Askofu Shoo: Maoni ya wananchi yatiliwe maanani, yaheshimiwe na yatekelezwe

Rabbon

JF-Expert Member
Apr 16, 2022
15,156
22,655
Salaam, Shalom.

Askofu Shoo ametoa kauli iliyojaa HEKIMA na BUSARA, akitoa maoni Kwa niaba ya CCT, amesisitiza kuwa maoni ya wananchi yatolewayo kuhusu namna Gani uchaguzi huru na HAKI ufanyike, yaheshimiwe, yatiliwe maanani na yatekelezwe.

Amesema pia kuwa Si vyema mchakato huo ukatawaliwa na usanii. Ametoa kauli hiyo katika mkutano mbele ya baadhi ya wabunge waliohudhuria mkutano huo.

Amesema kuwa ikiwa mambo hayo matatu yatafanikiwa, watabarikiwa.

Mungu ibariki Nchi yangu nzuri niipendayo TANZANIA 🇹🇿.

Amen.

Karibuni 🙏.

Source: Mwananchi digital.
 
Angeanza yeye kuheshimu maoni ya Waumini wake kwenye lile sakata la DPW na mchakato uliomrejesha Malasusa Madarakani ingependeza zaidi...
Wahi hospitali. Naona mambo yameanza kukuendea vibaya kiasi cha kushindwa hata kujua hoja inayojadiliwa. Pole sana. Tunakuombea urejelewa na ufahamu mapema.
 
Utawala wa demokrasia unapaswa kuzingatiwa na kuheshimiwa, bila kujali ni kanisani, msikitini, serikalini au chama cha siasa. Sote tuheshimu demokrasia.
 
Angetoa pia na mwelekeo kwamba maoni yasipotekelezwa atafanya nn?

Kule DRC viongozi wa dini walitoa msimamo kwamba endapo Kabila atabadili mihula ya urais tutaandamana. Sasa huyu anatoa ombi jeupe lisilo na mwelekeo!!?

Kelele za mlango hazimtishi mwenye nyumba.
 
Askofu Shoo ametoa kauli iliyojaa HEKIMA na BUSARA, akitoa maoni Kwa niaba ya CCT, amesisitiza kuwa maoni ya wananchi yatolewayo kuhusu namna Gani uchaguzi huru na HAKI ufanyike, yaheshimiwe, yatiliwe maanani na yatekelezwe.
Well
 
Salaam, Shalom.

Askofu Shoo ametoa kauli iliyojaa HEKIMA na BUSARA, akitoa maoni Kwa niaba ya CCT, amesisitiza kuwa maoni ya wananchi yatolewayo kuhusu namna Gani uchaguzi huru na HAKI ufanyike, yaheshimiwe, yatiliwe maanani na yatekelezwe.

Amesema pia kuwa Si vyema mchakato huo ukatawaliwa na usanii. Ametoa kauli hiyo katika mkutano mbele ya baadhi ya wabunge waliohudhuria mkutano huo.

Amesema kuwa ikiwa mambo hayo matatu yatafanikiwa, watabarikiwa.

Mungu ibariki Nchi yangu nzuri niipendayo TANZANIA 🇹🇿.

Amen.

Karibuni 🙏.

Source: Mwananchi digital.
Ukweli na usemwe tu
 
Asiyaite maoni ya wananchi bali maoni ya wanasiasa

Jiulize wewe kama mwananchi umeombwa lini kutoa maoni

Usiniambie mwanasiasa anakuwakilisha
 
Hivi haya maoni wanayokusanya kila siku huko bungeni, nani wanaokwenda kuyafanyia kazi?

Kama ni CCM, basi tunapoteza muda tu, sijui kwanini hatulioni hili miaka yote

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
Matapeli tu. Wanazuga ionekane nao wamo.

Maoni yalishamalizwa na Tume ya Warioba na hata Kikosi Kazi cha ccm pia.
 
Back
Top Bottom