Nimekutana na rafiki yangu mwarabu tuliesoma shule ya Msingi, Nasikitika kuona wageni wanavyotajirika huku wenyeji tumeridhika na vimafanikio vidogo

sky soldier

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
5,408
19,033
"USIPOTAJIRIKA TANZANIA HAKUNA SEHEMU UTAJA TAJIRIKA" Ni maneno niliyotamkiwa na moja ya rafiki yangu tuliesoma wote shule ya msingi leo hii tulipokutana na kupiga story zaidi ya lisaa, Yeye alipofika form 4 shughuli iliishia hapo.

Darasani na shuleni kiujumla nimewajua wahindi na waarabu kibao tu, nikiri wazi waarabu tulikuwa tunawaburuza "Sio Kitoto", uwezo wao ulikuwa mdogo mnooo, lakini leo hii sio wenzetu hata kidogo, ni story tu za kujuana nao lakini kimaisha tumepigwa gepu sio kitoto.

Wahindi angalau kulikuwa na upinzani ila tulikuwa tunaburuzana sana tu, vipanga wa kibongo waliburuzana na vipanga wa kihindi, huku wa kati nao walikuwepo tuliburuzana nao man to man, wengi wamesoma mpaka vyuoni lakini wanatumia elimu zao kwenye biashara zao hapa hapa Tz.

Tukija kwa upande wetu wabongo hali inatia huruma, tumesoma mpaka vyuoni + masters, mtu kapigiwa koneksheni na ndugu ama wazazi ama kapata ajira kivyake mshahra + posho vyote kwa jumla ni milioni 3 kwa mwezi yani hapo akiwa na gari na nyumba anaridhika kabisa cha kuwaza labda kuongeza mchepuko ama kuwahi viti virefu baada ya kazi, kwa wale wanaofanya biashara unakuta mtu akiingiza faida milioni around 8 kwa mwezi anajiona tayari mwamba.

Wenzetu hawa hawa tuliosoma nao suala la kuajiriwa hawataki kulisikia kabisa kwenye nchi hii, kuna muhindi moja aliniambia " Nchi hii ina untapped resources and oppurtunities kibao, hata elimu ya standard 7 inatosha kukutajirisha, Forest imejaa carrots ni wewe utaamua uwe punda ama mkulima" Sio siri nilihisi nimetupiwa dongo.

yani wao wanaunganisba nguvu kwenye timu zao (familia), kwa mwezi kulaza B na kuendelea ni kawaida.

MAPENDEKEZO

Nawajua matajiri wa hapa Tanzania wanataka watoto hawana exposure kabisa,yani mtoto maisha yake yote kasome Tz, matokeo yake mtoto anakuwa na akili za hapa hapa hata lugha inampiga chenga, hajui kumingle wala hana connections za watu wa mataifa mengine.

Fikra za 'KILA MTU AJITAFUTIE CHAKE' zimepitwa na wakati, unakuta tajiri anasubiria mpaka mtoto wake afikie miaka 25 ndio anampa mtaji akajitafutie chake, tena mtaji wenyewe unakuta ni milioni 20 wakati baba ni bilionea, NI UPUUZI!! hii ndio sababu kubwa biashara nyingi zinaanguka baba akifariki sababu watoto hawajui kuziendeleza, ukiona wenzetu mtoto hasubiriwi mpaka awe mkubwa, ni tangu akiwa mdogo anazoeshwa biashara maana hata kwa akili ya kawaida ukiwa na paka ama mbwa mdogo unaweza kumfunza vingi akiwa bado mdogo kuliko ukubwani, na hata mtoto akiwa mkubwa anaendeleza ama ku expand biashara za familia, hata baba akifariki biashara zinaendelea bila tatizo.
 
Waarabu na wahindi wa Tanzania, sio wageni, ni kabila la wahindi na waarabu tu ambao ni watanzania, na wengine ni watanzania kuliko hata wewe mwenye kabila la kibantu kwasababu wazazi wao wamekuja hapa miaka ya 1700 uko wakati wangoni wamekuja bongo miaka ya 1800 au 1900 kama sikosei. usiseme watu ni wageni kwa sababu ya rangi.
 
nilivyowaangalia wahindi na waarabu, binafsi nimejifunza kitu kwao, watoto wangu siwalei ili wakikua wawe wasomi walioajiriwa. wanatakiwa kuja kuwa wamiliki wa makampuni/biashara na kuajiri wengine.

Hilo pia linafanywa sana na wachaga na wakinga, anaanza kumfundisha mtoto biashara tangu akiwa mdogo.
 
Mtoa mada kashalowa baada ya kumuona classmate muarabu Katoboa
Ngozi nyeusi inalelewa kwa misingi ya ubinafsi, baba anayo nyumba ila mtoto akikua anaambiwa au anaamua mwenyewe akajitegemee anaenda kuanza 1 wakati hiyo pesa anayoenda kununua kitanda,godoro,kiwanja kujenga nyumba angeiwekeza kwenye biashara ambayo anauzoefu nayo baada ya miaka kadhaa angekua kapiga hatua .

ila wanaishi kwenye circle hiyohiyo ya kufika umri flan anaenda kulipa kodi kununua godoro kujenga kazeeka tayari, mtoto wake nae anarudia ujinga huohuo wajukuu hivyohivyo, akili ya biashara hamna akiajiriwa ye ndo anaonekana katoboa.
 
waarabu na wahindi wa Tanzania, sio wageni, ni kabila la wahindi na waarabu tu ambao ni watanzania, na wengine ni watanzania kuliko hata wewe mwenye kabila la kibantu kwasababu wazazi wao wamekuja hapa miaka ya 1700 uko wakati wangoni wamekuja bongo miaka ya 1800 au 1900 kama sikosei. usiseme watu ni wageni kwa sababu ya rangi.
Aliekudanya nani mkuu, mimi hao watu nimeishi nao sana shuleni kwa miaka saba, Kinadharia kwa uraia ni wenzetu ila kwa uhalisia bado ni wageni.

wanaishi kwa tamaduni za kiarabu na kihindi na sio za kitanzania, huji kuona mhindi ama muarabu kavaa hata kitenge, ni wenzetu hao ?

wanaoleana wao kwa wao, Kwa waarabu hata uwe mpemba ama msomali wao hukuona bado mwafrika huwezi kupewa binti yao labda uwe na mtu mzito sana, kwa wahindi sahau kabisa, ni wenzetu hao ?

Shughuli za kijamii iwe misiba ama sherehe huwa wanashiriki zao, ni wenzetu hao ?
 
Back
Top Bottom