Kilichosomwa bungeni ni maoni ya wananchi au ni taarifa ya kamati ya Bunge?

Resilience

JF-Expert Member
Jan 4, 2023
876
4,101
Nimemsikiliza Mwenyekiti ya kamati ya Bunge. Huyu ndugu alipewa majukumu mawili kwa wakati mmoja. Kusikiliza wananchi na kupeleka maoni yao bungeni au kusikiliza maoni ya wanakamati na kuyapeleka bungeni.

Kwa namna hali ilivyokwenda hata vyombo vya habari vimekosa cha kuwaambia wananchi. Walichopata wamepata hoja moja tu, nao ni KAMATI YA BUNGE YAPENDEKEZA KUBADILISHWA KWA JINA LA TUME YA UCHAGUZI LISOMEKE TUME HURU YA UCHAGUZI.

Kwa mantiki nyingine kamati imewasikiliza maaskofu, civil society, wasomi na wananchi mbalimbali wakagundua tatizo lao ni jina la tume.

Lakini kwa tuliokuwa tunafuatilia mjadala tulidhani wananchi watasikilizwa kumbe zamu yao bado. Hongereni sana kamati ya bunge kwa kusoma maoni yenu. Endeleeni kuyajadili maoni yenu na mtafika mbali
 
Back
Top Bottom