Kwani hiyo 1,000 nani kaitoa kama si mteja(consumer)?Hahahahaha jana nilijua tunaingizwa chaka na T. R. A
Tangu lini V. A. T akalipa mfanya biashara. V. A. T ni consumption tax.
Nchi ya miujiza hiii. Tangu lini kuwe na double standards kwamba bank ndo zilipe VAT ila biashara zingine mteja ndo alipishwe.
Yani tumefikia pabaya sana kama taasisi kubwa hivi za kuaminika zinapishana kauli hadharani.
Gazeti la Mwananchi: Wakati TRA ikiitaka BOT izichukulie hatua bank zilizotangaza kuongeza gharama za huduma za kibenk, BOT imesema mabenki yapo sawa!
Prof.Ndulu anasema mabenk watakuwa mawakala wa TRA tu katika kukusanya VAT lakini si walipaji,kwa hiyo hawezi kuwachukulia hatua.
Beno Ndulu ametolea mfano unapokua unauza duka unakuwa wakala tu wa TRA na sio mlipaji.....KUMEKUCHA
View attachment 362128
TRA jana na waandishi wa habari walipinga ongezeko hilo la gharama za kifedha kwa wananchi iliyofanywa na mabenki wakisema ni upotoshaji na kutaka BOT iwashughulikie
Hauko sahihi hata kidogo. Hakuna biashara yoyote inayoweza kuweka kodi ya bei kwenye bei zake haka hiyo bidhaa au huduma kisheria haitozwi VAT.
Wangekuwa wanafanya hivyo makampuni ya utalii yasingeilalamikia kodi ya VAT kwenye huduma za utalii.
WENYE AKAUNTI BENKI TULIPE TUU KODI YA SERIKALI BILA MANUNGUNIKO KWA MAENDELEO YA NCHI YETU
uko saw a bro ili dhana ya VAT iwe relevant selikalali ikae na taasisi za fedha ili wakubali kudeduct 18% ya tozo kwenye miamala, ili concept ya mlipaji VAT ibaki kwa last consumerSasa ulitaka afiche ukweli? Unajuwa kwamba VAT inalipwa na mtumiaji/mlaji? VAT ilikuwa exempted kwenye bank services kama iivyo kuwa exempted kwenye hospital services. Sasa unapo exemptuwa unataka service provider alipie yeye kwa kupunguza gharama zake by 18%? Possible lakini serikali ilikuwa wakae pamoja na financial sectors kabla ya kutowa maamuzi
Amefanikiwa kupata nafuu ya dhamiri yake kwa kusema ukwelilakini ,amesema ukweli
Mkuu ume nena ukweli mtupu, shida ni kwamba serikali imelemewa na deni kubwa la nje wakati karibia nusu ya makusanyo ya kodi yanaenda kwenye mshahara. Ukijumlisha na gharama nyingine kama umeme, mafuta ya kutumia kwenye mitambo ya serikali, maji gharama za simu nk unakuta govt inabaki na pesa kidogo6ya maendeleo lakini pia inakua kidogo kulipia madeni.
Pamoja na hayo serikali imeshindwa kubuni vyanzo vipya vya kodi na kushia kuwaumiza wafanyabiashara na wanachi wa kawaida bila kujua kwamba na yenyewe itakosa mapato in the long run.
Tutalimia meno.
ikitokea mabank yakanunua bidhaa au huduma kutoka kwa wafanyabiashara waliosajiliwa VAT,VAT itakayokusanywa na mabenk kwa mwezi itapungua, au hakuna kabisa, hivyo lengo LA TRA halitatimia, njia bora na sahihi ni kuzibana bank na taasisi za fedha ili selikali iweze kugawana nao mapato ya hii tozo ni kubadili sheria ya kodi ya mapato kutoka 30% hadi 48% nyongeza ya 18%, na kuhakikisha mabenki hayapandishi tozo ili kuwalinda wananchiKama vi VAT lazima mlaji wa mwisho ndio atailipa.
Kama ni makato si benki wanayalipia kodi kwenye jumla ya faida yao wanapokabidhi mahesabu kwa tra.
Najua makato katika huduma za kibenki ni sehemu ya mapato ya taasisi za fedha ambayo mwisho wa siku kodi yake hulipwa na hayo mabenki.
Haiwezekani mabenki yakalipa kodi mara mbili, alafu wao input Vat, itakua ni output tu sasa wao watadai refund kama hakuna imput vat?
Nadhani serikali ilichemka kwenye hili. Haya ndio matatizo ya kila kitu ndio bungeni bila kuwaza.
Walichokuwa wanatukata ni Bank charge na si VAT. kwakuwa VAT hulipiwa na mtumiaji wa mwisho, hawanabudi kutukata. Labda serikali ibadilishe jina la hii kodi, VAT ni zigo la mtumiaji wa mwisho.Zamani walikuwa hawatozwi na walikuwa wanatukata.. Basi wangeacha kukata.. Au wanataka walipe na zile zote za nyum?
Ukisikiliza mfano aliouto kamishna wa TRA ni kama vile kulikuwepo na kodi ambayo haikuwa inalipwa. Katoa mfano kwamba kama tozo lilikuwa 1000, na bank walikuwa wanachukua lote sasa itabidi tozo hilo hilo litozwe kodi ya 18% ambayo na kama sh 153 na sh 847 ndio ibaki bank. Ikiangalia vizuri huo mfano wake ni kwamba ile sh1000 iliyotozwa na bank tayari ina VAT ambayo ilikuwa hailipwi jambo ambalo sio kweli kwani kulikuwa na exemption kabla sheria kubadilishwa hivi karibuni. Kwenye hiyo 1000 TRA wanatakiwa wachukue 180 na sio 153. Na mteja ambaye hii kodi ya VAT ndiye hasa inamhusu atalipa 1180 badala ya 1000 ya awali ambayo ilikuwa imesamehewa VAT. Huo ndio ukweli nyingine ni porojo tu. VAT ni kodi ya mlaji wala sio ya mfanyabiashara.
Hujanielewa nilichoandika kwenye hilo bandiko; haya mabenki huwa wanaingiza hizi tozo za serikali kama gharama ya uzalishaji [ they factor them as costs] hivyo hulipwa na wateja wao!! Sasa kwavile ni tozo za serikali zinatakiwa zikusanywe na kuwasilishwa TRA lakini haikuwa inafanyika hivyo kwasababu ya uzembe wa TRA na BOT ambao ndio regulators who sanction these charges!! BOT walitakiwa waishauri serikali juu ya uwepo wa hizi fedha ili TRA ikusanye lakini badala yake walikuwa kimya mpaka hapo TRA walipozinduka kwenye bajeti ya mwaka huu na kuanza kuzidai kutoka kwa mabenki!!
Makampuni ya utalii yanalalamika kwa sababu yanalipa lakini mabenki yalikuwa yanakusanya lakini hayawasilishi na kwa mikisingi hii Ndullu anayaita mabenki wawakilishi wa TRA kwani wao walikuwa wanakusanya through bank charges.
ata jambo dogo kama hili at a mtoto wa form one anayesoma bookkeeping na commerce analielewa vizuri tu.Anaweza asijue awatumie wataalamu wa kodi wapo tra au chuo cha kodi,kodi inasomw saana na wahasibu
Siku hizi unafanyia kazi tawi gani vileProf. Ndulu yuko sahihi!
Na huo ndio UKWELI, yaani nimeshangaa magazeti ya leo yanasema VAT imepigwa marufuku. Yaani full ubabaishaji.Napata shida sana, pale wasomi nguli na wataalamu hawa wa mambo ya fedha wanapokwama kuelewa issue ndogo kama hii. Kwa upande wangu VAT hulipwa na mtumiaji wa mwisho
Kama sio new mbona wanakata sasa... mimi wamenikata VAT kwenye transaction za jana na leo.Huyo prof naye hajui. TRA wamesema mabenki yalikuwa yakusanya bila kulipa. Sio new makato. Mwee