Chonde chonde kamati ya bunge inayoratibu maoni ya wananchi kubalini yaishe

koryo1952

JF-Expert Member
Mar 7, 2023
382
764
Taasisi nyingi ikiwemo TEC, KKT, CCT, BAKWATA na mengineyo na pia watu wengi wametoa maoni yao kuhusu sheria 3 zilizowasilishwa Bungeni Novemba 2023 na kwa asilimia kubwa wameiomba Serikali na Bunge ifanye marekebisho katika sheria hizo. Nitatoa mifano michache:-

(1) Uchaguzi wote uende kwa pamoja kuanzia Serikali za Mitaa, Wabunge na Rais.

(2) Mwenyekiti wa Tume ya Taifa asiteuliwe na Rais. Yeyote atakayetaka kuomba kuwa Mwenyekiti aombe kama wengine na afanyiewe usaili. Hii ni pamoja na Mkurugenzi wa Tume ya Taifaya Uchaguzi.

(3) Wakurugenzi wa Halmashauri na watumishi wa Serikali wasisimamie uchaguzi badala yake TUME iajiri watumishi wake ili wasimamie uchaguzi.

(4) Dosari ndogo ndogo zilizoonekana kwenye chaguzi zilizopita mfano kukosea herufi moja kwenye jina, kutopiga muhuri n.k. zisiwe dosari za kumuengua mgombea.

Kama wote wametoa maoni hayo mimi naishauri Kamati ya uratibu wa Bunge wakubali yaishe na haya ni mawazo ya Watanzania wengi na mkumbuke kwa sasa Watanzania wengi wameamka. Mkubali yaishe ili CCM isipate taabu kwenye chaguzi zinazokuja.

TEC, KKT, CCT, BAKWATA wana wafuasi wengi nyumba mkubalini yaishe.
 
Back
Top Bottom