Game Theory
Platinum Member
- Sep 5, 2006
- 8,545
- 835
Oloronyo
Binafsi ninamfahamu Franco - naweza kusema kwamba ni rafiki yangu - muda mrefu sana. Niliporejea nyumbani mwaka 1992 baada ya kuishi ulaya muda mrefu, yeye, pamoja na rafiki yetu mwingine, Nicas, ndio waliokuwa wenyeji wangu, nisimsahau Baraka. Walinionesha njia. Pita hapa, usipite pale. Ongea na huyu, usiongee na yule.
Nilisikitika kwa yote yaliyomkuta, kwani hujui lini yatakukuta, hujui maisha yatakubadilikia kwa namna gani. Hata kama alikuwa "mlevi mbwa", huwezi kujua ni nini haswa kilitokea mpaka akawa hali hile. Nina HAKIKA hakupenda hali ile, lakini wewe hujawahi kupata MSONGO wa MAWAZO (mental depression). Utaiona dunia chungu, utatamani ardhi ipasuke dunia ikumeze! Utakimbilia kwenye pombe na anasa, lakini hazitakusaidia.
Usitumie "kuharibikiwa" kwa binadam mwenzako kama njia ya kujisafisha mwenyewe. Binafsi mimi nakuona kwamba una tatizo la "inferiority complex". Watu wenye hali hiyo hawajioni kama "wametimia" mpaka wapate nafasi ya kumbeza mtu mwingine. JIAMINI kaka, kwamba wewe ni wewe, na downfall ya mtu mwingine isiwe chanzo cha wewe KUONEKANA kwamba nawe umo. JIAMINI kwa jinsi ulivyo, nasi tutakuona kwamba UMO. Lakini ukitumia UWANDA HUU MPANA kumchafua ndugu yetu Franco Mtui, tutakupondaponda kwa mawe, viboko, matofali, ufe kama kibaka anayekamatwa kule Sokoni Kariakoo, akijaribu kumpora mama mhangaikaji vijisenti vyake.
Unadiriki kusema kwamba Franco alijiona yeye yuko juu? Unamfahamu kweli ama unaropoka tu?
Ficha upumbavu wako, onesha hekima zako! - Invisible
Usitukane wakunga, na uzazi ungalipo.
./Mwana wa Haki
Pole sana ndugu yangu Franco (aka Pinocchio!). Mola atakuafu mapema!
duh! mashikaji zako walikuwa akina NIcas? Duh! haya bwana
baraka unayemzingumzia ni yupi BIG RON au PISHI?