KIM KARDASH
JF-Expert Member
- Sep 21, 2011
- 5,139
- 1,150
Samahani kwa hilo Kaka,
Kwanza sikujua kwamba nina uwezo huo; Pili sikujua kumbe mbali ya kutoa hoja, pia wewe ni moderator na unaona mjadala naupeleka kusipo takiwa; Basi nimekuelewa naacha kuchangia kwenye uzi huu, na naomba wale wote ambao nimewaudhi kwa njia moja ya nyingine mnisamehe; Niwie radhi kaka, ila kumbuka - huu ni mgongano tu wa mawazo, na msukumo wangu sio kitu kingine zaidi ya uchungu juu ya jinsi gani chama chetu kinazidi kupotea, huku sisi vijana tukipigia debe malengo ya wazee ambayo ni ya muda mfupi sana, kwani in 10-15 yrs watakuwa hawapo tena katika siasa za nchi hii na watatuachia chama mfu au chenye migogoro mikubwa zaidi ya hii;
Hoja zangu humu hata kama zitakuwa zimekuudhi, naomba uelewe tu kwamba zililenga kujadili jinsi gani tunaweza kukirudishia chama chetu cha CCM hadhi yake ya zamani kwa kuangalia uhalisia wa mambo (sio ignorance and arrogance just because tumekamata dola), and in the process, mgongano wa mawazo ni jambo la kawaida; Nakuachia mjadala wako kwa moyo safi kabisa;
Na kuhusu wewe kuwa kiongozi wa taifa, mimi sijashindwa bali nimekataa kuwa mtumwa; kaulize;
Kila la Kheri;
Alamsiki;
Hapa nadhani waislam watakujibu, ilikuwaje Mtume Muhamad kuoa mtoto wa miaka 9! Sio binti mtoto wa miaka tisa.
Miaka ya 1989/90...Mwenyekiti wenu by then alioa binti mwanafunzi wa Jangwani Sec.School. Dar yote iliwasikia mabinti wa Janwani, Kisutu, ZAnaki nk. wakimwita mkuu pale ikulu shemeji yao.
Labda ni sawa, sheria ya ndoa inasemaje. Rais awe mkwale? Mwenye vimada kila kona, kila kabila,kila race?
- ha! ha! ha! ha! Especially mke anapokuwa 30 na Mume 70! ha! ha! ha! ha! yaani gap ya 40 years!!
Le Mutuz!!
- ha! ha! ha! ha! ha! ha! chama chetu hakipotei labda unapotea wewe tu ndugu yangu, sasa ninaanza hata kuelewa unatokea wapi kumbe ni wewe duh!! unajua sana kujificha ficha, ha! ha1 ha!
Le Mutuz!!
".........Wakati huna mke" KWANI Mh SLAA ANA MKE? Wewe kweli umechanganyikiwa.
Wewe kama unajitambua bado kijana na Willy anajiona bado kijana tatizo lipo? Usimlazimishe mtu na uzee kuna watu wanaweza kukuona mzee na huo umri wako wa miaka 31; siku akitaka kuwa mzee hatakusubiri wewe umwambie. Tatizo lenu makamanda mna mambo ya kulazimisha sana
Chama
Gongo la mboto DSM
wewe ni kada wa chama gani labda,maana hata mimi sasa umeanza kunichanganya,mwanzoni nilikua nakuona kama unafanya kazi nzuri ya kukikosoa chama chako wewe mwenyewe kwa nia ya kukijenga kwa kujkifanya kijirekebishe badala ya kuwaachia kazi hiyo wapinzani,lakini sasa unakwenda mbali zaidi na kunifanya nianze kukutazama kwa jicho la tahadhari,pengine unatumika kwa malengo maalum,otherwise vua joho la ccm nenda upinzani tuelewe moja kuliko kuuma uma maneno,ccm sio mamako ulikutana nayo barabarani na unaweza kuachana nayo huko huko kuliko kuendelea kuteseka nayo wakati unaamini haiwezi kusimama tena,nenda kajiunge na timu ya ushindi,tena mungu amekujalia una uwezo mkubwa sana wa kuandika,kupanga maneno na kushawishi,upinzani una safu nyembamba ya uongozi nenda kaongeze nguvu kule ili utupe changamoto sisi wafuasi wa chama mfu lakini kinachpendelea kukubalika na watz
wewe ni kada wa chama gani labda,maana hata mimi sasa umeanza kunichanganya,mwanzoni nilikua nakuona kama unafanya kazi nzuri ya kukikosoa chama chako wewe mwenyewe kwa nia ya kukijenga kwa kujkifanya kijirekebishe badala ya kuwaachia kazi hiyo wapinzani,lakini sasa unakwenda mbali zaidi na kunifanya nianze kukutazama kwa jicho la tahadhari,pengine unatumika kwa malengo maalum,otherwise vua joho la ccm nenda upinzani tuelewe moja kuliko kuuma uma maneno,ccm sio mamako ulikutana nayo barabarani na unaweza kuachana nayo huko huko kuliko kuendelea kuteseka nayo wakati unaamini haiwezi kusimama tena,nenda kajiunge na timu ya ushindi,tena mungu amekujalia una uwezo mkubwa sana wa kuandika,kupanga maneno na kushawishi,upinzani una safu nyembamba ya uongozi nenda kaongeze nguvu kule ili utupe changamoto sisi wafuasi wa chama mfu lakini kinachpendelea kukubalika na watz
sasa hii dhahiri ni jazba, mbona Mchambuzi anakosoa chama chake in bonafide ila wewe unatoa layman solution jumla jumla namna hii?? hebu punguza jazba mkuu.
Hatari:
Weka Mbali na Tembo.
- ha! ha! ha! ha! ha!ETi least wananchi hapa wana uhakika kwamba mimi kiongozi wao wa Taifa sio shoga, maana siku hizi Dunia imeharibika sana mnachagua kiongozi wa taifa kumbe shoga! ha! ha! ha!
- But in me what you see is what you get, kudadeki yaani Kiongozi Rijali! ha1 ha! ha! ha!
Le Mutuz!!
- Ahsante sana, ila ndugu yangu dalili za mvua huwa ni mawingu, uchaguzi wa udiwani majuzi ni ujumbe tosha kuhusu what to expect 2015 the budern is on the otherside sio kwetu CCM tena!!
Le Mutuz!!
Eti tuwaachie Wapinzani Kazi ya kuikosoa CCM; Hizi ni fikra mkunyazi na ndio maana chama kimeganda, hakiendi mbele;
mkuu Mchambuzi huyu @W.J. Malecela ni mmoja kati ya wanachama wa ccm anayekitia aibu chama chenu.
Hatari:
Weka Mbali na Tembo.
Hivi Kaka William,
Unajua kwamba chama chetu kimesha meguka ndani kwa ndani siku nyingi na tuna vyama zaidi ya viwili kimtazamo na kimalengo ndani ya CCM? Kinacho kosekana ni usajili wa tendwa; Isitoshe, viongozi wengi ndani ya CCM hawafanya kazi tena kwa mapenzi ya CCM, na hii ni hatari kwani wanasukumwa zaidi na UWOGA, UBINAFSI na UNAFIKI, masuala ambayo mwalimu aliyajadili sana jinsi gani ni tishio kwa uhai wa Chama;
Mimi ni Mwana CCM lakini kwa akili zangu timamu, naelewa kwamba kwa sasa CCM bado ni moja kwa sababu ya System tu, hakuna lingine; Chama kinacholindwa na system ni chama dhaifu;
Ni muhimu tukai sambaratisha CCM sasahivi kama nia yetu ni kuijenga upya, kuliko kusubiri kuja kusambaratishwa na Upinzani, kwani siku hiyo haipo mbali;
Hoja yako ya kutetea Chama chenye kansa ya kiungo ni hoja mfu kwani unachofanya ni kutetea na kuwa mtiifu kwa chama kwa mujibu wa katiba, sio kwa mujibu wa uhalisia wa soko la Siasa; Kaka, Kansa imesha sambaa, tukate tu hicho kiungo na tuanze maisha mapya
Re: Finally: Hongereni Wana-CCM Online!!
Napendekeza kama inwezekana Mods wabadilishe title iwe "HONGERENI WA-TZ WAPIGANIA MABADILIKO & UKOMBOZI WA FIKRA" maana siwaoni hao Wana-CCM wanaopongezwa kwa kujibu hoja online. Au wana mgomo hawajalipwa posho zao nini?
- Nimeshindwa kusoma yote maana it is toolong daamn! however naomba kusema hivi kama unaaamini CCM itameguka basi wahi Chadema, kama unaamini CCM imemeguka tayari basi wahi Chadema, CCM ni treni inaondoka haiwezi kusimama, ninasema CCM itshinda mwaka 2015, hakuna atakayemeguka wala kutoka, Chadema best net ilikuwa Sitta labda angetoka, lakini Slaa amemkorofisha na kusema sana now hakuna hope tena!!
-
Le Mutuz!!
Mchambuzi;Pengine ndio tiketi yake ya kutafuta madaraka kwani humu anajisifia eti "hawezi kujibizana na wanachama ambao sio viongozi wa kitaifa kama yeye"; Hicho chama kwani kinatumikia nani, viongozi au wanachama wasio kuwa na uongozi kama yeye? Kwa mtazamo wake huu, ni dhahiri yeye na wengine wengi huingia CCM Kutafuta:
- Social Status
- Wealth
- Prestige
Hawapo ndani ya chama kutumikia wananchi, hivyo ni vigumu sana kuelewana na watu wa namna hii kwa hoja;
Isitoshe, tumeshaona kwamba watawala huko CCM huwapa watu kazi au kuwapandisha vyeo kwa vigezo vifuatavyo:
- Ignorance (hata kwa makusudi);
- Irrationality;
- Stubbornness (hasa kuwavunjia heshima wapinzani na wananchi wanaowaunga mkono);
- Dishonesty;
Hizi ndio prefered features wanazoangalia watawala kabla hawajasema wewe ni mwenzao na unafaa; Kama hauna hizi sifa, sahau uongozi ndani ya CCM;
Tusije kushangaa Kaka yetu anateuliwa kuwa Mjumbe wa kamati kuu (CCM) kwani katika majibu yake kwangu katika bandiko moja, ameonekana kutukuza sana ukubwa alionao, na kwa sifa hizo hapo juu, hakika ataenda mbali sana ndani ya chama;