PreGE2025 G55 Moshi na Temeke waondoka CHADEMA

PreGE2025 G55 Moshi na Temeke waondoka CHADEMA

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
ccm wanatumia nguvu kubwa kuibomoa chadema
wananunua wanachama wa chadema, wanatumia polisi, wasanii, waandishi wa habari

Uzuri watanzania wameamka, wanaelewa uchafu unaofanywa na chama tawala
We ni mpumbavu tangia utungiwe mimba, mfanye upumbavu wenu humo msingizie CCM. Hamwezi siasa nyie washamba. Watu wamejitoa kwa ridhaa yao maana Lissu ni kibaraka, hao ni wazalendo. Chadema ni marehemu subiri mazishi
 
Wakuu,

Mpango wa kupiga kelele kwenye media ili wasisahaulike unaendelea :KEKLaugh: hivi hawaoni walivyokuwa majinga? Ukiamua kumla chura hakikisha unachagua aliyenona, sasa unakula chura afu unachagua chenye kimedhoofu na utapia mlo, unamla, anakuua, inakuwa ni fezea:KEKLaugh::BearLaugh::BearLaugh:

Wacha tuendelee kukinga maji yanayovuja tukaflashie chooni!

Pia soma Pre GE2025 - Ogopa Teknolojia na Mungu! Sasa ni rasmi G55 wametumwa kuifumuafumua CHADEMA mpaka isambaratike

Moshi wameanza kuunguruma


Meza kuu inajumuisha
  • Makamu Mwenyekiti Halmashauri ya Moshi DC - Exaudi Wilson Mamuya
  • Mwenyekiti Mstaafu wa Halmashauri ya Moshi DC - Michael Kilawila
  • Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake Kilimanjaro - Grace Kiwelu
  • Katibu wa BAVICHA Kanda ya Kaskazini - Rachel Sadiki
  • Mwenyekiti wa Mkoa wa Kilimanjaro - Gervas Mgonja
  • Katibu wa Mkoa wa Kilimanjaro

Gervas Mgonja Mwenyekiti wa Mkoa wa Kilimanjaro
Mwenendo wa chama chetu hauridhishi, tuliokuwa tunamsapoti Mbowe tumekuwa hatuishi kwa amani ndani ya kipindi hiki. Najivua rasmi vyeo vyangu na uanachama wa CHADEMA kuanzia leo Mei 11, 2025.

Rachel Sadiki Mwanachadema & na Founder wa CHADEMA jimbo la Mkinga-Tanga
Nilipeleka harakati kwa mara ya kwanza CHADEMA, nilifanya kazi mpaka nikafukuzwa serikalini, nikafirisika. Tulishauri lakini tulichukuliwa kama wahalifu. Hatujapewa haki ya kujieleza wala kusikilizwa, suala la kuondolewa/kushughulikiwa kwetu lina baraka za chama, sioni mwanga huko tunapoenda. Ninajitoa uanachama wa CHADEMA na kujivua nyadhifa zilizonazo na kufanya shughuli nyingine kama alivyosema Mbowe

Grace Kiwelu Mwenyekiti BAWACHA Kilimanjaro, Mwenyekiti Kamati ya Fedha Kanda ya Kaskazini, Mjumbe Kamati Tendaji BAWACHA Taifa

Tulizunguka nchi nzima na Mbowe kuitangaza CHADEMA toka 1992, badala ya kuvuna heshima tunavuna matusi. Tunawezaje kuzuia uchaguzi bila kushiriki? Kusema wananchi waandamane, nikiwaangalia wananchi kule vunjo wataanzia wapi kuandamana? Viongozi wanaona matusi hawakemei, kosa ni kumuunga mkono Mbowe. Nilimuunga kweli Mbowe kwasababu niliona kazi aliyoifanya ya mageuzi ndani ya chama na nchini, bila Mbowe tusingekuwa na CHADEMA ambayo tunayo leo. Kuanzia leo Mei 11, ninajiondoa CHADEMA, ninakwenda nyumbani kupumzika, nakwenda kulea mjukuu wangu, nimechoka matusi ya mtandaoni.

Michael Kilawila Mwenyekiti Mstaafu wa Moshi DC, na Mwenyekiti wa Mkoa Awamu ya 3 Kilimanjaro

CHADEMA yenye upendo na mshikamano imeanza kupotea, chuki ilianza baada ya kutompendelea mtu mmoja ili achaguliwe kugombea ubunge jimbo la Korogwe mwaka 2020. Kuna mtu alikimbia na familia yake na kutuacha hapa akataka tumpokee kishujaa wakati yeye sio shujaa, mimi na Basil tukaanza kushughulikiwa. Nimeamua kuondoka na maamuzi yangu binafsi, nimeona CHADEMA sio mahali salama tena pa kuendelea kufanya siasa. Leo Mei 11, 2025 ninaachana na CHADEMA, ninaenda kupumzika, kadi yangu nitaitunza ili wajuu wangu waje waione wajifunze kwenye historia kwamba nilitukanwa sana. CCM wasinipigie simu, sitaenda CCM, hamtasikia kwamba nimeenda CCM lakini lazima nitafute chama ambacho naona kitafikia malengo yale ambayo wananchi wanataka.

Exaudi Wilson Mamuya Makamu Mwenyekiti wa Moshi DC
Nimekuwa mwananchama wa CHADEMA toka nikiwa na umri mdogo, nimekitumikia chama kwa wivu mkubwa na mapenzi mpaka sasa tumefika mahali naumia moyoni. Kwenye uchaguzi Mkuu sisi tulichagua kumuunga mkono Mbowe, tulipambana pamoja naye kipindi cha magufuli na tulisimama naye kwenye uchaguzi wa chama kwakuwa tulimuamini, lakini baada ya uchaguzi tumekuwa tukiishi kwa hali ngumu sana, tunaonekana waasi, tutakaa pembeni wao waendelee. Leo Mei 11, ninatangaza kuachana na chama, nitapumzika kwa kipindi hiki kifupi lakini sitaacha siasa. Najua timu ya G55 tuna ushawishi, tutakuwana na wananchi tutawashawishi na tutafanya siasa kupitia chombo kingine cha siasa.

Answari Kimaro Mjumbe wa Kamati ya TEHAMA Kanda ya Kaskazini
Mimi nilimuunga Odero, lakini sasa hivi kuna ugomvi kati ya pande mbili, hatuwezi kufika popote. Nina ushahidi, watu walipewa nafasi kwasababu wanamuunga Lissu mkono si sababu wanna sifa. Natangaza kuondoka CHADEMA na nnajivua vyeo vyangu vyote! Pia nawapa changamoto waende kwenye kata yangu pale, wakipata hata mtu mmoja wa CHADEMA Mungu afanye atakachopenda.


Wengine waliojivua uanachama ni pamoja na;

- Mwenyekiti wa Moshi Vijijini - Rose Masuruali
- Kumsapoti Mbowe siyo kosa - Nimejitoa CHADEMA, nitaenda kwenye chama kingine - si CCM

- Katibu wa Vunjo Joseph Mosha
- CHADEMA kulikuwa na jambo ninaloliamini, sasa hivi hakuna - Nimejitoa CHADEMA na najivua rasmi nafasi zote nilizokuwanazo, nitatafuta forum sahihi ya kwenda kuwasemea wananchi

- Katibu Same Mashariki - Magreth Mbwambo - Nimeihangaikia CHADEMA kwa hela, nguvu na jasho na hatukupata chochote. Zamani chama kilikuwa na upendo, sasa ni manyanyaso, nikipata sehemu ambako kuna mwanga nitaenda - Najiondoa CHADEMA

- Katibu Mwanga - Togolani Sinzira - Viongozi wa chama taifa wanakumbatia watu wanaotutukana, tutafakari pa kwenda lakini sio CCM - Najiondoa CHADEMA

- Katibu Same Magharibi - Haika Ngowi - Chama chetu kimekuwa cha wanaharakati na diaspora, hao ndio wanakishauri chama, hakuna tena upendo, chama kimekuwa cha matusi - Nimejitoa CHADEMA, na kujivua vyeo vyote, naenda kutafakari niangalie pa kuelekea lakini sio CCM

- Katibu wa Jimbo la Same Mashariki
- Nimehangaikia chama sana lakini matokeo yamekuwa haya, wakati natumikia chama nilishaletewa bahasha na chama tawala, nikaikataa, kwahiyo sitegemei kurudi huko, sina mpango na CCM, wale niliokuwa nawaongoza tutafute mwelekeo mpya. Ilinipa uchungu kutosaini uchaguzi halafu baadaye wanakwambia tutaangalia namna, hiyo namna ni ipi? - Nimejivua uanachama CHADEMA

Wawakilishi wa Manispaa ya Moshi (G55) kwa niaba ya wengine, Halmashauri ya Moshi na Vunjo (G55) Jasmine Minja, Pius Mrema, Haika Letuu, Lilian Kimei, Vicky Massawe Mwenyekiti BAWACHA Moshi DC sitaenda CCM, Fredy Shayo Katibu BAZECHA na Mweka Hazina nasubiri G55 iniambie inaenda wapi ili nami niingie, Jabir Weta - Tunaondoka CHADEMA sababu ya ubaguzi kisa tulimsapoti Mbowe, walitakiwa kumpa tuzo Mbowe na si tuzo ya matusi

G55 Temeke


Meza kuu inajumuisha;

Mwenyekiti CHADEMA Mkoa wa Temeke - Herman Kiloloma najivua uanachama wangu CHADEMA pamoja na wenzangu kwasababu tumeona hatuko salama ndani ya chama chetu toka uongozi mpya upatikane, tunabaguliwa. Sababu nyingine ni ajenda ya chama kutoshiriki uchaguzi - mimi binafsi nilibaguliwa na Heche, watu 80 tuliokuwa nao hapa na wenyewe wanaondoka CHADEMA. Waliobaki tunawaheshimu na tunaowaacha waheshimu pia uamuzi wetu, tusishambuliwe na maneno. Tutawaita waandishi tutakapotaka kwenda kujiunga na chama kingine

Mwenyekiti Mstaafu Jimbo la Temeke Idi Mahuta

Mratibu wa BAWACHA Mkoa wa Temeke - Yvonne Haule
- Kokote utakapopita najulikana kama mama wa CHADEMA kwa uchungu sana, nawatakia wote wanaotaka kunifuata tunawakaribisha tutakapoenda- najivua uanachama CHADEMA

Mwenyekiti wa Kata ya Makangalawe - Josephine Mwenda - Najivua uananachama mimi na baadhi ya wananchi wangu amabo wananifuata.

Mwenyekiti wa Wilaya ya Temeke - Hamza Kinyema - Tumejitolea sana kwenye chama lakini sasa hivi kuna visa na visasi, kama sisi tunabaguliwa itakuaje kwa wananchi? Tunatukanwa sana kwenye magroup, nimezima simu siingii kabisa kwenye magroup sababu ya matusi. Tutashawishi na wananchi kwenye kwenye chama ambacho tutaelekea. Waandishi wa habari nahitaji kipindi maalum ili tuweze kuzungumzia mambo kwa undani - najivua uanachama wa CHADEMA,

Lissu ni motoooo, kaikomboa chadema....
 
Waende vyama vingine, kama wana mvuto tuone kama watafuatwa kama Maalim Seif alipohama CUF. Tena hao te Mbowe ndio walichangia kuifanya cdm ionekane ni chama cha wachaga.
Nasikia wanakwenda kula ubwabwa wa bure eti
 
Badala ya kuvuna heshima tunavuma matusi - Grace Kiwelo, mwenyekiti wa Chadema mkoa wa kilimanjaro :pedroP:
Nimefurahi Sana huyu dada kujitoa, Kila mwaka alikuwa anataka nafasi ya viti maalumu eti chama ni Chao, lissu ameikomboa chadema
 
Wanastahili kuheshimiwa maamuzi Yao.
Lissu alidhani kujenga chama kupayuka uzushi tu na kutoa vitisho. Siasa inahitaji uvumilivu na sacrifice sometimes
 
  • Thanks
Reactions: Tui
Leo watamsema nani? Jana ilikuwa zamu ya Lema. Sasa yule malaya Emma alikuwa mweka hazina wa kaskazini alikuja dar kufanya press na leo kule kwao viongozi wenzake wanafanya press. Au wanakutana kimafungu kutokana na mafungu ya mgao wa Abdul? Kila kundi na fungu lake?
Hawa watu wako 55 tuu mbona wengi na hawaishi?
 
  • Kicheko
Reactions: Tui
Nasikia wanakwenda kula ubwabwa wa bure eti
Hakuna mwenye mvuto nje ya cdm, ndio maana wameaga lakini hawakai kimya kila siku ni press ili waharibu haiba ya cdm kwa umma. Maalim Seif aliondoka CUF, aliitisha press moja tu akaondoka na wafuasi karibia wote. Mbona hatukuona press za kila wiki watu kuhama CUF?

Wote waliohama wanajirembulisha ili uongozi wa cdm uwaite waelewane, kisha wapenyeze hoja walizotumwa na ccm. Wanajua hivyo vyama vingine watakavyokwenda havina mvuto, na wao hawana mvuto.
 
Mbowe nilikuwa namheshimu. Napoteza imani nae kwa speed sana. Kama kweli yuko nyuma ya hawa mitu,atajishushia heshima sana. Bahati mbaya inaonyesha ni wote wa moshi na Arusha hawa mitu,ndicho kinachoaminisha kuna Mbowe nyuma yao
Muda utasema, G55 malengo yalikuwa zaidi ya kutoa Nia bali UASI ndani ya chama.Hivi ukitoa ushauri ndani ya chama ukikataliwa unahama chama? Hili kundi halikuwa na Nia njema kwenye chama
 
Wengi wao wakishutumu kuchoshwa na matusi na ubaguzi dhidi yao wameamua kujiondoa chadema.
Ni viongozi tu wanahama, ila wafuasi bado tupo sana na chama. Hao ndio walichangia cdm kuonekana ni chama cha wachaga, sasa chama hikiko mikononi mwa mchaga wanahama! Wamechelewa kuhama, maana sasa hivi NRNE imeshika kasi ya ajabu, wao waendelee na hizo press kwa hongo za ccm, lakini baada ya muda watatulia kama alivyotulia Msigwa baada ya kutumika kama kondom.
 
Akifanya Heche unazielewa?
Shida ni ipi yeye ni nani na hao G55 ni akina nani? Kwan kipindi mbowe akiwa mwenyekitu wa chama hawa wakina Heche na tundulissu walileta maneno yoyote,si walimuachia atekeleze majukumu yake na walimuunga mkono. Kwann all of a sudden tokea mbowe atolewe kwenye kitu yanaibuka makundi ya kipuuzi puuzi na demand za kibinafsi wakitaka wasikilizwe wao kwanza kama akina nani sasa katika chama?

Yaani wapuuzi wachache wajipe umuhimu na sauti ya mwisho kwenye chama ili iweje? Acheni kusapoti mambo ya kipumbavu,sapotini katiba ya chama na mwenyekiti aliyepo sasa sio huyo "Mbowe" wenu utadhani yeye ndie nani sasa hapo kwenye chama?
 
Back
Top Bottom