Faida nilizozipatakwa kupanda migomba michache kuzunguka nyumba yangu

kabila01

JF-Expert Member
Apr 21, 2009
4,023
2,000
Nawasalimu kwa jina la jamhuri

Mwaka jana mwezi wa kwanza nilipanda migomba kama 30 katikaeneo la nyumbani napoishi. Kabla ya kupanda niliwauliza wataalamu hasa watu wanaotokea maeneo ambayo wanalima sana ndizi kama Moshi, Bukoba na Tukuyu kujua aina za ndizi na matumizi yake na namna ya kupanda. Baada ya kupata maelekezo ya kitaalamu nikapanda aina zifuatazo za ndizi.

1. Mzuzu hii niliambiwa inafaa sana kukaangwa au kuchomwa
2. Bukoba hii kwa kupikwa
3. Mshale hii kwa supu
4. Malindi hii inafaa kuliwa ikiwa mbivu
5. Kisukari vile vidogo hivi navyo vinafaa kuliwa vikiwa vimeiva
6. Matoke hizi kwa kupikwa
Faida nayoipata kwa sasa;
1. Mazingira ya kuzunguka nyumba yangu yanavutia maana ni green tupu pamoja na kua tumeanza kiangazi
2. Nina chakula cha kutosha imenilazimu kununua fridge ya ziada ili ndizi zingine nizi freez humo maana zimenizia
3. Kipato changu (thamani ya shilingi kwangu imeimarika maana nimepunguza kwa kiasi kikubwa kutoa pesa nje kwa ajili ya kununua mahitaji )
4. Ninatoa sadaka hasa kwa wale ambao wanashida ya chakula angalau ninawapa ndizi kidogo kama sadaka na napata baraka kutoka kwa Mungu

NB
Kwa wale ambao tuna maeneo makubwa tumejenga basi tupande angalau migomba itatusaidia kuliko kujaza pavement na ukoka kwenye nyumba.

Kwa wale wanaotegemea kununua maeneo ya kujenga nawashauri mtoke kidogo nje ya mji mpate maeneo ambayo yatawawezesha kulima kidogo na kufuga.
 
Conquerer_

Member
Jan 10, 2021
10
75
Migomba inastawi Sana sehemu nyingi Cha msingi zaidi Ni mbolea na maji..kwa sehemu zenye miamba au mawemawe bado inawezA kufanya vizuri, muhimu Ni kuhakikisha shimo linakua refu na mzunguko Mpana Kisha changanya mbolea nyingi ya samadi na udongo...

Ndizi kubwa na zenye afya chagua Miche midogo midogo siyo unaotesha mche unalingana nao urefu😆 huu hautatoa ndizi yenye afya.napenda Sana garden iliyonakshiwa na migomba very appealing.
 
Mama Nehemiah

Senior Member
Sep 9, 2018
155
500
Nawasalimu kwa jina la jamhuri

Mwaka jana mwezi wa kwanza nilipanda migomba kama 30 katikaeneo la nyumbani napoishi. Kabla ya kupanda niliwauliza wataalamu hasa watu wanaotokea maeneo ambayo wanalima sana ndizi kama Moshi, Bukoba na Tukuyu kujua aina za ndizi na matumizi yake na namna ya kupanda. Baada ya kupata maelekezo ya kitaalamu nikapanda aina zifuatazo za ndizi.

1. Mzuzu hii niliambiwa inafaa sana kukaangwa au kuchomwa
2. Bukoba hii kwa kupikwa
3. Mshale hii kwa supu
4. Malindi hii inafaa kuliwa ikiwa mbivu
5. Kisukari vile vidogo hivi navyo vinafaa kuliwa vikiwa vimeiva
6. Matoke hizi kwa kupikwa
Faida nayoipata kwa sasa;
1. Mazingira ya kuzunguka nyumba yangu yanavutia maana ni green tupu pamoja na kua tumeanza kiangazi
2. Nina chakula cha kutosha imenilazimu kununua fridge ya ziada ili ndizi zingine nizi freez humo maana zimenizia
3. Kipato changu (thamani ya shilingi kwangu imeimarika maana nimepunguza kwa kiasi kikubwa kutoa pesa nje kwa ajili ya kununua mahitaji )
4. Ninatoa sadaka hasa kwa wale ambao wanashida ya chakula angalau ninawapa ndizi kidogo kama sadaka na napata baraka kutoka kwa Mungu

NB
Kwa wale ambao tuna maeneo makubwa tumejenga basi tupande angalau migomba itatusaidia kuliko kujaza pavement na ukoka kwenye nyumba.

Kwa wale wanaotegemea kununua maeneo ya kujenga nawashauri mtoke kidogo nje ya mji mpate maeneo ambayo yatawawezesha kulima kidogo na kufuga.
Hakika nakubaliana na wewe tutumie ardhi iliyotuzunguka vyema.Mimi ni shahidi mahali ninapoishi ninaeneo mwaka 2018 niliamua kupanda migomba...jamani nimekula ndizi mpaka raha.kiangazi ya dsm na jua lote mimi kwangu kwenye friji kuna ndizi za kila aina.halafu nilipanda Kama masihara tu
 
kabila01

JF-Expert Member
Apr 21, 2009
4,023
2,000
Hakika nakubaliana na wewe tutumie ardhi iliyotuzunguka vyema.Mimi ni shahidi mahali ninapoishi ninaeneo mwaka 2018 niliamua kupanda migomba...jamani nimekula ndizi mpaka raha.kiangazi ya dsm na jua lote mimi kwangu kwenye friji kuna ndizi za kila aina.halafu nilipanda Kama masihara tu
Raha sana mkuu kuna kipindi unakua umefulia hatari unapitia buchani unachukua nyama ya utumbo kg moja tu buku 4 ukifika home mnakula delicious food kama matajiri
 
Tuna

JF-Expert Member
Jan 21, 2019
813
1,000
images (8).jpeg
 
red apple

JF-Expert Member
Dec 6, 2012
538
1,000
Hongera sana, mimi pia kupitia JF kuna jamaa alianzisha uzi wa jinsi ya kupanda matunda nyumbani, niliutumia ule ujuzi...
Its five years now matunda hayakauki home, matunda kama..papai, ndizi aina zote, machungwa, miwa, mboga za majani, na nadhani next year tutaanza kula embe...
Halafu kumbe nyumba ikiwa ina greenish inapendeza na kufutia sana...
Unaweza kaa siku nzima unashangaa maua, majani, na miti ya matunda!

Ahsante kwa Jf...ilinipa idea nzuri.
 
kuna wakati hua nakaa hata masaa mawili naangalia tu green iliyopo hasa wakati wa kiangazi. Nyumba hata kama ya kawaida inapendeza sana ikizungukwa na miti pamojana maua kuliko kujaza pavement maana zikifubaa panaonekana kama garage
 
agudev

Member
Apr 5, 2016
43
125
Nawasalimu kwa jina la jamhuri

Mwaka jana mwezi wa kwanza nilipanda migomba kama 30 katikaeneo la nyumbani napoishi. Kabla ya kupanda niliwauliza wataalamu hasa watu wanaotokea maeneo ambayo wanalima sana ndizi kama Moshi, Bukoba na Tukuyu kujua aina za ndizi na matumizi yake na namna ya kupanda. Baada ya kupata maelekezo ya kitaalamu nikapanda aina zifuatazo za ndizi.

1. Mzuzu hii niliambiwa inafaa sana kukaangwa au kuchomwa
2. Bukoba hii kwa kupikwa
3. Mshale hii kwa supu
4. Malindi hii inafaa kuliwa ikiwa mbivu
5. Kisukari vile vidogo hivi navyo vinafaa kuliwa vikiwa vimeiva
6. Matoke hizi kwa kupikwa
Faida nayoipata kwa sasa;
1. Mazingira ya kuzunguka nyumba yangu yanavutia maana ni green tupu pamoja na kua tumeanza kiangazi
2. Nina chakula cha kutosha imenilazimu kununua fridge ya ziada ili ndizi zingine nizi freez humo maana zimenizia
3. Kipato changu (thamani ya shilingi kwangu imeimarika maana nimepunguza kwa kiasi kikubwa kutoa pesa nje kwa ajili ya kununua mahitaji )
4. Ninatoa sadaka hasa kwa wale ambao wanashida ya chakula angalau ninawapa ndizi kidogo kama sadaka na napata baraka kutoka kwa Mungu

NB
Kwa wale ambao tuna maeneo makubwa tumejenga basi tupande angalau migomba itatusaidia kuliko kujaza pavement na ukoka kwenye nyumba.

Kwa wale wanaotegemea kununua maeneo ya kujenga nawashauri mtoke kidogo nje ya mji mpate maeneo ambayo yatawawezesha kulima kidogo na kufuga.
Upo sehemu gani? maana sidhani kama aina hizi zote za migomba zinaweza kustawi sehemu zote Tanzania
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom