Form 4 na wengine, angalieni hapa!

Haya matokeo ndiyo hayo yametoka!! Kila kitu hadharani, sasa ukiwa hapa JF ndo mpango nzima!! Manake watu washaanza kuhoji, mi nina hiki au kile nitafanyaje, haya ngoja nitajaribu kuweka mwongozo na alternatively nyingine due to spme perfomances kwa wote, manake naona huku kitaa watu wanadanganyana sana!!

Hii ni kwa kadri ninavyofahamu mimi, kama kuna marekebisho basi yafuatie:

=> Credit Qualification kwa hali ya kawaaida ni 'C'-Na ili uende Form 5 unahitaji uwe na C 3, hapa ni either umebalance Combination(Comb) au hujabalance. Sasa kama una C 3 na comb hujabalance, hautachaguliwa serikalini bali shule binafsi utaenda kusoma mchepuo utakaofanana na masomo yako.
[ Mfano: Civ-C, Kisw-C, Geo-C...unaweza fanya HGK ama HGL ama kozi nyingine hata kama english na History una D].

=>Ukiwa na C 2 na D kadhaa(lets say 4 ya 26), hapa utaweza kwenda Form 5 shule za Private lakini utatakiwa utafute C ya 3 kw kureset wakati upo form 5. Same na C 1 You need to re-sit.

=> Hapa sasa ndipo kwenye utata. Ukiwa na D 3, kiukweli sahau Form 5 kama hauhitaji kurisit, sasa qualification hizi zina option zifuatazo:
1. Unahitaji kupiga long pass kwa kwenda Chuo kwa ngazi ya Certificates. Duraation ya hii kozi ni 1 year Certificate. Sasa hapa kuna vyuo kadhaa vinavyotoa certificates. Hapa ni D za masomo yoyote yale Basic(sina uhakika kama B/Knwoledge na Islam zinazingatiwa na ndio maana nasema D za Basic Subjects)
Mfano: Unaweza kufanya Certicates vyuo vya CBE-Mambo ya Biashara, IFM, TIA, Utumishi wa Umma(Public Service) Vyuo vya Kilimo na Ualimunk.
Nakozi nyingi tu wanatoa kwa certificates..mfano Procurement, Accounts, Public Admistration, Recording, Clearing and Forwarding, Social Development, Secretarial Duties, Education nk.

=> Ukiwa na D 4 upo qualified kufanya ngazi ya certificate kama nilivyoanisha hapo juu.

=> Ukiwa na D 5 sasa hapa wewe umeula!! Hapa unaruhusiwa kabisa kufanya Basic Diploma katika vyuo vyote wanavyotoa Duploma. Kwa mfano vyuo hivyo nilivyovitaja hapa JUU, chukua form yako kwa maringo achana na biashara ya kurisit omba kozi ya diploma, Teana kama una D ya hesabu na English ndo inakuwa rahisi zaidi kuchukuliwa.

=> Kwa wale waliosoma mahesabu kuna vyuo vingine kama DIT(Daar Institute), AIT(Arusha Inst) na Mbeya Tech Msishau kufanya maombi, na kwale waliopiga fresh Biology with minimum of D angalieni option za Nursing ni nzuri sana na katika vyuo vya MATC na COTC.

Kama kuna marekebisho yanakaribishwa na kama hoja ama daubt basi uwanja ndio huu. Most welcome!!

UPDATE:


2i9m911.jpg

jidhjp.gif
Kiongoz me naomba kuuliza nipo na mdogo wangu kafanya mtihani 2022 kapata ( D ) ya English, ( D ) ya Geography na ( D ) ya kiswahili Sasa sehem gn au chuo gn anaweza kusoma.
 
Jaman kwa haya matokea geo C HIST C BIO C KISW C CHEM D PHYS D ENG D CIV D MATH F NAWEZA KWENDA ACCOUNTANCY AU NURSING DIPLOMA
 
Back
Top Bottom