Netanyahu
Senior Member
- Oct 2, 2008
- 147
- 22
Mzee thanks so much about the info maana I have heard so many sickening stories about these people with them being associated with devil worshipping.
There are so many things about religion that is too hard to understand.The Catholics with Opus Dei and so many other stories about Mary Magdalene and Jesus are among some very contradicting things!
Nadhani kumwita mtu devil worshipper si sahihi kwa wataalamu wa demokrasia.
Lugha sahihi ni kumwita mtu asiyeabudu Mungu unayemwabudu wewe.Sababu huyo anayeabudu devil kwake huyo devil ndiye Mungu na huyo wako kwake ni devil.
Mfano mimi ni mpagani na nimebobea kwenye upagani.Kulikuwa na mjadala mkali wakishindana wapagani na wakristo AMSTERDAM ambapo wapagani waabudu shetani waliambiwa kuwa mbinguni kuna mwanga wakawakatalia wakristo wakawataka wakristo wawathibitishie. Wakristo walihangaika sana kUTHIBITISHA.Ilipofika zamu ya wapagani wakasema wanaamini mbinguni kuna giza kwa sababu hakuna moto uwakao ila jehanamu kuna mwanga kwa sababu kuna moto uwakao katika ziwa la moto milele na milele na penye moto hapakosi mwanga.Wapagani wakasema hawako tayari kukaa mbinguni kwenye giza.
Huo ni mfano mdogo wa kukuonyesha tu kuwa unayemwona wewe anaabudu shetani kwake yeye anaona anaabudu Mungu.Hivyo ni vizuri kusema mtu asiyeabudu Mungu unayeabudu wewe.Badala ya kutumia lugha kali za kuita watu ma-devil worshipper
Ndiyo maana katiba za nchi zimetoa uhuru wa kuabudu.Hazisemi uhuru wa kuabudu Mungu la hasha zinaishia kusema tu mtu ana uhuru wa kuabudu.Kitu gani anaabudu kama ni Mungu,shetani au kenge hilo si suala la serikali,katiba ya nchi,bunge au mahakama.Anachoabudu mtu hakitajwi katika katiba ni siri yake.Mtu yuko huru kujiabudu,kuabudu mavi yake akitaka au hata kumtangaza hawara yake kuwa ni mungu asitahiliye kuabudiwa.Ndio maana kitendo cha kuingiza Mungu wa Waislamu au wakristo atambuliwe katika katiba hakikubaliki.Katiba inabidi iishie tu kusema mtu ana uhuru binafsi wa kuabudu.
Hata wimbo wa taifa unaimbwa Mungu ibariki afrika.Ni mungu gani huyo? Kwa mwabudu mavi atakuwa anaimba akimaanisha mungu mavi,kwa devil worshipper akiimba mungu atakuwa akimaanisha Shetani ambaye ndiye mungu wake,Kwa mwislamu akiimba atakuwa akimaanisha Allah,Kwa mkristo akiimba anamanisha Yehova n.k Kwa yule aabuduye mbwa akiimba atakuwa akiimba akitaja Mungu anamaanisha mbwa wake anayemwabudu. Kwa hiyo kila mtu akiimba wimbo wa taifa Mungu amtajaye ni yule amjuaye yeye.
Waliotunga wimbo wa Taifa ni watu wenye akili mno.Wataalamu wa demokrasia waliobobea ambao walijua kila mtu wa kila dini waweza ungana kuimba wimbo mmoja wakiwa na imani tofauti kila mmoja akimtaja Mungu wake bila kugombana waimbapo huo wimbo.
Ni ushauri tu usimwite mtu devil worshipper mwite mtu asiyeabudu Mungu umwaduye wewe.Sababu huyo shetani kumbuka kwake ni mungu wake.
kuhusu swala la kujiunga na free masons si rahisi.Kuna viingilio na annual fees ambazo kwa mtanzania wa kawaida si rahisi kuingia.Kuna secret society moja marekani niliambiwa annual membership subscription yake kwa mwaka ni dola 100,000 kwa hesabu za haraka ni kama shilingi milioni 120 za Tanzania.Watanzania wangapi waweza jiunga.
Hata free masons si rahisi kuingia.Zina gharama kubwa watanzania wengi hawawezi kujiunga nazo ni wachache sana waweza kuingia.Ni matajiri wakubwa na wenye nazo ndio wanaweza.Free Masons si sehemu ya akina yahe wanaotafuta kuganga njaa baada ya kupigika na maisha.
Secret society hazihangaiki kutafuta waumini kama makanisa na misikiti wahangaikavyo.Hawana njaa ya wafuasi ndio maana hawajitangazi wala kuzurura huko na huko kusaka wafuasi.