Gavana Prof. Ndulu: Benki wapo sahihi

Gavana Prof. Ndulu: Benki wapo sahihi

Kama vi VAT lazima mlaji wa mwisho ndio atailipa.

Kama ni makato si benki wanayalipia kodi kwenye jumla ya faida yao wanapokabidhi mahesabu kwa tra.

Najua makato katika huduma za kibenki ni sehemu ya mapato ya taasisi za fedha ambayo mwisho wa siku kodi yake hulipwa na hayo mabenki.

Haiwezekani mabenki yakalipa kodi mara mbili, alafu wao input Vat, itakua ni output tu sasa wao watadai refund kama hakuna imput vat?

Nadhani serikali ilichemka kwenye hili. Haya ndio matatizo ya kila kitu ndio bungeni bila kuwaza.
Ninyi wote tatizo lenu ni kutaka kuvuna bila kupanda. Tangu lini value added tax ikatozwa kwenye hela? Tena ni hela ya mshahara au pensheni ya mtu iliyokatwa kodi kabla ya malipo! Hivi mamilioni waliyoficha ugaibuni wangekuwa wanakatwa vat wangefurahia kweli? Tusidanganyane lengo la kodi nchi hii ni kuwafilisi masikini tu! Beno nisikilize! Hii kodi inatozwa kwenye mapato ya benki yatokanayo na service charge, wewe unataka alipe "mlaji" eti kwakuwa inaitwa 'vat' tu? Ungeeleweka kama ungesema isiitwe 'vat' vinginevyo nia yako ni kukwepa kodi. Au ufute service charge kabisa kwasababu sisi wengine tunalazimishwa kupokea mishahara au vijipensheni vyetu kupitia vibenki vyenu ambako hatulipwi riba (interest) badala yake tunatozwa hiyo service charge! Huku ndiyo nasema ni kuvuna bila kupanda. Narudia: mshahara umeshakatwa kodi, halafu unanilazimisha nikaupate benki ili nitozwe service charge! Hii ni nini kama sio wendawazimu? Yule unyenilazimisha nimpelekee pesa yangu ndiye anayepaswa kunipa asante sio kuninyanyasa. Hebu nikuulize bwana BOT Gavana, Yale mamilioni ya epa na escro waliyogawana wakubwa angalau walilipa kodi yeyote? Tena baadhi yao wako bungeni wanapitisha sheria za kuwanyonya zaidi wanyonge wa nchi hii!
 
kodi inakusanywa na TRA Ndullu anachofanya ni kukwamisha ukusanyaji wa kodi anaihujumu sana serikali labda katumwa na Lowasa sina Imani kabisa na huyu gavana
hahaha. ..wewe hapo ndio zero brain
 
Prof Ndulu nafikiri anatakiwa aende tena chuo cha kodi walau akapate cheti ktk hii tasnia ili ajue kama mtu/taasisi ilikuwa haitozwi kiwi ktk huduma, inapoanza kutozwa haitakiwi kuhamisha burden kwa mlaji bali ni katika kiwango kile kile bila kuathiri kiasi kinatozwa kodi,, ninachokiona bank hawataki kupunguza mapato yao ndio maana wanaongeza hilo ongezeko, nafikiri serikali ina kila sababu ya kuchukua hatua na ikiwezakana hata huyu prof atoke tu ili waingie wengine yeye kashindwa kazi kwani TRA ndio kila kitu hata hiyo bot isipokuwepo kwani inategemea mapato ya tra ktk uwepo wake.
Jaribu kuwa objective kidogo kwenye haya mambo, usijaribu kusukumwa na utashi wako binafsi. Unaona sasa unafikia hatua ya kusema Prof. Ndullu aondoke tu! Kwanini iwe hivyo? Kwa sababu tu amekuwa na kauli usiyoipenda? Yeye alichofanya ni kueleza ukweli kuhusu implementation ya VAT, sasa wewe ulipaswa ufanye argument ukiangazia hilo, otherwise washauri tu serikali watafute namna nyingine ya kuhalalisha hiyo kodi, kama inawezekana, lakini siyo kupitia VAT!
 
Hii ni sirikali ya kazi tuu, kwani inaendeshwa vipi
 
Halafu nasikia mnalazimisha hata viduka vya vijijini vitowe risiti! Hivi kweli mtoto akienda dukani kununua peremende adai risiti? Kwanza huyo mwenye duka na mtoto wote pengine hawajui kusoma wala kuandika! Waende jela kwa risti tu? Kwani kuuza na kununua kunafanyika dukani tu? Vipi minadani na magulioni, kwenye vilabu vya pombe, baa, kanisani, misikitini, hospitali; mijini na vijijini, jamani ee! Kuuza na kununua sio uzalishaji, ni usambazaji wa bidhaa tu.
 
Huyo prof naye hajui. TRA wamesema mabenki yalikuwa yakusanya bila kulipa. Sio new makato. Mwee

Usipotoshe. Kuna baadhi ya huduma hazi chajiwi VAT kisheria. Sekta ya benki ilikuwa moja wapo. Sheria ya budget mwaka huu imeondoa exemption ya VAT kwa huduma za benki. Prof. Ndulu yuko sahihi. Hawawatu wamekurupuka tena na wameogopa outcry ya umma. Siku zote VAT hulipwa na mlaji na mfanya biashara ni wakala wa ukusanyaji tu. Wakitaka hivyo wassite ni VAT watafute jina jingine. benki na kampuni za simu hazitakubali huu mzigo watatafuta namna nyingine ya kumbebesha mtumiaji hiyo gharama. Tusifanyane watoto katika hilil.
 
mpaka leo nashangaa sana prof .Ndullu bado yuko ofisini...huyu anapingana sana na kauli za magufuli..anaikwamisha sana serikali bila shaka atakuwa mfuasi wa Lowasa
Hapa naona kuna ambao hawataki kujifunza. Wengi tumekuja na uelewa wetu ambao sio sahihi wachangiaji wanatuelemisha lakini bado tunashupaa, hii si sawa. Tumeingizwa chaka tukubali vinginevyo sheria ibadilishwe lakini kwa hii ya sasa haiwezekani. Prof. Ashikilie uzi wake ili wanasiasa waelewe walipoangukia. Hii ndio professionalism FULL STOP.
 
Hu
Hapa naona kuna ambao hawataki kujifunza. Wengi tumekuja na uelewa wetu ambao sio sahihi wachangiaji wanatuelemisha lakini bado tunashupaa, hii si sawa. Tumeingizwa chaka tukubali vinginevyo sheria ibadilishwe lakini kwa hii ya sasa haiwezekani. Prof. Ashikilie uzi wake ili wanasiasa waelewe walipoangukia. Hii ndio professionalism FULL STOP.
Kwa huo uprofessionalism wenu itabidi TRA nao walipe kodi kwa kodi wanayokusanya! Nilisema kwamba Sera zenu za kodi ni sawa na mtu anayetoa Pesa mfuko wa kushoto na kuzipeleka mfuko wa kulia halafu anajipongeza kwamba amevuna!
 
Ukweli ubaki kuwa ukweli hata kama unauma. Prof. yuko sahihi, mlaji wa mwisho (end user) ndio mlipaji wa VAT. Ktk hili tukubali kwamba watumiaji wa huduma za kibenki ndio tunabeba mzigo.
Si lazima tubebe mzigo. Serikali inaweza kubadili sheria na hiyo kodi ikalipwa bila kuitwa vat na bila kumuumiza mlaji. Taasisi za fedha zinapata super profit. Zinamkamua mwananchi bila huruma hata akikopa tu.
 
Duh....hawa TRA wamepatwa na nini? Taaluma yao wameweka pembeni? Ni vema siasa wakawaachia wanasiasa!

Kama serikali ilitaka kukusanya kodi kwenye miamala ya benki na simu, wangetumia sheria nyingine lakini sio sheria ya excise au VAT kwa sababu hizi mbili ni consumption tax na anayepaswa kubeba mzigo ni mlaji.

Prof Ndullu yupo sahihi na kwa kweli atatunza heshima yake zaidi akiendelea kusimama kwenye ukweli kama anvyofanya katika suala hili.
Nakubaliana na wewe. Jambo dogo tu sheria mpya iletwe hizo super profits za taasisi za fedha zikatwe kodi.
 
Nauliza hivi kwenye Salary Accounts ambazo zina misamaha ya charges.. sasa hivi inakuwaje?
 
Si lazima tubebe mzigo. Serikali inaweza kubadili sheria na hiyo kodi ikalipwa bila kuitwa vat na bila kumuumiza mlaji. Taasisi za fedha zinapata super profit. Zinamkamua mwananchi bila huruma hata akikopa tu.
Hiyo ya kubadili sheria I,Iowa mapema sana ni September. Kumbe UKAWA huwa eanaisaidia san serikali kufikiri
 
Japo ufahamu wangu siyo mkubwa saana ila kwako nimeelewa umeandika kuelimisha na si kushabikia
 
Zamani walikuwa hawatozwi na walikuwa wanatukata.. Basi wangeacha kukata.. Au wanataka walipe na zile zote za nyum?

Saint ivuga you better ask otherwise ho back to class....
hii ni taaluma mkuu na darasani inafundishwa... nilimshangaa mh. mpango na kidata... vipi wasimamizi hawa wa idara nyeti serikalin hasa phd holder mh mpango wanaongea anaongea uongo namna hii...
 
Nakubaliana na wewe. Jambo dogo tu sheria mpya iletwe hizo super profits za taasisi za fedha zikatwe kodi.

akseh if you dont know better ask.... wadhan hawakatwi kodi??? nmb year 2013 ivi ndo alikuwa mlipaji kodi bora....

pia wat d u mean kuwa wanapata supper profit??? umetafiti investment cost yao pia???? duh great thinker hawa kiboko
 
Tatzo watz wengi mnapenda namba lkn hamjui kuzisoma. Sasa acheni serikali ya sisiem iwasomeshe namba kwa lazma
 
Back
Top Bottom