe risiti ya EFD kwa kila mteja na kwa kila muamala. Je, uelewa wangu huo ni sahihi? Kama ni sahihi je, ilikuwa hivyo? Pili, Kwa vyovyote ilivyo kama taasisi hizo zilikuwa zinakusanya na hazipeleki makusanyo hayo TRA, maana yake ni kuwa taasisi hizi zilikuwa zinaiba kodi hiyo tangu zilipoanza kutoa huduma hiyo. Na kama hivyo ndivyo, taasisi hizo zina wajibika kisheria kulipa limbikizo la makusanyo hayo tangu zilipoanza kukusanya. Tatu, tozo inayotozwa kwenye miamala ya fedha ni service charge ambayo kimsingi ni kama rejesho la gharama za kutoa huduma hiyo, hivyo watoa huduma hao wanatakiwa kulipa kodi ya mauzo yaani sales tax na baadae watalipa income tax baada ya kufunga hesabu za mwaka na kupata faida. Pia hulipa corporate tax (sina uhakika inayotozwa).

Ninavyoelewa mimi, ni sahihi kabisa taasisi za fedha kuwataka wateja wake kulipa 18% ya ile service charge ili ipelekwe TRA. Hapa ninaamini pia kuwa taasisi hizo zitatoa Risiti ya EFD kwa kila muala unaofanyika. Je, kwenye miamala ya kielektroniki hasa kwa njia ya simu mteja atapataje risiti yake?

Jambo jingine linalohitaji kuangaliwa kwa kina ni kuwa, mishahara wa wafanyakazi wote wa Serikali hupitishiwa benki kwa mujibu wa maagizo ya Serikali na siyo kwa matakwa ya wafanyakazi. Mishahara huo unakuwa umeshakatwa kodi zote za serikali kabla ya kupelekwa benki. Lakini mfanyakazi huyo anapotaka kutoa mishahara/fedha zake benki ama kwa njia ya simu au ATM, hutozwa tena kodi. Kodi hii ni mzigo mwingine usio lazima wa tija kwa mfanyakazi. Na sasa anatakiwa tena kulipia VAT gharama anazotozwa kwa kutoa fedha zake za mshahara zilizopelekwa benki bila hiyari yake. Hii ni sawasawe? Ni halali? Siyo uonevu? Gharama hizi za kutoa fedha za mshahara benki kwanini zisilipwe na mwajiri?

Serikali ilitazame suala hili upya maana hata punguzo la kodi ya PAYE lililotolewa na Serikali kuanzia Julai 2016 halitakuwa na manufaa yoyote kwa mfanyakazi.

Vyama vya wafanyakazi wanaliona hili? Wanachukua hatua gani? Kama hawajachukua hatua yoyote watakuwa na uhalali wa kuwa viongozi wa vyama vya wafanyakazi.

Ninaomba kujuzwa zaidi.
 
Back
Top Bottom