Franco Mtui apooza mwili mzima

ahh nilikuwa napata tabu ya watoto wa kishua kumbe mpo

haya na wewe magazines ulikuwa unanunua wapi?

Mimi nilikuwa napata kutoka kwa Victor Mollel na Eric Mwenda...

Oooh na Francis pia...jamaa alikuwaga anakuja kutoka Nyamwezi....nakumbuka aliniletea Air Jordans
 
Mimi nilikuwa napata kutoka kwa Victor Mollel na Eric Mwenda...

Oooh na Francis pia...jamaa alikuwaga anakuja kutoka Nyamwezi....nakumbuka aliniletea Air Jordans

mhhh yale yale ya kudrop names

MOLLEL
MWENDA

hivi hukuwahi kununua magazines kwa Khery SALAMANDER?
 
Oooh kumbe ni watoto wa Ostabei...ndio maana nimeambulia kapa...hivi huko Ostabei bado kuna oneka mali kwa standards za kibongo? Mimi nakuona kuchafukuchafu na kukuukuu...nyumba zimejengwa karne ya 19..aaaagh
Mzee yaonyesha ulitimka kitambo enzi za O'bay ya karne ya 19!. Ukirudi utastaajabu, ndizo wameuziwa waheshimiwa watumishi wa umma watiifu kwa bei za sadakalawe, sasa ndio zimekarabatiwa kwa migao ya vijisenti na fungu kubwa la ufisadi. Ukirudi, utashuhudia...

Franco apone na kurudia enzi yake.
 
Lalasheee! Habari za kusikitisha nimezisoma kwa yule Nanhii wa Tegeta kuwa yule Will Smith wa wetu enzi zile 1990-2000 Bw.Franco Mtui amepooza mwili wake mzima alipopata ajali ya "kuangukia shimoni shambani kwake" na kwa sasa amelazwa hospitali ya Netcare Rehabilitation Centre J'burg.
Francis Mtui aka Franco alikuwa kijana mtanashati na pia sana enzi hizo za miaka ya mwisho ya mzee Ruksa ambapo wakati huo alikuwa anauza magari,alifunga pingu za maisha na Perece Kirigiti mwishoni mwa miaka ya 90 ambapo ilifuatiwa na reception ya kukata na mundu kama sio shoka iliyofanyika katika viwanja vya pale ilipo Multichoice Dar,ndoa yao iliyojaliwa kupata mtoto mmoja,iliingia doa na wawili hao walitengana mwanzoni wa miaka ya 2000 na hiyo kupelekea Franco aliyewahi kumiliki Bar ya kwanza ya aina yake ya kukesha usiku ya AQUA pale Msasani na pia Video library ya Aqua pamoja na watoto wa Kida,kuwa mlevi mbwa,na hivyo kumfanya awe anakunywa mpaka pombe za kienyeji nk
Mara kwa mara alikuwa anaokotwa amelala pembeni ya barabara na siku za karibuni alipotea katika hadhara hadi Mkuu wa nanhii alipomuweka katika Blog yake,kwa kuwa kule kwa mkuu wa wilaya ya nanhii anabania maoni,nikaona nilete habari hapa.
Wito wangu kwa hawa Macelebs wetu wa bongo wawe makini katika maisha haya ya sasa wakati huo wakumbuke sana baadaye kwani mambo yanaweza kuwaharibikia. Hospitali hiyo pia amelazwa Mzee wetu Timoty Apiyo na Mwandishi Athumani Hamisi.
Tunamtakia kila la heri Bw.Francis Franco Mtui apone haraka na amkumbuke muumba wake.
Habari uliyoitoa ni muhimu sana. Nimesikitika sana kusikia kuwa Franco Mtui anaumwa kiasi hicho. Ni siku nyingi tangu nionane nae kwa mara ya mwisho. Ila imenisikitisha sana.

Ila ndugu yangu, unapokuwa unatoa report za namna hiyo usiweke umbeya. Unachotakiwa ni ku-stick kwenye details za tatizo unalotaka kulitolea maelezo na si vinginevyo. Kumbuka hapa JF kuna kila aina ya watu, na kila mtu ana mawazo yake. Kama nia yako ilikuwa ni kukebehi kuumwa kwa Franco, basi ungeweka hivyo kwenye kichwa cha thread yako, na wadau wa kebehi za namna hiyo wangejumuika nawe kufanya hivyo (kama uongozi wa JF hautajali). Japokuwa sioni kama hilo ni jambo lenye tija kwa yeyote.

Mimi namuombea Franco apone haraka na zaidi aweze kurudi kwenye shughuli zake kama awali na awe mtu ambae wote tulikuwa tukim-admire kama awali.
 
Jamani Deo na Edwin Mtui wako wapi? sijawahi kuwasikia tena
Deo Mtui yupo hapo kwenye picha inayomuonyesha Franco akiwa hospitali. Mwingine kwenye picha hiyo ni M. Michuzi.

Deo yupo sana mjini Dar. Nadhani anajishughulisha na shughuli zake. Huwa nakutana nae sana Mkwepu street.
 
Ni mmoja wa wanafamilia wa Mzee Mtui, Baba alikuwa mtumishi wa umma akiishi O'Bay. Vijana watatu hawa Franco ndiye mkubwa akifuatiwa na Deo na mdogo wa alikuwa DJ Maarufu Fresh XE. I'm not sure na mdogo wao mwingine tena.

Mkuu niruhusu niweke infor zako fresh kidogo tu. Frank ni mdogo kwa akina Deo na Edwin Mtui. Wanae kaka yao mkubwa zaidi. Baada ya Frank kuna dada yao (simfahamu jina). Sina uhakika kama kuna wadogo zaidi ya huyo mdogo wao wa kike. Kama atakuwepo, basi alikuwa mdogo sana wakati huo.

Hivyo Frank ni mdogo kwa wanaume.
 
Mzee yaonyesha ulitimka kitambo enzi za O'bay ya karne ya 19!. Ukirudi utastaajabu, ndizo wameuziwa waheshimiwa watumishi wa umma watiifu kwa bei za sadakalawe, sasa ndio zimekarabatiwa kwa migao ya vijisenti na fungu kubwa la ufisadi. Ukirudi, utashuhudia...

Franco apone na kurudia enzi yake.
Yeah, ila bado kuna baadhi ya nyumba ambazo bado ziko choka mbaya. Inawezekana waliouziwa hawakuwa na uwezo mkubwa kama wenzao walioweza kuzikarabati na kuzifanya ziwe nzuri zaidi.

Zaidi ya hali ya utulivu ilioendelea kuwepo kule hadi leo, O'bay si eneo unaloweza kusema ni zuri kuliko sehemu nyingine Dar. Sehemu kama Mikocheni na Mbezi Beach. Ila bado iko poa tu.
 
Mzee yaonyesha ulitimka kitambo enzi za O'bay ya karne ya 19!. Ukirudi utastaajabu, ndizo wameuziwa waheshimiwa watumishi wa umma watiifu kwa bei za sadakalawe, sasa ndio zimekarabatiwa kwa migao ya vijisenti na fungu kubwa la ufisadi. Ukirudi, utashuhudia...

Franco apone na kurudia enzi yake.

Hivi ALI OKI yuko wapi?

what about ISLAM BARAFAA?
 
Sijaelewaa huyu ni nanii kwao wapiii

Dinazarde huyo ni kijana wa zamani mjasiriamali ambaye alifahamika sana hasa katika burudani ya muziki kwani mbali ya kuwa DJ alikuwa na Club maarufu pale Kimweri Rd Msasani ikiitwa Aqua. Juu ya yote hayo hakuwa na maringo kabisa
 
Back
Top Bottom