bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
14,259
2,000
26 May 2021
Nairobi, Kenya

MAHOJIANO EXCLUSIVE NA MWANASIASA FREEMAN MBOWE TOKA TANZANIAMaureen Medza akimkaribisha ktk mahojiano exclusive yaliyofanyika kupitia chombo cha media ya Mwanzo TV nchini Kenya akiongea na Freeman Mbowe .​

Anazungumzia hali ya kisiasa iliyopo nchini Tanzania baada Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kuchukua hatamu za kiuongozi toka kwa Hayati rais John Pombe Joseph Magufuli .

Mwenyekiti Freeman Aikaeli Mbowe afafanua kuhusu Haki, Uhuru na Maendeleo ya Watu pamoja na demokrasia ni miongoni mwa mambo mengi chombo hiki cha habari cha Kenya kilitaka ufafanuzi.

Freeman Mbowe agusia sera za biashara na kiuchumi ikiwemo kurejesha urali (balance of trade) baina ya Intercontinental trade ya nchi za Africa na dunia ni kubwa kuliko baina ya nchi za kiafrica .

Freeman Mbowe anataka kuona maroli yanayokwenda baina ya nchi za kiafrica yawe mengi kama yale yaendayo bandari za Mombasa au Dar es Salaam kupeleka biashara Ulaya na Asia .

Tanzania inapaswa kujiondoa ktk sera ya utengefu kikanda pia kimataifa na kuja na uwazi kwa kujongea kurejesha mahusiano mazuri ya kimataifa na diplomasia ya kiuchumi .

Chanzo: mwanzo tv

N.B

Mtanzania tunayeweza kumpatia cheo cha heshima kama Professor wa Siasa, Freeman Aikaeli Mbowe mwenyekiti wa chama cha CHADEMA nchini Tanzania
 
Kinuju

JF-Expert Member
Mar 20, 2021
2,384
2,000
Chadema imemfia kutoka wabunge 100 hadi 1!!!

Sasa hivi yuko bize kutetea wachaga ,tuone kama hao wachaga watampeleka Ikulu.
 
Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
91,357
2,000
Chadema imemfia kutoka wabunge 100 hadi 1!!!

Sasa hivi yuko bize kutetea wachaga ,tuone kama hao wachaga watampeleka Ikulu.
Angalia picha hii kwa makini

FB_IMG_1589397986327.jpg
 
bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
14,259
2,000
Huyu ni mjasiriasiasa

Wapi umeona kiongozi wa juu wa CCM akipata exclusive interview nje ya Tanzania.

Hii inaashiria CCM ni wajasiriasiasa kupitia vyombo vya dola kiasi hakuna anayetaka kufanya interview hata na wale waliokuwa kina Humphrey Polepole au Dr. Bashiru Ally Kakurwa.

Kwani viongozi wa CCM hawana ushawishi nje ya siasa kandamizi za dola .
Ukiwauliza biashara za kuvuka mipaka hakuna kiongozi pale Makao Makuu ya CCM Dodoma au Ofisi Ndogo mtaa wa Lumumba Dar es Salaam anaweza kuzielezea kwa ufasaha mguso wake kiuchumi, kibiashara na ktk maendeleo ya watu na nchi kwa ujumla wake.
 
Niza doyi

JF-Expert Member
Dec 10, 2019
2,337
2,000
Eti gwiji huyu gwiji wa ruzuku.
alizunguka na chopa kila mwaka wa uchaguzi na kuambulia sijui wabunge wawili tu.
Gwiji w la siasa Slaa alipoingia nchi ikatikisika.
Alipotoka Slaa na Lowassa sasa amerudia hali yake ya siku zote,mbunge mmoja.
Anacho subiri sasa mtu mmoja ameguke CCM aungane naye chapa kipate wabunge.
wadanganyeni mazezete wenu.
 
ielewemitaa

JF-Expert Member
Jan 7, 2014
5,482

Hili neno Gwiji siku hizi halina heshima kabisaa
 
bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
14,259
2,000
Hili neno Gwiji siku hizi halina heshima kabisaa

Legend / Legendary mtu-tajwa wa sifa za muda mrefu katika siasa za vyama vingi Mh. Mwenyekiti Freeman Aikaeli Mbowe wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA ambaye chama dola kimeshindwa kumyumbisha.
 
ielewemitaa

JF-Expert Member
Jan 7, 2014
5,482
2,000
Legend / Legendary mtu-tajwa wa sifa za muda mrefu katika siasa za vyama vingi Mh. Mwenyekiti Freeman Aikaeli Mbowe wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA ambaye chama dola kimeshindwa kumyumbisha.
Ayumbishwe mara ngapi wakati kabaki na mbunge mmoja tu kama wadawa, alikuwa ana muogopa JPM mpaka akakimbilia nje huko halafu unasema chama dola kimeshindwa? au ujamsikia kwenye hotuba yake baada ya JPM kufa akilia Lia na Jiwe
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom