Voltaire
JF-Expert Member
- Sep 1, 2013
- 1,851
- 1,950
Wakuu,
Mpango wa kupiga kelele kwenye media ili wasisahaulike unaendeleahivi hawaoni walivyokuwa majinga? Ukiamua kumla chura hakikisha unachagua aliyenona, sasa unakula chura afu unachagua chenye kimedhoofu na utapia mlo, unamla, anakuua, inakuwa ni fezea
Wacha tuendelee kukinga maji yanayovuja tukaflashie chooni!
Pia soma Pre GE2025 - Ogopa Teknolojia na Mungu! Sasa ni rasmi G55 wametumwa kuifumuafumua CHADEMA mpaka isambaratike
Moshi wameanza kuunguruma
Meza kuu inajumuisha
- Makamu Mwenyekiti Halmashauri ya Moshi DC
- Mwenyekiti Mstaafu wa Halmashauri ya Moshi DC - Michael Kilawila
- Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake Kilimanjaro - Grace Kiwelu
- Katibu wa BAVICHA Kanda ya Kaskazini - Rachel Sadiki
- Mwenyekiti wa Mkoa wa Kilimanjaro - Gervas Mgonja
- Katibu wa Mkoa wa Kilimanjaro
Gervas Mgonja Mwenyekiti wa Mkoa wa Kilimanjaro
Mwenendo wa chama chetu hauridhishi, tuliokuwa tunamsapoti Mbowe tumekuwa hatuishi kwa amani ndani ya kipindi hiki. Najivua rasmi vyeo vyangu na uanachama wa CHADEMA kuanzia leo Mei 11, 2025.
Rachel Sadiki Mwanachadema & na Founder wa CHADEMA jimbo la Mkinga-Tanga
Nilipeleka harakati kwa mara ya kwanza CHADEMA, nilifanya kazi mpaka nikafukuzwa serikalini, nikafirisika. Tulishauri lakini tulichukuliwa kama wahalifu. Hatujapewa haki ya kujieleza wala kusikilizwa, suala la kuondolewa/kushughulikiwa kwetu lina baraka za chama, sioni mwanga huko tunapoenda. Ninajitoa uanachama wa CHADEMA na kujivua nyadhifa zilizonazo na kufanya shughuli nyingine kama alivyosema Mbowe
Wajikusanye wote kwa pamoja watangaze kutoka, wanatupigia kelele!
hivi hawaoni walivyokuwa majinga? Ukiamua kumla chura hakikisha unachagua aliyenona, sasa unakula chura afu unachagua chenye kimedhoofu na utapia mlo, unamla, anakuua, inakuwa ni fezea