Kama kuna nchi inahitaji msaada wa hali ya juu basi ni Tanzania.
Hii nchi inahitaji kuombewa sana kwa watu wanadini.
Pia nchi hii inahitaji msaada wa kuwezesha viongozi kutoa maamuzi yenye kuokoa Taifa.
Mijadala, Mifisadi, Matatizo yaliyopo yanaonesha kumulemea kiongozi mkubwa wa nchi.
Balali Pamoja na mbio zote za kujiokoa lakini siku hizi dunia ni kama ni ndogo mno.
Kujificha Marekani ni sawa na kufichama kwenye nyumba yeye kuta za vioo.
Kilitime,
Hili swala la mafisadi kamwe haliwezi kutuondoa ktk wajibu wetu kama litakubalika kuwa ni kinyume cha sheria na hatua kali zitachukuliwa kwa mwenye kuvunja sheria. tatizo la Bongo ni kwamba hawa mafisadi wanaonekana kama ni heroes ambao wameweza kupenya serikalini na kuiba mali za Umma kisha wakapewa immunity na serikali yenyewe.
Swala la kusema haya maswla yapo dunia nzima ni upoteshaji kwani hata Majambazi wapo dunia nzima, Ubakaji na kadhalika ni vitu ambavyo vipo lakini vimetungiwa sheria kuhakikisha kuwa binadamu tunakuwa na control fulani ya madhara haya. lakini tunaposimama hapa na kuyaona ni mambo ya kawaida basi kesho usije kuanza kulalamika kwa nini kila mwananchi anakimbilia siasa ukasahau kuwa hakuna mtu asiyependa Utajiri wa haraka na hasa mahala unapopewa immunity na serikali yenyewe.
South Africa, Kenya na kwingineko kote huwaweka hatiani wahalifu na mpango wa kubebana ndio huzua husda,fitna na kutoelewana matokeo yake sote tutasimama kuzalisha tukitamani kushika nafasi hizo za Utajri wa haraka.
Kumbuka tu kuwa sisi binadamu ni wanyama wenye hisia zote za kinyama isipokuwa tumepewa akili za kuweza kuchagua mabaya na mazuri. Sasa leo tukianza kuhalalisha mabaya na kuyatungia sheria za uhuru tokana na legal obligations, basi mjomba tumekwisha!
[B]
"Kama ilivyoelezwa kwenye taarifa hiyo, ripoti iliyopokelewa ilikuwa ni ripoti ya awali ambayo ilifanyiwa kazi na ofisi yangu na kurudishwa kwa wataalamu walioifanya kazi hii ili kukamilisha ripoti hii. Huu ni utaratibu wa kawaida wa kufanya kazi za ukaguzi hasa ikichukuliwa maanani kuwa Kampuni ya Ernst & Young, imefanya kazi hii kwa niaba yangu," alisema Bw, Utouh.
.
Mpiga zumari ndiye mchagua wimbo. Tulidhani ni ripoti huru ya uchunguzi ambayo imeagizwa na CAG kwa maana ya kuchukuliwa kama ilivyo kumbe ni ripoti nyingine ya CAG ambayo amemtuma EY kufanya kwa niaba yake! Ndio, ni utaratibu wa kawaida kwa mtu ukimpa kazi kama hiyo kwa niaba yako kuipitia. Na ni utaratibu huo huo unaoweza kumpa maelekezo, hiki weka hiki ondoa, hivi weka hivi ili ripoti iwe na sura hii kwa malengo haya. Sasa ni wakati wa utaaluma wa EY kuwekwa kwenye jaribio- je, watafanya kazi yao kitaaluma na kusimamia utaaluma hata kama anayewalipa ana matakwa tofauti au watakubaliana naye na kufunika kombe mwanaharamu apite? Kupelekwa ripoti ya awali mapema na kuchukua muda mrefu bila kurudishwa kwa ajili ya kutoa ripoti ya mwisho kuna maelezo matatu tu: Ama ofisi ya CAG ni wavivu wanafanya kazi taratibu, au EY ni wabovu walifanya kazi mbaya ambayo ilihitaji maelekezo na maelezo marefu kabla ya kuwarudishia kuleta ripoti ya mwisho au Ripoti ilikuwa na mambo ambayo hayapendezi mbele ya umma kwa hiyo ilibidi CAG atumie muda mrefu kutoa maelekezo ya kuipendezesha ripoti. Nasema hivi kwa kuwa ni CAG mwenyewe na serikali ndio walisema ripoti ingekamilika siku nyingi lakini yani yani zinaendelea mpaka hii leo. Njia pekee ni kuisaka kwa udi na uvumba ripoti origanal ya awali ya EY na kuiweka hadharani kabla au mara baada ya ripoti iliyohaririwa na serikali ya Kikwete ya CCM kuwekwa hadharani
JJ
Mpiga zumari ndiye mchagua wimbo.
JJ
unadhani ni Rahisi?Nachokijua ambacho Muungwana amewaagiza watu wa Usalama Wa taifa,document ambayo imeandikwa SIRI,basi mtu akiivujisha ajue anapoteza kazi na kushughulikiwa kwa sheria za nchi,kuna usiri mkubwa katika kupata ripoti za serikali hasa zilizonadikwa ni siri.
Watapoteza mara ngapi, mbona tayari imeshavuja na wakati muafaka ukifika itawekwa hapa. Kinachosubiriwa sasa hivi ni hiyo ambayo serikali itatoa ili zilinganishwe na kama itakuwa tofauti basi kuna mtu si tu atafukuzwa kazi bali pia atapelekwa mafia na kufia huko!
Mwafrika mke na wengine salaam za Noel toka Mwigobero Musoma . Naelekea kuvua samaki sasa . Napenda kuunga mkono kwamba hata mimi nimepata copy ya report siku kama 10 nyuma sasa nangoja kuona watasema nini . Hakuna cha siri watu wamechoka .Tunayo but we cannot pre empty tunangoja .