Freeman Mbowe: Tunaanzisha wiki ya Maandamano kwenye Makao Makuu yote ya Mikoa nchi nzima

Atawachoka tu na yeye huyo ‘bi-tozo’ ipe muda. Hawanaga ushawishi zaidi ya maandamano, ayakuzuiwa burebure huko nyuma. Lakini pia hii si serikali ya kufanya kazi labda ndio maana awaoni tatizo.

Halafu CDM wanadhani watu wote wana (idle time) kama viongozi wao. Ni kama vile jeshi la polisi halina shuguli zingine za ulinzi zaidi ya kulinda maandamano ya CHADEMA na kufunga barabara ku entertain utoto wao. Na vyama vingine vikianza maandamano ya mtindo huu itakuwaje.

Ipe muda, akili zao zitakaa sawa huko serikalini kwenye hizi entertainment wanazotoa kwa jina la demokrasia

Only in Tanzania
 
Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe amesema chama hicho kitaingia kwenye awamu nyingine ya Maandamano yatakayofanyika kwenye makao makuu yote ya mikoa nchini...
Mnaacha kuhamasisha watu wakafanye kazi mnahamasisha waandamane? Samia anawafanyia mzaha sana.
 
Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe amesema chama hicho kitaingia kwenye awamu nyingine ya Maandamano yatakayofanyika kwenye makao makuu yote ya mikoa nchini, maarufu kama wiki ya Maandamano yatakayofanyika kuanzia Aprili 22-30, 2024.

Aidha, amewatangazia Diaspora kufanya maandamano makubwa kwenye miji mikubwa Duniani kupeleka Ujumbe duniani juu ya mambo yanayoendelea nchini.

Kamati kuu ya Chama hicho imepanga wiki hiyo ili kuwapa nafasi waumini wa dini zote kumaliza mfungo wao.
Hivi Yale maandamano yaliyofanyika Dar hayakupeleka ujumbe? Ujumbe uliotumwa kwa KM UN haukufanyiwa kazi?

Maandamano makubwa ya Mbeya na Arusha pia hayakuwa na impact?

Ama kweli ukimchekea Mbwa atakufuata hadi msikitini. Kwamba tuache kufanya kazi tuwe tunaandamana tu!? Mtatulipa posho kama mnavyojilipa?

Hovyo kabisa
 
Hao nyumbu hawana kazi za kufanya. Zito mtoto mdogo ameshaachia ngazi huyo makengeza anahangaika na maandamano. Ni mbinafsi sana.
Mimi mwenyewe nashangaa sana! Demokrasia niliyoiona ACT Wazalendo ni ya hali ya juu sana! Ila cha kushangaza huyu mzee wa Kishumundu a.k.a Makengeza daily yuko pale na hataki kutoka! Ujinga ujinga wa maandamano ni kutafuta huruma kwa wananchi!
 
Sema CHADEMA nao wanazingua, bora wakaze kwenye mikutano sio maandamano, hapa watakuwa wanawapa maneno wananchi kisema ndio mana JPM aliwazuia
 
wiki ya maandamano itafanyika katika makao makuu ya mikoa yote nchi nzima yatakayoanza tarehe 22 hadi 30 April 2024
 
Kwa sasa maandamano yenu yataegemea hoja ipi baada ya umeme na sukari kuanza kupatikana?

Au mtajitika katika swala la hayati mzee Mwinyi kuzikiwa Zanzibar badala ya kwao Mkuranga?
Kwa akili yako matatizo ya nchi hii ni Umeme na Sukari tuu ?! Kwa akili yako inavyo waza ?!
 
Kwa sasa maandamano yenu yataegemea hoja ipi baada ya umeme na sukari kuanza kupatikana?

Au mtajitika katika swala la hayati mzee Mwinyi kuzikiwa Zanzibar badala ya kwao Mkuranga?
Hii ya kushikia bango Mwinyi kuzikiwa Zanzibar badala ya Mkuranga kwa kweli inachekesha sana.

Yani mpaka najiuliza hawa hawa ndio watakuja kudai katiba mpya? Au hawa tofauti?
 
Hii ya kushikia bango Mwinyi kuzikiwa Zanzibar badala ya Mkuranga kwa kweli inachekesha sana.

Yani mpaka najiuliza hawa hawa ndio watakuja kudai katiba mpya? Au hawa tofauti?
Hao ndio wanasiasa wetu wa bongo, kukimbizana na matukio ili watrend mitandaoni kama kina Mwijaku, baba levo nk.

Swala la kudai katiba hawana umuhimu nalo. Lenye umuhimu kwao ni hilo la Mwinyi kuzikwa Mkuranga, au kung'ang'ania katika msiba wa Lowasa kuwa hakutajwa kuwa aliwahi kujiunga upinzani nk.
 
To be fair lakini hakuna kiongozi wa CHADEMA wa kitaifa aliyelishikia bango hilo, hao vi watu wa mitandaoni tu.

Viongozi kama Mbowe na Tundu Lissu wamekuwa very gracious.
 
Back
Top Bottom