PreGE2025 G55 Moshi na Temeke waondoka CHADEMA

PreGE2025 G55 Moshi na Temeke waondoka CHADEMA

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Wakiishaondoka wakaitumia tena hiyo nembo, nipo tayari kukuchangia pesa za kuweka Wakili Msomi uwafungulie kesi.
Waondoke mara 2? Hizi press zao zinawavuruga wajinga wa ccm, watu waelewa tunawachora tu. Wajinga wameshapungua siku hizi.
 
Hawawezi kufanya kimya kimya mpaka watupigie kettle, sisi ndiyo tuliwaambia wajiunge CHADEMA, kwa nini wakati wakijiunga hawakuita press? Hawa jamaa akili kisoda
Waacheni, msiwapangie.
 
Wakuu,

Mpango wa kupiga kelele kwenye media ili wasisahaulike unaendelea :KEKLaugh: hivi hawaoni walivyokuwa majinga? Ukiamua kumla chura hakikisha unachagua aliyenona, sasa unakula chura afu unachagua chenye kimedhoofu na utapia mlo, unamla, anakuua, inakuwa ni fezea:KEKLaugh::BearLaugh::BearLaugh:

Wacha tuendelee kukinga maji yanayovuja tukaflashie chooni!

Pia soma Pre GE2025 - Ogopa Teknolojia na Mungu! Sasa ni rasmi G55 wametumwa kuifumuafumua CHADEMA mpaka isambaratike

Moshi wameanza kuunguruma


Meza kuu inajumuisha
  • Makamu Mwenyekiti Halmashauri ya Moshi DC
  • Mwenyekiti Mstaafu wa Halmashauri ya Moshi DC - Michael Kilawila
  • Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake Kilimanjaro - Grace Kiwelu
  • Katibu wa BAVICHA Kanda ya Kaskazini - Rachel Sadiki
  • Mwenyekiti wa Mkoa wa Kilimanjaro - Gervas Mgonja
  • Katibu wa Mkoa wa Kilimanjaro

Gervas Mgonja Mwenyekiti wa Mkoa wa Kilimanjaro
Mwenendo wa chama chetu hauridhishi, tuliokuwa tunamsapoti Mbowe tumekuwa hatuishi kwa amani ndani ya kipindi hiki. Najivua rasmi vyeo vyangu na uanachama wa CHADEMA kuanzia leo Mei 11, 2025.

Rachel Sadiki Mwanachadema & na Founder wa CHADEMA jimbo la Mkinga-Tanga
Nilipeleka harakati kwa mara ya kwanza CHADEMA, nilifanya kazi mpaka nikafukuzwa serikalini, nikafirisika. Tulishauri lakini tulichukuliwa kama wahalifu. Hatujapewa haki ya kujieleza wala kusikilizwa, suala la kuondolewa/kushughulikiwa kwetu lina baraka za chama, sioni mwanga huko tunapoenda. Ninajitoa uanachama wa CHADEMA na kujivua nyadhifa zilizonazo na kufanya shughuli nyingine kama alivyosema Mbowe


Labda tuseme ukiongoza kwa muda mrefu mahali.Wale unawaongoza pamoja na wewe mnaweza mkajiona kama ni wamiliki wa taasis hiyo ya uma.Ukija uongozi mpya mnaanza kuulinganisha na uliopita bila kujua ni watu tofauti.kitakachotumika ni Miongozo ya Taasisi siyo personality.Lakini pia kiongozi mpya huwa lazima apange safu yake mpya hasa wale watakaomuelewa dhamira yake ndiyo wako likely kwenda naye.

Practically,ukianza kumlinganisha kiongozi wako na yule aliyepita ambaye alikuwa best yako, mwishowe utamchukia sana na yeye atakuchukia pia.

So Nadhani ukioata uongozi mpya jitahidi kumjua dhamira yake na aina ya uongozi wake.
 
Anaedharau kambi pinzani ndani ya Chadema huenda alikuwa mkimbizi wa muda mrefu kwamba hajui ambayo yanaendelea nchii hii. CUF ilikufa kwa sura hiyo..CUF has become history, almost no more. The same,kwa movement hii ya G55 Chadema is on the same path through which CUF took to it's total death. A matter of time. Anaebisha kuwa CCM ni GIANT muda utatuambia.
Kati ya wote wanaotangaza kuhama Chama nani ana influence kwa wanachama? Hapo Chadema ni watu wawili tu wanaweza kuyumbisha Chama; Mbowe na Tundu Lissu. Mbowe kwa hao wachumia tumbo ni kwa sababu ya utajiri wake, lakini amekwisha poteza mvuto baada ya kukaa muda mrefu madarakani. Lissu ana mvuto wa hoja na sera kwa hiyo ana mvuto mkubwa hasa kwa watu wa mikoa mingine ukiondoa Kilimanjaro na Arusha.

Hao usiwalinganishe na Mrema, Lowassa wala Seif. Kumbuka Membe alidhani ana mvuto kumbe CCM ndiyo iliyokuwa inambeba na hao wanaojivua magwanda wanabebwa na Chadema nje ya hapo ni takataka tu!
 
Inawezekana kuna mabilioni mengine wamepewa, maana tetesi toka Twitter mara ya mwisho kwenye uchaguzi wa ndani wa chadema isemekana kuna asali ya 12B iliingia chadema inawezekana hao g55 ndio walioilamba. Na sasa wamepewa dau jipya la mabilioni mengine 🤣🤣🤣


Subiria Huko Twitter na Dr Slaa watasema ni billioni ngapi wamepewa akina g55
Huu mwaka hela za udalali zitaenda kuwatokea watu puani kama kenge aliepigwa kichwani
 
Kwa hali hii, kama ingetokea 'kamanda wa anga' akashinda kiti cha Urais wa JMT, sidhani kama angeachia madaraka.

Fikiria tu huu ni uenyekiti wa chama ametoka na anaona ni bora chama kifie mbali kama yeye sio mwenyekiti.
 
Chadema atabaki Lisu na makamanda wa mitandaoni lkn Chadema kwasasa ndio imekuwa Chauma CUF ndio ACT kazi iyendelee ,, ACT imelikosa DODO kweupee!!!
 
Back
Top Bottom