Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,710
- 40,777
Waswahili ndio waliosema kuwa "kwanini tuandikie mate wakati wino upo" na ndio hao hao waliosema "kwanini tugonganishe mawe, wakati kibiriti kipo" (well that is my own saying). Nimekuwa nikidai mara nyingi pasipo hofu kuwa Fikra za Mwalimu zikiangaliwa upya zinaweza kutuonesha mwanga wa wapi tunataka kwenda. Mara nyingi hata hivyo kuna watu ambao wanapinga fikra hizo (hata kama hawazijui) na kutoa madai lukuki juu ya "mwalimu alisema nini".
Ni kwa sababu hiyo basi nimeona nianze pole pole kwa kuweka mawazo ya Mwalimu na nimeyatoa wapi ili wale wanaozipinga waseme mawazo hayo yana makosa gani, na kama wanakubali basi tuendelee na mawazo mengine.
Lengo ni kujaribu kuonesha kuwa mtu akichukua muda kujifunza alichosema Mwalimu basi anaweza akajikuta yeye tayari ni mfuasi wa fikra za Mwalimu. Katika kufanya hivi nitoe maangalizi ya mambo ambayo ni ya kuzingatia.
a. Katika hoja zangu zote za utetezi wa Mwalimu na fikra zake sijawahi kusema kuwa Nyerere hakuwahi kufanya makosa au hakutambua makosa. Mara zote nimeonesha na mifano kuwa yeye mwenyewe alijua baadhi ya makosa yake na alikuwa tayari kukiri hivyo.
b. Katika utetezi wangu wa Mwalimu na fikra zake nyingi nimekuwa nikionesha kuwa Nyerere kama wanadamu wengine alikuwa na mapungufu yake na nitakuwa mwongo na mzandiki nikidai kuwa Nyerere hakufanya kosa hata moja wakati wa utawala wake. Hivyo, sifuati mafundisho ya Mwalimu nikiwa kama kipofu.
c. Katika kuonesha fikra ninazokubaliana naye haina maana ninakubaliana na maamuzi yote yaliyotokana na fikra hizo au njia zote zilizotumika kutekeleza fikra hizo. Hivyo, kukubaliana na fikra fulani haina maana nakubaliana na vitendo au maamuzi yaliyofuata, ninachokubaliana ni ile principle kuwa fikra hizo zinaweza kutekelezwa kwa namna mbalimbali na zikaendelea kubakia kuwa kweli.
d. Mawazo ya Mwalimu ni mawazo ya kifalsafa zaidi na kimtazamo ingawa baadhi yao hayakutekelezeka au hayakuongoza utekelezaji wa sera fulani. Hata hivyo ninaamini kuwa fikra zake bado zinahitajika leo hii kama kweli tunataka kujenga Taifa lililoendelea kwelikweli.
e. Mwisho, na nyie leteni fikra za Mwalimu na mziseme ni zipi na mnipe changamoto kama nakubaliana nazo au la. Nawaahidi kuwa mkileta jambo ambalo lilikuwa ni mawazo au fikra ya Mwalimu na likaonekana kweli hapo Mwalimu alipotoka basi kwa pamoja tutalitupilia mbali. Lakini pia nikiwaonesha kuwa fikra au mawazo fulani ni sahihi ni jukumu lenu pia kukubali kuwa ni jambo zuri na linapaswa kuzingatiwa. Huo unaitwa uungwana.
NB: Fikra za Mwalimu - mkusanyiko wa maoni, hoja, mitazamo, mawazo, ya aliyekuwa Rais wa Kwanza wa Jamhuri ya Muungano Mwl. Julius Kambarage Nyerere ambayo yalitolewa tangu kuingia kwake kwenye siasa za Tanganyika (Tanzania) na za kimataifa hadi alipofariki Oktoba 14, 1999. Fikra hizo zinaweza kuonekana katika hotuba, maandishi, mahojiano, vitabu, na nyaraka mbalimbali alinukuliwa.
Katika hili nyaraka za sera ambazo zilipitishwa na mtu zaidi ya mmoja kama (Azimio la Arusha, Mwongozo wa TANU na ule wa CCM, n.k)sitovihesabu kama fikra za Mwalimu hata kama zinakubaliana na mawazo yake.
Mko tayari?