Fikra za Mwalimu: Hizi hapa.. mzikubali au mzipinge!

Fikra za Mwalimu: Hizi hapa.. mzikubali au mzipinge!

hivi vijiji vilivyopo sasa ambavyo leo vimekuwa ndio kiini cha chini ya miradi na shughuli za maendeleo na vilitokana na operesheni vijijini tuvifanye nini?
 
Vijiji vingekuweko hata bila hiyo operesheni.
Ongezeko la watu ndiyo limezaa hivyo vijiji na siyo operesheni vijiji ndo imefanya vijiji viwepo.

Vijiji vingi vilikuwepo tangu enzi za Mjerumani ushahidi upo.
Kulikuwa na watu kadhaa ambao walikuwa Satelite wa vijiji hivyo ambao walikuwa na mashamba makubwa huko pembezoni. Watu hao walilazimishwa kuhamia katika vijiji vile vya asili.
Leo hii ujenzi wa nyumba huko vijijini umefika na kuvuka pale waathirika walipo hama mwaka 1974.

Kwa sababu siyo Operesheni vijiji iliyozaa vijiji sidhani kama ni sahihi kuuliza sasa tufanye juu ya hivi vijiji.

Vijiji kama vijiji si wazo la asili la mwalimu Nyrere hata kidogo, vijiji ni sehemu ya asili ya maisha yetu Watanganyika. Vijiji vya lazima na vijiji vilivyoundwa bila kuzingatia kanuni za asili ya vijiji,kweli ni wazo lenye asili ya ndoto za Mwalimu Nyerere. Tatizo hili la kutozingatia kanuni za asili za ujenzi wa vijiji ndiyo chimbuko kubwa la karaha na songombingo nyingi zinazoendelea vijijini hadi leo hii.

Uharibifu wa mazingira, ukosefu wa huduma ya maji, kuzorota kwa kilimo,wanavijiji kuishi mbali na mashamba yao, kutumia muda mwingi kutembea kuelekea shambani badala ya kulima nk.
 
Nathubutu kusema ndoto nzima ya mwalimu Nyerere ilikuwa dhambi.
hivi tatizo ni ndoto ya kukaa pamoja katika vijiji vya ujamaa au utekelezaji wa ndoto hizo?.

naomba uniweke wazi kidogo kwa sbabu hapa chini unasema hivi

Kwanza ingebidi kuzingatia utaalamu wa ongezeko la watu.
Ningeita wataalamu waniambie nchi itakuwa na watu wangapi baada ya mika 20,25 50. Utaalamu wao ungesaidi kujua structureya vijiji iweje 1962 ili isilete matatizo 2000.
kwa mujibu wa hii quote ni kwamba na wewe huna pingamizi na vijiji vya ujamaa, ndo maana ungeita wataalamu ili wafanye tathmini au vipi?

sasa unadhani ni tatizo ni ndoto za nyerere za kuwa na vijiji vya ujamaa au tatizo ni jinsi alivyozitekeleza ndot hizo?
 
Kuhani Mkuu,
Nitakwambia kule nilikotoka mimi.. Wilaya ya Mwibara kuna mji unaitwa Kibara, nimeishi hapo toka mdogo, Nyerere aliweka mabomba ya maji safi kabisa mji mzima lakini kufikia mwaka 1985 ama maji yalianza kuwa taabu na mwisho mabomba mengine kutotoa maji kabisa. Kule kijijini Bulamba kwa bibi zangu vilijengwa visima hivi leo hakuna maji..Kisorya kwa mababu zangu hakuna maji lakini nilikuta pump ya kisima imesha shika kutu haifanyi kazi...
Pale Nansio, Ukerewe kwetu, kulikuwa na maji toka napata fahamu yangu tena kila nyuma ilikuwa na maji, kufikia mwaka 1985, maji yalikuwa taabu na mwishowe hakuna kabisa.. Yamerudishwa (2006-07) baadhi ya sehemu 1/10 ya mji huo ambao umekuwa mkubwa zaidi ndio una maji..
Mkuu Hata kama utatembea vitongoji na vijiji nje ya Dar tazama kwa makini sehemu zote mpya hazina maji isipokuwa zile zilizokuwepo Kama vijiji toka enzi za Mwalimu utakuta maji ama mabomba yasiyokuwa na maji..
Mkuu hivi visima vilichimbwa sana na Waswedish enzi za mwalimu hadi vijijini huko Singida ndani kabisa...Temebelea Genzaulole utashangaa kuna vyanzo vya huduma hizo kuliko Kipunguni, Ukonga...
Mkuu, mji mzima wa Dar umejaa visima vya maji ya kunywa halafu basi mji huo huo una vyoo asilimia kubwa ni vya mashimo ambayo bila shaka chemchem zake zinaungana na maji ya visima...
Choo kinachimbwa hadi uone maji ya chini futi 12 kwenda chini...Hapa tunazungumzia Dar mji mkubwa wa Tanzania!... acha huko mikoani....
Proof gani zaidi unataka..kuhusu Hospitali?..... hadithi ni hiyo hiyo mkuu.. Leo hii mnajenga zahanati mkizipa majina ya Hospital, madaktari wote ni waganga wa kila ugonjwa hata veterinary siku hizi anatibu binadamu!

Sawa. Sasa kwanini mabomba ambayo yako bado leo kule kwenye vijiji vya Nyerere hayatoi maji? Ni kwa sababu tumeacha siasa za vijiji vya ujamaa au ni kwa sababu tumeshindwa kuzisimamia na kuzikarabati?

Kwa sababu haya ni mambo mawili tofauti. Na Nyerere aliyejengewa hizi hudumu na Waskandinavia hatuwezi kumpima angewezaje kuzikarabati kwa sababu alinyopoka (tena hapa, kuepuka ushindani usio tusaidia kwenye majadiliano, nakupa kidhi kwamba 1985 hizi huduma zilikuwa bado hazijaanza kuota kutu, na sitakuomba takwimu zinazoonyesha Wasweden walileta huduma lini, na zilikuwa katika hali gani lini).

Kushindwa kusimamia hizi huduma ni tatizo lisilohusiana kabisa na kubadilika kwa siasa zetu. Najiamini kusema hivyo kwa sababu naangalia vitu kama mmomonyoko wa barabara zilizo achwa na wakoloni, na huduma nyingine zote ambazo haziko kwenye vijiji vya ujamaa peke yake. Juzi TANESCO wametuambia vyombo vyao havijawahi kukarabatiwa toka vijengwe karne nenda rudi zilizopita. Kwa hiyo kushindwa kusimamia hizi huduma sio kielelezo cha madhara ya kuachwa kwa siasa za kushurutisha vijiji.

Lakini kikubwa zaidi ninachotaka kusema ni kwamba unajua hoja yako inakufunga vibaya mno. Sababu ya kuwa na huduma za maji kijiji cha ujamaa Gezaulole na sio Kipungunu ni kwamba siasa za ujamaa zilisema mabomba yatajengwa Gezaulole na sio Ukonga, Mwisho wa Lami. Kwa hiyo unaionea Ukonga ukisema haina hizo huduma. Walipokuja Waskandinavia wakauliza: Geza lole wapi iko, tukawapeleka Gezaulole, sio Ukonga. Ilipangwa iwe hivyo.

Baada ya huu mpango kufutwa na siasa za Nyerere kutupwa mbona hatujajenga hizi huduma huko Kipunguni na Sitaki Shari Ukonga? Angalau wakati wa Nyerere kulikuwa na mabomba ya maji vijijini! Swali zuri. Na mimi nakuuliza: kwani yeye alijenga, au alijengewa? Aliwashawishi Waskandinavia wakatusaidia. Na sisi mbona tusishawishi? Siku hizi tunayaomba mashirika ya Bretton Woods yatusaidie, na hizo huduma leo zinajengwa kwenye vijiji vya hiari.

Ni kwa kiasi gani huduma hizi zimefanikiwa kwenye vijiji vya Nyerere kwa msaada wa Waskandinavia kuliko vya leo vya misaada ya Bretton Woods, sasa hapo ndio tutaombana takwimu!
 
hivi tatizo ni ndoto ya kukaa pamoja katika vijiji vya ujamaa au utekelezaji wa ndoto hizo?.

naomba uniweke wazi kidogo kwa sbabu hapa chini unasema hivi

kwa mujibu wa hii quote ni kwamba na wewe huna pingamizi na vijiji vya ujamaa, ndo maana ungeita wataalamu ili wafanye tathmini au vipi?

sasa unadhani ni tatizo ni ndoto za nyerere za kuwa na vijiji vya ujamaa au tatizo ni jinsi alivyozitekeleza ndot hizo?

Sijui mwenzangu kama umewahi kufika kwenye vijiji vya ujamaa vilivyoanzishwa na mwalimu Nyerere au umevisikia kwenye mbiu ya mikoa aua unavisikia kutoka mahali fulani pasipo kuwa kijiji.

Suala la vijiji halina uhusiano na ndoto ya mwalimu.
Ndoto ya Mwalimu inahusioano na vijiji vya ujamaa.

Vijiji vilikuwako tangu siku nyingi sana. hakuna mtu aliyewahi kuota ndoto kuanzisha vijiji Tanzania wala hakuna mkutano uliowahi kuitishwa wakati wowowte kuanzisha vijiji Tanzania.

Ila kuna mtu mmoja aliwahi kuota ndoto ya kuanzisha Vijiji vya ujamaa katika umbo analo litaka yeye na katika mtindo anaoutaka yeye.

Hapa kuna tatizo moja kubwa.
Kijiji kinatakiwa kuwa na eneo la ukubwa gani?
Mtu mmoja na familia yake wanatakiwa kuwa na eka ngapi?
Katika ndoto ya Mwalimu sioni akiota mambo haya,hivyo ukosekanaji wa sehemu hii muhimu katika ndoto ndiyo mwanzo wa tufani.

Naona mnakimbilia kulaumu utekelezaji. Suala la utekelezaji limeongelewa sana hapa.
Labda nitaomba mnieleweshe kwa undani mna maana gani mkisema kulikuwa na tatizo kwenye utekelezaji?

Kitaalamu kijiji kinajengwa kufuata Blue Print inayozingatia teritory ya eneo husika. hakuna Blue Print ya Kufit vijiji vyote Tanzania.
Kimsingi kijiji ni lazima kizingatia Upatikanaji wa maji ardhi nzuri ya kulima, usalama wa eneo zima( Huwezi jenga kijiji mita 20 kutoka eneo lenye wanyama wakali au njia ya vimbunga)na mambo yote muhimu yanayozingatia asili na utamaduni wa watu wanaojenga hivyo vijiji Maeneo ya matambiko,maziko na hata imani za nguvu zisizoonekana kama mwalimu mwenyewe alivyoainisha kwenye hotuba yake.

Nipeni maandishi yaliyomwagwa na Nyerere au wataalamu wake ya jinsi ya kuhamisha watu kutoka huko waliko na kuwaweka pamoja kuanzisha vijiji vya ujamaa, ili nikisoma huo mpango nikubaliane nanyi kwamba watekelezaji ndiyo waliochemsha.

Kama hakuna maelezo yaliyokamilika yanayoeleza wazi namna ya kuanzisha hivyo vijiji vya ujamaa, wazo kwamba utekelezaji wa ndoto ndiyo uliokuwa mbaya manalitoa wapi?
Mnalinganisha nini na nini kujua kwamba Ndoto ilikuwa sahihi ila utekelezaji ulikuwa mbaya?
Sivyo tukubaliane hapa kwamba ndoto ya mwalimu Nyerere kuhusu vijiji vya ujamaa kama kweli ilikuwa ndoto nzuri ilidokezwa kisha upana wake na urefu wake katika utekelezaji ulibakia ndani ya mawazo ya mwalimu Nyerere hadi kifo chake.
Kwa hiyo ni uzushi kusema ndoto ya mwalimu Nyerere juu ya vijiji vya ujamaa ilikuwa sahihi kwa sababu hakuna mwenye maelezo ya kina zaidi ya mwalimu Nyerere mwenyewe.

Vijiji vilivyoanzishwa na mwalimu Nyerere vilijengwa kwa kuzingatia utaratibu wa miji, sasa kwa sababu hakuna Blue Print mpaka leo sikubaliani kwamba lilikuwa tatizo la utekelezaji.

Utekelezaji wa mpangilio upi??

Sijui Nyrere angepata ushauri kutoka kwa wataalamu wa Demographic sijui wangemwambia nini?

Pendekezo langu la kuomba ushauri wa wataalamu halina uhusiano na kukubalina na vijiji vya ujamaa, pendekezo lina uhusiano na kukubaliana na namna ya kupeleka maendeleo katika vijiji vilivyokuwepo pamoja na watu waliovizunguka vijiji hivyo asilia kwa kiwango kilichoonekana mbali kwa kipimo cha 1962.

Nyerere hakuwa mtaalamu wa Demographic, economics, urban planning, Agriculture, environment, Engineering na hata siasa yenyewe. Lakini kwa kuderive knowledge kutoka katika uwanja wake wa English Literature na uelewa wake aliweza kufanya mambo mengi bila kuomba ushauri fahasa kutoka kwa watu wenye upeo wa mambo hayo.Matokeo yake hakuna haja ya kuyajadiri kila mtu anayafeel.
 
......hatimaye hapa kimyaaaaaaaaa kama pamepigwa bomu! hamna cha fikra wala nini ni upuuzi mtupu!.
mmeshindwa, thanks god sasa mmelegea.

Madela came hard on Nyerere and Mwanakijiji didn't want to engage him...so you make what you make of it...
 
...kobe akiinama kwa muda mrefu anakuwa 'babujinga'!!!

hamna lolote, mmeishiwa tu......wewe unadhani ukimpaka lipsticks na kumvesha highheels na gown nguruwe, jina litabadilika!!?? no way, atabaki kuwa nguruwe tu!!.

Aaaahh na wewe bana...umerudi hapa na mipasho yako....
Ulipoondoka palikuwa na amani bila mipasho...umerudi tu...umeanza tena.
 
Naamini kwa dhati Nyerere aliendelea kuota ndoto yake ya vijiji hadi siku ya kifo chake.
Kile tulicho kiona kikifanyika miaka ya 70 katika vurumai kubwa katika historia ya Tanganyika ya kuswaga watu kama Nyati au pundamilia huku nyumba zao na mashamba yakichomwa moto na mali nyingi kuharibiwa na kuibiwa, ilikuwa ni kukurupuka kwa kisiasa kuliko sababishwa na nia na hamu ya kuhodhi dola na mamlaka yake yote kusiko na uhusiano wala ushabihiano wowote na ndoto ya mwalimu Nyerere.
Maendeleo mengi ya watu waliotawanyika katika Tanganyika huru yalirudishwa miaka 100 nyuma kwa kitendo hicho cha operesheni vijiji kinachohusishwa nandoto ya Mwalimu Nyerere.

Nathubutu kusema ndoto nzima ya mwalimu Nyerere ilikuwa dhambi.

This was wrong and I will be the first one of defenders of Nyerere to fault him for his passive reaction to hold accountable those who created harm to Watanzania during the whole exercise of Vijiji vya Ujamaa.
 
Sijui mwenzangu kama umewahi kufika kwenye vijiji vya ujamaa vilivyoanzishwa na mwalimu Nyerere au umevisikia kwenye mbiu ya mikoa aua unavisikia kutoka mahali fulani pasipo kuwa kijiji.

Suala la vijiji halina uhusiano na ndoto ya mwalimu.
Ndoto ya Mwalimu inahusioano na vijiji vya ujamaa.

Vijiji vilikuwako tangu siku nyingi sana. hakuna mtu aliyewahi kuota ndoto kuanzisha vijiji Tanzania wala hakuna mkutano uliowahi kuitishwa wakati wowowte kuanzisha vijiji Tanzania.

Ila kuna mtu mmoja aliwahi kuota ndoto ya kuanzisha Vijiji vya ujamaa katika umbo analo litaka yeye na katika mtindo anaoutaka yeye.

Hapa kuna tatizo moja kubwa.
Kijiji kinatakiwa kuwa na eneo la ukubwa gani?
Mtu mmoja na familia yake wanatakiwa kuwa na eka ngapi?
Katika ndoto ya Mwalimu sioni akiota mambo haya,hivyo ukosekanaji wa sehemu hii muhimu katika ndoto ndiyo mwanzo wa tufani.

Naona mnakimbilia kulaumu utekelezaji. Suala la utekelezaji limeongelewa sana hapa.
Labda nitaomba mnieleweshe kwa undani mna maana gani mkisema kulikuwa na tatizo kwenye utekelezaji?

Kitaalamu kijiji kinajengwa kufuata Blue Print inayozingatia teritory ya eneo husika. hakuna Blue Print ya Kufit vijiji vyote Tanzania.
Kimsingi kijiji ni lazima kizingatia Upatikanaji wa maji ardhi nzuri ya kulima, usalama wa eneo zima( Huwezi jenga kijiji mita 20 kutoka eneo lenye wanyama wakali au njia ya vimbunga)na mambo yote muhimu yanayozingatia asili na utamaduni wa watu wanaojenga hivyo vijiji Maeneo ya matambiko,maziko na hata imani za nguvu zisizoonekana kama mwalimu mwenyewe alivyoainisha kwenye hotuba yake.

Nipeni maandishi yaliyomwagwa na Nyerere au wataalamu wake ya jinsi ya kuhamisha watu kutoka huko waliko na kuwaweka pamoja kuanzisha vijiji vya ujamaa, ili nikisoma huo mpango nikubaliane nanyi kwamba watekelezaji ndiyo waliochemsha.

Kama hakuna maelezo yaliyokamilika yanayoeleza wazi namna ya kuanzisha hivyo vijiji vya ujamaa, wazo kwamba utekelezaji wa ndoto ndiyo uliokuwa mbaya manalitoa wapi?
Mnalinganisha nini na nini kujua kwamba Ndoto ilikuwa sahihi ila utekelezaji ulikuwa mbaya?
Sivyo tukubaliane hapa kwamba ndoto ya mwalimu Nyerere kuhusu vijiji vya ujamaa kama kweli ilikuwa ndoto nzuri ilidokezwa kisha upana wake na urefu wake katika utekelezaji ulibakia ndani ya mawazo ya mwalimu Nyerere hadi kifo chake.
Kwa hiyo ni uzushi kusema ndoto ya mwalimu Nyerere juu ya vijiji vya ujamaa ilikuwa sahihi kwa sababu hakuna mwenye maelezo ya kina zaidi ya mwalimu Nyerere mwenyewe.

Vijiji vilivyoanzishwa na mwalimu Nyerere vilijengwa kwa kuzingatia utaratibu wa miji, sasa kwa sababu hakuna Blue Print mpaka leo sikubaliani kwamba lilikuwa tatizo la utekelezaji.

Utekelezaji wa mpangilio upi??

Sijui Nyrere angepata ushauri kutoka kwa wataalamu wa Demographic sijui wangemwambia nini?

Pendekezo langu la kuomba ushauri wa wataalamu halina uhusiano na kukubalina na vijiji vya ujamaa, pendekezo lina uhusiano na kukubaliana na namna ya kupeleka maendeleo katika vijiji vilivyokuwepo pamoja na watu waliovizunguka vijiji hivyo asilia kwa kiwango kilichoonekana mbali kwa kipimo cha 1962.

Nyerere hakuwa mtaalamu wa Demographic, economics, urban planning, Agriculture, environment, Engineering na hata siasa yenyewe. Lakini kwa kuderive knowledge kutoka katika uwanja wake wa English Literature na uelewa wake aliweza kufanya mambo mengi bila kuomba ushauri fahasa kutoka kwa watu wenye upeo wa mambo hayo.Matokeo yake hakuna haja ya kuyajadiri kila mtu anayafeel.

Madela,

The intention of Vijiji was not bad, however there was no thorough analysis and study done before bulldozing people in unknown territories.

The question to you today is this; Is there a need to have structured vijiji as you speak? can we leao forward to today and start planning for tomorrow using experience attained from past experience and mistakes?
 
imebaki historia tu, kila mtu anawajibu wa kufanya ili tutoke hapa tulipo. ukitegemea viongozi wafanye utabaki ukilaumu, maana hawatendi wanayoahidi. Akili kichwani, Play your party every thing is possible under the sun.
 
Mkuu heshima mbele, wewe ziweke hapa tuzichambue ukweli nitakubali, lakini ninataka kuwaonyesha wananchi kwamba hatuko hapa tumedumaa as a nation kwa bahati mbaya, na sababu nyingi za msingi zinapatikana kwenye maneno na fikra za Mwalimu,

Yes yanayotukuta sasa, mengi ni uzembe wetu wenyewe kibin-adam, as a nation, lakini kisiasa ni lazima kuwe na someone to point a fingure at,

Otherwise, mkuu ahsante kwa finally, kukubali kuwa Mwalimu alikuwa bin-adam kama sisi, alikuwa na mapungufu makubwa ambayo baadhi yake ndio yametufikisha tulipo as a nation. I am more than happy kukata ishus kama utaweka maneno maneno moja baada ya lingine ya Mwalimu, hapa tuyachambue kulingana na mazuri yetu kitaifa na mabaya yetu.

Ahsante.

Mkuu,

zNahisi kama vile kauli zako (hapo juu) umezitoa akilini na mdomoni mwangu!
Especially unaposema "alikuwa na mapungufu makubwa ambayo baadhi yake ndio yametufikisha tulipo as a nation."

Respect!
 
Nyerere he was a great thinker jaman,tukubali au tukatae,ukiangalia hata katika malengo ya MDG ye aliyasema hayo toka enzi za miaka ya sitin,ila kwa vile si ni vichwa ngum tukapuuzia,leo IMF na WORLD BANK ndo tunawaona ka wakombozi kumbe ni bule si lolote. Ideas zake zitaishi milele.
 
Hey just compare the advantages and disadvantages of both capitalists and ujamaa then think twice.
 
hizo fikra ziwekewe thread yake pekee kwa ajili ya kusomwa tu wala kusiwe na posts. zitachanganya. ni maoni yangu
 
Back
Top Bottom