Fikra za Mwalimu: Hizi hapa.. mzikubali au mzipinge!

Fikra za Mwalimu: Hizi hapa.. mzikubali au mzipinge!

Sijasema chochote kuhusu mwaka 1985 au kabla ya hapo zaidi tu ya kuwauliza mlete data za kabla ya 1960 for a complete analysis na pia mtolee maelezo ya kwanini kuna shock kubwa miaka around 1980?
....
Kama hakuna data zote za utawala wa Nyerere. Hizo data sio conclusive. Na kama data mlizonazo zinaonyesha kuwa around mwaka 1980 kuna mporomoko mkubwa wa uchumi wa Tanzania na nyie msiwe na maelezo ya kwanini mwaka 1980 kulitokea shock kiasi kikubwa hivyo ya uchumi basi data zenu sio conclusive.
Maswali rahisi tu jamani!

Lugha ya takwimu huelewi, lugha ya mantiki huelewi. Ngoja nijaribu kugomba:

NIMESEMA HATA NIKIKUBALI KWAMBA HIZO TAKWIMU ZA MIAKA YA '60 ZINGEONYESHA UCHUMI MBAYA, HOJA YAKO BADO MBOVU KWA SABABU UCHUMI ULISHUKA WAKATI WA AZIMIO LA ARUSHA. KAMA WA NYUMA WA AZIMIO ULIKUWA MZURI ZAIDI HIYO INAONGEZA NGUVU KWA HOJA YANGU. NA KAMA ULIKUWA MBAYA KABLA YA 1970, TAKWIMU TULIZO NAZO ZINAONYESHA ULIHARIBIKA ZAIDI.

Sio hatari Mwafrika wa Kike, usimaindi!
 
Lugha ya takwimu huelewi, lugha ya mantiki huelewi. Ngoja nijaribu kugomba:

Nitaelewa nini kitu ambacho hujasema? Nimeuliza data za uchumi wa Tanzania mwaka 1960-1970, katika hili hakuna ambacho nimedai kutoelewa. Leta data tuendelee na mjadala huu wa uchumi wa Tz chini ya Nyerere.

NIMESEMA HATA NIKIKUBALI KWAMBA HIZO TAKWIMU ZA MIAKA YA '60 ZINGEONYESHA UCHUMI MBAYA, HOJA YAKO BADO MBOVU KWA SABABU UCHUMI ULISHUKA WAKATI WA AZIMIO LA ARUSHA. KAMA WA NYUMA WA AZIMIO ULIKUWA MZURI ZAIDI HIYO INAONGEZA NGUVU KWA HOJA YANGU. NA KAMA ULIKUWA MBAYA KABLA YA 1970, TAKWIMU TULIZO NAZO ZINAONYESHA ULIHARIBIKA ZAIDI.

Sio hatari Mwafrika wa Kike, usimaindi!

Kumbuka kuwa mimi bado sina hoja hapa. Ukisema kuwa hoja yako ni mbovu sijui unakumbukia (refer to) wapi? Mimi nasubiri data zako na majibu ya maswali yangu ili niwe na basis ya kutoa hoja.

Mbona inakuwia vigumu sana kwenye simple requests kama hizi?
 
Pundit,
Sio tu tulikuwa na mwelekeo tulikuwa na dira, hizo ndizo fikra za mwalimu ambazo nazizungumzia hapa..
Kama umesoma vizuri report ya Tony Walter utaona kwamba baadhi ya fadhila zetu (pia fikra za mwalimu) zinazosifiwa humu ndizo zimekuwa angamizo la uchumi wetu baada ya kupoteza mwongozo na dira.
Bila kurudi nyuma nadhani ulisoma mahala nikikubaliana na FMES kuhusu siasa za mwalimu, hasa hivi vituo vya fadhila za kupakia abiria njiani toka kina Zimbabwe hadi hawa Rwanda na kadhalika hali sisi wenyewe hohe hahe mifukoni!..pamoja na kwamba ni uungwana na sifa ya Ukarimu. Hizi siasa za mwalimu ndizo napingana nazo kwani muda wake umesha pita Afrika nzima iko huru ugonvi wa ndani ya nyumba za watu hatuna haja ya kupoteza nguvu zetu..
Nje ya hapo maswala ya kilimo kuwa uti wa mgongo wa uchumi wetu bado ni reality kulingana na mazingira yetu pamoja na kwamba hawa waliofuata wameamua kuruka viunzi na kutegemea mirathi aliyotuachia Mungu...
Walter kazungumzia hilo pia kuwa Tanzania pamoja na yote haya hatuna cha ku offer ktk uchumi wa Amerika zaidi ya kuwa kituo cha kupambana na Ugaidi... Ikiwa hatuna kitu cha kubadilishana kiuchumi na nchi kama Marekani hivi kweli tuna tegemeo la kufika huko tunakokusudia?... Na ktk hali hii tunaongozwa na kitu gani hasa maanake hatuzalishi isipokuwa pato kubwa la serikali linategemea kodi za mali inayotoka nje..
Kuna fedha nyingi zimezagaa nchini kiasi kwamba mtu unashangaa hiyo purchasing power inatoka wapi ikiwa hatuna cha kuuza isipokuiwa kile kinachotoka nje..kumbe tunaiba akiba zetu wenyewe na isijekuwa tunayafanya ya Idd amin kuchapisha fedha nyingi zaidi kila mwaka.
Leo hii hakuna Mtanzania anayefahamu kesho itakuwaje unless tusikie kuna mafuta yamevumbuliwa.. yaani tunacheza kamari, huu uchumi unaokuwa kwa aslimia 6 sijui 7 hauna uhakika hata kidogo wala haumfikii mwananchi wa kijijini, kesho madini yakiisha (ambayo yatakuja kwisha) tutakuwa na kipi cha kukuza hiyo GDP ya kimaandishi..
 
1.
Taifa limedumaa kwa vile wanaccm na viongozi wa serikali wamefanya ufisadi na kuiba mali ya nchi kwa manufaa yao wenyewe na wala sio kwa sababu ya maneno ya Nyerere. Kama sera na mambo ya Nyerere ni maovu kama unavyosema, basi taifa limeoza kwa vile miaka kumi tangu kifo cha Nyerere bado kuna watu wanaamini kuwa ushetani wa Nyerere ndio unadunisha nchi.

Heshima wakuu MMJ na MWK,

Tatizo ni kwamba taifa halina sheria, hatujui sheria toka tupate uhuru, tuna sheria zinashika masikini tu, ndio maana tuna hayo yote uliyoyasema hapo juu!

2.
Sidhani kama mwalimu alikuwa the greatest ever na wala sio kweli alikuwa the worst ever. Kuna mema mengi mazuri aliyofanya Nyerere na kusema Nyerere na pia kuna mabaya aliyofanya au yaliyofanywa kwa jina lake.

Okay mkuu ninakupa this one, uko karibu na ukweli!

3.
Kinachotafutwa hapa ni yale mazuri yafuatwe na mabaya yaachwe. Hata hivyo inashangaza kuona kuwa nchi nyingi duniani leo hii zinaongozwa kwa sera za kijamaa zaidi kuliko za kibepari. Hii sidhani kama ni ajali. Ubepari typically ulishindwa na ujima pia ulishindwa. Mchanganyiko wa sera mbili ndio umefanikiwa. Ni heshima kujua kuwa Nyerere aliruhusu vyote - ubepari kidogo na ujamaa sana na kuchanganya na ujima kidogo.

1. Mabaya hayawezi kuachwa bila kujadiliwa kwa uwazi ili tuweze kujirekebisha na tusirudie makosa.

2. Hakuna nchi iliyoendelea sasa inayoongozwa na sera za kijamaa, nchi nyingi zilizoendelea zinaongozwa na sera za kibepari, US, UK, Germany, France, Japan, zinaongozwa na sera za kibepari, China peke yake ndio inajaribu kuchanganya lakini still bado wanaelemea kwenye ubepari, cha muhimu ni wanahakikisha kuwa serikali ina zi-fund sekta za afya, na elimu kwa asilimia kubwa hivyo kuwapunguzia mzigo mzito wananchi, lakini at heart ni ubepari,

3. Huo ubepari wa Mwalimu, aliuruhusu wapi? Yaaani uamuzi mdogo sana wa kuruhusu dala dala tu, ilibidi Sokoine aingilie kati if anything, hii peke yake na Chai maharage ndio ulikuwa ubepari wa Mwalimu, au?
 
Dont worry... there is always an explanation to everything. She is doing economics and she will look at this part of the thread as usual.

There will be an is for is and what you mean by is.... Bill C

Mkjj,

Samahani tulitoka kidogo kwenye mada yako (half time show!) si unajua tena u-inlaw wa marekani muda mwingine inatisha....lol

Nimekuachia message ndefu ya apology kwenye voice mail yako
 
Pundit,
Sio tu tulikuwa na mwelekeo tulikuwa na dira, hizo ndizo fikra za mwalimu ambazo nazizungumzia hapa..
Kama umesoma vizuri report ya Tony Walter utaona kwamba baadhi ya fadhila zetu (pia fikra za mwalimu) zinazosifiwa humu ndizo zimekuwa angamizo la uchumi wetu baada ya kupoteza mwongozo na dira.
Bila kurudi nyuma nadhani ulisoma mahala nikikubaliana na FMES kuhusu siasa za mwalimu, hasa hivi vituo vya fadhila za kupakia abiria njiani toka kina Zimbabwe hadi hawa Rwanda na kadhalika hali sisi wenyewe hohe hahe mifukoni!..pamoja na kwamba ni uungwana na sifa ya Ukarimu. Hizi siasa za mwalimu ndizo napingana nazo kwani muda wake umesha pita Afrika nzima iko huru ugonvi wa ndani ya nyumba za watu hatuna haja ya kupoteza nguvu zetu..
Nje ya hapo maswala ya kilimo kuwa uti wa mgongo wa uchumi wetu bado ni reality kulingana na mazingira yetu pamoja na kwamba hawa waliofuata wameamua kuruka viunzi na kutegemea mirathi aliyotuachia Mungu...
Walter kazungumzia hilo pia kuwa Tanzania pamoja na yote haya hatuna cha ku offer ktk uchumi wa Amerika zaidi ya kuwa kituo cha kupambana na Ugaidi... Ikiwa hatuna kitu cha kubadilishana kiuchumi na nchi kama Marekani hivi kweli tuna tegemeo la kufika huko tunakokusudia?... Na ktk hali hii tunaongozwa na kitu gani hasa maanake hatuzalishi isipokuwa pato kubwa la serikali linategemea kodi za mali inayotoka nje..
Kuna fedha nyingi zimezagaa nchini kiasi kwamba mtu unashangaa hiyo purchasing power inatoka wapi ikiwa hatuna cha kuuza isipokuiwa kile kinachotoka nje..kumbe tunaiba akiba zetu wenyewe na isijekuwa tunayafanya ya Idd amin kuchapisha fedha nyingi zaidi kila mwaka.
Leo hii hakuna Mtanzania anayefahamu kesho itakuwaje unless tusikie kuna mafuta yamevumbuliwa.. yaani tunacheza kamari, huu uchumi unaokuwa kwa aslimia 6 sijui 7 hauna uhakika hata kidogo wala haumfikii mwananchi wa kijijini, kesho madini yakiisha (ambayo yatakuja kwisha) tutakuwa na kipi cha kukuza hiyo GDP ya kimaandishi..

Nilijua tu kuanzia mwanzo nitapata shule ya nguvu hapa.

Asante Bob kwa hii shule!
 
FMES,
Kuendelea kupi unakokuzungumzia maanake tafsiri ya neno hili ina mapana yake!..
 
1.

....

2. Hakuna nchi iliyoendelea sasa inayoongozwa na sera za kijamaa, nchi nyingi zilizoendelea zinaongozwa na sera za kibepari, US, UK, Germany, France, Japan, zinaongozwa na sera za kibepari, China peke yake ndio inajaribu kuchanganya lakini still bado wanaelemea kwenye ubepari, cha muhimu ni wanahakikisha kuwa serikali ina zi-fund sekta za afya, na elimu kwa asilimia kubwa hivyo kuwapunguzia mzigo mzito wananchi, lakini at heart ni ubepari,

Mkulu FMES,

Tafsiri ya ubepari ninayoifahamu mimi ni hii:

Capitalism - a free-enterprise system where every economic unit is free to act in its own interests; Resources are owned privately and decisions are made individually thus economic questions are answered by the pricing mechanism of free markets

Katika hili mkuu, hakuna nchi yoyote yenye typical ubepari. Zote hizo zina element za ujamaa na nyingine nyingi zinakwenda zaidi kwenye ujamaa (ambao ni mchanganyiko wa typical ubepari na ujima)
 
Binafsi ninaongelea siasa amabazo hata mwananchi wa kawaida akinisoma atanielewa ninasema nini, kuendelea kwangu mimi ni pamoja na kuwa na muda mrefu wa kuishi, kuliko sisi bongo, urahisi wa matibabu ya uhakika, uwezekano wa kila mwananchi kuweza kula kwa kila siku inayoenda kwa Mungu, maana kwa mfano US inapofika saaa sita za usiku, fast food kabla ya kufunga zinatakiwa kugawa chakula kwa wasiojiweza na ma-homeless, then ndio wanaweza kumwaga, sasa katika mfumo huu anayelala na njaa na antaka mwenyewe, serikali inahakikisha kuwa kuna shelters kwa ajili ya wasiojiweza na kuwa na pa kulala, serikali ina programs za kuwasaidia wanaoshindwa katika mchakato wa ubepari, walevi, wagonjwa wa ukimwi, vilema, matahira,

kipato kazini ambacho kinalingana na maisha ya chini kabisa kwenye taifa, sheria ni msumeno inakata kote, uwe masikini au tajiri, the latest alikuwa Black Conrad, na utajiri wake wote sasa hivi yuko jela, anakula dona kwa kuvunja sheria za taifa, elimu inapatikana kwa njia ambazo ni resonable na kuna access kwa wananchi wote, kuna scolarship za kusaidia masikini wenye uwezo kiakili, system ya social security kwa wananchi wote wakifikia wakati wa ku-retire, I mean haya kwangu ni maendeleo, ambayo sisi hatuna, na yanapatikana kwenye chi zinazotumia sera za kibepari,

Wananchi wanamiliki utajiri na vitengo vya uchumi, serikali imekaa pembeni ina-regulate the rules of the game, na inakusanya kodi tu, lakini haijihusishi na biashara kabisaaa, serikali inahakikisha kuwa hakuna monopoly kama kwetu bongo na makampuni ya simu, sigara au bia.

Ahsante Mkuu
 
Mkuu maneno huenda ni kweli au sio, lakini nina uhakika sio the topic hapa, labda hii inafaa kule kwenye thread nyingine ya MMJ, mimi binafsi niko interested na mapungufu ya Mwalimu, na hasara zake kwa taifa letu, maana mazuri yake ninayaelewa na nimeshayasema tayari, na ninakubaliana na nyinyi wote kuwa Mwalimu, alikuwa na mazuri mengi sana, lakini ninachowaomba ni ikiwezekana angalau mguse tu kwenye mapungufu yakle ili tuweze kujua tulikosea wapi mpaka kufikia tulipo sasa.

Ahsante Mkuu!
 
Uchumi wa 1970 mpaka 1985 ndio uchumi wa Nyerere, uchumi wa Azimio la Arusha, uchumi wa Kijamaa!

Mwafrika wa Kike, utaonekana mbishi mbishi bure tu ndugu yangu.

Sasa ngoja nikumalize. Si huelewi lugha ya takwimu, basi nitatumia lugha unayoielewa, nimekusikia unaiongea: mantiki.

Tuseme nakubali -japo sijakubali - kwamba uchumi wa Tanzania ulikuwa mbaya toka mwaka 1970. Umedai - na tuseme ni kweli - kwamba Nyerere hakuachiwa Uchumi na Wakoloni. Ina maana hatukuwa na pengine pa kwenda ila juu. Tulikuwa sifuri!

Now, I have come across many assumptions, this one could go down in history as one of the worst attempted!

Takwimu tulizo nazo zinasema uchumi uliharibiwa kutoka mwaka 1970 mpaka 1985. Hii ina maana Ujamaa na Kujitegemea ilipokuja uliendelea zaidi kuua uchumi wowote uliokuwepo. Mnara wa Nyerere katika historia ya dunia ni siasa zake za Ujamaa, zilizo pandwa 1967, na athiri zake kuja miaka ya 1970 na 1980, na sio miaka ya 60. Kwa hiyo tulitoka sifuri tukaenda...? Haiwezekani. Darasa la pili ndio haiwezekani, la sita kuna jibu: Hasi!

Kwa hiyo vyovyote vile, takwimu za 1960 mpaka 1970 hata zikionyesha uchumi mbaya, Nyerere aliumalizilia mbali hata ule mbaya wa Mkoloni! Hoja yako -au ukaidi- hapa unakufanya ufaidi makorowedho.

Ukisema Uchumi wa Tanzania haukuwa mbaya 1985, siku Nyerere anaondoka, kuliko nyuma, unaonekana aidha unatania au huna dhana ya kinachoendelea.

Takwimu ni kitu kibaya sana! Inategemea nani anaziangalia. Nilichoona kwa muda ukikijaribu ni kunyakua takwimu toka kila kona ya dunia isipokuwa toka serikali ya Tanzania! Kwa mara nyingine tena unathibitisha kuwa hujui unachozungumzia. Nitakusaidia kwa furaha!

Mwaka 2002 serikali iliandika ripoti ambayo inajulikana kama Economic Survey na unaweza kuisoma hapa (assuming you can study a report not just read it) ECONOMIC SURVEY. Ukienda kwenye eneo la "Special Development Issues" utapata clue ya kile ambacho nimejaribu na wengine wamefanya hivyo kukuimbia kwa kila aina ya muziki kuwa ni oversimplification of history kuliko ambavyo mtu anaweza kujaribu.

Kuhusu hali ya uchumi ripoti hiyo iliyoandikwa miaka kadhaa baada ya Nyerere kufa na miaka mingine mingi tangu atoke madarakani iliangalia ulinganifu wa hali ya kiuchumi na kusema ifuatavyo:

REVIEW OF ECONOMIC TRENDS AND REFORMS​

The Period 1961 - early 1970s
164. Since independence in 1961, the economy of Tanzania has passed through two main socio-economic policies. From early 1960s till the announcement of the Arusha Declaration in 1967, the economic system was that inherited from colonial period which promoted the market economy and private sector. After the Arusha Declaration, socialism and self reliance were adopted as the guiding principles and putting all major means of production under the state. Public sector took a leading role in economic operations, and the provision of free basic social service to all become the means to combat poverty, ignorance and disease. The economy depended on agriculture, which contributed an average of 50 percent of GDP. The country witnessed a stable economic growth and on the average the economy grew at around 5 percent, from mid 1960s to early 1970s. In this period, Tanzania succeeded to strengthen and improve the social and economic welfare of its people.

The Period 1974 - 1985
165. Despite the achievements stated above, the later part of the 1970s started showing signs of an economy in difficulties, as a result of the rise of oil prices which started in 1973, adverse weather condition that affected crop output in 1974, collapse of East African Community in 1977 falling primary commodity prices in the world market, and war against Uganda’s Iddi Amin in 1978/79. The socio–economic crisis reached a crimax in the early 1980s due to shortage of foreign exchange caused by the above listed factors and the world wide economic recession underway during the time. In order to reverse the economic situation the country initiated the National Economic Survival Programmes (NESP) and the Structural Adjustment Programme (SAP). However, NESP was one year programme and was replaced by the three year SAP in 1982/83 which could not be implemented fully because of the extended negotiations between the Government and the Bretton Woods institutions.

Now, I can foresee a couple of your objections:

a. Kwanza, hii ni ripoti ya serikali ya CCM hivyo haiminiki kwa vile CCM ni ya Nyerere na Nyerere ndiye aliyeandika ripoti hii (somehow) na kuwatishia walioiandika ili waandike vinavyompendeza yeye huko kaburini.

b. Hatuwezi kuwaamini wasomi wa Tanzania maana walifukuzwa na waliobakia hawakuwa na uwezo wa kuangalia data objectively. Hivyo tunaziamini ripoti za IMF na New York Times.
 
Binafsi ninaongelea siasa amabazo hata mwananchi wa kawaida akinisoma atanielewa ninasema nini, kuendelea kwangu mimi ni pamoja na kuwa na muda mrefu wa kuishi, kuliko sisi bongo, urahisi wa matibabu ya uhakika, uwezekano wa kila mwananchi kuweza kula kwa kila siku inayoenda kwa Mungu, maana kwa mfano US inapofika saaa sita za usiku, fast food kabla ya kufunga zinatakiwa kugawa chakula kwa wasiojiweza na ma-homeless, then ndio wanaweza kumwaga, sasa katika mfumo huu anayelala na njaa na antaka mwenyewe, serikali inahakikisha kuwa kuna shelters kwa ajili ya wasiojiweza na kuwa na pa kulala, serikali ina programs za kuwasaidia wanaoshindwa katika mchakato wa ubepari, walevi, wagonjwa wa ukimwi, vilema, matahira,

kipato kazini ambacho kinalingana na maisha ya chini kabisa kwenye taifa, sheria ni msumeno inakata kote, uwe masikini au tajiri, the latest alikuwa Black Conrad, na utajiri wake wote sasa hivi yuko jela, anakula dona kwa kuvunja sheria za taifa, elimu inapatikana kwa njia ambazo ni resonable na kuna access kwa wananchi wote, kuna scolarship za kusaidia masikini wenye uwezo kiakili, system ya social security kwa wananchi wote wakifikia wakati wa ku-retire, I mean haya kwangu ni maendeleo, ambayo sisi hatuna, na yanapatikana kwenye chi zinazotumia sera za kibepari,

Wananchi wanamiliki utajiri na vitengo vya uchumi, serikali imekaa pembeni ina-regulate the rules of the game, na inakusanya kodi tu, lakini haijihusishi na biashara kabisaaa, serikali inahakikisha kuwa hakuna monopoly kama kwetu bongo na makampuni ya simu, sigara au bia.

Ahsante Mkuu

Mkulu FMES,

Hayo ya kwenye red na bold ni part ya sera za kijamaa (socialism). Na hayo ya serikali kutofanya biashara nadhani serikali nyingi sana zimeshindwa kujizuia hapa na kukikuta zikifanya biashara (wao wakiziita public services) kwenye mambo muhimu kama usafiri, energy, na hata muda mwingine huduma za afya - hii yote ni biashara na kinyume cha ubepari.

Kumbuka pia ukishaweka regulationa au kuanza kubail out companies kama Marekani ilivyofanya kwenye mashirika ya ndege mwaka 2002 au kwenye mabenki sasa hivi tayari unakwenda kwenye ujamaa wenyewe wa kina Nyerere.
 
Huu mjadala lazima utoke kwenye mojawapo ya magazeti nyumbani tunapokaribia siku ya kuzaliwa kwa Baba wa Taifa... kuna elimu kubwa sana hapa..!!
 
Mkjj,

Samahani tulitoka kidogo kwenye mada yako (half time show!) si unajua tena u-inlaw wa marekani muda mwingine inatisha....lol

Nimekuachia message ndefu ya apology kwenye voice mail yako

Ahahahahahaaaaa...wewe...Mwafrika...wewe...
 
Hee! hivi sio majuzi tu MLK ametukuzwa kitaifa..

tena YNIM kuna wazungu waliotukana kuliko wewe hapa lakini haipotoshi ukweli wa fikra za MLK..vipi mkuu mwenzetu Gabacholi ulipoteza urithi wako maanake naona waanza kumsifia The Truth!...(utani)
 
Ukweli ni kwamba Mwalimu alikuwa mwanafalsafa na ikawa vigumu kwa Mtanzania mwenye elimu ya siasa na ujamaa, kuelewa nini alichomaanisha. Wengi uwa tunapinga sana juhudi za Nyerere pasipojua nini alimaanisha. Nakumbuka Nyerere alihitwa kutoa hotuba bungeni mjini Cape Town 16 october 1997, akasema `south of the Sahara is not what it is believed to be because Africa is now changing' akongeza na kusema
Africa south of the Sahara is different - completely different. It's not in the orbit of any of those big areas. If you people here are unemployed, very few of you will want to go to the US. The unemployed here will stay here.But so will unemployed in Tanzania. We'llnot go to the US. We'll not go Europe. Certainly we'd never dream of going to Japan or anywhere else.Ukisoma sentensi hii tu ya Nyerere hutaelewa anamaanisha nini, lakini pale utakaposoma hotuba nzima, ndio utajua alitaka kuwashawishi vipi watanzania na wote wahishio kusini mwa Africa wajaribu kusafiri, kwanza , wajulikane kitaifa na pili waweze tatuliwa tatizo la ajira za kazi na mataifa yaliyoendelea. Kwamtanzano wa mtu ambaye ajasoma hotuba nzima utasikia akisema, `kweli Nyerere ni Mbinafsi sasa kwa hali hii ya uchumi tungesafirije' wengi hatuna tabia ya kusoma na kuelewa mtu anamaanisha nini ila ni wepesi wa kutoa sentensi moja na kuanza malumbano ambayo hatujui hata tunalumbana nini. Naamini kabisa Hotuba na mawazo ya Nyerere yakitumika sasa hivi tutafika mbali.
Nakumbuka pia Hotuba yake aliyotoa kwa wananchi juu ya elimu, alipoaanza ujenzi wa chuo Kikuu, ninauwakika hata mimi ningekuwepo nisingeelewa kwamba Mwalimu alikuwa na nia ya kuniona na mimi nifike Chuo Kikuu.Inahuzunisha unaposikia mtu akisema, `Mwalimu alitunyima kuwa hata na tv sasa utasemaje kwamba alijali masilai yetu?'je wajua kwanini alikunyima? ni swali ambalo wengi hatujiulizi.Kwa mtazamo wangu, aliamini kwamba kipindi hicho dunia ndio ilikuwa inaanzakuendelea na alipenda Watanzania wagundue technologia yao wenyewe, kwa sababu dunia yote ilikuwa haijafika popote, sasa kama mkikaa na kubweteka na hakuna ushirikiano, mtabaki kukalia lasilimali zenu alafu baadaye zijechukuliwa na wale ambao zao zimeisha, na hichi ndicho tunachokiona. Tumekalia Tanzanite na lasilimali nyingi tu, na sasa wanazichimba baada ya kumaliza madini yao. Inaniuma na inanikera kama Mtanzania
 
Hee! hivi sio majuzi tu MLK ametukuzwa kitaifa..

tena YNIM kuna wazungu waliotukana kuliko wewe hapa lakini haipotoshi ukweli wa fikra za MLK..vipi mkuu mwenzetu Gabacholi ulipoteza urithi wako maanake naona waanza kumsifia The Truth!...(utani)

Unajua kinachozidi kunishangaza kila siku kuhusu MLK ni kwamba amekufa miaka 40 iliyopita lakini interest ya maisha, falsafa, fikra, na harakati zake inazidi kupanda.
 
Cocosmas,
Kifupi mkuu, nilishawahi kusema hivi, ili nchi ipate kuendelea ni lazima ipitie mikondo mitatu ya kiuchumi..
Kwanza Uzalishaji wa mali ghafi, kisha viwanda (manufacturing) na mwisho ndio ni ku- service kile mlichozalisha.. Sawa kabisa na kuwa mtu huwezi kuwa MSOMI bila kwanza kupitia Primary school, sekondary kisha, Chuo kikuu...ndipo unaweza tangaza Usomi wako.

Wadanganyika wengi wanafikiria maendeleo hupatikana kama kipaji cha biashara ambapo hata yule ambaye hakwenda shule anaweza kutajirika maadam anao mtaji haya sio maendeleo ya nchi bob.
Kwa ujumla Watanzania we believe in Lucky! Kujaliwa na Mungu kupata chochote na ndio maana tuna muda zaidi makanisani,misikitini na sehemu za starehe kuliko kufikiria kuanza upya darasa la kwanza kiuchumi yaani kwetu umri umeshapita..
Hivyo basi aliyoyasema yote Nyerere yanakuwa hadithi ngumu kwa Mdanganyika ambaye anayataka maendeleo bila kwenda shule..mali ghafi hatuna, viwanda haviwezi jengeka kama hakuna mali ghafi, leo tunaendesha services ambazo zinahudumia wananchi sio mali zetu, zote Imported kama wanavyosema wenyewe - za mtoni, hivi kweli tutafika?
Sijaona Ubepari unaopinga taratibu kama hizo na hata China wameweza kwa sababu walikuwa na vitu vyote vitatu tayari kui face dunia...
 
YournameisMine,
kosa la kwanza Azimio la Arusha( mie sikuwepo ila alitia watu umasikini), kosa la pili, hujuma under umbrella ya uhujumu uchumi......wallahi kama Ziwa Victoria, lingekuwa linasema basi lingenisaidia!!! aibu sana......we acha tu.
Wala huko usiende hata kidogo maana umeshasema hukuwepo..Azimio la Arusha fimbo ya Magabacholi!...

Wakati wa Uhujumu uchumi, mkuu nilikuwa mfanya biashara haramu mkubwa ziwa Victoria (Nyanza) na nadiriki kusema tuli chukua mali zetu toka sigara, sukari, vitenge hadi matairi ya General kupeleka Uganda na Kenya... We were wrong and criminals sio wafanya biashara!
Tulitupa mali hizo baharini kila tulipoona mapolisi na hakika tulomwangusha Nyerere ni sisi wenyewe!..kwani aliyetupa sii yeye ila sisi...
 
Takwimu ni kitu kibaya sana! Inategemea nani anaziangalia. Nilichoona kwa muda ukikijaribu ni kunyakua takwimu toka kila kona ya dunia isipokuwa toka serikali ya Tanzania! Kwa mara nyingine tena unathibitisha kuwa hujui unachozungumzia. Nitakusaidia kwa furaha!

Mwaka 2002 serikali iliandika ripoti ambayo inajulikana kama Economic Survey na unaweza kuisoma hapa (assuming you can study a report not just read it) ECONOMIC SURVEY.

Kuhusu hali ya uchumi ripoti hiyo iliyoandikwa miaka kadhaa baada ya Nyerere kufa na miaka mingine mingi tangu atoke madarakani iliangalia ulinganifu wa hali ya kiuchumi na kusema ifuatavyo:..

Now, I can foresee a couple of your objections:

a. Kwanza, hii ni ripoti ya serikali ya CCM hivyo haiminiki kwa vile CCM ni ya Nyerere na Nyerere ndiye aliyeandika ripoti hii (somehow) na kuwatishia walioiandika ili waandike vinavyompendeza yeye huko kaburini.

b. Hatuwezi kuwaamini wasomi wa Tanzania maana walifukuzwa na waliobakia hawakuwa na uwezo wa kuangalia data objectively. Hivyo tunaziamini ripoti za IMF na New York Times.

WACHUMI WA NJE (YA SERIKALI, SIO LAZIMA WAZUNGU) HAWAKUBALIANI NA MAELEZO YA NYERERE

Kwanza, umekubali kwamba uchumi ulishuka kuanzia 1974, na sasa hivi ishu - au ubishi wako mpya - ni sababu za kushuka uchumi. Aaak Sante! Nimekumata, na nitakukamata tena huko huko kwenye sababu, amatuer wewe!

Mbili, unadhani sijui takwimu zinategemea nani kaziandika? Hivyo mbona vitu vidogo unavyotoa masomo mjomba? Unajua wewe unadhani una dili na watu watupu sana. Ndio maana una kinaya fulani hivi. Umetaka nikupe kidhibiti, nikakupa kinacho tetea upande wangu, unataka nikupe pande zote! Wewe ndio tetea upande wako. Vipi bro!

Tatu, naona sasa hivi ndio umeanza kutoa vi-link vya habari. Baada ya kupakwa! Unaficha habari, we namna gani?

Nne, tofauti na magazeti yetu ya Bongo, ile taarifa ya NY Times sio maoni ya NY Times peke yake. Anadondoa hata wachumi wa Tanzania mle. Isitoshe imesema hayo hayo uliyo yoyasema, kwamba Nyerere alidai kwamba ni sababu za nje ndio zilisababisha uchumi kuharibika. Halafu ikasema kwamba wengine wanatofautiana na hayo mawazo.

Mimi sikatai ripoti ya CCM kwa sababu ni ya CCM. Sina ubishi wa kishabiki. Isipokuwa nasema inawezekana watu wa nje wanaweza kuwa wana hoja ya ukweli kwa sababu inawezekana hawana upande katika haya majadiliano.

Mwanakijiji ukikataa hili basi usifikirie, kama ulivyo dokeza, kupeleka haya majadiliano kwenye magazeti halafu ukaweka jina lako. Huko kuna wanaoona pande mbili. Unatoa ripoti ya CCM halafu unakataa taarifa zinazohusishwa na IMF utachekwa.

Hebu tuisome tena, kama una uvumilivu. (Mimi tutaenda mpaka asubuhi hapa).

TANZANIA, IN STICKING TO ITS SOCIALIST PATH, STUMBLES

By ALAN COWELL, SPECIAL TO THE NEW YORK TIMES
Published: March 2, 1982

For the third year in a row, Tanzania is importing food donated by outsiders to feed mainly those city dwellers who do not have access to their country's own produce.

NY TIMES WANATOA HITIMISHO LAO HAPA MWANZO, HATUJUI WEMEJUAJE BADO!

The contrast between town and country is part of a tale of mismanagement, inefficiency and corruption that outsiders increasingly attribute to President Julius K. Nyerere's dogged commitment to a kind of socialism that his country does not have the manpower to sustain.

(Neno 'outsiders lilivyotumika hapo lina maana wachunguzi walioko nje ya Serikali, sio Wazungu, kwa sababu atataja Wachumi wa Kibongo baadae.) Sitaki kukusomea au kukufundisha, lakini tuanishe kile kitu hapa, maana we si unajifanya mbishi. Haya!

MAELEZO YA NYERERE, KAMA KWENYE AUA YAKO YA CCM

President Nyerere has in the past attributed much of his country's economic misfortune to outside factors. As an eloquent spokesman for what is called the third world, he has complained that adverse terms of trade, burgeoning oil prices and his war against the Ugandan dictator Idi Amin have strangled the economy.

WENGINE (OUTSIDERS), SIO NY TIMES, WANAKATAA MAELEZO YA NYERERE

Unpublished figures, compiled by Scandanavian and Western embassies, however, show a different picture. According to one such analysis, whose authors requested anonymity, the losses incurred by Tanzania because of falling agricultural output are more than double those created by high oil prices. Another analysis, noting that ''the future is ominous,'' said that, even if Tanzania received all of its oil free, there would still be a huge gap between imports and its exports of agricultural commodities, mainly coffee.

Ever since 1967, when President Nyerere charted a socialist course for his country, Tanzania has been organized on highly centralized lines that give a huge slice of the economy to state-controlled companies, called parastatals, which have generally proved unable to meet their obligations and have cost more to run than they have earned.

SERIKALI INAKUBALI KUFELI KWA UJAMAA

Professor Simon Mblinye, the President's economic adviser, said in a recent interview, ''We moved to the socialist approach and then we created institutions, and maybe we were overzealous in creating institutions.'' Lack of Experience Cited
''There are too many for the quality and quantity of the people we can generate to run them,'' he said. ''We created 300 parastatals in 10 years. You cannot do this in 10, 20 years of independence. There is a lack of experience. Most of the executives are young and they need leadership.''

HAPA MBILINYI ANATETEA NYERERE TENA -KAMA KA-RIPOTI KAKO KA CCM

Some of the companies, he said, are now to be dismantled and replaced by cooperatives. Tanzania's woes are not simply a result of socialist mismanagement; adverse prices for export crops, grandiose foreign aid schemes that cost the country too much to run, or were unsuitable in the first place, and a costly stab at industrialization all took their toll.

WACHUMI WATANZANIA NJE YA SERIKALI (OUTSIDERS) WANAPINGA MAELEZO YA NYERERE

But the upshot, according to Tanzanian and Western economists, seems to have been the creation of a society where many people live outside the formal economy, as subsistence farmers, or peasants selling their crops on the black market, or senior officials augmenting their meager salaries with vegetable plots at home, or bribes in the office.

KUJITEGEMEA KUNAADHIRIKA NA SERIKALI INAKIRI UFISADI

The request was not forthcoming until October 1981, when President Nyerere, claiming ignorance of the earlier warnings, ordered his officials to request international assistance and thus halted the plan to buy on the open market. A confidant of the President said that, at the time, he suspected corruption as a prime cause of the delay.

The Reagan Administration, which has little affection for Mr. Nyerere's socialism, contributed 25,000 tons of corn. The anomalies remain, however. At the same time as the food gifts began arriving at Dar es Salaam, news of another import began to leak out, though not in the official Tanzanian press. The country's Vice President, Aboud Jumbe, who is the leader of Zanzibar, a part of Tanzania with control over its own economy, has ordered a $5 million executive jet to wing his way from the island to the mainland, a 10-minute flight.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom