Franco Mtui apooza mwili mzima | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Franco Mtui apooza mwili mzima

Discussion in 'Celebrities Forum' started by Oloronyo, Jun 17, 2009.

 1. Oloronyo

  Oloronyo Member

  #1
  Jun 17, 2009
  Joined: Mar 29, 2009
  Messages: 80
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Lalasheee! Habari za kusikitisha nimezisoma kwa yule Nanhii wa Tegeta kuwa yule Will Smith wa wetu enzi zile 1990-2000 Bw.Franco Mtui amepooza mwili wake mzima alipopata ajali ya "kuangukia shimoni shambani kwake" na kwa sasa amelazwa hospitali ya Netcare Rehabilitation Centre J'burg.
  Francis Mtui aka Franco alikuwa kijana mtanashati na pia sana enzi hizo za miaka ya mwisho ya mzee Ruksa ambapo wakati huo alikuwa anauza magari,alifunga pingu za maisha na Perece Kirigiti mwishoni mwa miaka ya 90 ambapo ilifuatiwa na reception ya kukata na mundu kama sio shoka iliyofanyika katika viwanja vya pale ilipo Multichoice Dar,ndoa yao iliyojaliwa kupata mtoto mmoja,iliingia doa na wawili hao walitengana mwanzoni wa miaka ya 2000 na hiyo kupelekea Franco aliyewahi kumiliki Bar ya kwanza ya aina yake ya kukesha usiku ya AQUA pale Msasani na pia Video library ya Aqua pamoja na watoto wa Kida,kuwa mlevi mbwa,na hivyo kumfanya awe anakunywa mpaka pombe za kienyeji nk
  Mara kwa mara alikuwa anaokotwa amelala pembeni ya barabara na siku za karibuni alipotea katika hadhara hadi Mkuu wa nanhii alipomuweka katika Blog yake,kwa kuwa kule kwa mkuu wa wilaya ya nanhii anabania maoni,nikaona nilete habari hapa.
  Wito wangu kwa hawa Macelebs wetu wa bongo wawe makini katika maisha haya ya sasa wakati huo wakumbuke sana baadaye kwani mambo yanaweza kuwaharibikia. Hospitali hiyo pia amelazwa Mzee wetu Timoty Apiyo na Mwandishi Athumani Hamisi.
  Tunamtakia kila la heri Bw.Francis Franco Mtui apone haraka na amkumbuke muumba wake.
   

  Attached Files:

 2. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #2
  Jun 17, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Unashangilia au unatoa taarifa?
   
 3. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #3
  Jun 17, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Hizi habari za "ulevi mbwa" and all ni lazima katika thread ya kutoa taarifa za ugonjwa? No wonder Mkuu Kibs anashangaa whether unashangilia au unatoa taarifa.
   
 4. K

  Kyachakiche JF-Expert Member

  #4
  Jun 17, 2009
  Joined: Feb 16, 2009
  Messages: 911
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 45
  Imekaa kama kaumbea umbeya fulani hivi! Inatuhusu nini sisi hii? Ipeleke kwa origino komedi banaaaa.
   
 5. Oloronyo

  Oloronyo Member

  #5
  Jun 17, 2009
  Joined: Mar 29, 2009
  Messages: 80
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Natoa taarifa na kuonya wale wote wanodhani wapo juu haswa viongozi wa chama cha majambazi (Period)
   
 6. Mavere

  Mavere Member

  #6
  Jun 17, 2009
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 7
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huyu naona anashangilia... shame on you!!!! we mwenzako amelazwa, yu mahututi, unatuletea habari za ndani za maisha yake.... itusaidie nini sisi??? Kila mtu ana shida zake hata wewe una zako..... so acha unafiki, fanya kazi!! Bora hata yeye alithubutu ku invest... wewe kazi kupika majungu!
   
 7. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #7
  Jun 17, 2009
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  nakumbuka ile video library ilikuwa inasaidia saidia...si ile iko pale namanga karibu na saluni ya Caro Nyimbo?
   
 8. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #8
  Jun 17, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Hicho Chama kipo hapa JF? Una tatizo la wivu au una chuki binafsi na huyo Franco?

  Try to be open with you're presentention...
   
 9. Oloronyo

  Oloronyo Member

  #9
  Jun 17, 2009
  Joined: Mar 29, 2009
  Messages: 80
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Sina chuki Binafsi ila katika uwanja huu mpana wa JF ningeulizwa Franco ni nani kuwa Celebrity na kadhalika hivyo nikaona sio vibaya kuweka intro ndogo nikisema ndogo namaanisha ndogo,pia onyo kwa watoto wote wa mafisadi wanaodhani kuwa wapo juu!
   
 10. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #10
  Jun 17, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Una contacts za Caro?
   
 11. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #11
  Jun 17, 2009
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  ahhh wala sina ila nasikia alikwenda Europe sema ile frame yake paleNamanga imetulia sana
   
 12. M

  Mbalamwezi JF-Expert Member

  #12
  Jun 17, 2009
  Joined: Sep 30, 2007
  Messages: 803
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 45
  Uandishi wa aina huu unafanana sana na ule wa "yellow journalism," magazeti ya udaku. Ushabiki mtupu, hakuna mpangilio, na wala huwezi kujua anatoa taarifa gani, hata kutangaza mpira huwezi kutangaza hovyo namna hiyo.
   
 13. K

  Kyachakiche JF-Expert Member

  #13
  Jun 17, 2009
  Joined: Feb 16, 2009
  Messages: 911
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 45
  Kumbe wewe unafikiri umepangilia vizuri! Hongera kwa kuwa mtangazaji mzuri wa mpira. Kama wewe ni msomaji wa magazeti ya udaku lazima utashabikia mada za udaku kama hizi. Soma michango ya wengine wenye mitazamo chanya hapo juu na wewe tujue uko upande upi.
   
 14. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #14
  Jun 17, 2009
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,001
  Trophy Points: 280
  sasa huwo ugonjwa alioupata kwa kuanguka shimoni shambani kwake, inahusiana nini na mambo ya personal affair za mtu, yeye kwani ni wa kwanza kuoa na kuacha, ulevi wake mbwa unahusiana nini na maradhi aliyonayo,
  kama ulikuwa na ugomvi na jamaa basi we fanya sherehe yako kimya kimya bila kuwashirikisha wengine
  yaani blogu zingine hawapokei mambo ya upumbavu kama huu, ukaona hapa JF ni jalala la kupokea ujinga,
   
 15. N-handsome

  N-handsome JF-Expert Member

  #15
  Jun 17, 2009
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,317
  Likes Received: 128
  Trophy Points: 160
  Oloronyo, sikujui hunijui lakini huna ubinaadamu kabisaaaa, the guy is a vegitable now wewe unatuhabarisha about his past, zitatusaidia nini na yeye zinamsaidia vipi? Usimtukane Mamba ilihali hujavuka mto kaka.
   
 16. Oloronyo

  Oloronyo Member

  #16
  Jun 17, 2009
  Joined: Mar 29, 2009
  Messages: 80
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Habari ndo hiyo! Hapo sijaenda zaidi haswa kwenye ule mtandao wa tiGO! Yaliyotokea Mwananyamala,rejea mtundiko wangu wa awali. Watoto wa mafisadi na wanaoshirikiana nao wataumbuka tu!!!
   
 17. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #17
  Jun 17, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Mkuu unamaanisha Franco ni mmoja wa watoto wa mafisadi?
  FYI marehemu baba yake mzazi alikuwa mtu mwadilifu sana hadi anafariki na wenye kumfahamu na najua wako wengi tu hapa JF wataniunga mkono kwa hili.,
  Hii ni ajali kama nyingine.Leo ni Franco kesho hujui kama itakuwa wewe au mimi..ni suala la wakati tu!
  Tumuombee apate nafuu na apone haraka.
   
 18. Oloronyo

  Oloronyo Member

  #18
  Jun 17, 2009
  Joined: Mar 29, 2009
  Messages: 80
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Franco aliyewahi kumiliki Bar ya kwanza ya aina yake ya kukesha usiku ya AQUA pale Msasani na pia Video library ya Aqua pamoja na watoto wa Kida WOS umesahau kuhusu UFI?
   
 19. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #19
  Jun 17, 2009
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  sasa Morani, utawala wa Mzee Kida kiwanda cha UFI na ajali ya Franco Mtui inahusiana vipi bana? ...
   
 20. Mwawado

  Mwawado JF-Expert Member

  #20
  Jun 17, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 998
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 35
  Huu uhuru wa kujieleza tunajua haswa kuutumia!
  wakatabahu.....
   
Loading...