Fikra za Mwalimu: Hizi hapa.. mzikubali au mzipinge!

Fikra za Mwalimu: Hizi hapa.. mzikubali au mzipinge!

Jokakuu,
Mkuu samahani jibu lake umelisema wewe mwenyewe!..
Kwanza umesema Muingereza haku INVEST, Tanzania kwa sababu tanzania haikuwa koloni lake, sawa -
Sasa jiulize kama hakuweka investment zake nchini hayo mabenki na mashamba yao yalikuwa ya kitu gani?...

Umezungumzia pia kama Nyerere alikuwa good steward wa uchumi Mwinyi asingekuta nchi iko taabani kiasi hicho!... Huyu Mwinyi alikuwa wapi?.. sii ndio hao hao viongozi wenyewe waliotupeleka hapo ama naye kesha dai aliburuzwa!. Chama ni hicho hicho, sera zilezile isipokuwa tofauti ilikuwa mbinu za kiuchumi ambazo mwalimu Nyerere mwenyewe ndiye aliyezitangaza mwaka July 1984 kabla hajaondoka, Mwinyi alikuwa mtekelezaji tu wa sera za CCM.

Tunachozungumzia ni mabadiliko ya Malengo na dira yetu kitaifa kama alivyokusudia mwalimu...Na hakufanya hivyo (kufungua milango ya kiuchumi) kwa sababu ya kupindisha safari yetu isipokuwa mbinu za kufikia huko. Hata kina Mtei hapo nyuma walichompinga mwalimu ni mbinu za ku deal na mataifa makubwa kiuchumi ..UBEPARI..
Tatizo kubwa la mwalimu na Ubepari kama nilivyokwisha zungumza hapo nyuma ni kwamba Tanzania haikuwa na matajiri wazalendo wenye uwezo wa kuwekesha.. Hivyo utaanzia wapi na Ubepari?..Hao wageni wenyewe walikuwa hawawekeshi ktk miradi ya kudumu waswahili wanasema mguu mmoja nje, hivyo ulikuwa unyonyaji mtupu tofauti na wakoloni waliokuwa Kenya ama Zimbabwe...
Hakuna hata mtu mmoja aliyeweza kumpa solution mwalimu zaidi ya hali halisi ichukue mkondo wake ndani ya Ubepari..He was the President hawezi kukaa na kuacha Mungu atupeleke kama Haiti aambao walipata Uhuru miaka 200 iliyopita wakawa Mabepari hali wazalendo hawana kitu...wakowapi.. nani kisha invest huko kitu cha maana.. hakuna! Wamebaki maskini miaka yote 200 pamoja na Ubepari wao! Jamani kumbukeni mwalimu alipochukua nchi sisi na Haiti tulikuwa kapu moja!...msifanye mchezo...

Hata walichokiona kina Mtei ni ubaya wa UJAMAA wakayafumbia macho mabaya ya Ubepari na Mwalimu alichokiona ni Ubaya wa UBEPARI akayafumbia macho mabaya ya Ujamaa..
Kwa hiyo mkuu wangu nitarudia kuisema kwamba huwezi kuendelea kiuchumi kama nchi yako haiwezi timiza mikondo mitatu ya ufanisi ktk uchumi, hii ndiyo Nyerere alijaribu kuijenga.. He failed yes, lakini hata ukimwita Mchumi yeyote atakwambia hizo njia tatu ni muhimu kwa nchi kupata maendeleo ya kiuchumi..
leo hii pamoja na kuacha mwongozo wa mwalimu, tumeshindwa yote.. tumeshindwa kuzalisha, hatuna viwanda na tuna service mali za nje kiasi kwamba hata raia wetu wenyewe wana account zao nje ya nchi kuliko ndani..hakuna mahala pa kui nvest isipokuwa ktk services na product zote zinatoka nje, hivyo ni bora kuziweka fedha nje ambako ni rahisi kufanya transfer ya fedha..Nchi kama Switzeland zimetajirika kwa kutumia services kama hizi as a matter of fact kama sikosei nakumbuka Idd Simmba aliwahi kuandika kwamba Benki zote nchini zina account kama millioni 2 tu, nchi yenye population karibia millioni 40...huoni tatizo hapa.
Sasa mkuu ikiwa sisi hapa tunaweza kuyaona haya ndizo Fikra tunazozungumzia, hivi sasa hakuna kiongozi anayetazama upande huo.. hakuna kiongozi anayeweza kusema tanzania ya kesho baada ya madini itakuwa vipi kiuchumi hata kama atakosea lakini atupe mwanga -hakuna. Tunaelekea wapi kiuchumi?... hawafaham,u na majuzi umemsikia Gavana akisema karne 4 nyingine tena basi ikiwa uchumi wetu utaendelea kukua kwa asilimia 7.. hayo madini yanakwisha miaka 15 ijayo kwa kasi za Barricks!.. what next...
Hizi ndizo FIKRA mkuu wangu, mtu yeyote ambaye ataweza kutuandaa sisi kukabiliana na hayo ya mbele hata kama njiani atashindwa kama walivyoshindwa kina MLK, hizo fikra zinaweza kuendelezwa na kizazi kinachofuata... tanzania tumepoteza kabisa malengo, dira na leo hii asilimi 80 ya wananchi hatufahamu tunakwenda wapi isipokuwa darasa kubwa ni kutafuta uwezo wa kuweka chakula mezani kila kukicha..
 
Mkandara,

..labda nirekebishe kwamba Muingereza haku-invest hapa kulinganisha na alivyo-invest Kenya na Uganda.

..samahani, kama kauli yangu ilikupotosha ukafikiri kwamba Muingereza made ZERO investments in Tanganyika.

..hoja yangu ni kwamba kulikuwa na mapori mengi tu ambayo Mwalimu angeweza kusafisha na kuanzisha mashamba ya mkonge, chai, pareto etc.

..tatizo linakuja pale alipoamua kutaifisha mali/mashamba wakati hana utaalamu wa kuyaendesha.

..matokeo ya hatua hizo ni kuanguka kwa uzalishaji wa mkonge etc etc.

..maamuzi ya Mwalimu yalimuweka ktk nafasi ambayo, strategically, he had no where to fall back pale matatizo yalipotokea.

..tatizo haliko ktk FIKRA, tatizo liko katika utekelezaji wa fikra hizo.

..tatizo haliko ktk malengo, tatizo liko ktk mikakati ya utekelezaji ya kufikia malengo.

..Mwalimu alikuwa na fikra maridadi kweli kweli. Ni nani asiyetaka kuishi ktk jamii iliyo na HAKI na USAWA? problems arose when he tried to fix things that were not broken.

NB:

..ili tuendelee hatupaswi kujilinganisha na wale wanaofanya vibaya kama Haiti na Somalia.

..labda tujilinganishe na kina Seycheles,Mauritius,Malaysia etc etc ambao walikuwa na hali kama yetu miaka ya 1980.

..How did they manage to make economic progress? Why cant we emulate them?
 
Jokakuu,

Tatizo sio mapori tatizo ni kueleawa mipaka ya nyumba yako.. Hawa Waingereza hawakuwa - Kwanza, raia wa Tanzania, pili mashamba waliyokuwa nayo hayakuwa ni ardhi yao (Mugabe's rule), kama vile leo nije nijenge kibanda cha uani ktk kiwanja chako tofauti na Mzungu aliyeko Zimbabwe ambaye mwenyewe alikuwa Mzimbabwe acha mbali rangi yake ama South na hata Kenya wenye mashamba yale wengi wao wamekufa pale na kizazi chao kinaendelea....
Hivyo basi naposema mwananchi mzalendo ni pamoja na rangi zote kuwa hakuna aliyekuwa na uwezo wa kuwekesha.. hayo Ma- benki mkuu, ktk uwanja wa biashara inaruhusiwa mashindano lakini sio huna kabisa benki ila unategemea za nje...jambo ambalo kama unakumbuka nililipinga kule Bcstimes tulipo binafsisha benki zetu. Nikasema haiwezekani nchi ikawa inategemea Benki za nje hata kidogo hakuna nchi inayofanya hivyo isipokuwa Tanzania tu.. mwisho wa yote tumerudi wapi?... hizi ndio fikra mkuu vision ya kutoona mbele ndicho kilema cha uongozi huu...
Come on now, yaani unachojaribu kusema ni kwamba huoni kosa kuwa na mke (nchi) wajomba wanajifua...hiki ndicho alichokataa mwalimu basi.

Tofauti kubwa ambayo wengi mnashindwa kuitazama kwamba hatukuwa na wawekeshaji. hao wote walikuwa na mguu mmoja nje kwa nini tusitaifishe mali zao ikiwa wao bado wanaendesha biashara kwa sheria za Queen..
Mkuu, baada ya uhuru hata mahotel makubwa ya wazungu tulikuwa bado haturuhusiwi ngozi ya tako nakumbuka kuna kisa kimoja mayor wa kwanza wa jiji letu aliwahi tolewa nje juu juu kisa ngozi ya tako! kesho yake mwalimu alitaifisha hotel hiyo...

Kisha swala la kujilinganisha na haiti ni swala linalotokana na fikra za mwalimu wakati ule.. haya ya Seycheles, Mauritius ni maswala ya sasa hivi ambayo sina kabisa matatizo nayo isipokuwa mnapotaka turudishe historia yetu nyuma na msitumie vigezo vya nchi hizo hizo ambazo pia zilikuwa na matatizo ya kiuchumi kama sisi lakini wao wameweza kufungua kitabu kipya cha mbinu mpya bila kutoa lawama kwa viongozi wao waliowapa Uhuru...
Tunachofanya sisi ni sawa na mtu kumlaumu baba na mama yako kukuzaa kwa sababu ya matatizo ulokuwa nayo hali ni wewe mwenyewe unaye face dunia hii... hao wazazi wapo kaburini na hawakukuzaa ukiwa na kilema wala punguani. Hivyo tukizungumzia Malaysia tuzungumzie kina Mkapa na JK sio Nyerere kwani walioleta mabadiliko huko sio walioutafuta Uhuru.
This is my point!
 
Sio hatari!

Kazibure alishafariki. Shuruba yote ile ya Mchonga mwanangu angeishi maisha marefu?

Mwanangu ulikuwa kwenye mu Ivy League wa kuitwa Ilboru siyo? Si utani kichaa! Inawezekana we mwanangu wa karibu. Sasa sikia, hebu tutoke nje mwanangu, nitumie kipeperushi, tulonge mipango ya kutafuta hela mtu wangu, badala ya kubishana na wana vijiji wamekunywa maji ya bendera ukiwauliza kwa nini unampenda Nyerere wanasema kwa sababu yeye kasema yeye ndiye yule ajae. Wabishi kama ibilisi!

Nina mi-document ya watu wameteswa kuliko Kazibure. Ngoja niwawekee wenye misuli wasome!

Hii story inafanana na zile wanazotoa hapa watanzania na wakenya wanaotaka hifadhi ya ukimbizi Amerika ili wawe na status. Wengi husema mengi ikiwemo mama mmoja wa miaka 55 aliyesema kuwa huko kwao Dodoma analazimishwa kukeketwa (kazi anayodai inafanywa na serikali ya Kikwete ya kiislam).

Ukitaka story za hivi mbona utazipata nyingi sana!
 
Naomba nibandike hiki kisehemu cha Azimio la Arusha kusaidia baadhi ya majadiliano humu kuhusu Fikra za Mwalimu Nyerere. Nafikiri hili litasaidia sana kwa wale ambao wamelisikia Azimio na sifa zake lakin hawajawahi kukaa chini na kulisoma.

Fedha kutoka nje ya Tanzania, Je?

Njia moja tunayotumia kujaribu kuepukana na lazima hii ya kukiri
kodi zaidi ikiwa twataka fedha zaidi ni kutilia sana mkazo fedha za
kutoka nje ya Tanzania. Fedha hizi za kutoka nje ni za aina tatu:-
(a) Zawadi: Yaani Serikali ya nje iipe Serikali yetu fedha za bure
tu kama sadaka kwa ajili ya mpango fulani wa maendeleo.
Wakati mwingine shirika lo lote la nje liipe Serikali yetu au
Shirika jingine katika nchi yetu msaada fulani kwa ajili ya
maendeleo.
(b) Mkopo: Sehemu kubwa ya fedha tunazotazamia kupata
kutoka nchi za kigeni si zawadi au sadaka, bali ni mkopo.
Serikali ya nje au Shirika la nje, kama vile Benki, hukopesha
Serikali yetu fedha fulani kwa ajili ya kazi zetu za
maendeleo. Mkopo huu huwa una masharti yake ya kulipa,
kama vile muda wa kulipa, na kima cha faida.
(c) Raslimali ya Kibiashara: Aina ya tatu ambayo pia ni kubwa
kuliko ya kwanza, ni ile ya fedha za watu au makampuni
yanayotaka kuja katika nchi yetu kuanzisha shughuli mbali
mbali za uchumi kwa manufaa yao wenyewe. Na sharti
kubwa walitakalo jamaa hawa wenye fedha zao ni kwamba
shughuli yenyewe iwe ni ya faida – kwao – na pia kwamba
Serikali iwaruhusu kuondoa faida hiyo Tanzania na kuipeleka
kwao. Hupenda pia kwa jumla Serikali iwe na siasa
wanayokubaliana nayo au ambayo haihatarishi uchumi wao.

Hizo ndizo njia tatu kubwa za kupata fedha kutoka nje ya
nchi yetu. Kuna mazungumzo mengi ajabu juu ya jambo hili
la kupata fedha kutoka nchi za kigeni. Serikali yetu na
viongozi wetu wa makundi mbalimbali hawaachi kufikiria njia
za kupata fedha kutoka nje. Na tukizipata au japo tukipata
ahadi tu ya kuzipata mara magazeti yetu, au radio zetu na
viongozi wetu hutangaza jambo hilo ili kila mtu ajue kuwa
neema imekuja au iko njiani inakuja. Tukipata msaada
hutangaza; tukipata mkopo hutangaza; tukipata kiwanda
kipya hutangaza; tukiahidiwa msaada, mkopo au kiwanda
kipya hutangaza. Japo tukianza mazungumzo tu na nchi au

shirika la kigeni juu ya msaada, mkopo au kiwanda, mara
hutangaza japo hatuna hakika ya matokeo ya mazungumzo
hayo. Na kisa? Ni kuwajulisha wananchi kwamba, tunaanza
mazungumzo ya neema!

TUSITEGEMEE FEDHA KULETA MAENDELEO

Ni jambo la kijinga kuchagua fedha kuwa ndiyo chombo chetu
kikubwa cha maendeleo na hali tunajua kuwa nchi yetu ni maskini.
Ni ujinga vile vile, kwa kweli ni ujinga zaidi, tukidhani kuwa tunaweza
kuondoa hali hii ya unyonge wetu kwa kutegemea fedha za kutoka
nje badala ya fedha zetu wenyewe. Ni ujinga kwa sababu mbili.
Kwanza, hatuwezi kuzipata. Ni kweli kwamba zipo nchi ambazo
zaweza na zapenda kutusaidia. Lakini hakuna nchi moja duniani
ambayo iko tayari kutupa misaada au mikopo au kuja kujenga
viwanda katika nchi yetu kutimiza shabaha zake zote za maendeleo.
Nchi zenye dhiki ni nyingi sana duniani. Na hata kama nchi zote
zenye neema zingekubali kuzisaidia nchi zenye dhiki, bado ingekuwa
msaada huo hautoshi. Lakini nchi zenye neema hazitakubali. Hata
katika nchi ile ile, matajiri huwa hawatoi fedha zao kwa hiari ili
zisaidie Serikali kuondoa dhiki.

Njia ya kuzipata fedha za matajiri ili zisaidie umma ni kuwatoza
kodi wakipenda wasipende. Hata hivyo huwa hazitoshi. Ndiyo
maana japo tungewakamua vipi wnanachi na wakazi wa Tanzania,
matajiri na maskini, hatuwezi kupata fedha za kutosha kutimiza
mipango yetu ya maendeleo. Wala duniani hakuna Serikali ambayo
yaweza kuyatoza kodi mataifa yenye neema, yakipenda yasipende, ili
kusaidia mataifa yenye dhiki. Hata hizo zisingelitosha. Hakuna
Serikali ya Dunia nzima. Fedha ambazo nchi zenye neema hutoa
huwa kwa wema wao, au hiari yao au kwa manufaa yao wenyewe.
Haiwezekani basi, tupate fedha za ktuosha kwa njia hiyo.

MISAADA NA MIKOPO VITAHATARISHA UHURU WETU
Pili, japo kama tungeweza kuzipata; hivyo ndivyo tunavyotaka
kweli? Kujitawala ni kujitegemea. Kujitawala kwa kweli
hakuwezekani ikiwa Taifa moja linategemea misaada na mikopo ya
Taifa jingine kwa maendeleo yake. Hata kama pangetokea Taifa au
mataifa ambayo yako tayari kutupa fedha zote tunazohitaji
kuendesha mipango yetu ya maendeleo isingekuwa sawa kwa nchi
yetu kuipokea misaada hiyo bila kujiuliza matokeo yake yatakuwa nini
kwa Uhuru wetu na uzima wetu.

Msaada ambao ni kama chombo cha kuongeza juhudi, au
nyenzo ya juhudi, ni msaada ambao una manufaa. Lakini msaada
unaoweza ukawa sumu ya juhudi si msaada wa kupokea bila kujiuliza
maswali.

Kadhalika mikopo. Kweli mkopo ni bora kuliko misaada ya
“bure”. Mkopo nia yake ni kuongeza jitihada au kuifanya jitihada
itoe matunda mengi zaidi. Sharti moja la mkopo huwa ni kuonyesha
jinsi utavyoweza kuulipa. Maana yake ni kwamba sharti uonyeshe
kuwa unakusudia kuufanyia kazi itakayoleta manufaa ya
kukuwezesha kuulipa.

Lakini hata mikopo ina kikomo. Sharti upime uwezo wa kulipa.
Tunapokopa fedha kutoka nje mlipaji ni Mtanzania. Na kama
tulivyokwisha sema Watanzania ni watu maskini. Kuwabebesha watu
maskini mikopo ambayo inawazidi kimo si kuwasaidia bali ni
kuwaumiza. Na hasa inapokuwa, mikopo hiyo ambayo wanatakiwa
walipe haikuwafaidia wao, bali ilifaidia watu wachache tu.
Na Viwanda vya wenye raslimali zao je? Ni kweli tunavitaka.
Hata tumepitisha katika Bunge sheria ya kulinda raslimali ya wageni
wanaoanzisha mipango mbali mbali ya uchumi katika nchi yetu. Nia
yetu na matumaini yetu ni kuwafanya waone kuwa Tanzania ni nchi
inayofaa kuingiza raslimali zao. Kwani raslimali yao itakuwa salama
italeta faida. Na faida hiyo wenyewe wataweza kuiondoa bila
vipangimizi. Tunayo matumaini ya kupata fedha za maendeleo mbali
mbali kwa njia hii. Lakini hatuwezi kupata za kutosha. Lakini hata
kama tungeweza kuwaridhika kabisa Wageni hao na Makampuni
hayo mpaka yakubali kuanzisha mipango yote ya uchumi tunayohitaji
katika nchi yetu, hivyo ndivyo tunavyotaka kweli?
Kama tungeweza kushawishi wenye raslimai wa kutosha kutoka
Amerika, na Ulaya kuja kwetu na kuanzisha Viwanda vyote, na
mipango mingine yote ya uchumi tunayohitaji katika nchi hii, hivi
kweli tungekubali bila kujiuliza maswali? Tungekubali kweli kuacha
uchumi wetu wote uwe mikononi mwa wageni kwa ajili ya kupata
faida na kuipeleka katika nchi zao? Hata kama wasingedai
kuhamisha faida na kupeleka makwao, bali faida yote watakayopata
wataitumia hapa hapa Tanzania kwa maendeleo zaidi. Hivi kweli
tungekubali jambo hili bila kujiuliza hasara zake kwa Taifa letu? Huu
Ujamaa tunaosema kuwa ndiyo shabaha yetu tungeujengaje?
Twawezaje kutegemea nchi za nje na Kampuni za nje kwa
misaada na mikopo na raslimali kwa maendeleo yetu bila kuhatarisha
uhuru wetu? Waingereza wana methali isimayo “Amlipaye mwimbaji
ndiye huchagua wimbo”. Tutawezaje kutegemea nchi za kigeni na
Makampuni ya kigeni kwa sehemu kubwa ya maendeleo yetu bila
kuzipa nchi hizo na makampuni hayo sehemu kubwa ya uhuru wetu
wa kutenda tupendavyo. Ukweli wenyewe ni kwamba hatuwezi.
Tukariri basi. Tumefanya makosa kuchagua fedha, kitu
ambacho hatuna, kiwe ndicho chombo kikubwa cha mipango yetu ya
maendeleo. Tunafanya makosa kudhani kuwa tutapata fedha kutoka
nchi za kigeni. Kwanza, kwa sababu kwa kweli hatuwezi kupata
fedha za kutosha kwa maendeleo yetu. Na pili, hata kama
tungeweza, huko kutegemea wengine kungehatarisha uhuru wetu na
siasa nyingine za nchi yetu.

TUMEKAZANIA MNO VIWANDA
Kwa sababu ya kutilia mkazo fedha tumefanya kosa kubwa la
pili. Tumekazania mno viwanda. Kama vile tulivyosema “Bila Fedha
hakuna maendeleo,” ni kama twasema pia “Viwanda ndiyo
maendeleo. Bila viwanda hakuna maendeleo”. Hii ni kweli siku
tutakapokuwa na fedha nyingi, tutaweza kusema kwamba
tumeendelea. Tutaweza kusema, “tulipoanza mipango yetu tulikuwa
hatuna fedha za kutosha na upungufu huu wa fedha ulitupunguzia
nguvu za kuendesha maendeleo yetu haraka zaidi. Lakini leo
tumeendelea na tunazo fedha za kutosha”. Tumeendelea,kwa hiyo,
tunazo fedha za kutosha”. Yaani fedha zetu zitakuwa zimeletwa na
maendeleo.
Kadhalika siku tutakapokuwa na viwanda tuna haki ya kusema
kuwa tumeendelea. Maendeleo yatakuwa yametuwezesha kupata
viwanda. Kosa tunalofanya ni kudhani kwamba maendeleo yetu
yataanza kwa viwanda. Ni kosa maana hatuna uwezo wa kuanzisha
viwanda vingi vya kisasa katika nchi yetu. Hatuna fedha
zinazohitajiwa na hatuna ufundi unaohitajiwa. Haitoshi kusema kuwa
tutakopa fedha na kuazima mafundi kutoka nje kuja kuanzisha
viwanda hivyo. Kosa hili jibu lake ni lile lile kwamba hatuwezi kupata
fedha za kutosha na kuazima mafundi wa kutosha kutuanzishia
viwanda hivyo tunavyotaka. Na pia kwamba hata kama tungeweza
kupata msaada huo kuutegemea huko kunaweza kukapotosha siasa
yetu ya Ujamaa. Siasa ya kualika msululu wa mabepari kuja kuhozi
viwanda katika nchi yetu ingefanikiwa kutupatia viwanda vyote
tunavyotaka, basi ingefanikiwa pia kuzuia maendeleo ya Ujamaa. Ila
labda tuwe tunaamini kwamba bila kujenga ubepari kwanza hatuwezi
kujenga Ujamaa.

TUMJALI ZAIDI MKULIMA VIJIJINI
Vile vile mkazo wa fedha na wa viwanda unatufanya tukazanie
zaidi maendeleo ya mijini. Tunatambua kuwa hatuwezi kupata fedha
za kutosha kuleta maendeleo katika kila kijiji na ambayo yatamfaa
kila mwananchi. Tunajua pia kuwa hatuwezi kujenga kiwanda katika
kila kijiji ili kisaidie kuleta maendeleo ya fedha na viwanda katika kila
kijiji; jambo ambalo tunajua kuwa haliwezekani. Kwa ajili hiyo, basi,
fedha zetu huzitumia zaidi katika miji na viwanda vyetu pia hujengwa
katika miji.

Na zaidi ya fedha hizi huwa ni mikopo. Japo zijenge shule,
hospitali, majumba au viwanda ni fedha za mikopo. Hatimaye lazima
zilipwe. Lakini ni dhahiri kwamba haziwezi kulipwa kwa fedha
zinazotokana na maendeleo ya mijini au maendeleo ya viwanda.
Hazina budi zilipwe kwa fedha tunazopata kutokana na vitu
tunavyouza katika nchi za nje. Kutokana na viwanda vyetu hatuuzi
na kwa muda mrefu sana hatutauza vitu vingi katika nchi za nje.
Viwanda vyetu zaidi ni vya kutusaidia kupata vitu hapa hapa
ambavyo mpaka sasa tunaviagiza kutoka nchi za nje. Itapita miaka
mingi kabla ya kuweza kuuza katika nchi za nje vitu vinavyotokana na
viwanda vyetu.

Kwa hiyo ni dhahiri kwamba fedha tutakazotumia kulipa madeni
haya ya mikopo ya fedha kwa maendeleo na viwanda mijini
hazitatoka mijini na wala hazitatokana na viwanda. Zitatoka wapi,
basi? Zitatoka vijijini na zitatokana na KILIMO. Maana ya ukweli huu
ni nini? Ni kwamba wale wanaofaidi maendeleo yanayotokana na
fedha tunazokopa sio kwa kweli watakaozilipa. Fedha zitatumika
zaidi katika miji lakini walipaji watakuwa zaidi ni wakulima.
Jambo hili linafaa kukumbukwa sana, maana kuna njia nyingi
za kunyonyana. Tusisahau hata kidogo kwamba wakaaji wa mijini
wanaweza wakawa wanyonyaji wa jasho la wakulima wa vijijini.
Hospitali zetu kubwa zote ziko katika miji. Zinafaidia sehemu ndogo
sana ya wananchi wa Tanzania. Lakini kama tumezijenga kwa fedha
za mkopo walipaji wa mkopo huo ni wakulima, yaani wale ambao
hawafaidiwi sana na hospitali hizo. Mabarabara ya lami yako katika
miji, kwa faida ya wakaaji wa mijini na hasa wenye magari. Kama
mabarabaraba hayo tumeyajenga kwa fedha za mikopo walipaji ni
wakulima; na fedha zilizonunua magari yenyewe zilitokana na mazao
ya wakulima. Taa za umeme, maji ya mabomba, mahoteli na
maendeleo mengine yote ya kisasa yako zaidi katika miji. Karibu
yote yametokana na fedha za mikopo na karibu yote hayana faida
kubwa kwa mkulima, lakini yatalipwa kwa fedha zitakazotokana na
jasho la mkulima. Tusisahau jambo hili.

Japo tunapotaja unyonyaji hufikiria mabepari, tusisahau kuwa
bahari ina samaki wengi. Nao hutafunana. Mkubwa hutafuna mdogo
na mdogo naye humtafuna mdogo zaidi. Katika nchi yetu twaweza
kugawa wananchi kwa njia mbili. Mabepari na Makabaila upande
mmoja; na wafanya kazi na wakulima upande mwingine. Pia
twaweza tukagawa wakaaji wa mijini upande mmoja na wakulima wa
vijijini upande mwingine. Tusipoangalia tutakuja kugundua kuwa
wakaaji wa mijini nao ni wanyonyaji wa wakulima.
 


WACHUMI WA NJE (YA SERIKALI, SIO LAZIMA WAZUNGU) HAWAKUBALIANI NA MAELEZO YA NYERERE
Unpublished figures, compiled by Scandanavian and Western embassies, however, show a different picture. According to one such analysis, whose authors requested anonymity, the losses incurred by Tanzania because of falling agricultural output are more than double those created by high oil prices. Another analysis, noting that ''the future is ominous,'' said that, even if Tanzania received all of its oil free, there would still be a huge gap between imports and its exports of agricultural commodities, mainly coffee.
...Professor Simon Mblinye, the President's economic adviser, said in a recent interview, ''We moved to the socialist approach and then we created institutions, and maybe we were overzealous in creating institutions.'' Lack of Experience Cited
''There are too many for the quality and quantity of the people we can generate to run them,'' he said. ''We created 300 parastatals in 10 years. You cannot do this in 10, 20 years of independence. There is a lack of experience. Most of the executives are young and they need leadership.''
...The country's Vice President, Aboud Jumbe, who is the leader of Zanzibar, a part of Tanzania with control over its own economy, has ordered a $5 million executive jet to wing his way from the island to the mainland, a 10-minute flight.[/COLOR]


sasa kama hizi ni data basi tunakazi!! angalia maneno niliyoyabold..
 
ndugu zangu,

..hivi kulikuwa na ulazima gani wa kutaifisha mashamba ya mkonge, chai, pareto etc? kwanini hatukuanzisha yetu wenyewe kuongezea na yale yaliyokuwepo?

..kulikuwa na ulazima gani wa kutaifisha mabenki binafsi, na za ushirika, pamoja na viwanda? kwanini tusianzishe zetu wenyewe za umma?

..Mwingireza haku-invest Tanganyika kwasababu hatukuwa koloni lake. Kwa msingi huo kulikuwa na maeneo mengi ambayo serikali ingeweza ku-invest bila kulazimika kutaifisha mali, wether zilikuwa za binafsi au ushirika.

..jamani kama Mwalimu alikuwa a good steward wa uchumi, Mzee Mwinyi asingekuta nchi na wananchi tuko taabani kiasi kile.

..Mwalimu amefanya mengi mazuri. lakini legacy yake imetiwa doa baya na jinsi alivyo-respond kwa economic challenges za utawala wake.



NB:

..ile article ya NYT inayom-quote Prof.Mbilinyi ni ya kuangaliwa kwa umakini zaidi. siyo vizuri kuipuuza moja kwa moja.

Alafu tunasema alikuwa na uwezo wa kuona mbali lakini hatuambiwi angeweza kuona umbali gani. kama aliweza kuona mbali kwanini hakuweza kuona madhara ambayo yalitokana na plans zake?

anyway i still believe that he failed in many things.
 
Alafu tunasema alikuwa na uwezo wa kuona mbali lakini hatuambiwi angeweza kuona umbali gani. kama aliweza kuona mbali kwanini hakuweza kuona madhara ambayo yalitokana na plans zake?

anyway i still believe that he failed in many things.

mbona unasema lililokwisha semwa?
 
Hii ni sehemu ya hotuba ya Baba wa Taifa akihutubia Bunge Disemba 10, 1962. Hii ilikuwa ni siku moja baada ya Tanzania kuwa Jamhuri. Msisitizo wote wangu.

The Reasoning on Establishment of Proper Villages:

To build this country we have to make many changes. And in order to change it we must be willing to try what is new. It is useless to long for the good things of today if we are not prepared to change the habits of the past which prevent our making of the means to achieve those good things. I shall take this opportunity, then, to deal with one aspect of our traditional way of life which we shall have to alter very quickly during the next few years.

The population this country is about en million. Of that ten million not more than 250,000 to 300.000 live in the towns. All the rest work on the land. Which is to say that Tanzania is, in fact, a country of peasant farmers. We have proportionately very few wage-earners. For this reason in drawing up our three years Development Plan, Government decided to lay the greatest emphasis on agriculture.

It is ridiculous to concentrate on agriculture if we are not going to make any change in our old methods of cultivation and our old ways of living. If we want to develop, we have no choice but to bring both our way of living and our way of farming up to date. The hand-hoe will not bring us the things we need today.

Very often it has not even sufficed to bring us enough to eat. We have got to begin using the plough and the tractor instead. But our people do not have enough money, and nor has the Government, to provide each family with a tractor. So what we must do is to try and make this possible for groups of farmers to get together and share the cost and the use of a tractor between them. But we cannot even do this if our people are going to continue living scattered over a wide area, far apart from each other, and still haunted by the old superstitious fear of witchcraft, just as in the days of our grandfathers. The first and absolutely essential thing to do, therefore, if we want to be able to start using tractors for cultivation, is to begin living in proper villages. So if you ask me what our Government is planning to do during the next few years the answer is simple.

For the next few years government will be doing all it can to enable the farmers of Tanganyika to come together in village communities. And if you ask me why the government want us to live in villages, the answer is just as simple; unless we do we shall not be able to provide ourselves with the things we need to develop our land and to raise our standard of living. We shall not be able to use tractors; we shall not be able to provide schools for our children; we shall not be able to build hospitals, or have clean drinking water, it will be quite impossible to start small village industries, and instead we shall have to go on depending on the towns for all our requirements; and even if we had a plentiful supply of electric power we should never be able to connect it up to each isolated homestead.

However, I don’t want anybody to start thinking that just by going to live in a village he will himself miraculously supplied with the good things I have mentioned. No. That is not what I am saying. I know that we shall still be very long way from overcoming all our difficulties even by the time we have made it possible for every peasant family in Tanzania to live in a village. All I am saying that if we do not start living in proper village communities then all our attempts to develop the country will be just so much wasted effort.

What is more, the growth of village life will help us in improving our system of democratic government. It is true that at present both the Central Government and our Local Government bodies are elected by democratic methods. But, although the methods may be democratic, the operation of democracy itself is not yet what it should be, nor can it be while the majority of our rural population remains so widely scattered…

My Take:


Kwenye hizi fikra, ni kosa gani kutaka watu waishi katika vijiji au kupanga Taifa ambalo kimsingi ni la kijima kuwa katika maeneo ambayo yanaeleweka ili kuharakisha maendeleo?

Je, fikra hizi za kuunda vijiji badala ya kuacha watu waishi kwa kutawanyika zina ubaya gani?
 

My Take:


Kwenye hizi fikra, ni kosa gani kutaka watu waishi katika vijiji au kupanga Taifa ambalo kimsingi ni la kijima kuwa katika maeneo ambayo yanaeleweka ili kuharakisha maendeleo?

Je, fikra hizi za kuunda vijiji badala ya kuacha watu waishi kwa kutawanyika zina ubaya gani?

Hizi fikra, nzuri amba mbaya, zilisababisha maafa.
 

My Take:


Kwenye hizi fikra, ni kosa gani kutaka watu waishi katika vijiji au kupanga Taifa ambalo kimsingi ni la kijima kuwa katika maeneo ambayo yanaeleweka ili kuharakisha maendeleo?

Je, fikra hizi za kuunda vijiji badala ya kuacha watu waishi kwa kutawanyika zina ubaya gani?

Mkuu Mwanakijiji,

Unafikiri kwanini watu walikataa kuhamia katika vijiji hivyo?

Halafu, unapotaka watu wahamie mahali fulani si inabidi uwe umepatayarisha interms ya maji, umeme na mengine?

Mimi ndio mtazamo wangu hapa ingawa sipingi hoja ya kuanzishwa kwa vijiji vya ujamaa.

By the way, huku Cyber Village kuna wazo la kuanzisha Eco-Villages ambavyo vitatumia vyanzo ya umeme vitokananvyo na vitu kama takataka na mimea pamoja na vipunga hewa lakini tayri watu wanapinga ingawa kunahitajika more consultation juu ya wazo hilo la Eco- Villages.
 
Very often it has not even sufficed to bring us enough to eat. We have got to begin using the plough and the tractor instead. But our people do not have enough money, and nor has the Government, to provide each family with a tractor. So what we must do is to try and make this possible for groups of farmers to get together and share the cost and the use of a tractor between them. But we cannot even do this if our people are going to continue living scattered over a wide area, far apart from each other, and still haunted by the old superstitious fear of witchcraft, just as in the days of our grandfathers. The first and absolutely essential thing to do, therefore, if we want to be able to start using tractors for cultivation, is to begin living in proper villages. So if you ask me what our Government is planning to do during the next few years the answer is simple.


Ni yeye mwalimu alikuwa akiamini uchawi au kila mtu huko vijijini alikuwa akiamini uchawi?
MWalimu hajawahi kusema kwamba alifanya utafiti juu ya imani za kichawi za Watanzania.

Ila kuna ushahidi mkubwa kwamba Nyerere aliogopa sana uchawi kiasi cha kuwaita Machifu wote Tanzania(1963) na wapiga madogoli wao pale Ikulu na kuwaamuru wazindike ili mkoloni asije tena.
Mara baada ya Ibada hiyo kwisha na Machifu kurudi kwao Mwalimu Nyerere alipiga marufuku Uchifu nchini Tanzania. Ni machifu wawili tu ndo walibakia na vyeo vya uchifu Adamu Sapi na Mazengo aliyempa zawadi ya Kifimbo.

Nyerere anaongelea uchawi 1962 kama moja ya sababu za kuweka watu pamoja vijijini.
Mara nyingi imani za uchawi hufanya mtu au watu kuhama eneo moja kwenda jingine au hata kujitenga na na walio wengi.
Kimsingi ndoto au maono ya Nyerere maka 1962 hayakuzingatia ukweli wa kwa nini watu wengi wamezagaa katika kona wanazoishi na hawaishi maeneo ambayo yeye Nyerere hataimaye alikuja kuwahamishia.
Nyerere haongelei namna ya kuelimisha watu hatua kwa hatua kuondokana na imani za uchawi( Kuanzia yeye Nyerere Mawaziri Wabunge wakurugrenzi na makamishna mapka Magenerali wa jeshi wote wanaamini uchawi kwa nguvu zote mpaka leo hii karne ya 21).
Anatumia muda mwingi kuanzia mwaka 1962 mpaka 1974 kutimiza ndoto yake ya kurundika watu pamoja bila kutaka ushauri wao wenyewe wala ushauri wa wawakirishi wao ,Wabunge.
Huu ulikuwa ni Udikteta wa hali ya juu.


Nyerere anaongelea kilimo cha Tractor kama moja ya sababu za kuweka watu pamoja vijijini.
Nyerere anawaza Kilimo cha Trekta mwaka 1962 lakini mpaka anang'atuka mwaka 1985 hajawahi kuwa na ndoto yeyote ya kusadikika juu ya namna ya kuwageuza Watanzania alio wakusanya vijijini kama mbuzi wawe wakulima wa Matrekta.
Kilimo cha Trekta lilikuwa ni tamko la kisiasa tu.
Nyerere mwenyewe mapaka mwisho wa maisha yake alihusudu jembe la mkono kwa Vitendo.
Nikiwa na maana alikuwa phyisically akilima pale kijijini Butiama kwa bidii zote akimaini kabisa kabisa kwamba jembe la mkono ni ukombozi.

Nyerere huyo huyo hakueleza wazi ni vipi eneo la kuhamia litafanyiwa Utafiti ili kuhakikisha kwamba idadi ya watu katika eneo moja haiwi tatizo baada ya miaka 20-50.
Ndoto na maono ya Nyerere yalikuwa nusu nusu yasiyoshirikishi wala yasiyo jali utu na heshima kwa wananchi wa Tanzania.

Ndoto ya Nyerere ya kuhamisha watu kwa nguvu kutoka maeneo yao ya asili ilitakiwa kwenda na mipango halisi na ya wazi kabisa itakayoonyesha namna kusogea mbele hatua kwa hatua.
Alitakiwa kuwa na ndoto ya kuhamisha watu kwa nguvu na kuwabadirisha kwa nguvu kuachana na jembe na kutumia Matrekta katika vikundi alivyowahi kuwaza.
Sasa sijui ni vipi vikundi hivyo vingeundwa wakati Ndoto nyingine ya Nyerere ilikuwa ni kuua Vyama vya Ushirika( Vikundi) ili kuua nguvu za kiuchumi za wananchi walio wengi na kuwanyima sauti kuruhusu yeye kutawala bila Mzengwe.

Nimefuatiliana historia ya nchi ya Marekani sijawahi kuona kiongozi aliyekuwa na ndoto kama za Nyerere.
Wenzetu walikuwa na mawazo ya kupanua nchi iwe kubwa kama Bara na kuruhusu watu kutawanyika vile wapendavyo.

Kwa nchi ndogo kama Tanzania ni Uzushi kusema watu wametawanyika hata kama watu hao ni 10,000,000 kama Population ya 1962 ilivyo kua.

I see a lot of contradiction katika ndoto zake Mwalimu. Laiti kama Mwalimu angeweka ndoto katika mjadala wa Bunge na baadhi ya wananchi walikua na uwezo wa kushiriki mjadala, ndoto zake fikirivu zingempeleka alijojo.
 
Madela, najaribu kuelewa; tatizo ni kujenga vijiji, kutokuwepo ulazima wa vijiji; kuamua kuvunja vijiji vilivyo sasa (maana karibu vyote ni mazao ya wazo hili la vijiji); au tatizo ni jinsi gani utekelezaji wa wazo hili ulifanyika?

Kama ungelikuwa wewe unaitwa kutoa mawazo yako kuhusu jamii ya Tanzania ya mwaka 1962, ungeweza vipi kuleta huduma ya maji, umeme, na barabara mahali ambako hakuna watu? au ungeweka umeme kwenye eneo gani kwanza halafu ndio watu waufuate?

Angalia eneo la Tanzania, halafu chukua watu milioni kumi na kati yao hao ni laki tatu tu walikuwa wanaishi mijini na uniambie mtawanyiko wa watu ulikuwa kiasi gani kwa KM moja ya mraba?
 
Mwanakijiji,
Unajua kuna wakati wa kubishana na kuna wakati inabidi Ukae Kimya...maanake utaumia kichwa mkuu wangu..

Hawa watu wanafahamu kabisa kwamba pamoja na kuwa watu wengi hawakutaka kuhamia vijijini wakati wa Nyerere leo hii hao hao wanahami Mijini kutokana na hali ya Uchumi..ambayo baadhi wakati ule vilikuwa ni vijiji tu. Nitawapoa mfano mdogo naoukumbuka vizuri... Bunda kule mkoani Mara kilikuwa Kijiji tu, Nzega huko Usukumani kilikuwa kijiji tu nenda leo sehemu hizo uyaone mabadiliko...
tatizo moja kubwa ni kwamba kuna watu wanataka kuibadilisha hali ya kuhamia vijijini kama vile hata waliokuwa mjini walitakiwa kisheria waondoke kwenda vijijini... Na sii kweli isipokuwa wale waliosemekana kuwa ni Wazururaji wasiokuwa na kazi.
Guys hata wazungu walianza jenga vijiji kabla ya miji na tuliyaona haya ktk sinema za Ma - Cowboys..enzi hizo za kina John Wayne na Wataliano Gulliano Gema leo kwetu imekuwa kosa!..
Yes kweli wananchi hawakuta kuhamia vijiji hivi kwa sababu - NDIVYO TULIVYO!.. vijiji hivyo ndivyo vina maji, umeme na Zahanati kama sio hospital... bahati mbaya tu ni kwamba Nyerere alipoondoka madarakani na huduma zote zimekufa vile vile!...
 
Unajua watu wanasahau kuwa Nyerere alijaribu hilo la kuanzisha huduma za jamii halafu watu wazifuate. Kule Mbulu, Hanang na sehemu za Umasaini walijaribu kujenga shule, visima vya maji n.k ili kuvutia jamii za wafugaji.. guess what.. walikaa pale kwa muda ng'ombe walipohama kutafuta malisho na wenyewe wakahama... na hili nililiona kwa macho yangu sikusimuliwa.
 
... ...bahati mbaya tu ni kwamba Nyerere alipoondoka madarakani na huduma zote zimekufa vile vile!...

Mimi sidhani hiyo ni kweli. Unaweza ukathibitisha? Kwanza nilitaka kuandika hivi:

Ukisema kitu kama hicho unatia mashaka kama kweli unaijua Bongo. Tena, umekuwa mjanja umeweka hiyo sentensi mwisho, manake ingekuwa vigumu kuendelea kukusoma mtu kama wewe.

Lakini nikaona kwanza nikuulize. Unaweza kuthibitisha kwamba Nyerere alipoondoka huduma zote zimekufa?
 
Kuhani Mkuu,
Nitakwambia kule nilikotoka mimi.. Wilaya ya Mwibara kuna mji unaitwa Kibara, nimeishi hapo toka mdogo, Nyerere aliweka mabomba ya maji safi kabisa mji mzima lakini kufikia mwaka 1985 ama maji yalianza kuwa taabu na mwisho mabomba mengine kutotoa maji kabisa. Kule kijijini Bulamba kwa bibi zangu vilijengwa visima hivi leo hakuna maji..Kisorya kwa mababu zangu hakuna maji lakini nilikuta pump ya kisima imesha shika kutu haifanyi kazi...
Pale Nansio, Ukerewe kwetu, kulikuwa na maji toka napata fahamu yangu tena kila nyuma ilikuwa na maji, kufikia mwaka 1985, maji yalikuwa taabu na mwishowe hakuna kabisa.. Yamerudishwa (2006-07) baadhi ya sehemu 1/10 ya mji huo ambao umekuwa mkubwa zaidi ndio una maji..
Mkuu Hata kama utatembea vitongoji na vijiji nje ya Dar tazama kwa makini sehemu zote mpya hazina maji isipokuwa zile zilizokuwepo Kama vijiji toka enzi za Mwalimu utakuta maji ama mabomba yasiyokuwa na maji..
Mkuu hivi visima vilichimbwa sana na Waswedish enzi za mwalimu hadi vijijini huko Singida ndani kabisa...Temebelea Genzaulole utashangaa kuna vyanzo vya huduma hizo kuliko Kipunguni, Ukonga...
Mkuu, mji mzima wa Dar umejaa visima vya maji ya kunywa halafu basi mji huo huo una vyoo asilimia kubwa ni vya mashimo ambayo bila shaka chemchem zake zinaungana na maji ya visima...
Choo kinachimbwa hadi uone maji ya chini futi 12 kwenda chini...Hapa tunazungumzia Dar mji mkubwa wa Tanzania!... acha huko mikoani....
Proof gani zaidi unataka..kuhusu Hospitali?..... hadithi ni hiyo hiyo mkuu.. Leo hii mnajenga zahanati mkizipa majina ya Hospital, madaktari wote ni waganga wa kila ugonjwa hata veterinary siku hizi anatibu binadamu!
 
Madela, najaribu kuelewa; tatizo ni kujenga vijiji, kutokuwepo ulazima wa vijiji; kuamua kuvunja vijiji vilivyo sasa (maana karibu vyote ni mazao ya wazo hili la vijiji); au tatizo ni jinsi gani utekelezaji wa wazo hili ulifanyika?

Kama ungelikuwa wewe unaitwa kutoa mawazo yako kuhusu jamii ya Tanzania ya mwaka 1962, ungeweza vipi kuleta huduma ya maji, umeme, na barabara mahali ambako hakuna watu? au ungeweka umeme kwenye eneo gani kwanza halafu ndio watu waufuate?

Angalia eneo la Tanzania, halafu chukua watu milioni kumi na kati yao hao ni laki tatu tu walikuwa wanaishi mijini na uniambie mtawanyiko wa watu ulikuwa kiasi gani kwa KM moja ya mraba?

Kwanza ingebidi kuzingatia utaalamu wa ongezeko la watu.
Ningeita wataalamu waniambie nchi itakuwa na watu wangapi baada ya mika 20,25 50. Utaalamu wao ungesaidi kujua structureya vijiji iweje 1962 ili isilete matatizo 2000.

Ningechukua maoni ya wabunge ambao ni wawakirishi wa wananchi na kuwapa mapendekezo yangu wayajadiri kwa uwazi.

Ningetafuta nchi kadhaa zilizo pata uhuru miaka ya zamani na kunagalia ni vipi walishughulikia tatizo la mtawanyiko wa watu.

Ningetenga eneo moja katika kila mkoa na kutekeleza ndoto zangu ili kujua matokeo kabla ya kutekeleza ndoto hizo nchi nzima.

Ningejiuliza mara mbili mbili je hakuna namna nyingine ya kuwapa watu huduma zaidi ya kuwalazimisha kuwa katika vijiji?

Najua ushirikiano ni jamnbo muhimu na la lazima.
Je kujenga vijiji vya lazima ni jambo la lazima?

Ili kutumia matrekta ni lazima watu waishi vijijini?
Trekta linauhusiano na kijiji?

Unahisi tatizo liko kwenye utekelezaji?

Leo hii mwaka 2008 unaweza kunionyesha kwa ushahidi wa maandishi watafsiri ya utekelezaji ndoto ya mwalimu Nyerere ulio andikwa kitaalamu kuanisha jambo moja hadi jingine na hatua moja hadi nyingine katika utekelezaji wa operesheni vijiji na vijiji vya ujamaa?

Tatizo halikuwa kwenye utekelezaji, tatizo lilikuwa kwney ndoto yenyewe. Ndoto hakuianishwa, haikuwekwa wazi.
Ndoto ya Nyerere haikuwa communicated hata kidogo.

Nyerere alipoota ndoto yake ya Vijiji aliendelea na utekelezaji kama vile baada ya yeye Nyerere kuota ndoto hiyo watanzania wote waliota ndoto hiyo kwa hiyo hakukuwa na haja ya kuiweka wazi kwani ilikuwa ni ndoto ya wote.

Hakuna aliyeshindwa kuitekeleza ndoto ya Nyerere ya Vijiji na vijiji vya ujamaa kwa sababu Nyerere hakuwahi kuianisha ndoto hiyo zaidi ya kueleza faida za kukaa pamoja kijijini.

Faida za kukaa pamoja kijijini hazina uhusiano na maelezo yenye mikakakti ya kuelezea hatua kwa hatua za kujenga vijiji.

Naamini kwa dhati Nyerere aliendelea kuota ndoto yake ya vijiji hadi siku ya kifo chake.
Kile tulicho kiona kikifanyika miaka ya 70 katika vurumai kubwa katika historia ya Tanganyika ya kuswaga watu kama Nyati au pundamilia huku nyumba zao na mashamba yakichomwa moto na mali nyingi kuharibiwa na kuibiwa, ilikuwa ni kukurupuka kwa kisiasa kuliko sababishwa na nia na hamu ya kuhodhi dola na mamlaka yake yote kusiko na uhusiano wala ushabihiano wowote na ndoto ya mwalimu Nyerere.
Maendeleo mengi ya watu waliotawanyika katika Tanganyika huru yalirudishwa miaka 100 nyuma kwa kitendo hicho cha operesheni vijiji kinachohusishwa nandoto ya Mwalimu Nyerere.

Nathubutu kusema ndoto nzima ya mwalimu Nyerere ilikuwa dhambi.
 
Back
Top Bottom