Fahamu kisa cha Jasusi John Gweru, Afisa Usalama aliyeikimbia Zimbabwe kwa kuchoka kuua

IBRA wa PILI

JF-Expert Member
Oct 12, 2017
1,448
2,289
Bila Shaka mko poa wakuu yesss twenzetuni uandishi tuvumiliane

John gweru alikua Jasusi kutoka nchini Zimbabwe katika shirika la kijasusi la central intelligence organization (CIO).

Alikua ni kijana aliependa kufanya kazi za kijasusi bila kujua kama ilikua na kazi ngumu ya ukatili na umwagaji damu kisha kupewa sifa kutoka kwa wakuu wao.

Sasa pasipo kutambua undani wa kazi hii akaona apambane ili aweze kujiunga na shirika la ujasusi la nchi ya Zimbabwe na kutokana na ushupavu wake alijikuta akipangwa katika kitengo cha Death squad (DQ). Kikundi cha mauaji na kingne cha ndani zaid kiliitwa CHAL FOUR ambacho ndio kilikua cha hatari Zaid.

Vikosi hiv viliundwa lengo kuu kumlinda na kumkinga Rais Robert Mugabe yaaani kupambana na watu ambao ni wapinzani wake, wakosoaji wa serikali yake na kila ambae alikua mstari wa mbele kumpinga raisi basi kikosi hiki kili muhusu.

Robert Mugabe rais wa Zimbabwe ni moja ya Marais ambao walipambana na wakoloni kupigania Uhuru wa nchi na mpaka kufanikiwa ivyo basi ujiona ni miamba ya Africa na wanastaili kukaa madarakan kwa kipindi chote cha maisha Yao.

Sasa kadri siku zilivyokua zikisogea na wasomi kuongezeka na kuanza kuleta vuguvugu la mabadiriko ndipo nguvu inahitajika kutumika kwa kuwatisha watu hawa au kuwapoteza kabisa KUSIKOJULIKANA MHHHHH
Na hii ndipo Jasusi john gweru ambae si jina halisi Bali ni jina la kijasusi alipewa ndipo anapokuja na mkasa mzima kuhusu central intelligence organization.

John gweru alijiunga na chuo kikuu cha midland state kilichopo nchini Zimbabwe ni chuo kinachotajwa kutoa majasus wengi na ni chuo kinacho semekana ni cha kisiasa kilochotokana na chama cha ZANU PF kma hapa kwetu chuo kikuu cha Udom.

Ivyo chuoni hapo kulikua na majasus pia ambao wao kazi Yao ni kuangalia vijana gani wanafaa kujiunga na shirika la kijasusi ivyo John gweru aliku ni mmoja wapo wa alie onekana kufaa katika shirika la ujasusi.

Ivyo shirika lilikua likiendelea kufanya uchunguzi ili kujilizisha na pia kuwashawishi vijana hao kujiunga na program maalumu ya National youth services lengo ni kuwajaza vijana uzalendo katika mchi Yao kuepusha vibara waovu au mapandikizi lilikua ni lengo Bora lakini sio kilicho kua kikifanyika uko kwenye makambi ni vitu viwili tofaut.

Uko makambini walipewa itikad za mafunzo ya kijeshi kulinda usalama wao na wa raisi Robert Mugabe zidi ya mabeberu ambao kwa mataifa ya wazungu waliona Mugabe ni kama dikteta na pia upinzani na vijana wengi walio onekana kupinga utawala wa Mugabe kwa kudai mabadiliko.

John gweru mwaka 2005 alijiunga kwenye hii program akiwa na umri wa miaka 22 kijana mdogo na mbich shupavu akaanza kupata mafunzo na uku akisimamiwa na kifwatiliwa na wasimamiz pasipo yeye kujua, uko mafunzoni kupitia mafunzo gweru alionekana kufaa katika ripoti za wasimamiz na kuonekana ni mtu sahihi na ivyo kupewa taarifa na wasimamiz kua anahitajika CIO alofurahi lakini pia akua peke ake alikua na wenzake ambao nao walikua na wasimamiz wao ivyo walitakiwa kujiunga.

Walipewa miiko ya kazi Yao na usiri mkubwa pia kuchunguza myenendo majasus wengine sababu kipindi icho raisi Robert Mugabe alikua kwenye migogoro ya kuwatimia wakulima wa kizungu nchini humo ambao walimiliki heka kwa maheka kwa kilimo na ufugaji pasipo kulipia chochote ilikua uamuzi mgumu ambao ulipelekea Taifa hilo kushuka kwa uchumi na misaada kutoka nchi za mahjaribi kukoma.

Na pia kuleta uhadui na CIO ndio ikawa kama kingio kwa chochote ambacho kitatokea kwa lengo la kupambana na rais Mugabe.

John gweru apo bado akujua kapangiwa wapi na tayari viongoz wake wa idara walisha miweka kwenye death squad na ivyo alitakiwa aende kwenye kambi maalumu kwaajili ya mafunzo zaidi, alielekea kambi ya bidula na huko mafunzo yake huchukua takribani miezi sita bila ukomo uko alipewa mafunzo yote ya kutumia silaha, kupigana na silaha, kutesa kwa ukatili kuhoji na mbinu zaidi za uchunguzi na kutunga uongo au propaganda na John gweru alionekana kua Bora katika mafunzo na ivyo rasmi kuanza kupangwa kwenye vitengo vyao na yeye kuwekwa katika kitengo cha death squad.

Kitengo cha hatar akua na namna pia kilikua na mshahara mzito kutokana na kazi ngumu ya kitengo icho inayo hitaji usiri mkubwa na ushupavu, lengo serikali isije chafuka ndan na nje ya nchi.

John gweru alipangiwa kazi ya Kwanza kupambana na chama kikuu cha upinzani cha Movement democratic Change kilichompa shida bwana Robert Mugabe na watu wengi walikiunga mkono kwa kutaka mabadiliko kilimnyima usingizi chama hiki.

Bwana mdogo John gweru kwa mara ya Kwanza alipangiwa kazi yeye na wenzake kuvamia nyumba na ofisi za upinzani kwa kuzivunja na kuzichoma Moto kwa ustadi pasipo kuacha ushahidi nyakati za usiku na bila kukamatwa na kesho jeshi la polisi lotafika kujua A to z kama kuzuga Ila wakijua kazi imefanywa na miamba wa kazi DQ na walifanikiwa kama wangeshikwa basi wangekua wamefeli katika zoezi hilo.

Mtihani wa pili walipewa ilikua ni kuvuruga mkutano wa chama cha upinzani na mkutano huu bwana John gweru anakumbuka kwa kumvunja mkono mwana harakati wa chama cha upinzani na kuleta taharuki mkutanoni na kuvurugika pia hili zoezi walifaulu vizuri pasipo kutambulika.

Wakapewa kazi nyingine ya kuharibu njia za reli kwa kutenganisha Kati ya jiji la Harale na Bulawayo hii ilikua mbinu ya kuonekana chama cha upinzani kimfanya ivyo ili kumuhujumu raisi Mugabe na kuwatengenezea fitna cha pinzani ili pia Death squad walifaulu.

Wakapewa kazi ya ushushu kwa kupewa kazi za kufanya katika nyumba za viongozi wakuu wa nchi kama mabeki tatu na kazi ndogo ndogo lengo ni kuchunguza na kurudi na ripoti kamila bila kijulikana na hapa John gweru alifanikiwa sana.

Ivyo apo waka ambiwa wameiva na sasa wote watajiunga katika kikundi cha Chalfour ambacho unakua tayari kwa lolote ata kuua Baba yako, mam ,mtoto au ndugu pasipo kujali chochote kwa maslai ya nchi na apo wakawa katika kikundi hatari na wakarudi kambini bindula kwenda kwenye mafunzo mengine ya ukatili uliopitilizan wa kinyama na kutisha.

Walitambulishwa kwa walimu wao wa tatu waliokuep kwa majina ya kijasusi Muza,mazwombwe na mkarati na wao kina John gweru walijitambulisha kwa majina halisi na hapo wakaambiwa ayo sio majina yenu kwa sasa na ndipo John gweru alipopata jina hili lake akuweka wazi kwa usalama zaidi hapa walipandikizwa chuki na roho ya ukatili pasipo kujali kitu.

Wanaondoka na mazwombwe mpaka makao makuu ya chama Harale na uko wakatambulishwa kwa ma boss zao wengine katika kazi ivyo akuna kuwashangaa.

Mazwombwe aliwachukua na kuwapeleka mpaka kwenye gereji ya makao makuu ya zamani ya ZANU PF ambayo ipo chini ya jengo mazwombwe. Baada ya kufika huko alitoa rimoti na kubonyeza kitufe na mlango kufunguka ambapo uwezi jua kama kuna mlango ki kawaida.

Wakiingia ndani ambako kulikua na gereza la Siri humo walishikiliwa watu ambao walionekana kuwa wasumbufu kwa serikali ya bwana Robert Mugabe na walianza kuoneshwa chumba kwa chumba.

Kuna chumba kimoja walikuta kina Wazungu wawili wanashikiliwa ambao bwana mazwombwe aliwaambia walikua ni majasusi wa CIA waliokua wakipanga kutingisha Uurais wa bwana Mugabe na walikua katika hali mbaya Sana ya kiafya ivyo akuna kuogopa mtu kwamba katoka shirika gani la kijasusi ni kitekeleza kazi Tu bila uoga.

Waliendelea kuzungushwa na kukuta watu zaidi wakishikiliwa ni wafungwa wa kisiasa wakiwa kwenye mateso makal na wengine wakikata roho mbele Yao na akuna anaejua kua wako wapi Ila ukitoka nje habari zao ni kua watu hao wamepotea na watu wasio julikana na aijulikani walipo au katika mazingira ya kutatanisha.......

Tutarejea kwa muendelezo.

NB: Source ijue historia na komrade kabuli & davistar mata.
 
Kuna jamaa yangu aliniambia yeye pepo yake ni hapahapa duniani kwa jinsi mikono yake ilivyojaa damu anasema haamini kama Mungu atamsamehe. The guy lives his life to the fullest ila moyoni najua ana baka kubwa sana linamtesa.
Duh
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom