Pole sana Mkuu!
USHAURI WANGU
1. Muulize anapenda nini.
Katika maelezo yake kama unashindwa kumuelewa anapenda nini basi fanya yafuatayo.
2. Mpeleke shule aanzie na masomo ya Form III kwa mwaka huu na mwakani apige NECTA. Dhumuni la kuanza Kidato cha 3 ni kujipanga zaidi, na Kidato cha ndani ndo msingi mzuri wa kufanya vema kidato cha 4. Wakati anarudia hakikisha unamtafutia sehemu inayotoa elimu bora. Pia na wewe uwe mfatiliaji sana kwake, uwe na namba hata za walimu na unawapa ela ya vocha ili wakufatilie zaidi. Wakisema wanahitaji tuition basi fanya hivyo. Mtoto aliyepata O mpaka aje kupata IV yenye D walau 5 sio kazi rahisi Mkuu. Pia nitapendekeza asome Sayansi, Sayansi inalipa sana Mkuu huko mbeleni, tofauti na Arts.
3. Akimaliza Form IV peleka Chuo, achana na mambo ya Advances, kupitia Form IV akienda chuo na kupata Diploma kama ya sayansi hivi anaweza akaajiriwa. Hapa atakupunguzia mzigo Mkuu, Diploma za Sayansi zinauzika maana mtu anakuwa na maarifa mengi tuu, akiendelea Degree akitokea Diploma haitamsumbua sana kama mtu aliyetokea Six.
***** KILA LA HERI MKUU *****