Gavana Prof. Ndulu: Benki wapo sahihi

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Aug 24, 2011
52,035
114,473
Gazeti la Mwananchi: Wakati TRA ikiitaka BOT izichukulie hatua bank zilizotangaza kuongeza gharama za huduma za kibenk, BOT imesema mabenki yapo sawa!

Prof.Ndulu anasema mabenk watakuwa mawakala wa TRA tu katika kukusanya VAT lakini si walipaji,kwa hiyo hawezi kuwachukulia hatua.

Beno Ndulu ametolea mfano unapokua unauza duka unakuwa wakala tu wa TRA na sio mlipaji.....KUMEKUCHA

image.jpeg


TRA jana na waandishi wa habari walipinga ongezeko hilo la gharama za kifedha kwa wananchi iliyofanywa na mabenki wakisema ni upotoshaji na kutaka BOT iwashughulikie
 
kitendo cha ile kodi kuiita VAT,Basi mzigo unaenda moja kwa moja kwa mlaji.Labda ibadilishwe jina na isiwe VAT.Profesa yuko sahihi.TATIZO HII NCHI KWA SASA MAAMUZI YA TULIOWAPA DHAMANA YANATOLEWA KWA HOFU YA KUTUMBULIWA.
Zamani walikuwa hawatozwi na walikuwa wanatukata.. Basi wangeacha kukata.. Au wanataka walipe na zile zote za nyum?
 
TRA KIDATA
BOT Prof Ben Ndulu
CCM Jpm
WIZARA Dr Mpango

Ina Maana Wananchi Sasa Ndiyo Habari Yetu Kwisha Kabisa Tutahangaika Mpaka Mwisho
Yaliyosemwa Bungeni Na Utekelezaji Ni Vitu Tofauti
Kuweka Pesa Hakuna Maana
KwakuwA Hayo Makato Yanamaliza Pesa Yote
 
Huyu gavana hana msaada wowote nchini..ndio maana BOT ina mauzauza kibao..atoke tu hizi nyakati zimemzidi uwezo.
Sasa ulitaka afiche ukweli? Unajuwa kwamba VAT inalipwa na mtumiaji/mlaji? VAT ilikuwa exempted kwenye bank services kama iivyo kuwa exempted kwenye hospital services. Sasa unapo exemptuwa unataka service provider alipie yeye kwa kupunguza gharama zake by 18%? Possible lakini serikali ilikuwa wakae pamoja na financial sectors kabla ya kutowa maamuzi
 
Zamani walikuwa hawatozwi na walikuwa wanatukata.. Basi wangeacha kukata.. Au wanataka walipe na zile zote za nyum?
Bank Charges Haziepukiki,ziwe na kodi ndani yake ama zisiwe na kodi ndani yake.Kumbuka Zile ni sehemu ya gharama unazotozwa kwa huduma unazopata za kibenki.Sasa kama Serikali yako haikuwa inatoza chochote kwenye charge hizo si kosa la Benki ama jukumu la benki kuiambia Serikali iwacharge.Na vyovyote vile,Tozo hiyo ikiitwa VAT basi automatically jukumu linakuwa kwa mlaji,na hata iwe excise duty nyingine,Mabenki yatatafuta namna ya kuongeza mzigo kwa wateja kwa kigezo cha kupanda kwa gharama za uendeshaji.
 
Kama vi VAT lazima mlaji wa mwisho ndio atailipa.

Kama ni makato si benki wanayalipia kodi kwenye jumla ya faida yao wanapokabidhi mahesabu kwa tra.

Najua makato katika huduma za kibenki ni sehemu ya mapato ya taasisi za fedha ambayo mwisho wa siku kodi yake hulipwa na hayo mabenki.

Haiwezekani mabenki yakalipa kodi mara mbili, alafu wao input Vat, itakua ni output tu sasa wao watadai refund kama hakuna imput vat?

Nadhani serikali ilichemka kwenye hili. Haya ndio matatizo ya kila kitu ndio bungeni bila kuwaza.
 
Hahahahaha jana nilijua tunaingizwa chaka na T. R. A

Tangu lini V. A. T akalipa mfanya biashara. V. A. T ni consumption tax.

Nchi ya miujiza hiii. Tangu lini kuwe na double standards kwamba bank ndo zilipe VAT ila biashara zingine mteja ndo alipishwe.

Yani tumefikia pabaya sana kama taasisi kubwa hivi za kuaminika zinapishana kauli hadharani.
 
Huyo prof naye hajui. TRA wamesema mabenki yalikuwa yakusanya bila kulipa. Sio new makato. Mwee

Alichokisema Prof. Ndulu Ni kweli, TRA wanaleta siasa.

Hiyo ni indirect tax (VAT) inayotozwa kwa mlaji moja kwa moja, iweje mabenki yalipe. Anayetakiwa kulipa ni mlaji wa mwisho ( Final consumer). Mabenki yanaisaidia tu serikali kukusanya.
 
Wangekutana kujadilii na kupata muafaka kabla ya kuutangazia umma ingekuwa safi sana kuliko hii aibu ya taasisi za umma zote ziko Dar hii aibu ya kubishana hadharani isingekuwepo. Ni kama Hamna coordination katika hii mipango na hatimaye inakuwa aibu na kusumbua wananchi bila sababu.
 
Tusiwe wavivu wa kupata taarifa sahihi mabenki yapo sahihi na prof yuko sahihi tatizo tuna wabunge wengi wa ccm uelewa wao wa mambo ni mdogo saaana hawasomi.Naomba watu waaome income tax practise notice number 05/2013 iliyotiwa sahihi tarehe 1/11/2013 inayozungumzia business income ndio utajua sasa wakuu wameamua kwa makusudi kupindisha sheria za nchi.

Na lazima tujue VAT as per international taxation laws mlipaji ni final consumer and not otherwise.kama tumeamua kuwa na ' VAT' ya definition ya kibongo kibongo well and good lakini is not health kwa elimu yetu watu wako vyuoni wanasoma hivi halafu in practices wanakuta vike its ridiculous and shame kwa watu walioshiriki kupitisha mambo ya hovyo kama haya
 
Back
Top Bottom