Faida nilizozipatakwa kupanda migomba michache kuzunguka nyumba yangu

Mimi pia nimelima ndizi sehemu iliyobakia baada ya kujenga. Kitu ambacho watu wengi wanatakiwa kujua Ni kuwa migomba inataka mbolea, shimo kubwa na maji.
Kwenye maji Wala usipate tabu sana kwani maji ya sabuni hayaui mgomba.
Sasa Basi Mimi nilichokifanya ni kuwa ile migomba ambayo ninaitaka Sana Kama kimalindi, mchare, mzuzu na mkono wa tembo nimeipanda karibu kabisa na nyumba na nyumba ili maji ya kufikia au kuoshea vyombo yamwagwe pale. Ile mingine kama kisukari nimeipeleka mbali na hiyo inasubiria maji ya mvua tu.
Kwangu ndizi hazikosekani angalau Mara 2 kwa mwezi. Note that nipo Mbezi.
Naambatanisha na picha kadhaa.

Pia nimeipanda mboga za majani, pilipili na mapasheni. Mapapai yamegoma kwa sababu ardhi ya huku ni mfinyaziView attachment 1818258View attachment 1818261View attachment 1818259View attachment 1818262View attachment 1818260
IMG_20210513_085614_459.jpg
 
Nimeona mdau mmoja hapo juu analalamika kuhusu mgomba kutoa ndizi ndogo. Naomba nikushauri kuwa Kama shina la mgomba limetoa watoto wengi jitahidi upunguze ili Miche usipate kazi kubwa ya kumtafuta chakula. Inashauriwa shina moja liwe na Miche mitatu tu. Pia Kuna migomba Kama mzuzu shimo lake lazima liwe kubwa kwani Mara nyingi mizizi yake huwa inapendelea kuja juu. Kumbuka kuongeza mbolea hata Kama ni ya Kuku ili kuupa udongo rutuba. Kwa wale wenzangu wa Dar migomba ambayo ukipanda haitakuangusha ni kimalindi, mzuzu na mkono wa tembo. Hata kisukari kipo vizuri zaidi
 
Nawasalimu kwa jina la jamhuri

Mwaka jana mwezi wa kwanza nilipanda migomba kama 30 katikaeneo la nyumbani napoishi. Kabla ya kupanda niliwauliza wataalamu hasa watu wanaotokea maeneo ambayo wanalima sana ndizi kama Moshi, Bukoba na Tukuyu kujua aina za ndizi na matumizi yake na namna ya kupanda. Baada ya kupata maelekezo ya kitaalamu nikapanda aina zifuatazo za ndizi.

1. Mzuzu hii niliambiwa inafaa sana kukaangwa au kuchomwa
2. Bukoba hii kwa kupikwa
3. Mshale hii kwa supu
4. Malindi hii inafaa kuliwa ikiwa mbivu
5. Kisukari vile vidogo hivi navyo vinafaa kuliwa vikiwa vimeiva
6. Matoke hizi kwa kupikwa
Faida nayoipata kwa sasa;
1. Mazingira ya kuzunguka nyumba yangu yanavutia maana ni green tupu pamoja na kua tumeanza kiangazi
2. Nina chakula cha kutosha imenilazimu kununua fridge ya ziada ili ndizi zingine nizi freez humo maana zimenizia
3. Kipato changu (thamani ya shilingi kwangu imeimarika maana nimepunguza kwa kiasi kikubwa kutoa pesa nje kwa ajili ya kununua mahitaji )
4. Ninatoa sadaka hasa kwa wale ambao wanashida ya chakula angalau ninawapa ndizi kidogo kama sadaka na napata baraka kutoka kwa Mungu

NB
Kwa wale ambao tuna maeneo makubwa tumejenga basi tupande angalau migomba itatusaidia kuliko kujaza pavement na ukoka kwenye nyumba.

Kwa wale wanaotegemea kununua maeneo ya kujenga nawashauri mtoke kidogo nje ya mji mpate maeneo ambayo yatawawezesha kulima kidogo na kufuga.
Mgomba una matumizi mengi sana, hujaumaliza. Yapo kama;
1. Mti wa mgomba wenyewe unaliwa, yani ile sehemu nyeupe iliyopo katikati kabisa mwa mti. Yana Potasium na Vitamini kwa wingi.
1623756284684.png

2. Majani yale unaweza kutumia kama Foil Paper, pia kama sahani disposable.
1623756252013.png

1623756349721.png

3. Tafuta ndama jike apate msosi wa uhakika, chakula pendwa ukichanganywa na magadi kwa mifugo kama mbuzi na ng'ombe.
4. Magome yake hutumika kama kamba pia
 
Siku moja chemsha utumbo utupie malindi mbichi kitunguu, hoho na pilipil mbiuz ya kishkaji
we mama umenifurahisa sana vile umeandikaa yani watu wa mapishi hapo tunajua hicho ni kitu gani kinaenda kutoka hasa ukijumlisha na aina ya ndizi ilotumika
 
Nakubaliana na wewe..mimi awali nilipanda mipapai kama 100 hivi..ikasumbua wadudu na baadae wateja.Ila.toka nimeoanda migomba nakula.ndizi kama.kawa
Hahaha migomba haitakiwi kuwa chini ya miti. Haizai mbee... inagoma kabisaa. Ulifanya jambo sahihi sana kuitoa.
 
Hongera ardhi yako ina rutuba. Kwangu migomba ipo shina moja lakini mkungu ulioko pale ni mdogo kama nanasi.
Kiongozi
Jaribu Kuchimba shimo kubwa ni seme fanya meta moja kina na upana;
Weka mbolea ya ngombe au wanyama hadi nusu au ya masalia ya mimea ila iliyo oza vizuri hadi nusu
Changanya na udongo kidogo Otesha mgomba. Kama ni kiangazi mwagilia walau Ndoo moja ya lita 20, mara mbili kwa wiki au pengine mara moja kama upatikanaji wa maji sio rafiki.
Hiyo nusu ya juu iache wazi. Hiyo mbinu niliona huko kanda ya kaskazini
 
Mgomba una matumizi mengi sana, hujaumaliza. Yapo kama;
1. Mti wa mgomba wenyewe unaliwa, yani ile sehemu nyeupe iliyopo katikati kabisa mwa mti. Yana Potasium na Vitamini kwa wingi.
View attachment 1819383
2. Majani yale unaweza kutumia kama Foil Paper, pia kama sahani disposable.
View attachment 1819382
View attachment 1819384
3. Tafuta ndama jike apate msosi wa uhakika, chakula pendwa ukichanganywa na magadi kwa mifugo kama mbuzi na ng'ombe.
4. Magome yake hutumika kama kamba pia
Umetisha mkuu
 
Kiongozi
Jaribu Kuchimba shimo kubwa ni seme fanya meta moja kina na upana;
Weka mbolea ya ngombe au wanyama hadi nusu au ya masalia ya mimea ila iliyo oza vizuri hadi nusu
Changanya na udongo kidogo Otesha mgomba. Kama ni kiangazi mwagilia walau Ndoo moja ya lita 20, mara mbili kwa wiki au pengine mara moja kama upatikanaji wa maji sio rafiki.
Hiyo nusu ya juu iache wazi. Hiyo mbinu niliona huko kanda ya kaskazini
Asante kwa muongozo huu.
 
Hongera sana, mimi pia kupitia JF kuna jamaa alianzisha uzi wa jinsi ya kupanda matunda nyumbani, niliutumia ule ujuzi...
Its five years now matunda hayakauki home, matunda kama..papai, ndizi aina zote, machungwa, miwa, mboga za majani, na nadhani next year tutaanza kula embe...
Halafu kumbe nyumba ikiwa ina greenish inapendeza na kufutia sana...
Unaweza kaa siku nzima unashangaa maua, majani, na miti ya matunda!

Ahsante kwa Jf...ilinipa idea nzuri.
Lazima kujifunza kuwa na bustani nyumbani
 
Raha sana mkuu kuna kipindi unakua umefulia hatari unapitia buchani unachukua nyama ya utumbo kg moja tu buku 4 ukifika home mnakula delicious food kama matajiri
Raha sana mkuu kuna kipindi unakua umefulia hatari unapitia buchani unachukua nyama ya utumbo kg moja tu buku 4 ukifika home mnakula delicious food kama matajiri
Sema utumbo sio nyama ya utumbo
 
Back
Top Bottom