FC Barcelona (Barça or Blaugrana) | Special Thread

FC Barcelona (Barça or Blaugrana) | Special Thread

Eti zidane hajawahi fungwa na barca camp nou wakati bernabeu anatobolewa tu daily
 
PAUL Pogba alijipimisha kimo na Lionel Messi walipokutana kwenye fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya mwaka 2015, akamwona Muargentina huyo dogo tu kwake.

Lakini, mechi ilipoanza akaona ufundi wa dogo huyo na kuishia kusema ‘Acheni Messi aitwe Messi’.

Pogba alisema mpira uliochezwa na Messi fainali hiyo na ule anaoendelea kuucheza siku zote, hakuna mwingine anayeweza kufanya hivyo.

Siku hiyo, Juventus ya Pogba ilichapwa mabao 3-1. Messi hakufunga, ila shughuli yake na namna alivyokuwa akiwachambua wachezaji katikati ya uwanja, ilidhihirisha ni wa daraja la juu zaidi.

Kimo cha Messi hakiendani na mambo anayoyafanya ndani ya uwanja. Staa huyo wa Barcelona ameripotiwa alipokuwa mdogo alikumbwa na tatizo la kihomoni, lililomfanya ashindwe kurefuka zaidi na ndiyo maana ana kimo hicho, futi 5 na inchi 7.

Messi mwenyewe anafichua kile alichokifanya huko utotoni hadi kumfanya afanikiwe kupata kimo hicho alichonacho kwa sasa, la sivyo hali ingekuwa mbaya zaidi.

Pengine Messi angekuwa mfupi zaidi na hilo lingemtibulia kisoka.

Katika mahojiano na America TV, Messi amefichua kila kitu, kwamba ilibidi ajichome sindano ya homoni kila siku kuanzia akiwa na miaka minane hadi alipofikisha miaka 14 ili kupata kimo alichonacho sasa.

Messi anasema mwanzoni wazazi wake ndio waliokuwa wakimchoma sindano hizo miguuni kila siku usiku na alipofikisha miaka 12 alianza kujichoma mwenyewe.

Messi alikumbwa na tatizo la kukosa homoni za kumfanya arefuke wakati alipokuwa kwenye mji wa kwao, Rosario, Santa Fe, Argentina.

“Nilikuwa najichoma sindano kwenye miguu mara moja kila usiku. Nilianza kujichoma mwenyewe nikiwa na umri wa miaka 12, si jambo nilililokuwa nikilifurahia,” alisema Messi.

“Huko nyuma wazazi wangu ndio waliokuwa wakinichoma hizo sindano tangu nikiwa na umri wa miaka minane na walinifundisha ili nianze kujichoma mwenyewe. Sindano haikuwa ikiuma, kwa sababu ilikuwa ndogo na nilikuwa najichoma kawaida tu.”

Wazazi wake walikuwa wakizigharimia sindano hizo za Messi, Pauni 1,069 kwa mwezi, sawa na Sh3,369,340 za Kitanzania, ikiwa ni zaidi ya Sh100,000 kwa siku.

Baadaye, klabu yake ya zamani, Newell’s Old Boys, ilichukua majukumu ya kulipia gharama hiyo ya sindano za Messi.

Mwaka 2001, akiwa na umri wa miaka 13, Messi na familia yake walihamia Barcelona na klabu hiyo ilikubali kulipia gharama zote za matibabu yake hadi dozi yake ya sindano ilipofika mwisho alipokuwa na umri wa miaka 14.

Gwiji huyo wa Barcelona alisema: “Halikuwa jambo gumu kabisa kwangu kuja Barcelona. Mimi niliyazoea mazingira kwa haraka sana, lakini familia yangu ilishindwa kufanya hivyo. Ndugu zangu walitaka kurudi nyumbani Argentina na walifanya hivyo.

Barcelona tulibaki mimi na baba tu na kuna siku moja aliniuliza ‘tunafanyaje?’ Nilimjibu baba yangu ‘mimi nataka kubaki’.”

Ndipo hapo staa huyo alipobaki Barcelona, mahali ambako anacheza soka la kiwango bora na kuvunja rekodi kibao zilizowahi kuwekwa kwenye mchezo huo duniani.

Akitoa huduma yake kwenye kikosi hicho, Messi amefanikiwa kubeba tuzo ya Mwanasoka Bora wa Mwaka wa Dunia mara tano na kuwa mmoja wa wachezaji wanaotajwa kuwa ni bora kuliko yeyote aliyewahi kutokea katika mchezo wa soka duniani.

Shida ya kukua haikuwa tatizo kwa Messi na kumfanya aendelee kucheza soka maridadi, akifunga mabao 374 katika mechi 410 alizoichezea Barcelona kibingwa.

Messi amekiri wasiwasi wake kuhusu kurudi Argentina wakati atakapostaafu soka huko Barcelona ikiwa ni sehemu tu ya kubainisha kile anachotamani kukifanya baada ya soka lake huko Nou Camp.

Messi ameifanya Barcelona kuwa moto msimu huu ikielekea kubeba taji la La Liga baada ya kuweka pengo la pointi 11 katika msimamo wa ligi hiyo.

Barcelona ipo kwenye robo fainali pia ya Ligi ya Mabingwa Ulaya ambapo itakipiga na AS Roma ya Italia, huku wakiwinda pia rekodi yao ya kunyakua mataji matatu makubwa kwa msimu huu kwa sababu wanalisaka pia taji la Copa del Rey.
 
Barca huwa wana kaubaguzi kiaina na nyeusi mnajua Gomez analipwa mshahara mkubwa kuliko umtiti!?

Sasa Man U wametoa 9M Euro... Kama Mimi ni umtiti mapema nasepa zangu Man U.
nikuulize swali unafikiri kwanini Salah wa Liverpool anapitwa mshahara na players wengi wa hiyo timu
 
nikuulize swali unafikiri kwanini Salah wa Liverpool anapitwa mshahara na players wengi wa hiyo timu
Hii inaweza kuwa sababu but hata kwa negotiations zinazoendelea hawataki kumpa mshahara ambao Man U wako willing kumpatia wa 9M Euro.

Case ya salah na umtiti ziko sawa kimaudhui ila kimantiki ni tofauti.
 
Mkuu uko sahihi...hil swala barca huwa wana fail sana..kama unakumbuka issue kama hii ili rise kutoka thiago alcantara..dogo ilibid asepe zake..nafkr hata umtiti atasepa..siku hiz team yetu inapenda sana michezaj mizee kuliko dam changa.., kwa kwel huwa siwaelew kabsa..nafkr utawala Wa rosell ulikua ni utawala bora zaid huu uliopo
 
Nimesoma barca live,wanasema kuwa kama watamlipa eti hiyo anayo taka wata violet financial act
 
GOAT
Screenshot_20180327-090524.jpg
 
Uyu kipa namba 2 wa barca anaeitwa jasper nmemcheki jana mechi ya uholanzi nmemuona mkali yani anafaa kucompete namba na ter stegen so nikajua labda ni kinda wa kurithi mikoba ya stergen uko badae....ila nmechek umri jamaa kumbe ana 28 mkubwa kwa ster gen kumbe...ili jambo sikuexpect kabisa
 
Lionel Messi has recovered from a muscle injury, while team-mate Sergio Aguero is still ruled out
BBC coverage
How to follow:
Listen on BBC Radio 5 live and BBC local radio; text commentary on the BBC Sport website

Lionel Messi looks set to return for Argentina in Tuesday's friendly match against Spain.

The captain sat out the 2-0 win over Italy in Manchester on Friday because of a muscle injury but has been cleared to lead his country out in Madrid.

Argentina coach Jorge Sampaoli said Messi trained "normally" on Monday and is available to play.

"Before the game against Italy, Leo said he could not play. But he has trained the last two days," he added.

Speaking before his coach's news conference at Atletico Madrid's Wanda Metropolitano stadium, Messi said he felt "good".

Argentina's all-time record goalscorer could be lining up against Barcelona team-mates Gerard Pique and Jordi Alba.

Spain drew 1-1 with Germany in Dusseldorf on Friday, extending their unbeaten record under Julen Lopetegui to 17 matches.

7.jpg
 
Tetesi

Barcelona wanapanga kuwasilisha ombi la kutaka kumchukua beki wa Manchester United Luke Shaw mwisho wa msimu. Beki huyo wa kushoro wa miaka 22 kutoka England amekosolewa sana na meneja wa United Jose Mourinho wiki za karibuni. (Mirror)

Mchezaji nyota wa Brazil Ronaldinho amefichua wkamba alikuwa saa 48 karibu na kujiunga na United mwaka 2003 kujaza nafasi ya David Beckham aliyekuwa amehamia Real Madrid. Badala yake mchezaji huyo wa miaka 38 alijiunga na Barcelona pale Sandro Rosell alipoteuliwa rais wa klabu hiyo. (FourFourTwo)
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom