FC Barcelona (Barça or Blaugrana) | Special Thread

FC Barcelona (Barça or Blaugrana) | Special Thread

hahahahaaaaaaaa jana wakati naangalia mechi ya barcelona maeneo fulani nilikuwa nimekaa pamoja na kijana ambaye anaonekana ni muathirika wa ulevi wa kiswahili (gongo kali) basi baada ya lionel messi kufunga goli lake la 32 dhidi ya sevilla aliuliza swali moja la ajabu sana lililofanya wadau wote wanaoipenda barcelona na wanaoichukia barcelona wacheke kama vichaa.
aliliza swali lifuatalo:-

"hivi jamani hawa waandishi wa habari wa ulaya mpaka leo wameshindwa kuwafanyia mahojiano wazee wake lionel messi na kuwauliza walikuwa wanatumia chakula gani nyakati za usiku kabla hawajaingia kwenye pambano la kumtafuta mtoto lionel messi, kama walikuwa wanakula chipsi mayai nyakati za usiku basi watwambie na sisi wengine tujishindilie chipsi kabla hatujalala na wake zetu ili tupate mtoto mwenye kipaji kama Lionel messi".

baada ya dakika tatu mungu wa mpira akapata majeruhi kwa hali ilivyo inaonekana kuna malaika alichukizwa na kauli ya mlevi yule, na mimi nikaamua kwenda nyumbani kulala nilijihisi kama nitapoteza muda wangu kuangalia mechi bila ya sheikh messi kuwepo uwanjani.

nimebaki najiuliza muda huu kwa kipindi cha wiki tatu ambazo mungu wa mpira atakuwa likizo je ni nani atakayeuendesha ulimwengu wa mpira?
View attachment 906003
Hahah daah hii kali sana eti "Shekh Mess"
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom